Gas ni ya watanzania si mtwara

Acha kuropoka.., tembelea KILIMANJARO, ARUSHA & MANYARA halafu nenda LINDI, MTWARA & RUVUMA.
Utapata sababu ya madai yao
 
Where is the Logic?, Gas ipatikane Mtwara ipelekwe Dar then umeme ukishazalishwa upelekwe mikoa ya kusini (MTWARA)
Dah!
 
Kwahiyo wana mtwara msituletee ukabila na ukanda . je na dar nao wakisema bandari ni ya dar itakuwaje. kama hujaridhika ruksa kuhamia mkoa wowote uupendao
Wana bandari yao mkuu, hujawahi sikia bandari ya mtwara?
 
Kwani wamekatazwa kuhamia mikoa mingine? Mbona wachaga wamesambaa
 
Hivi Wana Mtwara mnadanganywa na nani.Kwani hiyo gesi ikija dar mnafikiri haitawafaidisha?Mbona kuna watu wa Mtwara wengi tu hapa mjini.Acheni kudanganywa na wanasiasa uchwara
 
du watu mmempa za uso mtoa mada,nadhan kuna aja ya kujua madai yao kwanza,kabla ya kukurupuka
 
Kwahiyo wana mtwara msituletee ukabila na ukanda . je na dar nao wakisema bandari ni ya dar itakuwaje. kama hujaridhika ruksa kuhamia mkoa wowote uupendao

Jamani msiwafanye watu wa Mtwara ni wajinga wasiojua hata haki yao. Hivi hujui kama Dar wanafaidika sana na bandari kuliko mkoa wowote? Kikufaacho mtu chake. Hukumbuki hata Baba wa Taifa Julius Nyerere alivyowaunga mkono Biafra yenye utairi mkubwa wa mafuta nchini Nigeria walipotaka kujitenga? Tanzania wote tuliwaunga mkono na tukauchangishwa pesa iliipelekwe kama msaada katika vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe vya kutaka kujtenga. Kwa nini iwe mwao kwa Mtwara? Msimamo wenu uwe thabiti na msiyumbishwe. Kama kila rasilmai ni za watanzania wote, mbona mkoa wenu uko nyuma kimaendeleo kuliko mikoa mingine? Wanataka muendelee na kuteseka na maisha ya dhiki na umasikini wa kupindukia ili wanufaike wengine. KATAENI TENA MKATAE SANA:eek:hwell:
 
Kwahiyo wana mtwara msituletee ukabila na ukanda . je na dar nao wakisema bandari ni ya dar itakuwaje. kama hujaridhika ruksa kuhamia mkoa wowote uupendao

Hatusemi kuwa wanamtwara hawataki gesi iendi mikoa mingine tunachotaka kuona ni kwamba mchakato wa kuchakata gasi uanzie mtwara halafu mbwembwe zingine ziendelee hadi dar jamani kuna tatizo gani kujenga kiwanda cha kuchakata mtwara halafu umeme ukatoka hapo na kugawanywa maeneo mengine hivi ni lazima ukaanzie dar. haiwezekani kaweka kwenye grid ya Taifa umeme uliotengenezwa mtwara kwani wa mtela umeruka mtela ukaenda dar kisha kurudi mtela. tuache siasa swali hili ni laisi ila mnakomplikati majibu. Mtwara ianze dar ifuate kupata umeme na vinginevyo vitokanavyo na gesi katiba ndo inavyosema.
 
Kichwa cha habari ni 'gesi kwenda dar' hiyo ndiyo inaleta mfarakano. mbona hamuangalii jambo hili kwa kina? na kulizungumzia kiutaalamu? sio wana JF tu hata viongozi wa serikali. mfano kiongizi anasema "gesi lazima iende Dar". hayo sio maneno ya kitaalam. gesi ina matumizi mbalimbali hivyo huenda kiasi fulani cha gesi kinapaswa kwenda Dar n aikiwezekanakiasi kingine kufanyiwa kazi Mtwara basi ifanyike hivyo.
Kwaheri!
 
Wewe una akili ya kushikiwa. Kwa hiyo Mtwara siyo sehemu ya Tanzania? Basi tuambieni siye ni raia wa nchi ipi? Au kwa akili yako hiyo ya kushikiwa,Dar es salaam ndiyo Tanzania?
 
Hivi Wana Mtwara mnadanganywa na nani.Kwani hiyo gesi ikija dar mnafikiri haitawafaidisha?Mbona kuna watu wa Mtwara wengi tu hapa mjini.Acheni kudanganywa na wanasiasa uchwara

Hatudanganywi na yeyote bali tunajitambua na hakuna wanasiasa wanaohusika katika hili.
 
Mtwara bongo lala mnataka gesi ya kuwashia vibatali
Mtwara wanatumia 1% ya gas inayozalishwa wanataka wanataka wajengewe mtambo
Prof anaweza jipiga risasi
Korosho imewashinda mnataka gas ndio mko karibu na ardhi kama yule jamaa aliwahi kuwa president
 
Ni kweli kabisa ila ingawa bila kufahamu tunatetea ukweli wa kuwa Dar ni Tanzania kuliko Kigoma, Mtwara na hata Dodoma ambayo ilitangazwa kuwa makao makuu miaka lukuki nyinyi pro Dar mmeyakalia. Tungebadili mawazo na kuiona Dar kuwa sehemu ya Tanzania sawa naa sehemu zingine tungekuwa na maendekeo yanayopunguza mrundikano wa watu Dar bila sababu. Fahamu kinachoendelea huku Mtwara ni kuwa kwa kupatikana kwa gesi bei ya viwanja ilikuwa imeshapanda kwa vile watu wengi walikuwa wanakuja kuwekeza lakini sasa kumezima ghafla ina maana kwa Tangazo hilo Dar itegemee ongezeko la watu ambayo linaleta maana kwa Pro Dar lakini halina maana kiuchumi. Ila kwa vile kwa vle tunaendeleza mawazo mafu ya kuabudu tuendelee hivyo hivyo
 
Wanamtwara wanatambua hilo na ndiyo maana walikubali yafuatayo:
Kuichagua ccm miaka yote pamoja na kung'olewa reli huko, kuhamishwa baadhi ya miundombinu kupelekwa maeneo mengine ya tanzania.
Mikoa ya kusini kuwahifadhi wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa afrika na kuzua wasiwasi kwa serikari ya wakati ule kuwekeza mikoa hiyo.
Bandari yenye kina cha asili kudharauliwa.
Wakati umefika rasimali za nchi zinufaishe wananchi wote na si waliopo dar. Tu, ndiyo maana jiji hilo kutokana uhamiaji wa wananchi kutoka mikoani kuendelea kwa kasi kubwa serikali imeshindwa kuwa na miundombinu kukabili hali hiyo. Wakati umefika viwanda vingi vijengwe mikoani waliko watanzania wengi. Haiwezekani watanzania wote tujekuishi dar.

We mtu hata ukija Mtwara ubunge unapata achana na hawa jamaa ambao kila kitu Dar hata kungekuwa na njia nyingine watanzania wote wangefaidika. Gesi nyingine ikipatikana Temeke tutapeleka wapi
 
Kwahiyo wana mtwara msituletee ukabila na ukanda . je na dar nao wakisema bandari ni ya dar itakuwaje. kama hujaridhika ruksa kuhamia mkoa wowote uupendao

View attachment 78385
pata maneno ya leo ya wana mtwara bado wamekomaa! hapa soko kuu mtwara kwenye mkutano leo tarehe 5-01-2013
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom