Gari gani poa ya ''kifamilia?''

Wanasema gari yenye zaidi ya miaka 10 huwa inatozwa gharama zaidi inapoingizwa nchini.Sasa utajuaje kuwa hili gari ni la zamani limezidi miaka kumi.?
 
Wanasema gari yenye zaidi ya miaka 10 huwa inatozwa gharama zaidi inapoingizwa nchini.Sasa utajuaje kuwa hili gari ni la zamani limezidi miaka kumi.?
Assumption ni kuwa unaagiza gari nje ya nchi, wauzaji huwa wanaweka mwaka wa gari ilipotengenezwa na mwaka wa gari iliposajiliwa, kwa hiyo wewe angalia mwaka wa ilipotengenezwa...kwa kurahisisha hata tangazo la gari huwa linaanza na mwaka wa gari ilipotengenezwa, mfano "2006 Toyota iSt ..." , na likifika watu wa bandari wanalikagua kwa kuangalia vibandiko kwenye mikanda (seat belts) ambapo mwaka wa gari kutengenezwa huandikwa na pia wanaangalia VIN (vehicle identification number) ambayo hata wewe unaweza kuangalia kupitia website mbalimbali kujihakikishia kama gari hilo ni la mwaka unaotajiwa na muuzaji...ila njia rahisi ni hiyo ya kuangalia prescription iliyotolewa na muuzaji (wengi wanatoa exact date kuepuka kitu kinaitwa misrepresentation)
 
Mkuu hayo yote magari yaliyotanjwa hakuna hata moja family car mkuu. Gari ya family na ambayo inaimili halisi ya barabara za kwetu na spears zake zinapatikana kwa urais na pia ni rais sana kuliuza kama umechoka kulitumia .lipo sokoni sana mkuu ni Toyota Noah model 1999.hii car sisi macardeal tunaiita roho ya paka ni gari ngumu sana na hata mafuta inatumia vizuri sana
Bei yake inakuwaje kwa kima cha juu na cha chini?
 
Mkuu tafuta Carina Ti. Huwezi kuamini niliweka full tank lita 50 kutoka moshi nimefika dar bado mafuta yapo juu ya robo tank. Ti ni cc 1490
Usije kununua carina Si
N kweli kabisa,,, mm nilitumia hivyo xmas ya mwaka juz
 
Wakuu wajuzi wa JF,

Naombeni mnishauri mimi na wadau wengine watajifunzia hapa. Mwaka jani niliagiza Chaser GX 100,C.C 2300 ya kuanzia maisha,kiukweli nilikurupuka sana wadau.

Wese lilikuwa linachuruzika balaa,sometimes nalazimika kupaki! Sasa naja kwenu kwa unyenyekevu kijana wenu mnipe ushauri ni gari gani poa ya kifamilia inayofaa,in terms of spare parts na fuel consumption.

Nina bajeti ya Shs.8,000,000!

Asanteni wadau
Huna jinsi kwa bajeti yako hii chukua hiii garii... Angalau kwa familia zetu za kiafika na .... Ila usiwe mtu wa kufunguka sana kwenye kona na hii gari ... Tutakusahau mkuu
1469865257731.jpg
1469865274392.jpg
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Hivi bado mnatoa tu ushauri kwenye hii post ya mwaka 2014??
ha ha haa kweli aisee, ila kuna wengine wanataka kununua gari leo kwa hiyo kwa faida yao ndio ushauri unendelea kutolewa
 
Zipo nyingi Toyota IST cc 1300/1500, Toyota CarinaTi cc 1500, Toyota Runx cc 1500, Toyota Allex cc 1500 ila kama unaweza ogeza kama 2mln chukua Toyota Allion 1500cc. Hizo zote mjini kwenye foleni zinakula 1ltr/11km na highway ni 1ltr/16km.
Mkuu Kibirizi, Toyota Allion kutoka Japan to Dar hadi ninaishika mkononi inaweza kunila bei gani?
 
TOYOTA ALPHARD ni gari zuri sana kwa matumizi ya kifamilia hasa ya kiafrica,tatizo bei yake bado ipo juu kidogo,pia ina engine nzuri za 2AZ cc 2360 ....Lakini tahadhari zipo zingine zina engine kubwa cc3000.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom