"GAZETI LA CHAMA" Chama kipi nyie watangazaji?

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Leo asubuhi nikiwa nasikiliza mapitio ya magazeti kwenye Radio Magi FM nimesikia kwa mara nyingine tena mtangazaji akisema kwa kujiamini "Sasa nimeshika gazeti xyz "GAZETI LA CHAMA"Kwa kuwa mimi ni wa kizazi cha enzi hizo za chama kimoja nimeelewa mtangazaji alimaanisha nini anapozungumzia juu ya "CHAMA". je aliyezaliwa baada ya kuanzishwa kwa vyama vingi hapa aeleweje? Na cha ajabu ni vyombo vingi vya habari hurudia kauli hii Gazeti la CHAMA.. Wana JF mlio karibu na hawo watangazaji jaribu kuwaelimisha.
 
Tatizo watz wengi magamba yalishayaota mpaka kwenye ubongo, kiasi cha kutojitambua kwamba tayari tuna vyama vingi. Wao wanajua chama ni kimoja tu cha magamba.
 
unashangaa gazeti la 'chama' kwani hulijui, si hili gazeti la Uhuru
 
Kama nimekuelewa vema mshangao wako ni kusema "Gazeti la Chama" badala ya "gazeti la chama cha......" na hii ikiashiria kuwa bado kuna mgando wa mawazo wa Chama kimoja na hivyo huhitaji ku-identify jina la chama kwa kuwa kipo kimoja.

Lakini swali ni moja, je CDM wana gazeti? Vipi kuhusu CUF? kama hawana basi itakuwa rahisi kwa maana chama pekee chenye gazeti ni kimoja
 
Umeuliza swali la aina hiyo kwa kuwa unaishi Tanzania na unajua kuwa Chadema CUF nk hawana magazeti. Je akawa mgeni kutoka nchi jirani au kwingineko anayezungumza kiswahili na akasikia mtangazaji wa Magic Fm akisema "sasa nimeshika gazeti la CHAMA" huzani rwamba atanza kujiuliza CHAMA GANI HICHO?
 
Wawe wanasema nimeshika gazeti la chama cha mapinduzi (Gazeti la uhuru).
 
Back
Top Bottom