Gazeti la rai laondolewa sokoni leo

Naona hii kweli hata hapa librarykwetu hayapo na wakati si kawaida
 
Gazeti la Rai limekusanywa leo na halipatikani kabisa. Taarifa tulizonazo zinaeleza kuwa lilikuwa na habari inayoonyesha kuwa Beno Malissa na Ridhwan Kikwete wanaandaa mapinduzi ya kumng'oa Katibu wa UVCCM Martine Shigella. Taarifa za ndani kutoka Habari Cooperation zinaeleza kuwa habari hiyo iliwanukuu wenyeviti 17 wa UVCCM mikoa ambao walikuwa wakipingana na harakati hizo. Tena inaelezwa kuwa Usalama wa Taifa wamepewa jukumu la kuhakikisha gazeti hilo haliingii mtaani. Wenye taarifa zaidi mnaweza kuendelea ikiwemo kutupa habari iliyosababisha gazeti kukusanywa.

Hii habari inatia shaka, kwanza katika kutaja jina la Gazeti nadhani alikusudia kusema kama alivyo sema kuwa ni Rai (habari corp), lakini content inanipa shida kidogo, yaani Rai
Mmiliki RA
RA ni CCM
RA na JK ni marafiki achilia mbali kuwa wote wana CCM
Ridhiwani mtoto wa JK
Ridhiwani kada maarufu wa CCM
Wote uliowataja (pamoja na Rai) ni CCM
How comes CCM wenyewe waumbuane?

Mtoa maada jitokeze ufafanue hapa, au umetumwa nini? Maana CCM wakati mwingine wanafanya mambo ya kitoto halafu wanaita 'INTERJENSIA'
 
Mimi nimelitafuta tangu jana sikulipata.

Kama ni hivyo tunaomba mutufanyie scanning na sisi tupate kuona ni kitu gani kimeandikwa. Au Generali afanye sacrifice kidogo alipost kwenye web.

rai sio la generali wewe!!!!!!!!
 
Angalieni. Lengo la mkakati huu ni kulitangaza ili mkimbilie kulinunua - maana ktk hali ya kawaida halinunuliwi au kusomwa
 
rai sio la generali wewe!!!!!!!!

Wana Jf naomba nichangie hapa. Taarifa za uhakika ni kwamba Gazeti ni RAI ni kweli limekusanywa na Mikoani ma Agent wote wamezuiliwa wasiliuze inasemekana ni AMRI wahusika wa kuu ni IDARA inasema kwamba kwa muda Mrefu magazeti ya New Habari yamekua ni chombo pekee kinacho wasaidia CCM na serekali,lakini tangu mwezi November kumekua na Mabadiliko makubwa.
Nimeongea na mtu ndani ya New Habari amesema ni kweli Gazeti lao limekusanywa leo na mikoani wamezuiwa kuliuza,kisa limeandika habari inayohusu MGOGORO WA UVCCM ambao umeanzia pale makao makuu ya jumuiya hiyo.

Kwahiyo wana JF story yenyewe ina Headline inayosema MGOGORO MKUBWA UVCCM na imeelezea mpango unaendeshwa na vigogo wa jumuiya hiyo kumuondoa katibu mkuu wa UVCCM kisa anapingana na simba mtoto.
 
Gazeti la Rai limekusanywa leo na halipatikani kabisa. Taarifa tulizonazo zinaeleza kuwa lilikuwa na habari inayoonyesha kuwa Beno Malissa na Ridhwan Kikwete wanaandaa mapinduzi ya kumng'oa Katibu wa UVCCM Martine Shigella. Taarifa za ndani kutoka Habari Cooperation zinaeleza kuwa habari hiyo iliwanukuu wenyeviti 17 wa UVCCM mikoa ambao walikuwa wakipingana na harakati hizo. Tena inaelezwa kuwa Usalama wa Taifa wamepewa jukumu la kuhakikisha gazeti hilo haliingii mtaani. Wenye taarifa zaidi mnaweza kuendelea ikiwemo kutupa habari iliyosababisha gazeti kukusanywa.
usiwashushie heshima wikileaks

wale wako na uhakika na wanachapisha things with evidene sio wewe uinakuja na tetesi kama kawaida

na gazeti sio Rai ni Raia Mwema na wengi wanalo

Unashusha hadhi ya wikileaks... maybe you should change the name and call yourself gossipleaks
 
