Gazeti la habari leo linapotosha umma

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,652
2,627
Leading story ya leo eti wanafunzi vyuo vikuu na maudhui ya kumpongeza JK wakati jana Nape aliwachukua wanafunzi wa chuo cha mapishi cha Datastar na kuwapa buku kumi.hawafiki hata 15..imekaaje?
 
jambo leo ni janga la kitaifa

Kwa sababu hao vijana walikuwa kichama, mbona kikao cha chadema na Sabodo hawajaandikwa na habari leo kama si la chama.

Na iweje Habari Leo na dada yake Jambo Leo waandike habari moja kawa waandishi si wamoja? Police na usalama wa taifa mko wapo na siasa za vyuoni? Mnatia kichefuchefu

Mimi ni mwanachuo ila ni uwongo na siasa chafu wanazifanya CCM sio ile za miaka ile siku izi ukionyesha kuwa wewe ni ccm unaonekana unamatatizo na fisadi
 
Kwani habari leo wanadhani wanafunzi wa chuo ni mambumbu namna hiyo mpaka waandamane kwa kusifu ubadhilifu mkubwa kama huo!? Nadhani hata ukimwambia mwanafunzi wa chekechea hawezi kufanya kitu kama hicho na wasipoacha upumbavu kama huo watakufa na ccm soon
 
Hakuna jipya katika magazeti yote yanayozalishwa TSN, si Daily News, Habari Leo au Spoti leo. Hii yote ni kwa sababu ofisi inaendeshwa kichama badala ya kiuweledi! Umewahi kuona mtendaji mkuu wa kampuni akiwa ana Diploma huku akiongoza watu wengine wenye Masters? Fika TSN utayakuta hayo.
Bahati yao migazeti yao inasambazwa kinguvu kwenye ofisi na idara za serikali otherwise yangetegemea mauzo kwa jamii kitambo yangekwisha baki kuwa historia.
 
Tulizeni mioyo wakuu, CCM inaweweseka. Nyie hamuoni hata baba mwanaasha akiwa konad anachofanya ni kuwakusanya wacheza bao wa mwembe yanga na kuwahutubia badala ya ku-address intellectuals. Sasa tangu leo mjue kuwa Datastar ni chuo kikuu
 
Gazeti bora katika Dunia ni Tanzania Daima.
PAMOJA SANA KAMANDA..........REFER: HABARI YA JK ALIVYOSHUKA KUTOKA BRAZILI Pinda akampa taarifa kamili kuwa mawaziri 8 wanastaili wajiuzulu yeye akakataa AKASEMA NI UPEPO TU UTAPITA, IKULU IKAKANUSHA J2 J3 WATANZANIA TUKASHUHUDIA UKWELI WENYEWE
 
Kama bado unaendelea kusoma magazetiaina ya habarileo, hakika unapotoshwa vya kutosha na unapoteza muda wako bure, soma mwananchi au mwanahalisi na mengine lakini si habari leo na uhuru.
 
HABARI LEO

WANAFUNZI ambao ni wanachama wa
Shirikisho la WanaCCM Vyuo vya Dar es
Salaam, wamempongeza Rais Jakaya
Kikwete kwa nia yake ya kutaka
kuwaondoa madarakani mawaziri
wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu na kupendekeza uamuzi huo uchukuliwe
haraka. Wanafunzi hao jana waliandamana
hadi katika Ofisi Ndogo za CCM, Mtaa
wa Lumumba, Dar es Salaam wakiwa
na mabango mbalimbali, baadhi yao
yakisomeka ‘Wasaidizi wa JK
wajibikeni kabla ya kuwajibishwa,’ ‘ Wezi wasisimamishwe wafukuzwe na
kuchukuliwa hatua’, ‘CCM itadumu’ na
‘Viongozi wala rushwa watatupeleka
kuzimu hatuwataki.’ Mengine yalisomeka ‘JK vunja ukimya,
chukua hatua jenga chama na Taifa
kwa ujumla,’ ‘Takukuru kuweni kama
CAG’, ‘JK kawapa uhuru wa kutosha’
na ‘Nape chukua hatua la sivyo
tuambie lini tuingie wenyewe maofisini.’ Katika ofisi hizo, Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na
Uenezi ya CCM, Nape Nnauye
aliwapokea na kabla ya kuzungumza
nao, walitoa risala yao. Katika risala yao iliyosomwa na
Mwenyekiti wa shirikisho hilo,
Assenga Abubakari, wanafunzi hao
walitoa mwezi mmoja kwa Serikali iwe
imewachukulia hatua mawaziri wote
waliohusika vinginevyo shirikisho hilo litawatoa lenyewe maofisini. Nape awajibu Akijibu risala hiyo, Nape
alisema kitendo cha Rais Kikwete
kuruhusu kujadiliwa kwa uwazi ripoti
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), ndicho
kilichowezesha kuibuliwa na kubainishwa kwa viongozi
wabadhirifu wa fedha za Serikali. Alisema msimamo wa CCM kwa sasa ni
kuisimamia Serikali na kuhakikisha
mawaziri wote na wale wote
watakaobainika kuhusika katika
kashfa ya ubadhirifu wanawajibishwa. Kwa mujibu wa Nape, tayari Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM,
imemshauri Rais Kikwete kuwa
wahusika wote washughulikiwe na
kufikishwa mahakamani. “Kwa hili halina mjadala, naomba
niwahakikishie kuwa waliohusika
wote lazima wawajibike tena kisiasa
kwa kuwa huku hakuna haja ya
ushahidi, ikiwa mtu umetajwa kuwa ni
mwizi lazima tukuweke pembeni,” alisisitiza. Alisema pamoja na hayo NEC pia
imemshauri Rais katika suala la
kusuka upya Baraza la Mawaziri,
lisichukue muda mrefu ili wahusika
wote wakiwamo makatibu wakuu na
watendaji waliohusika katika ubadhirifu uliobainishwa katika ripoti
ya CAG, wanachukuliwa hatua. Nape alisema kitendo cha ripoti za CAG
kujadiliwa bungeni kwa uwazi, kina
baraka ya Rais Kikwete na lengo
likiwa ni kuhakikisha utendaji wa
Serikali unafanyika kwa uwazi tofauti
na zamani ambapo ripoti hizo zilikuwa zikiwasilishwa na kujadiliwa katika
vikao vya ndani pekee. Alisisitiza kuwa mara baada ya suala
hilo kuibuliwa bungeni, wabunge
walitoa mapendekezo yao, Kamati ya
wabunge wa CCM nayo ilitoa
mapendekezo yake ndipo NEC nayo
ilipokutana na kuwasiliana na Rais juu ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya
wahusika wote. “Rais tulipomuuliza alisema wazi kuwa
hadi taarifa hiyo ya CAG ilipofikia ina
baraka zake, napenda niwahakikishie
kuwa CCM ndio iliyosaini mkataba wa
kuongoza nchi kwa miaka mitano,
kamwe haiwezi kunyamazia suala kubwa linalowatafuna wananchi
kama hili,” alisisitiza Nape. Katika Bunge la 10, mkutano wa saba
uliomalizika jijini Dodoma hivi
karibuni, iliibuka hoja nzito
iliyowatupia lawama mawaziri kwa
madai ya kutumia vibaya nyadhifa
zao. Ijumaa iliyopita, Kamati Kuu ya CCM
ilikutana jijini Dar es Salaam chini ya
uenyekiti wa Rais Kikwete na
kukubaliana na hoja ya Rais Kikwete
ya kutaka kufanya mabadiliko katika
Baraza la Mawaziri. Kutokana na hiyo, inatarajiwa kuwa wakati wowote Rais
Kikwete atafanya mabadiliko hayo
ikiwa ni mara ya kwanza tangu
aliposhinda muhula wa pili na wa
mwisho wa uongozi wake, Oktoba 31,
2010. Miongoni mwa mawaziri wanaotajwa
katika kashfa mbalimbali baada ya
kutoka kwa ripoti ya CAG ni Waziri wa
Fedha Mustafa Mkulo, Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda,
Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami na Naibu wake, Lazaro
Nyalandu. Mawaziri wengine
wanaohusishwa na ubadhirifu huo ni
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Profesa Jumanne Maghembe, Waziri
wa Nishati na Madini William Ngeleja, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa George Mkuchika na Waziri
wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige
 
Hii inaonyesha kodi za wananchi kutumika kupotosha umma. Serikali na chama tawala wasitupotezee muda kwa kutumia propaganda ya kuandaa maandamano na kutmia magazeti yao kujisafisha. Haikuwa muda ndefu watu hao hao wakiiambia vyama vya upinzani waache siasa vyuoni wakati kwa chama tawala ni sawa.
Serikali Ndiyo inayokusanya kodi kutekeleza wajibu wake haihitaji opinion ya jamii kuwachukulia hatua mafisadi kwakuwa ni jukumu lake kufanya hivyo. Hii isiwe danganya toto kuwapoza wananchi hasira waliyonayo. Kinachohitajika hapa ni kuchukua hatua siyo bla bla inayoendelea.
 
jaman wanafunzi wa ccm vyuo ni wahuni tu kwan wanaufisadi kama ule wa ccm kwa mfano chuo kikuu DSM yupo waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi huyu jamaa ni mwizi kulikua na student galla huyu jamaa alifisadi pesa nying,kuna kodi ya steshenary hapa chuon huyu jamaa anakula tu wala hajal,mradi wa mashato haka kajmaa kanakula pesa za wanaDARUSO na hukuna wakumchukilia hatua kwani hata upeleke utawala hawez kumsimamia.utawala wenyewe washapigwa changa na huyu bwana.yan vijana wa ccm wanaanza wiz toka wakiwa wadogo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom