Gazeti la Rai: Mukama adaiwa kutaka kujiuzulu kisa Nape; Mwenyewe akanusha!

Source Gazeti la Rai Nguvu ya Hoja

Katibu mkuu wa CCM a.k.a Magamba amemwandikia barua nwenyekiti wake wa CCM Rais Jakaya Kikwete kuomba kujivua gamba na sababu kuu ya kujiuzulu huko ni mvurugano ndani ya chama hicho na msababishi mkuu ni Katibu mwenezi wa chama bwana Nape Nnauye kuchukua majukumu yote ya chama na kufanya maamuzi kama atakavyo yeye.

Sasa maamuzi ya kujiuzulu kwake yatategemea mwenyekiti na kamati ya CCM kuamua kujiuzulu kwake au la.

Concern

Nape Nape iko wazi yeye ndio mwenyekiti, katibu mkuu, msemaji wa chama. Bila shaka kuna kundi anallilitumikia kwa maslai binafsi. Nashukuru kwa kuongeza kasi ya kukipeleka chama kuzimu

ccm ni sawa na mgonjwa mahututi na hakuna jinsi ya kuiokoa isiende upotevuni.
RIP CCM!
 
JZ hajaingilia kati hapo kwa kutuma kile kikosi kazi kikamalize uasi?
 
Kuhusu yusuf makamba namtetea nape!
Makamba alimwachie Lowassa apige dili ya kuuza jengo la umoja wa vijana nape akapigia kelele lowassa.
Makamba akakasirika na kuamua kumvua uanachama nape...hivyo hawa wana ugomvi binafsi.

Hivi kweli ile kamati ya Chenge ilifikia wapi katika "uchunguzi"? Na je, baada ya kupewa cheo CCM, nape mbona HAONGELEI kabisa suala hilo ambalo alikuwa analisemea kwa nguvu mpaka mapovu yanamtoka?
Nape,kwa kuwa umo humu jamvini naomba unisaidie majibu ya maswali yangu, tafadhali ndugu.
 
Hivi sababu siyo taarifa ya kamati yake juu ya hali ya chama ambayo ilisababisha Makamba kutoka na yeye kuingia? Alichodhani amekiainisha kwenye taarifa yake alipoingia ndani ameona mambo hayaendi hivyo na hivyo kufanya yeye na Makamba kuwa sawa sawa. Katibu Mkuu wa CCM hafanyi chochote isipokuwa kile kilichoamuliwa na JK pamoja na familia yake.

Mkuu sasa hivi chama kizima hakina nidhamu, demokrasia ndani ya chama imekufa. Kilichobaki ndani ya CCM sasa ni kukosa nidhanu, kupuuza itifaki za chama, na kufanya mambo kiswahiliswahili, kiasi kwamba Mwenyekiti anakuwa na kazi ngumu na kutakiwa kufanya mambo ambayo kimsingi hayakuwa kazi za mwenyekiti.

Kwa sasa kila mtu ni msemaji wa chama, na kila msemaji ni mtu wa chama, hata mipaka haionekani. Kutokana na ubovu na kutoheshimu itifaki, hata aje nani uovyo utaendela kuwepo, iwe ni Makamba, Mukama au magamba.
 
Akiwa kagera Nape alinukuliwa akisema wacha watu wahame ataakibaki yeye peke yake CCM itatudumu! Sijui tendwa atamruhusu kuwa na chama yeye peke yake! Lakini Mkama yy ni katibu mkuu wadhifa mkubwa sana anaweza kumwajibisha Nape, Kimemshinda nini? Shida alikuwa na ajennda moja tu ya kuvua watu magamba imegonga mwamba han plan B.
 
Hana lolote huyu mzee, ameshaona vuguvugu limewashika pabaya sasa wanatafuta njia ya kutokea

Ameona afadhali asepe mapema kwani wazee wakina KISUMO wenye chama, walishaanza kusema kuwa Mukama ni mzigo kwa chama kazi kulamba ulabu tu!!
 
Code:
Kuhusu yusuf makamba namtetea nape!
Makamba alimwachie Lowassa apige dili ya kuuza jengo la umoja wa vijana nape akapigia kelele lowassa.
Makamba akakasirika na kuamua kumvua uanachama nape...hivyo hawa wana ugomvi binafsi.
..kweli, sasa Mmomonyoko rasmi wa makundi kuanzia pale hasa uvccm ndo ulipoanzia.
ndugu yangu hili Jengo hapa 'Faya' limezua mengi baba....Subiri sinema iendelee
 
tunajuwa cdm mnamuogopa nape mnapindisha maneno2..

MNAMBOWA
Mkuu hivi kuna uhusiano gani kwa CDM kumuogopa Nape na thread iliyoanzishwa? Rudia tena kusoma, na FYI CDM haimwogopi Nape kama dhamira yako ya ndani inavyokushuhudia.. nadhani umenisoma.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Subash Patel mwarabu, muhindi sijui singa wa pale Lugoba chalinze si ndo inasemekana ndo aliyechukua dili la uvccm kumbe anafika mpaka monduli au ni uvivu wa kufikiri tu. monduli na chalinze mbona mbali sana?
Kuhusu yusuf makamba namtetea nape!
Makamba alimwachie Lowassa apige dili ya kuuza jengo la umoja wa vijana nape akapigia kelele lowassa.
Makamba akakasirika na kuamua kumvua uanachama nape...hivyo hawa wana ugomvi binafsi.
 
Hivi sababu siyo taarifa ya kamati yake juu ya hali ya chama ambayo ilisababisha Makamba kutoka na yeye kuingia? Alichodhani amekiainisha kwenye taarifa yake alipoingia ndani ameona mambo hayaendi hivyo na hivyo kufanya yeye na Makamba kuwa sawa sawa. Katibu Mkuu wa CCM hafanyi chochote isipokuwa kile kilichoamuliwa na JK pamoja na familia yake.

Of course chanzo cha sera ya kujivua gamba ni ushauri uliotolewa na kamati yake.
Kimsingi, CCM huenda hawajatekeleza fully kile ambacho alikiainisha katika ripoti ile, ili kutibu mpasuko chamani.
Tutaona mengi sn kabla ya 2015
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom