Gazeti la raia mwema; Dr Slaa ag'ara zaidi kisiasa mwaka 2011

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu, gazeti la raia mwema la leo limeujadili ktk ukurasa wa pili hali ya kisiasa ya mwaka 2011 na kusema kuwa ulikuwa ni mwaka wa kisiasa zaidi kutokana na matukio kadhaa yaliyoorodheshwa ambayo ni katiba mpya, Sakata la Arusha, Wabunge wa chadema kususia hotuba ya Rais, maandamano ya chadema nk. Matukio yote yalimweka DR Slaa kuwa ktk ya matukio hayo hasa suala la katiba mpya ambalo ni agenda ya chadema na ilipata msukumo kutokana na Dr Slaa kudai kuibiwa kura na kususia kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Kikwete. Likaja sakata la wabunge wa chadema kudai katiba mpya nje na ndani ya Bunge.

Gazeti limewaorodhesha viongozi wengi wa kisisasa wa vyama vya ccm, Chadema na CUF Kila mmoja kwa jinsi alivyopanda au kushuka kisiasa. Lipumba na Maalim wanaonekana kushuka Hamad Rashid akionekana kuja juu zaidi. Kwa upande wa Chadema wengi kwa kuwa ndio wanachipukia wameonekana kupanda zaidi.

Lakini kubwa kuliko zote ni pale gazeti linaposema, ninanukuu;
KATIBU MKUU WA CHADEMA DR W Slaa amezidi kung’ara kwa umaarufu wa kisiasa pengine kuliko wanasiasa wengine ndani ya Chadema , huku akionekana kuwa kiongozi wa kitaifa zaidi, na baadhi ya watu waliamini kuwa kuanguka kwake kisiasa (urais 2010) kungeweza kuwa ni ishara ya chadema kupoteza umaarufu.

Viongozi wengine waliofanya vizuri ni kila mmoja ktk nafasi yake Mbowe, Lisu, Zitto, nk

My take; Hayo ni maoni ya gazeti niliyoya paraphrase naomba maoni yenu
 
Ni kweli uyu jamaa namuona kama ngome yangu na atang'ara mpaka 2015 inshallah.....
 
Lema...............

mkuu Saint Ivuga,
kwenye gazeti walimtaja kama mpambanaji wa haki za binadamu na mwenye msimamo. Samahani nilimsahau kidogo, na Lissu amejipambanua kama mwenye uelewa mkubwa wa masuala ya kitaifa na kimataifa. Kumbuka niliwataja baadhi tu.
 
na bado shenz type zao!! ccm watashika adabu mpaka ifike 2015.

vipi shosti Nape yuko kwenye position gani? maana mwaka 2011 alikuwa anapayuka sana.
 
na bado shenz type zao!! ccm watashika adabu mpaka ifike 2015.

vipi shosti Nape yuko kwenye position gani? maana mwaka 2011 alikuwa anapayuka sana.

Nanukuu,
Mwaka huu wa 2011 unaisha huku ccm ikiwa ktk kitendawili cha namna ya kuhitimisha kujivua gamba ambayo ilitangazwa rasmi february, baadhi ya wajumbe wa secretarieti wakiishiwa mbinu za kufanya siasa zenye ufanisi zaidi kwa chama hicho,END OF QUOTE.
 
Ndugu yangu Aweda,

:juggle:Jambo hili lipo wazi si tu kimtazamo bali pia kiutafiti. Watu wanapanda au wanashuka umaarufu kutokana na mambo wanayoyafanya au maneno wanayoyaongea na mambo hayo au maneno hayo yawe ya kijamii (kitaifa). Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa si tu kwamba anasema na kutenda kiutafiti bali pia ni makini katika kusema au kutenda kwake.

Wakati wa tadhimini ya kumalizika kwa kikao cha bunge (2009), Dr. Slaa aliongoza kwa kuwa makini katika kujenga na kutetea hoja zake bungeni si tu katika jimbo lake la Karatu bali pia mambo yote ya kitaifa. Utakumbuka alipotaka kuleta hoja ya mafisadi bungeni na spika kuizima, aliweza kuiweka kwa wananchi pale Kidongo chekundu na wote waliotajwa hawakuweza kushitaki japo alijigamba kufanya hivyo mpaka spika wa wakati huo kuibukia TBC1 akidai nyaraka alizonazo Dr. ni feki.

Mambo ni mengi sana kwa Dr. Slaa, hivyo ni haki yake anayostahili. Tusiwasahau makamanda wengine G. Lema, J. Mnyika, Z. Kabwe, H. Mdee n.k wakiongozwa na kamanda mkuu F. Mbowe chini ya mwavuli mkubwa - CHADEMA.:lol:
 
Ndugu yangu Aweda,:juggle:Jambo hili lipo wazi si tu kimtazamo bali pia kiutafiti. Watu wanapanda au wanashuka umaarufu kutokana na mambo wanayoyafanya au maneno wanayoyaongea na mambo hayo au maneno hayo yawe ya kijamii (kitaifa). Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa si tu kwamba anasema na kutenda kiutafiti bali pia ni makini katika kusema au kutenda kwake.Wakati wa tadhimini ya kumalizika kwa kikao cha bunge (2009), Dr. Slaa aliongoza kwa kuwa makini katika kujenga na kutetea hoja zake bungeni si tu katika jimbo lake la Karatu bali pia mambo yote ya kitaifa. Utakumbuka alipotaka kuleta hoja ya mafisadi bungeni na spika kuizima, aliweza kuiweka kwa wananchi pale Kidongo chekundu na wote waliotajwa hawakuweza kushitaki japo alijigamba kufanya hivyo mpaka spika wa wakati huo kuibukia TBC1 akidai nyaraka alizonazo Dr. ni feki.Mambo ni mengi sana kwa Dr. Slaa, hivyo ni haki yake anayostahili. Tusiwasahau makamanda wengine G. Lema, J. Mnyika, Z. Kabwe, H. Mdee n.k wakiongozwa na kamanda mkuu F. Mbowe chini ya mwavuli mkubwa - CHADEMA.:lol:
nimeipenda hii, maelezo safi yenye mashiko, yani imejitosheleza,, wabeja sana...........
 
Nipo huku KAHAMA magazeti yanachelewa sana kufika huku ungetumwagia habari yote hapo tukafaidi wote,jamani nimeiona buzwagi simchezo kuna ukuta wanajenga kwa ajili ya kuzuia wizi ni ukuta wa nguvu hapa dhahabu zinabubwa na ndege nazingine kwa makontena kilasiku jioni wakuu inatisha kunabarabara zimengwa hapa mjini za kubabaisha wamenyunyizia rami ya danganya toto hapa nivichekesho tu hali ya kiuchumi hapa mjini ni ngumu sana mvumko wa bei usiseme wananchi wamechoka sana nimejaribu kuongea na hawa madreva pikipiki wote wanakwambia wanakiu ya mabadiliko lakini hawana mtu wakuwaongoza huku sasatunahitaji juhudi za makusudi kuwakomboa wana KAHAMA.
 
Nipo huku KAHAMA magazeti yanachelewa sana kufika huku ungetumwagia habari yote hapo tukafaidi wote,jamani nimeiona buzwagi simchezo kuna ukuta wanajenga kwa ajili ya kuzuia wizi ni ukuta wa nguvu hapa dhahabu zinabubwa na ndege nazingine kwa makontena kilasiku jioni wakuu inatisha kunabarabara zimengwa hapa mjini za kubabaisha wamenyunyizia rami ya danganya toto hapa nivichekesho tu hali ya kiuchumi hapa mjini ni ngumu sana mvumko wa bei usiseme wananchi wamechoka sana nimejaribu kuongea na hawa madreva pikipiki wote wanakwambia wanakiu ya mabadiliko lakini hawana mtu wakuwaongoza huku sasatunahitaji juhudi za makusudi kuwakomboa wana KAHAMA.

Mkuu huwa kila mara najiuliza kama Buzwagi ni mgodi wa Barrick kweli,maana uendeshwaji wake na hasa suala la mishahara nitofauti kabisa na migodi ya Barrick North Mara na Bullyanhulu,mishahara ni midogo na kuna wachache wanalipwa vizuri na tena increaments hufanyika kwa siri utadhani ni kwa wadosi vile.Kuna kitu kitakuja julikana tu mbele ya safari,yangu macho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom