FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,192
Chadema inaelimisha na inafundisha hakuna ubishi itajizolea wanachama wengi tu!
Inafundisha nini zaidi ya majungu na ufataani?
Chadema inaelimisha na inafundisha hakuna ubishi itajizolea wanachama wengi tu!
tatizo ni kuwa pinda amesema kuwa pamoja na mgao uchumi unakuwa,sasa huyu gavana na pinda nani mkweli?
* Taifa lapoteza sh. trilioni 1 kwa mwezi
Si nyinyi ndio mlipinga hii mitambo ya Dowans isinunuliwe?
* Hofu yatanda maelfu ya vijana kukosa ajira
Wasiokuwa na ajira ndio watapata ajira serikali hii ikiondoka? Ajira alizoahidi ni million moja, mpaka sasa kisha towa zaidi ya hizo.
* Ukali wa maisha wawaacha Watanzania hoi
Hoi kuliko wakati wa Nyerere? Hata viwembe vya kunyolea ilikuwa havipatikani! Ukikogea Lux, harufu tuu, unaonekana wa maana? Wakati upi hoi zaidi?
* Serikali yang'ang'ania mchezo wa Dowans
Mchezo upi wa Dowans? Jee, Dowans wanakosa lipi? Na inawahusu nini siasa yenu?
Kwa nini mnaingiza matatizo ya umeme kwenye siasa? Kwani matatizo ya umeme yalianza kwa JK?
Mlianza na kutomtambuwa Rais, mkaona hapa pagumu!
Mkaja na Katiba, mkanuyamazishwa kiulaini.
Mnakuja na Dowans, kaja mwenye Dowans bado hamtaki. Na majuha wanawasikiliza.
Gavana kasema kweli, na hawa wanafik wa Chadema ndio opportunity wanayotumia ya kuwarubuni (brainwash) hawa vijana wasio na kazi maalum. Wanawadanganya kuwa Serikali iliyopo madarakani ikiondoka leo, kesho nyie wote mna kazi tena za kuwaongoza hawa tunaowatoa madarakani. Duhh, uongo mtupu!
Ndio wanagutuka??? What do you expect if 60% of youth in urban areas are unemployed (Wizara ya kazi statistics, 2006)???
Gavana alisema kuwa ingawa lengo la serikali ni kwa uchumi kukua kwa asilimia 7.1 mwaka huu, kuna uwezekano kuwa lengo hilo lisifikiwe kutokana na hofu ya ukame na kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia.
SASA HIVI VISINGIZIO VIMEKUWA VINGI LAKINI KWA KWELI HAKUNA UBISHI UCHUMI UNAYUMBA
Wacha vijana waingia kwenye maandamano 5 years ago I was a lone voice nikiwapiga vita wageni kupendelewa na kuchukua kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania hivi sasa sioni ajabu kwa nini wanagutuka. Wamechelewa wanavuta shuka wakati jogoo amewika khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeee na bado hilo jinamizi la EAC likiingia vizuri ndio watajua zipi ni mbivu.
"Vijana wengi maeneo ya mijini na kwenye vyuo vikuu wanaichukia sana CCM na serikali kutokana na hali ngumu ya uchumi na ukosefu wa ajira. Ndiyo maana wapinzani wameonekana kuwa na nguvu kwenye miji mikubwa hapa nchini," alisema kada mmoja wa CCM.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa ufisadi serikalini, ukosefu wa ajira na ukali wa maisha vimechangia kwa kiasi kikubwa kukisaidia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujizolea umaarufu miongoni mwa Watanzania, wengi wao wakiwa ni vijana.
(Source: KULIKONI Toleo la Machi 4, 2011)