Gari la CCM likiwa na Mama Makamba lapata ajali

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Taarifa kutoka ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam zinaonyesha kwamba gari mpya kabisa aina ya land cruiser ya CCM mkoa wa dsm imepata ajali na kupinduka na kuwa write off wakati ikiwa safarini kumpeleka mke wa Yusuph Makamba - katibu mkuu wa CCM mkoani Tanga kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Inadaiwa kuwa Makamba alichukua gari hilo la CCM mkoa kibabe kwa kutumia cheo chake. Kama angefuata utaratibu CCM makao makuu inayo magari mengi ambayo yangefaa kwa shughuli hiyo, badala ya kujichukulia gari la mkoa ambalo sasa limepata ajali na kuharibika kabisa.

naomba kuwasilisha
 
mkuu hapa hakuna haja ya kuangalia gari tena.. Tunataka kujua kama mtu ni mzima basi tunashukuru manake hawa mambo yao na ubadhirifu tunaujua na hakuna wa kuwazuia kufanya hivyo
 
Kaka asante lakini mimi i love Makamba na naomba mkulu amwongezee kazi ili atutengenezee Chadema vizuri. Maana akiendelea utashangaa wanachama wa ccm wenzake wanahamia Chadema.
 
CCM wametoa hizo taarifa kupitia chombo kipi? Mapunziko wa mwisho wa mwaka upi?
 
Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka au Mwanzo wa Mwaka. Najua huu ni uzushi unajaribu kupima hali ya upepo.

Ikitokea siku ikawa mkewe, mwanae hasa anayemtegemea sana ama mkewe ukiacha yule aliyemjaza ujauzito shuleni...... amepatwa na tatizo la nguvu za asili basi itapendeza sana, maana najua hatasita kutuambia "Biblia inasema Bwana alitoa na Bwana ametwa, Jina la Bwana libarikiwe":A S-confused1:
 
"Kiinteligensia" Unajua hawa wasomi wanatufumba macho sana na maneno yao ya kiswahili cha kisasa....mara mpango kazi, mpango mkakati, kikosi kazi, mjasiriamali, semina elekezi.

Hivi karibuni kila Polisi wanapotaka kuzuia watu kutekeleza haki zao za kikatiba wanazuiliwa kwa maneno kama ......habari za kiinteligensia.



Nadhani hii ya kuanguka gari ya CCM imepatikana kwa habari za KIINTELIGENSIA
 
Nadhani hapa ni kutoa pole kwa aliyeumia,si sote ni binadamu tupo safarini.Hata kama Makamba alionekana kushabikia mauaji ya Arusha,tumuachie yeye na Mungu wake.Makamaba asitujaze Roho ya kinyama...Namuombea Mhanga wa ajali hiyo awe hai
 
kama kuna majeruhi basi Mungu awanusuru na kifo na awape huruma yake, kwani si kila baya litalipwa kwa baya.
Mnakumbuka Mungu alimruhusu mtumishi wake mmoja aoe kahaba ili kudhihirisha machukizo aliyofanyiwa na wana wa israel?
 
"Nitafurahi kusikia kua hajapona mtu kwenye hiyo gari"

Hivi kweli tumefikia hatua hii? I dont know how far is too far when it comes to politics
 
Back
Top Bottom