Gazeti la Raia Mwema lakosekana Tabora

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,826
966
Kutokana na taarifa za sintofahamu zimesababisha nakala zote za gazeti la raia mwema kutoweka katika hali ya kutatanisha kutokana na kuandika habari zinazomuhusu mmoja wa ndugu wa Mbunge wa viti maalum CCM kukamatwa na madawa ya kulevya katika kiwanja cha ndege cha Mwl. J. K. Nyerere.

OMBI. Ninaomba aliye na taarifa ya kilichoandikwa atupie humu.

Update: Nimempigia mtendaji mkuu kasema taarifa zimewamefikia kesho watu wa tabora watalipata gazeti.
 
Wasiliana na Mtendaji mkuu wa Gazeti Ndugu Boaz Moses (0715 834971 au 0754 834971) ili asaidie upatikanaji wa nakala nyingine huko Tabora!

Pia nimemuuliza kama ana taarifa hizi!!
 
Kutokana na taarifa za sintofahamu zimesababisha nakala zote za gazeti la raia mwema kutoweka katika hali ya kutatanisha kutokana na kuandika habari zinazomuhusu mmoja wa ndugu wa Mbunge wa viti maalum CCM kukamatwa na madawa ya kulevya katika kiwanja cha ndege cha Mwl. J. K. Nyerere.

OMBI. Ninaomba aliye na taarifa ya kilichoandikwa atupie humu.

Update: Nimempigia mtendaji mkuu kasema taarifa zimewamefikia kesho watu wa tabora watalipata gazeti.

Nenda www.raiamwema.co.tz
 
Kazinunua zote kwa agent,yule pusher,pedler wa kike munde tambwe.hapa tabora taarifa zimeshaanza kuzagaa za mbunge wao kuhusishwa na biashara ya marijuana,pia kuuzia tanesco matairi fake.
 
Mbunge ahusishwa na ‘wauzaji’ bangi
Mwandishi WetuToleo la 252
1 Aug 2012

MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokea mkoani Tabora, Munde Tambwe Abdallah, anahusishwa na wanawake waliokamatwa wakisafirisha bangi kwenda nje ya nchi, Raia Mwema limefahamishwa.

Raia Mwema limejulishwa kwamba mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa na bangi na kufikishwa mahakamani, Hadija Magesa ni ndugu wa mbunge huyo na jina lake halisi ni Hadija Tambwe Abdallah, na kwamba walikuwa pamoja muda mchache kabla ya wote kuanza safari kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana zinaonyesha kwamba Munde aliondoka nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates namba EK 726, Julai 28, 2012 kwenda Italia, saa chache kabla ya Hadija na mwenzake, Sasha Mnyeke, kukamatwa wakitaka kuondoka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki TK 604 Julai 29, 2012 kwenda* Instabul, Uturuki.

Uchunguzi wa Raia Mwema umethibitisha kwamba Munde ambaye ni mmoja wa wabunge waliomo ndani ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayotuhumiwa kwa rushwa, aliaga bungeni kuwa anasafiri kwenda nchini India, kumpeleka mama yake mzazi kwa matibabu.

Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel amesema mjini Dodoma kwamba Munde ana ruhusa ya shughul binafsi kwenda nje ya nchi.

“Amekwenda India kumpeleka mama yake mzazi kwenye matibabu,” amesema Joel.

Tayari Khadija na Sasha wamekwishakufikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na biashara hiyo wakati Munde akiwa nchini Italia akitarajiwa kurejea nchini Agosti 2, mwaka huu kupitia Dubai.

Katika mazingira tata Hadija anamiliki hati ya kusafiri AB 151604 ikiwa na jina la Hadija Magesa wakati tiketi yake ikiwa na jina la Hadija Tambwe, jambo ambalo limeelezwa kuibua utata uliosababisha kukamatwa kwao kabla ya kuondoka Dar es Salaam.

Uchunguzi wa Raia Mwema unabainisha ya kuwa Julai mosi mwaka huu Munde Tambwe alipata kusafiri nje ya nchi na kurudi akitokea Dar es Salaam kwa njia hiyo hiyo aliyosafiri Julai 28, 2012 kwa ndege ya Emirates EK 726.

Juhudi za kuwasiliana na Munde huko aliko azungumzie tuhuma zinazoelekezwa kwake hazikuzaa matunda.

Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa, ameliambia Raia Mwema kwamba makachero wanaendelea na uchunguzi kujua mtandao mpya wa dawa za kulevya unaohusisha watu maarufu kutokana na taarifa wanazopokea.

Raia Mwema *inazo taarifa za ndani ya kuwapo kwa mtandao wa wafanyabiashara wanaotumia baadhi ya wanawake kusafirisha ya dawa za kulevya kwenda nje ya nchi, baadhi wakiwa watu wenye mahusiano ya kidugu.

Kuhusishwa kwa Munde katika taarifa hizi za bangi kunachangia katika wiki* ambayo inaweza kutajwa kuwa ni mbaya sana kwa Mbunge huyo wa Viti Maalumu ambaye amekuwa akitajwa sana katika sakata lililoibuka bungeni wiki iliyopita likiwawatuhumu baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kwa kufisadi Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

Kamati hiyo sasa imevunjwa na Spika Anne Makinda kutokana na hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Namtumbo, Vita Rashidi Kawawa, akiomba kamati hiyo ivunjwe kwa kulidhalilisha Bunge, pamoja nayo na kamati nyingine zenye kuelekezewa tuhuma za ufisadi.

Kati ya tuhuma zinazoelekezwa kwa Munde, ambazo kwa pamoja na nyingine zitachunguzwa na Bunge lenyewe ni kampuni yake kufanya biashara ya kuiuzia matairi TANESCO.
 
Kutokana na taarifa za sintofahamu zimesababisha nakala zote za gazeti la raia mwema kutoweka katika hali ya kutatanisha kutokana na kuandika habari zinazomuhusu mmoja wa ndugu wa Mbunge wa viti maalum CCM kukamatwa na madawa ya kulevya katika kiwanja cha ndege cha Mwl. J. K. Nyerere.

OMBI. Ninaomba aliye na taarifa ya kilichoandikwa atupie humu.

Update: Nimempigia mtendaji mkuu kasema taarifa zimewamefikia kesho watu wa tabora watalipata gazeti.

ni kweli mkuu....

nimelitafuta jana na leo hapa Tabora nimelikosa....stendi pale sokoni hakuna, pale mtaa wa rufita kama unaelekea kwa akina Rage nehi...

habari nlizonazo ni kuwa mheshimiwa aligiza vijana wake kununua nakala zote na kisha kuzichoma moto ili kuzuia wana Tabora wasijue nini kinaendelea kuhusiana na kesi ya ndugu yake kukamatwa na bangi hivi majuzi...

......na si unajua kuwa kuna tuhuma za mheshimiwa kujihusisha na biashara za ile kitu nyeupe kutoka america ya kusini(Colombia kwa akina hayati Pablo Escobar)....nadhani anajiaminisha kuwa kwa mbinu hii atazuia habari hizo za nduguye na zake binafsi kujulikana....by the way, mwisho wa ubaya ni aibu.

It is a shame kwa kweli!!!!
 
Hivi tabora kwa sasa pakoje? mana siku za nyuma nilikua napitapita hapo ukame kinoma, baiskeli kwa wingi, wezi stesheni ndio usiseme!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom