Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 579
Mungu atunusuru na hili na lingine lijalo. Kuna siri nzito sana inakuja
Uko sahihi Mkuu Kiranja, hili ni janga la kitaifa. Naomba ninukuu mjadala mmoja sitotaja wapi na nani alisema maneno haya, aalisema yafuatayo;
"Gazeti la Tanzania Daima lilianzishwa na Freeman Mbowe kwa jina la mkewe Dk.Lilian Mbowe, na mwandishi mwanzilishi kwa maana ya mipango na mikakati alikua Deodutus Balile akiwa na wenzake Jacton Manyerere na Mbaraka Islam na wengineo wakajiunga nao. Balile alitumia uzoefu wake wa kuanzisha gazeti la Mwananchi (kabla halijanunuliwa na Nation) na walipanga timu na mikakati yote ikiwa ni pamoja na kuita waandishi wengine kama vile Erick Anthony, Joseph Senga na wengineo kujiunga nao japo Islam aliwatosa na kwenda kushirikiana na wengine kuanzisha Thisday.
"Wakati wa kuanzishwa kwa Tanzania Daima ilikua kipindi cha mchakato kuelekea 2005 ambako aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, hakuwa akimtaka Jakaya Kikwete na Edward Lowassa, na hivyo JK na Lowassa walianza kufanya mazungumzo na Mbowe kuangalia uwezekano wa kujiunga na Chadema ikiwa watatoswa na CCM.(Nitajadili siku nyingine). Mazungumzo hayo yaliratibiwa vyema na Rostam Aziz na Lowassa japo Mbowe aliona Lowassa anafaa zaidi kuwa Rais kuliko JK. Kwa msingi huo upo uwezekano mkubwa kwa Tanzania Daima kupata msaada kutoka kwa kina Lowassa maana lilianzishwa kwa mtaji mkubwa na lilitumika hata wakati wa mchakato 2005. Kwa ujumla pamoja na yote, bado Mbowe binafsi ana siri nzito na Lowassa na pengine ndio maana Kibanda ana jeuri ya kufanya hayo bila kuguswa na wamiliki. Hata Balile aliondoka lakini akapokewa Mtanzania aliko hadi sasa na iko siku histroria itaanikwa. Hata suala la Fredrick Sumaye kuzungumza na Chadema lilipoibuika, JK aliambiwa hakuna dhambi maana hata yeye 2005 alizungumza na Chadema."
Naomba kuwasilisha mengine nitayaleta wakati mwafaka na baadhi ya waliotajwa ni member wa JF wataongezea nyama nyama.