RAI ninalo hapa,habari yenewe iko front page yenye heading "MGOGORO MZITO UVCCM" lakini hakuna anapotajwa Ridhwani,ila waliotajwa ni Malisa na Shigela.
Hata kama kuna watu hawalinunui lakini linaandika habari na huwa zinafanyiwa kazi,nakumbuka zile habari za Mkuu wa KKT zilivyofanyiwa kazi,pia lilmbomoa sana Dr.Slaa wakati wa kampeni
 
Wana Jf naomba nichangie hapa. Taarifa za uhakika ni kwamba Gazeti ni RAI ni kweli limekusanywa na Mikoani ma Agent wote wamezuiliwa wasiliuze inasemekana ni AMRI wahusika wa kuu ni IDARA inasema kwamba kwa muda Mrefu magazeti ya New Habari yamekua ni chombo pekee kinacho wasaidia CCM na serekali,lakini tangu mwezi November kumekua na Mabadiliko makubwa.
Nimeongea na mtu ndani ya New Habari amesema ni kweli Gazeti lao limekusanywa leo na mikoani wamezuiwa kuliuza,kisa limeandika habari inayohusu MGOGORO WA UVCCM ambao umeanzia pale makao makuu ya jumuiya hiyo.

Kwahiyo wana JF story yenyewe ina Headline inayosema MGOGORO MKUBWA UVCCM na imeelezea mpango unaendeshwa na vigogo wa jumuiya hiyo kumuondoa katibu mkuu wa UVCCM kisa anapingana na simba mtoto.

Kwahiyo ni aidha uko naye aua uende na maji..afu ndo wanajiita wana demokrasia..
 
Acheni kuchakachua maneno/majina.

Ni Raia Mwema ndilo limekuwa adimu.

Rai? Hii toilet paper iko tele kwa newspaper vendors.

Raia mwema tumeipata jana , hiyo toilet paper hata mimi nimeona muuzaji mmoja anayo sasa sijui imekusanywa vipi! Kwani huwa linaandika nini? Nililisoma zamani sana.
 
RAI ninalo hapa,habari yenewe iko front page yenye heading "MGOGORO MZITO UVCCM" lakini hakuna anapotajwa Ridhwani,ila waliotajwa ni Malisa na Shigela.
Hata kama kuna watu hawalinunui lakini linaandika habari na huwa zinafanyiwa kazi,nakumbuka zile habari za Mkuu wa KKT zilivyofanyiwa kazi,pia lilmbomoa sana Dr.Slaa wakati wa kampeni

Sasa si uweke hapa tuone kama unayosema wewe ni kweli!! Mleta hoja kasema Simba mtoo katajwa....wewe unakataa. The weka evidence hapa.
 
Ukweli ni kwamba gazeti la Rai kweli limekusanywa japo wamecheleweshwa sana baadhi ya maeneo limeshasambazwa.

Utata ni kwamba hata Raia Mwema jana lilikua chache sana kiasi likaisha sokoni, hata sasa baadhi ya maeneo halipo.
 
Raia mwema lipo mitaani. Hata mimi huku mikoani ninalo. Front page:1. vita ya umeya: siri yafichuka 2. Mkapa amponza kikwete, taarifa za faragha zaanikwa, vigogo wakana. Kuna picha za hosea, mkapa na mkwerer
 
Sina mchango apa maana aya majarida mawili sijawahi kuyasoma na sina mpango wa kuyasoma maishani! Hata kama Yesu Mwokozi atarudi kupitia vijarida ivi viwili basi mi ataniacha maana sitamjua kwani sisomi vijarida vya mafisadi.
 
Back
Top Bottom