Gari yenye cc 660 na safari ndefu za kutoka dar kwenda mikoani

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
456
Je gari zenye cc 660 (mfano: Mitsubishi pajero mini, suzuki kei, suzuki carry, suzuki alto, suzuki jimny, daihatsu mira, daihatsu miragino) zinaweza tembea safari ya kilomita 500-1000 kwa siku moja? Zinaweza kupanda milima au zinachemsha njiani?
 
Hazina shida kabisa mkuu - kuchemsha haingiliani na safari ndefu ni matatizo ya kawaida ambayo kila gari linaweza kupata. Ila usikanyage sana - ingini ndogo zinanguruma sana kwenye mwendo wa kasi!! Taratibu taratibu utafika
 
hata mm ndio naitumia suzuki jimmy cc543 mwaka sijaona tatizo, na pana jamaa hapa kariakoo ana Daihtsu kid 660cc anadai mara kadhaa anaenda nayo Arusha toka Dar bila shida kabisa,

Je yako ni ipi ? ningependa kujua matumizi ya mafuta, yangu mjini km 13.5 /lita nje 14.5/lt wewe unatumiaje kwani kwenye vitabu na internet wanadai hadi km 18/lt inawezekana ? ? ?
 
Zinafaa kwa safari ila si kwa mwendo mkali, pia isiwe njia ya vumbi yenye milima.
 
Unajua ikishafika kwa Main road accelerator unanyunyizia tu, yaani haukanyagi ile kwa nguvu mpaka RPM inafika mwisho, hapana.
We piga juu juu tu!!
 
Aaaah unaenda nayo vizuri tu ukiiandaa kwa safari(Service); mie nna swahiba wangu anayo Suzuki ile kama ki hiace ipo kama boflo hivi anapiga nacho Arusha wakati wowote akitaka na mwendo ni wa hatari (anacheza Speed ni 120 kwa 140) hadi anatamani kukopa.
Hanyanyasiki barabarani naye anawachapa raba kama yupo na VX vile.
Na hivi sasa yupo nako Singida huko kwao.
 
Iga Ufe!!
 
Hahahahahahah. thanx for makin me laugh loud and all ma stresses are released nw
 
Yangu mi 20.5cc napiga ruvuma{mbinga} hadi mwanza{magu} we chomoka nayo tu 120
 
Acha woga wewe, kifo kipo tu ikitokea ndo siku tarajiwa itakua ishafika"

Baadhi ya vijana wa siku hizi siwaelewi!! "Wanaweka maisha rehani kirahisi tu" ukimuuliza aliyetengeneza hizo gari haku-design kwa shurba kama hizo na ndio maana leo hii taifa letu linaongoza kwa ajali za barabarani katika ukanda huu, hii ni aibu.
 
Wasi wasi wako tu lkn hata mie napenda sana kuishi lkn kwa safari ndefu ukikuta sehem imenyooka uzuri speed 120/130 ni ya kawaida tu kufikika!!
 
Nawashukuruni nyote kwa michango yenu. Nimejifunza kwa nikiwa na gari ndogo hasa cc chin ya 1000, niasafiri mwendo wa kawaida walau 80km/hr, service ni muhimu kabla ya safari. Pia nimegundua gari yoyote inaweza safiri umbali wowote ili muradi barabara ni nzuri. Asanten sana wakuu wangu
 
Back
Top Bottom