Gari hili gari gani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Gari gani limekuwa kama mganga wa kienyeji!? Kila siku.. lete kuku, lete mayai, lete mbuzi pacha, mara lete vifaranga vya kijani.. kwenda halendi limebakia kuunguruma tu!! Mwisho watu wanaanza kudandia madaladala hivi hivi!!
 
Heheh hehhe kwa utunzi nakupa 100, ila nahisi hilo gari litakuwa TATA!!:clap2::clap2:
 
HIILO GARI LITAKUWA GARI BOVU, BADO HALIJAPATA SPEA IMARA...NDO MAANA KILA SIKU LATAKA SPEA MPYA.........!NA WEWE KWA NINI UNG'ANG'ANIE GARI BOVU? AU KWA KUWA LINA UMBO ZURI (prado,baloon,shangingi)? ACHANA NALO.....NENDA SHOWROOM CHUKUA GARI MOJA MATATA AMBALO LITAKUWA HALIITAJI SPEA BALI NI KUENDESHA TU.....UKIONA VIPI AGIZIA MOJA KWA MOJA JAPAN...WEWE MWENYEWE UTATOA MAKARATASI KITU BADO MMA!!!!!!ILA USI-TEST KWANZA ....ONCE GOODS ARE BOUGHT ARE NOT RETURNED....!(christianity)
 
Nimeumiza kichwa mwisho nimeishia kushangaa hili gari ni gari gani MMM?
Nadhani lishakuwa srappper tafuta Brand new ....
 
is a matter of choice!! kununua jingine, au kulitengeneza hilo bovu.Ila kumbuka ili upate mti wenye matunda mazuri ni sharti tunda life, likauke, lioze na hatimaye kuchipua mti mchanga!!! wenye matunda matamu!! Hilo gari bovu ni mtaji wa kutafuta jipya!!
 
Hv sijawaambia eeh!..Nimetumwa niwaambie kwamba msubiri maana Dereva wake amesafiri, dereva msaidizi kenda kwenye Arusi kusini mwa nchi, konda wake kaenda shambani(kilimo kwanza) japokuwa amegundua kuwa huko shambani hakuna pembejeo, wasaidizi wengine wa gari hiyo wako kupiga debe huko majimboni ili gari ipate abiria wa kutosha...
Kwahiyo tuwe wavumilivu, ila wenye haraka wawahi na ma-Saibaba mengine, japo yana abiria wachache!
 
Gari gani limekuwa kama mganga wa kienyeji!? Kila siku.. lete kuku, lete mayai, lete mbuzi pacha, mara lete vifaranga vya kijani.. kwenda halendi limebakia kuunguruma tu!! Mwisho watu wanaanza kudandia madaladala hivi hivi!!

nunua mini cooper kama hii haitakusumbua
 
Hv sijawaambia eeh!..Nimetumwa niwaambie kwamba msubiri maana Dereva wake amesafiri, dereva msaidizi kenda kwenye Arusi kusini mwa nchi, konda wake kaenda shambani(kilimo kwanza) japokuwa amegundua kuwa huko shambani hakuna pembejeo, wasaidizi wengine wa gari hiyo wako kupiga debe huko majimboni ili gari ipate abiria wa kutosha...
Kwahiyo tuwe wavumilivu, ila wenye haraka wawahi na ma-Saibaba mengine, japo yana abiria wachache!

asante nadhani unaongelea Chama Cha Mafisadi!! tumekupata...
 
ni bora kuliacha gari la aina hii
we gari gsni kila siku linalalamika, ukileta mayai leo kesho linadai soseji.
halina faida , mimi ndp naumia tu, halizalishi, halijitunzi, halijithamini kama wengine

mi naona bara niliache walau nikae kae ili siku ziende mawazo yatulie maana toka nimelipata garii hili
mateso yamezi sana kila siku narud usiku sana ili walau nilikute limelala

nakumbuka hata maneno ya mama yangu aliposema '' mwanangu edy gari hili umelichunguza kwanza kabla hujalinunua?
maana si kila gari ulionalo bara barani linafaa...........
 
Duh...utunzi mnao nyie......gari kila siku spare spare mara oil, mara sijui brake fluid ilhali halikufikishi unakokwenda ha;lina faida....nunua pikipikimoja moja kwa moja lita moja inakupa kilomita 80!
 
Kwa kuwa gari ulilipenda na ulinunua mwenyewe inabidi uwe mvumilivu maana aliyeuza gari hataki lirudi kwake tena. Ukitaka liendesha inabidi ulisukume kwanza ndo liwake. magari yana behaviour tofauti.
 
Hivi wewe unaye sema gari ni Gari! Unaipenda Roho yako kweli. Wewe gari Center Bolt Imepinda. Springs zimepiga kutu. Usukani umefungwa na manati. Matairi yana viraka! :angry: bado unasema Gari ni Gari tu!
 
Gari hii tulipouziwa ilikua imepakwa rangi , ikaonekana murua, bahati mbaya muuzaji alikuja na maneno matamu ya kutuaminisha kuwa gari hii ni mpya, na bahati mbaya zaidi walikuja wakiwa wamevaa makoti ya bei mbaya, tukawaamini wakutazama wajihi na afya zao, na chakustajabisha wale majirani wachache waliowaona wanunuaji, walipigwa butwaa huku wakiwasiii kuwa hilo gari ni kuukuu, halifai, zee limezeeka, hiyo ni rangi tu, oooh masikini kufumba na kufumbua tukalinunua kwa bei ya gharama za maisha yetu....halitengenezeki, halihuziki na wala halipigiki mnada...hahaaa Mwanakijiji njoo usaidiane na ndugu na jamaa kuliuza tena.
 
Back
Top Bottom