Gaucho amsuta Dunga...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Magoli mawili ya kiungo mshereheshaji anayeaminika kucheza kandanda toka Mbinguni na pia inaaminika kuwa awapo uwanjani basi shughuli zote huko mbinguni husimama Ronaldo De Assis Moreirra al maaruf kama Ronaldinho Dinho the Saint ama Dinho Gaucho yameisaidia klabu yenye mafanikio zaidi duniani yaani Assozionale di Calcio Milan kuibuka na ushindi wa magoli matatu dhidi ya wajukuu wa bibi Laverchia Signora yaani Juventus.

Katika mechi hiyo ya mwisho ktk msimu huu wa ligi ya serie A tulishuhudia timu ya juve ikikubali kulambwa goli 3-0 dhidi ya AC Milan katika uwanja wa Sansiro Meazza hapa Milan.

Goli la kwanza la Milan liliwekwa kimiani na Beki chipukizi Luka Antonini kabla ya mtakatifu Gaucho kuja kumalizia magoli mawili ambayo ni mpasho na msuto kwa Kocha wa Brazil Dungayembe ambaye amejichumia dhambi kwa kuacha kumjumuisha mtakatifu ktk kikosi kinachotaraji kuja Bondeni hivi karibuni.

katika mechi hiyo saint Gaucho aliitumia kwa kuisaidia Milan kupata ushindi na kutambuliza aina mpya ya chenga na skills ambazo hazijapata kuonekana hapa duniani.

Pia Katika mechi hiyo Milan pia walimuaga rasmi kocha wao Leonaldo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takriban miaka 13 akiwa kama mchezaji, kiongozi na kocha.

Kwa niaba ya washabiki wa AC Milan waliopo ktk nchi hii iliyojaa ufisadi na kuogopana napenda kumshukuru Leo kwa yoote mema aliyotutendea, na kama kutakuwa na mapungufu basi tunamwomba atusamehe, kwani yoote yalitokea ktk hali ya ubinaadamu.

Forza Milan.
Sempre Dinho.
 
Ningependa sana huyu awemo kwenye timu ya Brazil ili dunia iweze kuona kipaji chake kikubwa alichokuwa nacho cha kutandaza kandanda.
 
Kama mbingu zinasikia kilio chenu basi risevu Dinho ataitwa punde mmoja wa wachezaji 23 wa kikosi cha kwanza atakapojitoa!
 
kufuru hizi hazifai, eti awapouwajani shughuli zinasimama mbinguni kwa yeye nani? upuzi huu.
 
Magoli mawili ya kiungo mshereheshaji anayeaminika kucheza kandanda toka Mbinguni na pia inaaminika kuwa awapo uwanjani basi shughuli zote huko mbinguni husimama Ronaldo De Assis Moreirra al maaruf kama Ronaldinho Dinho the Saint ama Dinho Gaucho yameisaidia klabu yenye mafanikio zaidi duniani yaani Assozionale di Calcio Milan kuibuka na ushindi wa magoli matatu dhidi ya wajukuu wa bibi Laverchia Signora yaani Juventus.

Katika mechi hiyo ya mwisho ktk msimu huu wa ligi ya serie A tulishuhudia timu ya juve ikikubali kulambwa goli 3-0 dhidi ya AC Milan katika uwanja wa Sansiro Meazza hapa Milan.

Goli la kwanza la Milan liliwekwa kimiani na Beki chipukizi Luka Antonini kabla ya mtakatifu Gaucho kuja kumalizia magoli mawili ambayo ni mpasho na msuto kwa Kocha wa Brazil Dungayembe ambaye amejichumia dhambi kwa kuacha kumjumuisha mtakatifu ktk kikosi kinachotaraji kuja Bondeni hivi karibuni.

katika mechi hiyo saint Gaucho aliitumia kwa kuisaidia Milan kupata ushindi na kutambuliza aina mpya ya chenga na skills ambazo hazijapata kuonekana hapa duniani.

Pia Katika mechi hiyo Milan pia walimuaga rasmi kocha wao Leonaldo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takriban miaka 13 akiwa kama mchezaji, kiongozi na kocha.

Kwa niaba ya washabiki wa AC Milan waliopo ktk nchi hii iliyojaa ufisadi na kuogopana napenda kumshukuru Leo kwa yoote mema aliyotutendea, na kama kutakuwa na mapungufu basi tunamwomba atusamehe, kwani yoote yalitokea ktk hali ya ubinaadamu.

