Gari la Mpendazoe lakamatwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
Mpendazoe%2811%29.jpg

Msemaji wa Chama Cha Jamii (CCJ), Fred Mpendazoe.

Polisi katika kituo cha Karume jijini Dar es Salaam, imelikamata na kulishikilia kwa muda, msemaji wa Chama Cha Jamii (CCJ), Fred Mpendazoe.
Gari hilo lenye namba T 776 BAE, aina ya Corolla, lilishikiliwa jana kwa takribani saa sita, kwa madai kuwa kibali cha kuendesha kilikuwa kimeisha.
Wakati gari hilo likikamatwa, lilikuwa linaendeshwa na dereva wake, Vitalis Henzi Mpendazoe, anayesadikiwa kuwa mtoto wa Mpendazoe.
Akizungumza na gazeti hili jana nje ya kituo hicho, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema mtoto huyo alikamatwa eneo la Msimbazi Centre, wakati akitokea Kigogo kuelekea Ilala-Boma.
Alisema askari wawili waliokuwa kwenye pikipiki, walilitilia shaka na kuanza kulikagua, ambapo ilibainika bima yake ilikuwa imemalizika muda wa matumizi.

CHANZO: NIPASHE
 
Si habari ya kushangaza, mtu yoyote akihama CCM huwa anafuatiliwa na kuwa-harrased. Tunajua yaliyomkuta Mrema, Kolimba etc lakini sasa huenda hali inaweza kuwa tofauti, opposition wengine ni very useful, si hopeless kama zamani. Hapo naona ilikuwa inatafutwa njia ya kum-blackmail wameikosa. watatafuta nyingine.
 
Ukifuatiliwa kwasababu umetenda kosa kuna ubaya gani? Kama yeye anakosoa wenzake lazima na yeye ahakikishe hana makosa.

I don't care about the motive, so long you committed or you are committing a crime, it fine with me if police decide to put you behind bars.
 
kama anamakosa basi sheria ichukue mkondo wake jamii isianze kuangalia kila kitu kinachofanywa na serikali kwa mabaya zaidi kwani si kwamba ukiwa kiongozi wa upinzani basi gari lako liendeshwe hata kama vibali vyake vimeisha muda usiambie lolote, cha msingi kwa wao wanaotaka kuwa viongozi wa baadae wawe mstari wa mbele katika kufanya mema na si kutaka sheria ziwapendelee
 
Ukifuatiliwa kwasababu umetenda kosa kuna ubaya gani? Kama yeye anakosoa wenzake lazima na yeye ahakikishe hana makosa.

I don't care about the motive, so long you committed or you are committing a crime, it fine with me if police decide to put you behind bars.

Am sure that is a cheap excuse they might have used to reach their motive. Am as well sure that our police officers have better and much more efficient ways of doing that, than motobike chase. Kuna kitu walikuwa wanatafuta walikosa, hichi walitumia kisingizio, ambacho mimi naona ni kizuri sana. Lakini subiri tu uone yanayofuata.
 
Ndugu zangu
Mbona kosa hilo ni la kawaida sana hasa hapa Dar?????? Tunakamatwa sana kuhusu bima kutokana na kutokuwa makini na expiry dates.
Wasomi wangu, si mnajua athari ya kuendesha gari bila bima????? mbona mnalifanya suala hili kuwa kubwa kuliko linavyostahili????
Au kwa sababu ni Mpendazoe???????? Jee ndugu yako akigongwa na gari lisilokuwa na bima unaijua adha yake?????????????
Tuache ushabiki usio na msingi. This is a traffic case and thats' it.
 
Hivi ni vitu vya kawaida jamani, kwani bima/Motor vehicle licence kuisha muda wake sio inshu wala nini, kakate Mpendazote uachane na hao jamaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom