Gazeti la Freeman Mbowe latumika kumsafisha LOWASSA

Kwani kuna tofauti gani kati ya mbowe na chadema? Chadema ni mali ya mkwe wake kwahiyo ni mali yake pia na gaazeti pia ni mali yake unauliza kitu gani?

Kwa hiyo tunaweza kusema ccm ni mali ya nyerere? chama kinakuwaje mali ya mtu? fikra za kibaguzi na uchochezi bana, mgando kweli kweli.

hivi kuna chama ambacho hakikuanzishwa na binadamu? kama vyama vyote vilianzishwa na binadamu basi vinaangukia kwenye definition yako kwamba chama ni cha mtu. hivyo, vyama vyote vilivyopo sasa hivi ni vyama vya mtu fulani, including ccm. na kama basi tunataka kinyume chake, basi tuweke utaratibu ambao vyama vitakuwa vinaanzishwa na robot.
 
Informer,

Je wewe ni mwandishi wa gazeti gani? Ni vizuri kulijua gazeti unaloandikia ili tujue kama wewe ni tofauti na hao unao watuhumu.


Huyu jamaa informer ni mwandishi wa magazeti ya ThisDay na Kulikoni. Aidha anaandikia pia gazeti la Raia Mwema na wakati mwingine huandikia MwanaHalisi. Siku zote amekuwa mchimvi na mnafiki. Ni mtu ambaye mnapozungumza kama marafiki huonekana kuwa ni mtu mwema sana na mwenye busara wakati ukweli ni kwamba amejawa chuki na uchimvi wa namna nyingi. Amekuwa informer katika system akiripotia habari za ndani zinazohusu wakubwa wengi ndani ya nchi hii. Nimepata kufanya naye kazi katika chumba kimoja cha habari na ukitukuta pamoja unaweza ukadhani sisi ni marafiki wakubwa. Huyu mtu haoni tabu kabisa kukuzushia jambo lolote na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ameshiriki kikamilifu kuzusha mambo mengi. Chini ya zulia anawasilisha maslahi yasiyo yake bali ya tajiri mmoja ambaye ana hasira na watu wengi wanaokwenda kinyume chake. Ni mtu asiye na rafiki wa kudumu kutokana na tabia yake ya uchimvi. kwa kifupi kwa hulka ni multi dealer kwani ameshavuka daraja la kuwa double dealer.
 
mmmmmhhhh Mbowe natumaini utayafanyia kazi mawazo ya Umma kama kweli unahitaji nguvu ya Umma kuijenga CHADEMA. Huyo Kibanda nae ajiuzulu kama huyo bosi wake asije akatuharibia gazeti letu kwa kupa hicho kinyesi tena kwenye front page.
 
Huyu jamaa informer ni mwandishi wa magazeti ya ThisDay na Kulikoni. Aidha anaandikia pia gazeti la Raia Mwema na wakati mwingine huandikia MwanaHalisi. Siku zote amekuwa mchimvi na mnafiki.
Kibanda je kweli wewe ni mhariri wa magazeti ya Umoja?

Itawapunguzia watu gharama ya kununua magazeti kupata habari za pande mbili a shilingi

Isije ikawa mtu ananunua gazeti X na gazeti Y kusoma pande zote za shilingi kumbe ..................
 
On Waberoya

How could you remember someone in relation to his writing while you could not remember exactly what he wrote. It seems you just remember the title of my opinion 'Naliona Anguko la Zitto' and not the content.

First you must understand that being a journalist and political commentator i'm entitled to write my views on issues of national interest. I warned Zitto not to vie for the position then not because I was against him, but because of the political climate within Chadema then. I insisted and I still insist that it was wrong for Zitto to vie for the position at that time. The wounds of his decision haunts him and Chadema to-date. I thank God that Zitto and Chadema elders saw it then and his decision to pull out his name has enabled that party to grow against all odds.

Unless you do not know Tanzanian politics well. Had it not been Mbowe as a chairman today, Dr. Slaa wouldn't have vied for the presidency in October elections, henceforth the party you seems to hate most wouldn't have been stronger and the champions of the opposition politics as it is now. Watch out your sense of arguments. Next time you need to be more smarter.

Wow! this is Kibanda you never cease to amaze me, I am not smarter like you, for your reasons it is better we urgue that because of the political wind of our country it is better for CCM to stay in power!! this 'political situations mentioning here are imaginations, are never real never existed , DEMOCRACY has no boundary if you dont know-smarter guy!

I didn't hear! you are saying chadema is stronger and champions of the opposition!!! since when you have been singing taarabu nkulumba? ENTERING IN ELECTIONS knowing for sure NEC is part of ccm was right? You mean that having few MP members who can do nothing in that house is being champions , is that what you guys are cheating and teaching yourselves? your message bear lots of things that you guys out there belong to the group of elite people who decide the fate of this country!!! we know you guys we know excatly what you are doing , by your poor views if you think in global scale then, there are times we can compromise democracy because of 'situations' then NEC decided to give JK the position because ''from their views" may be they think is not time for another political party to be in power! Kibanda kibanda, there are things that are very serious that keeping silent is better because no one will ever quote you..ona sasa!!
 
Huyu jamaa informer ni mwandishi wa magazeti ya ThisDay na Kulikoni. Aidha anaandikia pia gazeti la Raia Mwema na wakati mwingine huandikia MwanaHalisi. Siku zote amekuwa mchimvi na mnafiki. Ni mtu ambaye mnapozungumza kama marafiki huonekana kuwa ni mtu mwema sana na mwenye busara wakati ukweli ni kwamba amejawa chuki na uchimvi wa namna nyingi. Amekuwa informer katika system akiripotia habari za ndani zinazohusu wakubwa wengi ndani ya nchi hii. Nimepata kufanya naye kazi katika chumba kimoja cha habari na ukitukuta pamoja unaweza ukadhani sisi ni marafiki wakubwa. Huyu mtu haoni tabu kabisa kukuzushia jambo lolote na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ameshiriki kikamilifu kuzusha mambo mengi. Chini ya zulia anawasilisha maslahi yasiyo yake bali ya tajiri mmoja ambaye ana hasira na watu wengi wanaokwenda kinyume chake. Ni mtu asiye na rafiki wa kudumu kutokana na tabia yake ya uchimvi. kwa kifupi kwa hulka ni multi dealer kwani ameshavuka daraja la kuwa double dealer.

Asante sana mkuu, nafikiri nimekuelewa vizuri. Hiyo kazi yenu ya uandishi wa habari imechafuka mno.
 
Gazeti halijamsafisha ila limetoa upande wake wa habari. Nini maana ya demokrasia? Lowassa ana haki pia ya kusikilizwa. Naskitika mtoa hoja kapotoswa na haelewi nini maana ya gazeti kumsafisha mtu
 
"I didn't hear! you are saying chadema is stronger and champions of the opposition!!! since when you have been singing taarabu nkulumba? ENTERING IN ELECTIONS knowing for sure NEC is part of ccm was right? You mean that having few MP members who can do nothing in that house is being champions , is that what you guys are cheating and teaching yourselves? your message bear lots of things that you guys out there belong to the group of elite people who decide the fate of this country!!! we know you guys we know excatly what you are doing , by your poor viewbecause ''from their views" may be they think is not time for another political party to be in power! Kibanda kibanda, there are things that are very serious that keeping silent is better because no one will ever quote you..ona sasa!!s if you think in global scale then, there are times we can compromise democracy because of 'situations' then NEC decided to give JK the position"



I salute your poor arguments
 
Nilikuwanatazama Channel ten kipindi cha mahojiano nilishangaa jinsi Kibanda alivyokuwa akimponda Sitta kwamba alisababisha anguko la CCM kwa kuruhusu mijadala ya EPA na RICHMOND kujadiliwa mjengoni.Maoni ya Kibanda ni kwamba CCM ilifanya vyema kumtosa kwenye Uspika na haitakuwa rahisi JK kumteua kwenye baraza la mawaziri.

Bahati nzuri au mbaya kwake Sitta kapewa uwaziri sijui atajisikiaje.Mara kadha nilikuwa nalishangaa gazeti la Tanzania Daima lilivyokuwa likijitahidi kuwapiga nyundo wapiganaji Sendeka,Mwakiembe,Kilango na Seleli kuna siku nilimuuliza mwanahabari msimamo wa Tanzania daima alibaki akinicheka.The Informer pengine umechelewa mno kugundua Tanzania Daima ni gazeti linalomilikiwa na Freeman Mbowe kuisaidia CHADEMA lakini wakati huo huo kuwajenga mafisadi walioko ndani ya CCM.Unaweza kujiuliza kulikoni mwenye majibu yasiyo na ukakasi ni Mbowe mwenyewe.


Nakubaliana na wewe kwa 1oo%. Kwa takribani kama miaka miwili sasa hali ya Kibanda imebadilika sana . Kibanda wa sasa si yule wa zamani, ni wazi anatumika.
 
Nakubaliana na wewe kwa 1oo%. Kwa takribani kama miaka miwili sasa hali ya Kibanda imebadilika sana . Kibanda wa sasa si yule wa zamani, ni wazi anatumika.


Ni kweli kabisa kwamba, mimi si Kibanda wa zamani. Kwa nini? Kwa sababu nimejifunza mengi. Nimezijua vyema siasa za kutumia akili na kutumikishwa kiakili. Kibanda wa zamani ni yule aliyekuwa akikichambua kitabu kwa cover lake la juu. Ni yule ambaye alisimama kupigania mambo ambayo alikuwa haujui undani wake.

Kibanda wa leo anaujua undani wa vita ya ufisadi inayopiganwa ndani ya CCM. Ni yule anayejua kwamba ufisadi ni zao la kimfumo ndani ya CCM na kwamba vita hiyo inahusisha wanasiasa wanaogombea mkate wa madaraka (urais) ambao wameliingiza taifa zima katika mapambano yao kwa kisingizio cha uzalendo. Kibanda wa leo ni yule anayetambua vyema namna idara ya usalama wa taifa inavyoshiriki kikamilifu kumlinda mkuu wa kaya yetu kwa gharama za kuwachafua wengine hata kwa makosa ambayo kimsingi yamefanywa na yeye.

Kibanda wa leo ni yule anayepigania mabadiliko ya kweli na yasiyo bandia. Ni kwa sababu hiyo basi Kibanda wa leo hawezi kamwe kuzikubalia propaganda za makamanda wa ufisadi ambao wenyewe ni mafisadi na mawakala wa wafanyabiashara wanaowalipa fedha kuwatukana wengine.

Kibanda wa leo ni yule ambaye amekubali kuitwa majina yote mabaya, mnafiki, msaliti, wakala na mengine yote kwa sababu tu ya kusimamia kile anachokiamini na kukitetea. Naamini kwa dhati kwamba ndani ya CCM hakuna kiongozi wa kitaifa mwenye ubavu wa kumnyoshea mwingine kidole, kwani historia imethibitisha kwamba wote wanapikwa katika chungu kimoja. Tujiulize ni kwa nini Slaa alimuita Sitta fisadi wakati wa kampeni! Je Slaa naye alikuwa amenunuliwa? Tujiulize ni kwa nini Sitta aliizima hoja ya Richmond bungeni? Alikuwa amenunuliwa na nani? Tujifunze kufikiri badala ya kuwa mabingwa wa kushangilia hata mambo ya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom