Gazeti la "Kulikoni" lafungiwa miezi mitatu; kutoka Jumatatu?

Nakubaliana na wew kabisa. Wakati wa uchaguzi inatia shaka, je kuna wakati maalum wa kuyafungia? Halafu uchaguzi unaanza lini hadi sasa hivi uwe wakati wa uchaguzi? Kisingizio cha uchaguzi ndio iwe sababu ya uvunjunjaji wa sheria? Mwanahalisi ilikuwa wakati wa uchaguzi? Nadhani hoja iwe kwenye sheria na namna ambavyo hawa jamaa walivyoitwa kujitetea na wengine wakagoma kutoa ushirikiano.

1.
FMEs!

- However: Ni vyema tukajua sheria inasema nini kuhusu sources za habari za magazeti yetu inasema nini? Maana ninakumbuka ile kesi ya TIMEs kule US, ambapo muandishi aliishia jela kwa kukataa kusema source yake, ingawa mwishowe aliishia kuisema na kuachiwa jela, hapa kwa maoni yangu linakuwa ni tatizo la interpretation ya sheria zaidi kuliko siasa.

2.
- FMEs
Tatizo hapa na nitaliweka in a speculation manner linaweza kuwa the timing ya hizi adhabu, katika kuelekea kwenye uchaguzi na hasa baada ya onyo la Rais kule Mwanza kuhusu magazeti yetu, hilo linatia wasi wasi sana na timing hapa.

- Mkuu ungesoma vizuri haya maelezo yangu kwenye hizi two quotes, kwanza kama unavyokubali nimesema hapa kuna tatizo la sheria zaidi kuliko siasa,

- La timing na uchaguzi nimesema ninaliweka katika speculation manner na sio as a fact of the matter, inaonekana hukunielewa, ingawa ukweli hapo juu kwenye qoutes unajisema wenyewe!

Respect.


FMEs!
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya 1976 " ''seditious publication'' ina tafsriwa kuwa "publication having a seditious intention"...... Sheria kinafafanua zaidi kuwa:
''seditious intention'' is an intention- Seditious
(a) to bring into hatred or contempt or to excite disaffection against the lawful authority of the United Republic or the Government thereof; or

(b) to excite any of the inhabitants of the United Republic to attempt to procure the alteration, otherwise than by lawful means, of any other matter in the United Republic as by law established; or
(c) to bring into hatred or contempt or to excite disaffection against the administration of justice in theUnited Republic; or
(d) to raise discontent or disaffection amongst any of the inhabitants of the United Republic; or
(e) to promote feelings of ill-will and hostility between different categories of the population of the United Republic.

(2) An act, speech or publication is not seditious by reason only that it intends-

(a) to show that the government has been misled or mistaken in any of its measures; or
(b) to point out errors or defects in the government or constitution of the United Republic as by law established or in legislation or in the administration of justice with a view to the remedying of such errors or defects; or
(c) to persuade any inhabitants of the United Republic to attempt to procure by lawful mean the alteration of any matter in the United Republic as by law established; or
(d) to point out, with a view to their removal, any matters which are producing, or have a tendency to produce feelings Of ill-will and enmity between different categories of the population of the United Republic.

(3) In determining whether the intention the with which any act was done, any words were spoken or any document was published, was or was not seditious, every person shall be deemed to intend the consequences which would naturally follow from his conduct at the time and in the circumstances in which he so conducted himself-

........Any Person who
(a) does or attempts to do, or makes any preparation to do, or conspires with any person to do, any act with a seditious intention; (b) utters any words with a seditious intention; (c) prints, publishes, sells, offers for sale. distributes or reproduces any seditious publication; (d) imports any seditious publication, unless he has no reason to believe that it is seditious,

shall be guilty of an offence and shall be liable upon conviction for the first offence to a fine...........



Chapisho linalohatarisha usalama na utulivu (seditious story) ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti na aliyehusika anapaswa kuchukuliwa hatua za jinai ikithibitishwa hivyo......

Katika Sheria ya Usalama wa Taifa (National Security Act, 1970) na hata hiyo ya Magazeti, hakuna kifungu chochote kinachompa Waziri Mwenye dhamana ya Magazeti kuchukua hatua kama hii ya kulifungia gazeti pasipo kuwepo kwa ushahidi wa kuthibitisha kosa linalodaiwa kutendwa na wala pasipokuwa na uthibitisho wa maslahi ya umma (public interest) ambayo chapisho husika limeathiri au lililenga kuathiri......Je, huo uvunjifu wa amani au chuki zimetokea huko Jeshini???

Hii ni ajabu na kweli, hivi mbona vyombo vya habari vya nchini nyingine vinaanika hata uwozo wa Geshini??? What kind of "unrest" au uvunjifu wa amani utatokea Jeshini kwa kuanika uozo kuwa mitihani ni udanganyifu?, Kwani Jeshi lina chombo huru cha kusimamia uendeshaji wake kama NECTA kwa Baraza la Mitihani na Vyuo vya Elimu???nani sasa atatufahamisha yanayoendelea huko?? kama kuna uonevu ni wapi wanajeshi watalalamikia???.

Je, kuna chuki gani iliyogengwa au ipo "uvunjjifu upi wa utulivu (Unrest)umetokea au unatarajia kutokea kufautia kutolewa kwa habari hiyo na Gazeti la Kulikoni??? Na Je, kwa hatua ya kulifungia Gazeti, kuna uhakika gani kuwa uvunjifu wa amani hautakuwepo????.

Eti, mbona ya Usalama wa Taifa na pia ya Jeshi la Polisi, na Idara nyingine nyeti za Serikali Kama PCCB yanawekwa wazi na vyombo vya habari na hakuna hizo hoja za "kuleta chuki na uvunjifu wa amani au kushusha hadhi ya tasisi husika??

Kuna umuhimu gani kwa Jeshi la Wananchi (Jeshi letu) kuwa na maafisa Habari, iwapo mapungufu ya kazi za Jeshi hilo hayapaswi kuanikwa kwa hofu ya kulivunjia hadhi???.Ili linamaanisha hata ufisadi Jeshini unalindwa??

Hapa Waziri Mkunjika, am sory,...Mkuchika kama lilivyo jina lake atakuwa amefanya kazi ya "upelelezi, uendesha mashtaka, utoaji ushahidi na baadae uhakimu/ujaji.




 
Hivi hamjajiuliza ni kipi kinaweza kusababisha uasi? kuhusishwa na vitendo vya ufisadi (kama kwenye Meremeta) au habari ya kucheat mitihani?
 
Uamuzi wa Waziri hauhojiwi na mahakama yoyote.
.
Mzee Mwanakijiji, no one is above the law unless uamuzi wa waziri ameutoa kama quesy judicial body. Sheria zetu nyingi tuu ni mbovu mbovu, kama 'preventive detention order' ya rais imewahi kuwa challenged mahamani na ikafumuliwa, leo itakuwa haya maamuzi ya waziri?.

Huo sasa ndio wakati wa Mzee Mengi, to prove that he has the power and the muscle to stand for what he belive is the right, nasi tutamwamini, hata ukufika muda wa private candidates, akisimama, tutakuja nyuma yake.

Akuifyata baada ya kujua JK is behind, na yeye ni mtu wa kujipendekeza na kujikomba komba kwake, then its the begining of his downfall, naikumbuka ile thread kuhusu anguko lake, this might be the begining.
 
.
Mzee Mwanakijiji, no one is above the law unless uamuzi wa waziri ameutoa kama quesy judicial body. Sheria zetu nyingi tuu ni mbovu mbovu, kama 'preventive detention order' ya rais imewahi kuwa challenged mahamani na ikafumuliwa, leo itakuwa haya maamuzi ya waziri?.

Huo sasa ndio wakati wa Mzee Mengi, to prove that he has the power and the muscle to stand for what he belive is the right, nasi tutamwamini, hata ukufika muda wa private candidates, akisimama, tutakuja nyuma yake.

Akuifyata baada ya kujua JK is behind, na yeye ni mtu wa kujipendekeza na kujikomba komba kwake, then its the begining of his downfall, naikumbuka ile thread kuhusu anguko lake, this might be the begining.

Ulisha sema katika thread moja kuwa una beef na Mengi juu ya mademu ( alikutenda or something ukibisha silali leo naitafuta) hivyo inakuwa vigumu sana kukuchukulia positively thread zako unazomzungumzia Mengi!
 
Hivi hamjajiulizi ni kipi kinaweza kusababisha uasi? kuhusishwa na vitendo vya ufisadi (kama kwenye Meremeta) au habari ya kucheat mitihani?


Hapo umemgonga JK kwenye kitosi.

Viongozi wa serikali ya Chama Cha Majambazi wanachekesha sana. Wao baada ya kufuatilia na kuwashughulikia wahalifu wa hiyo story ambayo ni kweli wanawaandama watoa habari.

Hivi Tanzania tulikuwa na ile sheria ya kuwalinda Whistle blowers tangu enzi ya Mikingamo ni silaha ya Umma. Bado ipo au ilifutwa? Kwani Tanzania huwa wanafuta mambo kienyeji enyeji.
 
Ulisha sema katika thread moja kuwa una beef na Mengi juu ya mademu ( alikutenda or something ukibisha silali leo naitafuta) hivyo inakuwa vigumu sana kukuchukulia positively thread zako unazomzungumzia Mengi!
Sijawahi sema nina beef tha Mengi, who I'm I kuwa na beef na wakubwa hawa?. Nilichosema Mengi ninayemfahamu mimi, siye huyu mneyemuona nyinyi, na ni kweli alishawahi nitenda mahali (siyo mambo ya kipuuzi ya mademu), hivyo namfahamu the really man, na naamini is capable of fighting back unless analinda interest zake nyingine. What is Kulikoni anyway? afterall ni 90 Days only zinaisha April 15!.
 
- Mkulu Pasco, just curious unasema kwa jinsi unavyoijua sheria ya magazeti ya mwaka 1976, Mkuchika amekosea sana, vipi ukaiweka hiyo sheria wazi tuione hapa na hii aliyoinukuu ya mwaka 1966, ambayo unasema haihusiki?

- Kama ninakuelewa vizuri, sheria ya mwaka 1976 inaruhusu what Kulikoni did na kuishia kufungiwa na kwamba hiyo sheria ya mwaka 1976 inaweka wazi kwamba walichokifanya Kulikoni sio kuhatarisha usalama, isipokuwa wamewavua nguo JWTZ,

- Very interesting I wish usingejali kuiweka hapa hiyo sheria ninaamini kwamba hii ni fani ya uandishi ni yako na hutajali sana.

Respect.

FMEs!
Mkuu FMES, Yes Mkuchika amekosea, its a matter of interpretation ya sheria, ila nikitulia baada ya kuiona the really argument, nitakuwa kwenye position nzuri ya kulijibu hili.
 
Huyu Mkuchuka ni dbdbdbdbdbd kweli kweli.

.................unfortunately, weakness yake hiyo ndiyo inayompa "kula" sasa sijui tutasemeje tena.

Tutamkumbuka sana Rais Mwinyi kwenye ruksa ya magazeti.
 
Mbona hakuunda tume kama alivyoshauriwa?
Jeshi bana,kuna kundi moja huko jeshini nasikia linaitwa LUSIMBI INTAKE,liliingia humo kwa kashfa mbalimbali na baada ya uchunguzi nasikia LUSIMBI ALIACHISHWA KAZI.
Kashfa ni nyingi na ingekuwa magezeti hayajikombi kwa serikali,yalitakiwa yaandike uozo huo then tuangalie kama yatafungiwa yote?
Maana kuna MEREMETA,KUFUNDISHA DRC KISIRISIRI,MATUMIZI MABAYA YA FEDHA,ETC
 
Invisible, kwa hiyo sasa mkwara unaofikiriwa ni JF siyo?
 
Nchi yetu ina udikteta wa kisiri,hasa ex soldiers ambao ndio viongozi wetu!Katika demokrasia ,free of information is vital.kama gazeti limeeandika habari sio za kweli kuna MAHAKAMA.Mkuchika angekwenda mahakami kuseek injuction ya publication sio
kufungia tu!

Nchi hii inaelekea wapi?
 
jeshini nasikia linaitwa LUSIMBI INTAKE,liliingia humo kwa kashfa mbalimbali na baada ya uchunguzi nasikia LUSIMBI ALIACHISHWA KAZI.
Kashfa ni nyingi na ingekuwa magezeti hayajikombi kwa serikali,yalitakiwa yaandike uozo huo then tuangalie kama yatafungiwa yote?
Maana kuna MEREMETA,KUFUNDISHA DRC KISIRISIRI,MATUMIZI MABAYA YA FEDHA,ETC

who's that Guy Lusimbi???? ni Mkuu wa Geshi lipi la ntchi!
 
lakini Jeshi sini taasisi ya UMMA, kwani kucheat exams imeanza leo ? mimi kuna mwanajeshi namjua aliingia kazini akitumia cheti cha rafiki yake, kwani kuna usalama wa nnchi unatikiswa ukimtaja mwanajeshi anaeiba mitihani, mbona kuna wanajeshi kadhaa wanakamatwa na POLICE kwa kujihusisha na ujambazi, lipi ni kinyaa ni hili la askari wa JWTZ kujihusisha na uhallifu kama ambavyo mara kadhaa imewahi kulipotiwa ama kuiba mitihani.
nafikiri JESHI LINGEUNDA TUME KAMA mUHARIRI ALIVYOSHAURI, then tungejua nani mkweli na nani muongo. otherwise Mkuchika na mtumia nguvu nyingi kuliko uwezo wa kufikiri.
 
Je atalifungia na cheche ya fikra? si walieleza in and out ya meremeta pamoja na kusema ni siri za jeshi? siri za jeshi katika kutuibia? Hivi sasa jeshi linakubali kutumika kutuibia watanzania? haya basi...........
Ujinga tu wa mkuchika lakini message sent!
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 24 (2 members and 22 guests) !!!!!!
Nyie guest karibu jamvini!
 
Back
Top Bottom