Gari la Mbunge wa Mtera lapigwa jiwe; aapa kuwapiga bao CHADEMA!

Hapa tusichanganyane, hao ni CCM wenyewe ili waisingizie CDM, walianza kumwagiana tindikali, wakapigana mapanga, wakabakana, wakachukuliana wake zao.
 
Hoja siku zote hujibiwa kwa hoja si mawe na kuharibu mali au kupigana. Hii ni taswira mbaya kwa CDM.
 
Na Yule Fisadi Kikwete aliyepopolewa Mawe kule Mbeya ilikuwaje? Kweli sasa Watanzania wamechoka wanaonyesha kwa vitendo wakisema hawasikilizwi inaweza hii ikwa ni ujumbe kwa Magamba kuwa sasa mwisho wao unakaribia.

Utasikia nako walikuwa CHADEMA tu
 
Jamani CCM isitumie njia za hila kuzusha mambo ya ajabuajabu ili ionewe huruma na wananchi.Wananchi kwa sasa wana upeo mkubwa sana juu ya mambo ya nchi na dunia hii kwa ujumla yanavyokwenda. Haingii akilini gari lipigwe mawe na hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na muhusika.Matukio mabaya yote yanapelekwa kwa washindani wao.sidhani Lusinde na uelewa wake mdogo wa sheria hajui taratibu za kufuata.Aache uzushi wa kipuuzi kwa jamii na atumie hoja katika midani ya siasa.Hopeless Lusindi!!!!!!!!!!
 
Sawa sawa kupigwa mawe, yeye alivyoongea pumba zake kwa wazee wa kisukuma ulitegemea wamfanyaje? zaidi ya kumpiga mawe.
Unakumbuka Mtikila naye Tarime walimfanya nini? nashangaa mida hii hajaja IGUNGA yulo bize na mahakama kuuzwa.
 
wanasiasa kuweni makini sana mnapomtaja Dr. Slaa mbele ya halaiki, lusinde anadhani alimshinda mzee malecela kwamba yeye ni bora, hamna lolote! anawadhalilisha wapigakura wake.
 
Hao ni ccm wenyewe, hata baba Riz1 alishasema kuwa ndani ya ccm hawapendani.
 
Huyu lusinde hajitambui, ila yeye kwa kutojitambua kwake amekubali kuwa devil-used creature. Tumuombee arejeshewe ufahamu.
Mtu aliye timamu hawezi kumporomoshea matusi mwenzia wa rika lake wala wadogo zake, sembuse wazee kama Dr. Slaa mwenye umri unaopaswa kuwa mzazi wake?
Kibaya zaidi hajachokozwa na yeyote toka kambi ya Slaa.
Tumsamehe hajui alitendalo huyu, kwani angejipa hata dakika moja kufikiria alichoropoka, angelia na kwenda kwa Slaa kuomba msamaha.
 
Hao ni magamba tushawazoe, njaa zake tu hana lolote, kujikomba tu kama mwanamke shenzi taip livingstone, wapi tambwe hiza alisema kurudi ccm mara mia alale na mama yake yako wapi !hao magamba wote wana sifa sawa! Mwisho wao upo karibu sana!
 
Huyu Lusinde nicampoon kabisa....hivi hajui kuwa wapambe wa Rostam bado wana hasira na mtu wao kulazimishwa kujivua gamba? S nao wanaweza kutupia mawe magari ya hao waliolazimisha Rostam kujiuzulu?
 
img_1637.jpg


hali tete uchaguzi mdogo igunga; magari ya ccm yapigwa mawe


mbuge wa mtera, livingstone lusinde, akiwaonesha maafisa wa polisi sehemu ya kioo cha gari lake kilichopasuka baada ya kurushiwa mawe na watu waiojulikana wakati masfara wa magari ya kampeni ya ccm, kurushiwa mawe katika kijiji cha nkinga.
picha na victor makinda




haya yalitokea baada ya mbunge livingstone lusinde kuongea yafuatayo kwenye mkutano wa hadhara.

kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la igunga, zimezidi kupamba moto baada ya mbunge wa mtera, livingstone lusinde (ccm), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza na wanakijiji wa ugaka kwenye kata ya nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa ccm, dk. Peter kafumu, lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za ccm na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.

“hapa nimewaona waandishi wa gazeti la mbowe (mwenyekiti wa taifa wa chadema); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, ccm tukishindwa nakunywa sumu,” alisema na kuongeza:

“nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia mzee kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa,” alisema lusinde.

“kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa chadema wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita,” alisema lusinde mjumbe wa halmashauri kuu (nec) ya ccm.

tanzania daima


safi sana piga fisadi hao!!!!!! Na siku ya uchaguzi onesheni kuwapiga kwa kutowachagua, wamezoea kutudanganya na kutuona sisi kama mandondocha wao. Tusiwachague hao watatuangamiza kwa kulipiza kisasi cha kugharamia fedha za kununulia kioo au gari jipya!!!!!!!!!!
 
Nasikitikia kitendo cha msafara wa CCM kwenye kampeni kurushiwa mawe kijijini Nkinga huko Igunga, maana ni dalili za kukosa uvumilivu, maana tunaishi watu wa itikadi tofauti na mwenye mvuto zaidi wa itikadi kukubalika na wengi avumilike. Lakini jeuri inapozidi kulazimisha kuungwa mkono taratibu zilizokubaliwa kisheria zitumike badala ya njia ya mkato kama ilivyotumika.

Na kwa hatua hii vyombo vya usalama vinabeba uzito wote kwa hoja ya kuelemea upande wa chama kimoja kukipa upendeleo kinyume cha wajibu wao. Hali hiyo inasabisha kutia hasira wananchi kwa vile hawana njia nyingine ya kutetea demokrasia yao inayobakwa ila kujichukulia sheria mkononi.

laiti kama sheria zote zilizopo zingekuwa zinafuatwa japo kwa 50%, kusingekuwa na kujichukulia sheria mkononi lakini kwa kuwa sheria hazifuatwi, ndio maana watu wanaonesha hasira zao kwa kuchukua hatua.

ninavyoamini, nchi nyingi zimefika hapo zilipo kwa kuwa kuna watu walijifunga vibebwe wakawa tayari kupoteza uhai wao kwa maslahi ya baadae ya watoto au ndugu zao. hivyo kwangu kwa democrasia ya Tanzania, bila kuwapiga hawa wanaoikandamiza kamwe tusitarajie mabadiliko kwani hawako tayari kuyaachilia maslahi wayapatayo kwa kuibaka democrasia.

sasa kwa nini mtu aape eti wengine wakishinda atakunywa sumu? si maana yake wamesha jiandaa kuibaka democrasia? nawaunga mkono waliowarushia mawe kwani wamegundua kuwa ni kuonyesha chuki moja kwa moja, naamini itatusaidi
a.
 
wananchi hawana makosa, hakuna jeshi la polisi tanzania kuna jeshi la polisi ccm hivyo wananchi inawabidi wajitetee wenyewe kwa kuwa jeshi la polisi limekuwa jumuiya ya chama cha mapinduzi.
 
Back
Top Bottom