Gazeti la Mtanzania wasema Zitto ni mbunge wa CCM!

acheni upuuzi wenu, nani ambaye hajawahi kuandika taarifa kisha ikaja kuonekana ina mapungufu ya uandishi? kwani ni kompyuta au binadamu anayeyaandika hayo? kuna mhariri, sawa, lakini makosa mengine ni minor sana, kiasi hata mhariri anaweza kupitiwa kuyaona. so bila shaka walitaka kuandima chadema wakaandika ccm, sioni shida kwani zitto si mbunge wa ccm hata kidogo.

sioni mantiki ya kumhusisha zitto na CCM, tusiwe wepesi wa kuweka dhana nyingi zisizo na msingi. zitto kabwe ni mbunge wa chadema , period.

after all zitto yuko active zaidi pengine kuliko hata hao wabunge wengine mnaowaona wako loyal mno kwa chama. tatizo letu watanzania(wapinzani hata ccm) bado tuna uleule mtazamo wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama, kwamba, mwenyekiti yu ndio yupo sahihi na yeyote atakayekuwa na mawazo tofauti basi ni adui, sio mwenzetu, mara anatumiwa, sijui kibaraka n.k tujifunze zaidi demokrasia, kwani demokrasia ni kutoa fursa kwa kila mwenye sifa kugombea nafasi yoyote impasayo na pia kutoa mawazo yake yoyote hata kama yanatofautiana na ya kwako.
 
Ktk hali ya kushangaza,nimekutana na habari ya kushangaza ktk gazeti la Mtanzania ambalo lilikuwa linampigia kampeni mzee kikwete,EL,RA,yani lile gazeti la kutetea ufisadi limesema ktk ukurasa wa kwanza na wa pili kuwa mbunge Zitto ni CCM.

Mwenye kopi atazame pale kulia kulikoripotiwa kuwa Zitto (CCM) ameibua ufisadi mpya. Limeripoti ivo wakati Zitto akiandamwa na wananchi kuwa hawamwelewi.

Je, ni harakati za kumgonganisha Mh. ZITTO na wananchi? Au ndo kujivua gamba uko kuamua kuanika dhamira yao? Ktk hili kama ni kweli bora wasivue gamba, wafunike pale palipoandikwa Zitto Kabwe (CCM), waondoe CCM na wamwombe Samahani Mbunge Zitto ndani ya masaa 24 kabla hasira zangu kupandwa %.

Haraka sana, ZITTO ni wa CHADEMA full stop!
Mmmh!....sasa hii kali,tena kali sana.....au ndiyo maana lilihujumiwa ili lisiingie mitaani leo?
haya mambo ya kujivua gamba....tutasikia mengi sana mwaka huu.
 
acheni upuuzi wenu, nani ambaye hajawahi kuandika taarifa kisha ikaja kuonekana ina mapungufu ya uandishi? kwani ni kompyuta au binadamu anayeyaandika hayo? kuna mhariri, sawa, lakini makosa mengine ni minor sana, kiasi hata mhariri anaweza kupitiwa kuyaona. so bila shaka walitaka kuandima chadema wakaandika ccm, sioni shida kwani zitto si mbunge wa ccm hata kidogo.

sioni mantiki ya kumhusisha zitto na CCM, tusiwe wepesi wa kuweka dhana nyingi zisizo na msingi. zitto kabwe ni mbunge wa chadema , period.

after all zitto yuko active zaidi pengine kuliko hata hao wabunge wengine mnaowaona wako loyal mno kwa chama. tatizo letu watanzania(wapinzani hata ccm) bado tuna uleule mtazamo wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama, kwamba, mwenyekiti yu ndio yupo sahihi na yeyote atakayekuwa na mawazo tofauti basi ni adui, sio mwenzetu, mara anatumiwa, sijui kibaraka n.k tujifunze zaidi demokrasia, kwani demokrasia ni kutoa fursa kwa kila mwenye sifa kugombea nafasi yoyote impasayo na pia kutoa mawazo yake yoyote hata kama yanatofautiana na ya kwako.

Hakuna bahati mbaya hapa. This is a calculated move. And Zitto if not CHADEMA is owed here!
Ni mpango wa kumchafua Zitto na CDM.
 
Jamani kama kuna mtu kaona nakala ya gazeti la Mtanzania la leo, Habari kuu ni kashfa ya bilioni 48 zilizoibuliwa na Zitto Kabwe.

Chakushangaza mwandishi wa habari hiyo anaaandika: Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CCM) ....

Swali ni je,
1. Tokea mwanzo walikua wanamchukulia Zitto kama mbunge wa CCM pengine kwa sababu labda walikua wanamtumia kichinichini? au
2. Ni kwasababu gazeti hili limezoea kuandika habari za kuifagilia CCM sasa leo (baada ya uvuaji wa magamba) wameamua kuziandika habari za upinzani wanasahau wanadhani ni ya ccm (mazoea) au
3. Uhuni wao tuu?

Maswali mazuri sana,inabidi wamuombe radhi kesho ama sivyo watakuwa wana juana
 
Zito ni wa CHADEMA kwa ajili ya CHADEMA, ukimuona sehemu nyingine ujue anatafuta mambo yakusaidia kuokoa jahazi, nimjanja sana, wengine humdhania hivyo wakimuona katka harakati kama hizo, ukimuona yuko na watu wa ccm wala usihofu ila subiri uone baada ya hapo kombola atakalo toa, i trust a man. Umesikia walivyo muonea huruma mwl. CHADEMA Mbeya akasema amekimbilia ccm chama ambacho kaelekea kufa.
Tuko Pamoja Mkuu.
 
Gazeti la Mtanzania mnalijua...lengo ni ku-destabilise chadema at any cost.Hakuna cha kujadili hapo....
 
Hyo ni janja tu wadau ...hawa mtanzania ni kawaida yao kula kwa kupuliza,ni popo maana hata JK mda mwingine ukiona cha moto kupitia gazeti hili hili
 
si ndo kawalipua kwa bilioni48 za ujangili wa watawala,sasa wanamripoti kama mwanaCCM ili kuwanyima msimamo wafuasi wa zitto,sisi tuko makini sana hawatudanganyi hawa na wasidai wamekosea wakati Wana Mhariri anayekula kodi kubwa ya wananchi. Wakae chonjo kwa kashfa iyo kila kosa litatozwa!

Hawawezi kuwa wamekosea hiyo ni makusudi kabisa!! Hiyo itakula kwao tu (CCM), CHADEMA iko imara na makini!
 
.

Ni muda wa kujivua gamba hivyo wameona ni bora wamsaidie Zitto kulivua lol !

.
 
Kusema ni wao wamesema sawa na hilo ni jambo moja, je yeye Zitto kasemaje juu ya hayo madai mazitto sana????????????????
 
Ok mimi sisomagi Mtanzania kwa sababu ya fisadi RA mmiliki mpaka na wahariri na waandishi, litajifia lenyewekwa uwongo wake,Kwanini wasiandike Rostam alivyotaka kunyang'anywa uraia.
Kwa Zitto sijui ? ni lazima awadai wasipofuta neno hilo
 
acheni upuuzi wenu, nani ambaye hajawahi kuandika taarifa kisha ikaja kuonekana ina mapungufu ya uandishi? kwani ni kompyuta au binadamu anayeyaandika hayo? kuna mhariri, sawa, lakini makosa mengine ni minor sana, kiasi hata mhariri anaweza kupitiwa kuyaona. so bila shaka walitaka kuandima chadema wakaandika ccm, sioni shida kwani zitto si mbunge wa ccm hata kidogo.

sioni mantiki ya kumhusisha zitto na CCM, tusiwe wepesi wa kuweka dhana nyingi zisizo na msingi. zitto kabwe ni mbunge wa chadema , period.

after all zitto yuko active zaidi pengine kuliko hata hao wabunge wengine mnaowaona wako loyal mno kwa chama. tatizo letu watanzania(wapinzani hata ccm) bado tuna uleule mtazamo wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama, kwamba, mwenyekiti yu ndio yupo sahihi na yeyote atakayekuwa na mawazo tofauti basi ni adui, sio mwenzetu, mara anatumiwa, sijui kibaraka n.k tujifunze zaidi demokrasia, kwani demokrasia ni kutoa fursa kwa kila mwenye sifa kugombea nafasi yoyote impasayo na pia kutoa mawazo yake yoyote hata kama yanatofautiana na ya kwako.

matambo,ivi umeamua ku speak your mind? Kwani kwenye thread kuna popote umesoma wakimshindanisha Zitto na hao uliosema wako loyal? Ivi kukosea ivo we waona kitu kidogo?ndo nyie mnaoona saini ni ndogo na kutuwekea kwenye mikataba feki. Watu kama wewe hamuitajitiki sana ktk kuleta hoja critical maana kila kitu mwaona kidogo sana. Sikushangai maana nshawahi kumuona mtu kama wewe amewekewa 'female' badala ya 'male' kwenye cheti chake cha kuzaliwa naye anatake simple eti 'walikosea wakati wa kuchapwa',huku ni kutoelewa maana halisi ya maneno,uzito na impact yake. Unauliza eti kwani ni komputa au binadamu anayeandika hayo kwani komputa inaweza kuandika bila ya binadamu kuwepo?cjui unafikiria nini ndugu. Zidumu fikra za m/kiti na iyo analysis ya kutumiwa,kibaraka n.k vinaendanaje?ivi chama gani kwa sasa mwenyekiti anatoa uamuzi peke yake?cdm wana hadi kamati ya wabunge,kamati kuu,wanachama na uongozi wa wazee tofauti na mwenyekiti,sasa zidumu fikra za m/kiti zi wapi?unaongelea siasa za wakati gani ndugu?? Hata ivo ulivo quote si sahihi,inawezekana hata context ya philosophy iliyopingwa huijui,we umesema ..."zidumu fikira 'sahihi' za mwenyekiti" hapa sawa kama ziko 'sahihi' acha zidumu tu ila context tuipingayo ni "zidumu fikra za mwenyekiti" hapa hata kama si sahihi udumishwa,ilo ni tatizo ila kama ziko sahihi zidumishwe tu! Gazeti lenye mhariri halipaswi kuwa kama jarida ,liwe makini ktk kuleta taarifa makini,kama hawajui wanachomaanisha basi ilikuwa vyema kukaa kimya,maana si sheria watutajie ni mbunge wa chama gani kuliko kuuchanganya umma!
 
Ok mimi sisomagi Mtanzania kwa sababu ya fisadi RA mmiliki mpaka na wahariri na waandishi, litajifia lenyewekwa uwongo wake,Kwanini wasiandike Rostam alivyotaka kunyang'anywa uraia.
Kwa Zitto sijui ? ni lazima awadai wasipofuta neno hilo

du mkuu kweli RA umemchoka! Hata ivo si kwamba tunanunua mtanzania ila kwenye govt.institutions wananunua kwa lazima kwa iyo huwa tunajikuta tunayapitia kwa kuwa ndo yaliyo mezani. Ukitaka TanzaniaDaima huwa unazama mfukoni. Ila wazalendo tunayatafuta nje,otherwise usome ya serikali!
 
Nakubaliana na mtoa mada aliyesema si sawa kuharibu kiswahili, tukatae kushabikia upumbavu. Hakuna kiswahili IVI wala ameama na huyu anayetuhadaa kwamba ni kiswahili cha rwanda na burundi ni mchawi, anatupoteza. Hakuna kiswahili cha rwanda wala kenya wala burundi, soma historia ya lugha hii kabla hujaropoka
 
Hiyo si kwa bahati mbaya ndo walipanga hivyo
ni mkakati mpya wa new habar corp baada ya bosi wao kuitwa gamba sasa wanataka kuipaka matope ccm... waacheni wamalizane
 
sio "Ivi" nadhani ni "Hivi" jamani kiswahili hamna anayekimiliki kama Kampuni ya Dowans. Tehe! Tehe! Teheeee!

Kama unaelewa kuwa 'ivi'='hivi' si endelee mbele? maana mada yetu haihusu sarufi ya Kiswahili. Watu wana matatizo yanayotokana na lugha zao za asili lakini pamoja na tatizo hilo tusiwanyime kutoa mawazo yao. Panapokuwa na nafasi ya kurekebisha tufanye hivyo lakini isitufanye kuwa tunahama kwenye mada zingine.
 
Back
Top Bottom