Gari la Mkurugenzi wa NSSF-DAU, laibwa 'gesti'

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Gari la Mkurugenzi wa NSSF laibwa 'gesti'


Mahija Mpera


GARI la Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau, limeibwa, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilisema jana.


Kamanda wa kanda hiyo, Sulemani Kova, aliwaambia waandishi wa habari kuwa gari hilo liliibwa Novemba 10 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.


Kova alisema hata hivyo siku iliyofuata, gari hilo lilikamatwa mkoani Kilimanjaro.


Alisema mbali na kukamata gari hilo, polisi pia wamewakamata watu saba wakiongozwa na mwanamke katika wizi huo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, kundi hilo linahusisha pia na wizi wa magari kadhaa nchini.


Kamanda Kova alisema kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi huyo mara baada ya kuibiwa.


Alisema kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa NSSF, alisema wizi huo ulitokea usiku wa Novemba 10 baada ya majambazi kumvamia dereva wake Yusuf Magogo, mkazi wa Tabara.


Kova alisema hata hivyo uchunguzi wa polisi ulibaini kwamba taarifa hizo za awali hazikuwa sahihi kwa sababu gari hilo liliibwa na mwanamke ambaye aliyekuwa na dereva huyo katika nyumba ya kulala wageni.


"Kuna mwanamke (jina tunalihifadhi kwa sasa) akiwa na dereva wa gari hiyo walikwenda kwenye gesti ya Comfort iliyoko Kinondoni kwa lengo la kufanya mapenzi, wakiwa katika chumba namba 12 mwanamke huyo alimwekea madawa ya kulevya dereva huyo katika kinywaji chake aina ya vitamalta," alisema Kova.


Alisema baada ya kunywa kinywaji hicho, dereva alipoteza fahamu, jambo lilitoa fursa kwa mwanamke huyo kuchukua funguo za gari na za chumba hicho na kutokomea nazo.


Alisema hata hivyo polisi mkoani kilimanjaro kwa kushirikiana na Kampuni ya Cartrack, waliweza kukamata gari hilo katika Kijiji ncha Lyasongoro, likiwa na namba bandia.


Kova alisema Novemba 9 mwaka huu, polisi wa Kikosi cha Maalumu cha Kuzuia Wizi wa Magari, walimkamata mwanamke huyo na kumhoji.


Kwa mujibu wa kamanda huyo, mwanamke huyo alikiri kuhusika na ujambazi huo na kwamba yeye anatumiwa na kijana mmoja.


Katika tukio lingine, polisi wamekamata majambazi sita sugu wakiwa na bunduki aina ya rifle yenye namba AU-160 ikiwa na risasi 19.


Kamnda Kova amesema kwa majambazo hayo yamekiri kuhusika na ujambazi
 
Jina la dereva limefichwa, jamaa anaitwa Hassan ndiye dereva wa Dau na anapenda sana kutembea na gari hilo usiku kwente vigrocery vya Kinondoni. Ni kiwembe sana!
 
Jina la dereva limefichwa, jamaa anaitwa Hassan ndiye dereva wa Dau na anapenda sana kutembea na gari hilo usiku kwente vigrocery vya Kinondoni. Ni kiwembe sana!

Ni kiwembe sana

Aiseee safisana.......sema marayaaaaaaaaaaaaaaa kabisa huyu anatakiwa aisadie polisi
 
Mimi naona tumsikitikie huyo Dareva kwani UKIMWI UPO KARIBU naye. hakuna kidume katika ngono zembe.
 
Jina la dereva limefichwa, jamaa anaitwa Hassan ndiye dereva wa Dau na anapenda sana kutembea na gari hilo usiku kwente vigrocery vya Kinondoni. Ni kiwembe sana!

safi sana, watu kama hawa weka hadharani! kwanza amedanganya polisi!
 
unaambiwa kuna demu wa kitusi anawanyanyasa madereva hawa wanaoendesha magari ya fahari serikalini, anajilengesha unajiona una bahati kumbe umeuvaa mkenge jamaa akawekewa drugs kwenye malta guiness akalala demu kama analia vile alasepa na mkoko ila amekamatwa huyo demu na jamaa yake anayemtumia km chambo
 
Jina la dereva limefichwa, jamaa anaitwa Hassan ndiye dereva wa Dau na anapenda sana kutembea na gari hilo usiku kwente vigrocery vya Kinondoni. Ni kiwembe sana!

Kwa nini atembee na gari la shirika usiku bila bosi wake?
 
Gari la Mkurugenzi wa NSSF laibwa 'gesti'

GARI la Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau, limeibwa, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilisema jana.


Taarifa ilivyowekwa awali nilielewa kuwa ni Bwana Dau aliyekuwa huko gesti na gari lake binafsi. Kumbe ni gari la Mkurugenzi wa NSSF !!!!!!!!!!! Kumbe aliyeibiwa gari gesti ni dreva wa Mkurugenzi wa NSSF?
 
Jamani si nae dereva anataka kutanua ili aonekane naye ni MD bana sio kumbeba Dau tu
 
Kwa nini Dau aliwadanganya polisi?

Inawezekana dereva alimdanganya bosi wake ili kuficha source ya kuibiwa gari; nae kwa kutokufahamu akawapa information hiyo hiyo polisi.

Kazi ya polisi ni kuchunguza ukweli upi na uongo ni upi si kazi ya mkurugenzi.

Ni mtazamo wangu.
 
jamani huyu Dau mmezidi kumuandama. Kesi ya dereva lakini kichwa cha habari ni Dau.
 
chazo cha kufufua huu uzi ni nini?huu uzi ni wa mwaka 2009 miak 6 iliyopita mnaufufua leo kwanini au ndo muendelezo wa kimuandama dr dai
 
Back
Top Bottom