Forza Milan.
Sempre Dinho.

huu ni ukosefu wa akili, hauwezi kukufuru kuwa shughuli zinasimama mbinguni. haufai, unatumiwa na shetani, mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, mpe yeye sifa zote, epuka kitu chochote kitakachomshushia Mungu hadhi....Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu, hapendi mtu achukue utukufu wake wowote ule, mtu anayefanya hivyo huwa ana face death on the spot. kumbuka mfalme herode alipokuwa anahutubia watu ktk kitabu cha matendo ya mitume, watu walipiga kelele wakisema "hiyo ni sauti ya mungu", pale pale Mungu alimtuma malaika wake akampiga kwa chango akafa pale pale. kuna mifano ya watu wengi wanaoiba utukufu wa Mungu, na Mungu hawaachi. wewe una bahati, ni neema ya Mungu kuwa bado upo, Mungu anakupenda sana, anataka ubadilishe njia zako mbaya...umrudie yeye naye atakusamehe dhambi zako zote. kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi ndivyo atakavyoziweka dhambi zako zote kama ukimwendea kwa kumaanisha.

mpira tu ukufanye umkufuru Mungu na mbingu yote, mpira ni nini ndugu yangu, mpira unakusaidia nini na utakupeleka wapi, umepata nini hadi ulivyoanza kuushabikia hadi leo, hamna lolote...na ndo uutukuze mpira kiasi hicho? Mungu akusamehe na akusaidie. UTUKUFU NA HESHIMA NI ZAKE MUNGU aliyeumba mbingu na nchi, uweza wake haupimiki, nguvu zake ni za milele, nguvu zake hazishindwi wala kusimamishwa na kitu chochote, mamlake yake yadumu vizazi vyote, yeye ana huruma na neema, fadhili zake ni za milele, na uaminifu wake wadumu vizazi vyote. anastahili sifa, utukufu, ukuuu, mamlaka milele na milele. Haleluya to the Lamb of God forever and ever more!
 
mkuu gang chomba beef ya dunga na ronaldinho imeanza zamani sana.ronaldhino alimzalilishe Dunga akiwa bwana mdogo sana.

hii ndio sababu kubwa ya ugomvi wao.
 
Last edited by a moderator:

Wewe unakurupuka kama mwanariadha wa mita mia.
hebu Onyesha mahali nilipomtaja Mungu...
Kisha kwa taarifa yako wewe unayependa kukurupuka ukae ukijuwa kuwa maandiko yanasema Mungu yuko mahali kote.
Sasa wewe unayejitia kumjua sana ukae na kulijuwa hili.
 
mkuu gang chomba beef ya dunga na ronaldinho imeanza zamani sana.ronaldhino alimzalilishe Dunga akiwa bwana mdogo sana.

hii ndio sababu kubwa ya ugomvi wao.

Hapo mkuu Wenger umenena vema.
Hebu nijuze je ni bifu gani linalotokota kwa wabrazil hawa?
 
Last edited by a moderator:
mkuu gang chomba beef ya dunga na ronaldinho imeanza zamani sana.ronaldhino alimzalilishe Dunga akiwa bwana mdogo sana.

hii ndio sababu kubwa ya ugomvi wao.

Duuuhhhhh! Kijana mkali!!! Mwache aende zake alimuaibisha sana jamaa, lakini pamoja na kuabishwa kwake bado Dunga angestahili kumuweka kijana huyu kwenye timu ya Taifa ili kuongeza nguvu zaidi katika safu ya washambualiaji.
 
Last edited by a moderator:
Hapo mkuu Wenger umenena vema.
Hebu nijuze je ni bifu gani linalotokota kwa wabrazil hawa?
bifu lilianzia kwenye manjonjo hayo ya ronaldinho kanzu hizo Dunga akahisi kwamba Dinho anamfanyia maksudi na kwanini mtoto mdogo anamuaibisha kiasi kile.Dunga alimwambia Dinho amuombe msamaha jamaa akakataa.basi toka hapo ndio bifu kubwa.
 
Wakati huo Dungayembe alikuwa anacheza au alikuwa ni kocha?
 
Mbingu zinaingiaje hapa? Nimejaribu kufikiri nikashindwa kupata uhusiano!
 
Sina haja ya kuangalia hilo kombe la dunia kama gaucho hayupo kwanza tbc washafanya biashara ya kuuza ving'amuzi
 
Ronaldinho shrugs off Dunga's roster
Sun, 16 May 2010 06:09:35 GMT

fazeli20100516060909747.jpg

Brazilian midfielder Ronaldinho

Brazilian midfielder Ronaldinho has insisted that he was not bitter at being overlooked by Brazil's manager Carlos Dunga for the 2010 World Cup in South Africa.

"My response was here on the pitch, but if he (Dunga) doesn't pick me for the national team it's his choice and I respect that," Ronaldinho said on Saturday.

The FIFA World Player of the Year in 2004 and 2005 further pointed out that he was unwilling to compare himself with his other team-mates.

"I've done many good things this season and I don't want to compare myself to others to see if I've done much more or much less."

Ronaldinho shrugs off Dunga's roster
 
Hivi Dunga haelewi kuwa anaua morali ya wachezaji wake aliowachagua? Au hajui kuwa wachezaji hao ni mashabiki na wafuasi wa Ronaldinho? Yaani haoni kuwa watakuwa hawajiamini kila wanapokumbuka kuwa hawastahili kuwepo katika timu hiyo ilhali Dinho aliye fiti 100% hayupo?
 
Huyu jamaaa anakipaji cha aina yake! Ile kanzu enzi zangu ningelamba red card
 
Mi nawaamini Brazil. Kule kuna vipaji sio vya kubembelezana. Kama mtakumbuka kile kikosi cha Brazil wakati wa Confederation Cup, kuna watoto wabaya kutoka Santos na Collithians si wa mchezo.

Mbona Romario alishawahi kuachwa timu ya Taifa na wakachukua ubingwa!!!!!?????
 
Back
Top Bottom