Gazeti la Raia Mwema la leo mmmh..

mtoa hoja amepotosha ukweli kwa malengo binafsi anayoyajua yeye!! Muundo wa gazeti la Raia Mwema la leo (6/7/2011 toleo namba 193) upo kama ifuatavyo-sehemu ya kwanza ni ile ya kawaida ya matoleo yote yaani ina kurasa 1-16 ambapo kurasa 1 tu (ya 9) ndio ipo tangazo full, the rest (kurasa 15) ni habari na makala motomoto kama kawaida yake; na sehemu ya pili kuna insertion ya kurasa 20 za Hotuba ya Waziri Mkuu na Mawaziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hotuba hizo zipo separate na kurasa za kawaida na zipo katika namba za kirumi (i to xx). Kwa hiyo mtoa hoja ni muongo, mfitinishaji na mzandiki aliye tayari kupindisha ukweli kwa maslahi yake binafsi yasiyo na tija kwa maslahi ya umma na naombwa wana JF apuuzwe, azomewe na alaaniwe. Namsihi mtoa mada ajaribu kufanya reference matoleo mengine ya Raia Mwema ambayo hayana insertion kama hii huwa yana kurasa ngapi? Tuwe wakweli ili tuwekwe huru!!
 
Tunapaswa tutambue magazeti bila matangazo yanakufa,unless kama utaendesha gazeti hilo kwa kutumia pesa za mifukoni mwa watu,na hapo ndo itabidi uwatumikie hao waliokununua,ambapo kimsingi ni matangazo pia maana wanakulipa ili uwatangaze hao waliokununua.
 
Unanitia mashaka. umeanza kusoma magazeti lini?

Hata mimi huyu mtu ananitia mashaka, kwanza uvivu wa kufikiri unajudhihirisha wazi. Je amewahi kujiuliza biashara ya magazeti inaendeshwaje kama yeye ni msomaji wa siku nyingi. Pili gazeti la Raia Mwema lilipotoka mara ya kwanza kabisa katika toleo lake namba 1 lilitanabaisha malengo yao na kusema wao wametoka wapi kufikia hapo. Walieleza changamoto za kuendesha gazeti na walieleza makosa waliyowahi kuyafanya awali wakiendesha gazeti lingine kabla ya raia mwema, Katika makala yao sisi ni akina nani waliyasema mengi. Kama huyu jamaa kweli ni msomaji wa siku nyingi ni wazi asingeweka post hii au angeweka katika angle nyingine. Jamani tumefika hapa tulipo na nchi hii kwa uvivu wetu wa kufikiri. Tuamke basi angalau tujilazimishe kufikiri kwanza kwa kutafuta taarifa na maarifa sahihi.
 
Back
Top Bottom