Gari Moshi (Train) zaanza safari jijini Dar es Salaam!

Status
Not open for further replies.
mbona hii picha iko tangu jana ? Si hii ilikuwa ni ya majaribio ya tazara?
 
Natoa angalizo kwa madereva wa Daladala, Bajaji, Boda Boda, kuweni makini tabia zenu za kuchomekea zitakula kwenu, treni ni hatari mkileta mbwebwe zenu.

Angalizo muafaka kwa wakati muafaka. Lakin ni vyema pia tukazikumbusha Mamlaka zinazohusika kurudisha vizuizi kwenye makutano ya reli na barabara
 
Mkuu, unanikumbusha hadithi ya mtoto aliyeambiwa achore picha ya treni akampa mwalimu wake karatasi nyeupe, alipoulizwa mbona hujachora kitu akasema naona mmechelewa kuiona, hiyo treni imeshaondoka na kuanza safari!

Na wewe mkuu naona kwenye picha yako treni haipo tena, imeshaondoka!
 
Hongera Dkt Mwakyembe. Kwa hali yeyote ile kila mmoja wetu amuunge mkono kwani kero ya usafiri Dar imekuwa tishio la kweli kwa uchumi wa nchi. Tunaomba na mradi wa mabasi ya kasi uharakishwe na pia ikiwezekana ziwekwe boat za kasi kutoka Ununio hadi posta. Hii itapunguza sana msongamano. Penye nia pana njia.
 
Big up Dr. wa ukweli ila uko ndani Magamba. Mi najua TZ tukiamua tunaweza na uwezo tunao ila tuache wizi.
 
Nampongeza sana Dr Mwakyembe na wizara yake kwa kuwezesha mpango huu kufanikiwa, kuna mafisadi waliwaleta wahindi kufanya kazi ambayo watanzania tuna uwezo nayo.

Nji hii!!
 
safi sana ratiba na muda maalumu kwa kila kituo nadhani wataweka kadri siku zinavozidi kwenda
cha muhimu watanzania wazingatie ratiba ili tren liende kwa muda unaotakiwa.
 
hizi treni ni mwanzo mzuri sana kwa maisha ya usafiri dar es salaam..........

Mwakyembe ni jembe la ukweli sana...big up mkuu mungu yuko pamoja na weye
 
Msongamano wa magari na foleni nadhani utaisha.
..Mkuu nina wasiwasi kama kweli foleni itapungua kama tunavyofikiria. Baadhi ya watanzania tuna kasumba ya kuona ufahari kuzunguka mjini wakiwa na magari yao. Kwa hiyo mswahili kuacha gari yake nyumbani akapande treni mh!!... Huenda ikatumika tu kwetu sisi tusiokuwa na magari.
 
Nafikiria kuamia DAr kwa sasa,
naona wenye nyumba kandokando na hiyo RELI bei itakuw aishapanda, hata wenye Viwanja kw avyovyote bei juu sasa.
Ushahuri tu wangeiwekea time table inayoelewa kwani ni muhimu mtu aqwwe anajau kuw aakifika ubungo au Station muda fulani ataikuta ipo na sio kutoka ofisini na kuja kukesha kituoni kusubiri train!
 
Reli kibamba-ubungo-katikati ya jiji imejengwa lini? Au reli ya kati inapita maeneo haya?
 
Mwanzo mzuri...kumbe kila ki2 ni maamuzi na kikubwa kupata watu waadilifu wenye uchungu na nchi yao na si kufanya kazi kwa ajili ya kutaka 10% na hili ndilo linalotugharimu watz kwa sasa, hizi 10% ziko kila kona...ila kwa staili hii tutafika sasa. Hongera sna Waziri Mwakyembe umeonyesha njia..,tuombe ushirikiano.
 
Hili linahitaji pongezi za hali ya juu... Hopefully Mwakyembe kajipanga vema na huu ni mwanzo tu wa hio huduma ya treni kushamiri nchini, hasa jiji la Dar lenye msongamano wa transportation.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom