Gazeti la Mwananchi na gamba la CCM!

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Ukipita katika website hii, Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza utakutana na kipengele cha kupiga kura chenye title ya CCM kujivua ‘Gamba' inatosha kujisafisha? Kwa kweli maswali yaliyowekwa ili yapigiwe kura ni shubiri kubwa kwa CCM, yaani yamekaa kuchekesha chekesha, dharau na kejeli kwa CCM juu ya zoezi hilo. Hebu cheki Questionnaire yao hapa chini kisha uniambie hawa jamaa Msekwa si anaweza kuwaita JF2!
Maswali yenyewe ndiyo haya hapa,


  1. Ndiyo kutaimarisha chama, na kuja na mikakati mipya ya kujenga nchi
  2. Hapana huu ni ubabaishaji wa siasa za maji taka, wanazunguka mbuyu
  3. Wataleta mabadiliko ya nukta baadaye watarudi katika hali yao ya ufisadi
  4. Ni bora wakifutilie mbali na kuanzisha chama kingine, gamba huwa linakomaa tena
Yaani kwa mashabiki wa CDM wanaweza kushindwa kuvote kwa jinsi maswali hayo yanavyoleta raha na kero kwa CCM!
Mimi binafsi yangu, namba mbili ndiyo kura yangu je wewe namba ngapi imekufurahisha?
 
dahh namba 4 imekaa mbaya kinoma....wakifutilie mbali...hii itakuwa CDM kulamba dume ikitokea!! Nadhani akina RACHEL watakuwa wapo kazini sasa!!
 
dahh namba 4 imekaa mbaya kinoma....wakifutilie mbali...hii itakuwa CDM kulamba dume ikitokea!! Nadhani akina RACHEL watakuwa wapo kazini sasa!!
Ili tupishe zoezi la kila mara kuvua magamba maana halichelewi kurudi tena.
 
Back
Top Bottom