Gaddafi: The end of a miserable despotic Tyrant!

Qaddafi alimwamini Amin Dada cz at tht tym walihitajika viongozi wa aina ile! Alikuwa m2 thabiti kutetea haki na rasilimali za mwafrika hakuogopa ngozi nyeupe kama walivyo viongozi wetu wote wa Africa ambao hawana msaada wowote! limebaki jembe1 nalo ni Mugabe

Upuuzi mtu, kwa nini hao mnaowaita majembe ni wale wenye tamaa za kutawala milele? Nyie vipi bana?
 
sasa kwa nini tusiichukie na uganda yenyewe kwa kuwa tulishapigana nao? mbona ma white wanachukuwa utajiri wetu mchana kweupe na bado tumewakumbatia na tunapokea misaada yao ya kinafiki?
 
mtoa mada naona ka mtu wa kijiweni vileikali
soma historia yake na mazuri yake alioifanyia afrika
wapuuzi sana wamarekani na BBC wanasema alikuwa dikteta kwa miaka 40 HII YA KWELI? ni nchi gani
ya afrika inatoa misaada na kummjali mzawa?imangine ukiagiza gari unalipiwa nusu ya garama na serikali. ukimaliza chuo huna kazi
unalipwa mshahara kiasi fulani hadi upate kazi.maskini walisaidiwa Libya haikuwa na shida,tatizo lake alikataa kuwa kibaraka wa nchi za mgharibi
na hakupenda mafuta yake kutawaliwa na hawa wazungu kama ilivo saudi arabia nk.mtoa mada think twice.libya itasambaratika milele
nimeumia sana kifocha ghadafi watajuta baadae,
 
kweli ng. kipeperushiaisee............... maana unapima uzalendo kwa kifo cha gaddafi badala ya kujenga nchi yako

kituko cha mwaka
 
Qaddafi alimwamini Amin Dada cz at tht tym walihitajika viongozi wa aina ile! Alikuwa m2 thabiti kutetea haki na rasilimali za mwafrika hakuogopa ngozi nyeupe kama walivyo viongozi wetu wote wa Africa ambao hawana msaada wowote! limebaki jembe1 nalo ni Mugabe
kwa hiyo serikali unayoitaka ww ni ya ki dictator?
 
Kwa wale wenye kuendeshwa na vitu kama vile misikiti tende na nyamafu toka Saudi Arabia Gaddafi alikuwa mwafrika wa kupigiwa mfano. Kwa wale wenye kutafiti mambo hakuwa mali kitu. Tuwape usemi wake wa mwisho kabla hajapotea kuhusiana na waafrika. Baada ya kuona nchi za Ulaya hazimsaidii alizitishia kwa kusema kuwa atafungulia waafrika wajinga na maskini wafurike Ulaya. Hakuishia hapa. Alizitishia nchi za kiarabu baada ya Arab League kumpiga kibuti akisema, "Kuanzia leo mimi si mwarabu bali mwafrika." Hii maana yake ni kwamba alipokuwa akikutana na watawala mbwa mwitu wa Afrika na kuwahadaa hawakujua kuwa moyoni Gaddafi hata kama nchi yake iko barani Afrika hakuwa mwafrika. Bahati mbaya sana, watu wengi wanafikiri uafrika ni kuwa mweusi zaidi ya kuwa katika bara la Afrika. Gaddafi alikuwa mnafiki na msanii wa kawaida. Hata waislamu wanaopoteza muda na heshima yao kumwombea ni kwa vile wako kizani.Ni Muislam gani mwanamme anaruhusiwa kuvaa wig? Kuna haja ya kupoteza muda kutafuta ukweli badala ya kupoteza muda kwenye ushabiki. Kwanini watu hawajiulizi ni kwanini walibya ambao ni waislam na ndugu za Gaddafi wanasherehekea kifo chake wakati sisi tusiohusika tunajifanya kusikitika. Kweli kitanda usicholalia hujui kunguni wake. Au waswahili wanashabikia ile hali ya Gaddafi kuiba pesa ya walibya na kujenga misikiti kusini mwa Sahara. Tafuteni utajiri badala ya kutegemea makombo.
 
Huyu msemaji anaonekana kuwa juha asiye na la kusema. Anadhani watu wote ni majuha kama yeye? Kama huyu amesoma kwa pesa ya Gaddafi aliyowaibia walibya asidhani wote ni wajinga na tegemezi kama yeye. To hell with you guy who is bootlicking Gadaffi.
 
je Tanzania baada ya kumuondo Amini Ktk Mipaka ya Tanzania Kwanini Waliendelea na Vita? Pili Nyerere Mwenyewe alirudisha uhusiano na Libya baada ya vita na hata Msikiti wa Nyerere Kule Butiama Umejengwa kwa udhamini wa Serikali ya Libya. Hivyo Vita ya Kagera ilikuwa ni ya kimaslai wala sio kama unavyofikiria wewe.
Katika vita kati Tanzania na Uganda Libya ikiwa chini ya utawala Gaddafi ilitoa msaada wa kijeshi kwa nchi ya Uganda. Kutokana na msaada huo mamia ya watanzania waliokuwepo kwenye maeneo yalivamiwa na Uganda ( wakati huo ikiwa chini ya utawala wa Idi Amin Dada) walipoteza uhai wao. Hivyo leo hii mtanzania ambae anasikitishwa na kifo cha Gaddafi hana moyo wa kizalendo. Au mnasemaje wanaJF kuhusu mtazamo wangu?
 
sasa kwa nini tusiichukie na uganda yenyewe kwa kuwa tulishapigana nao? mbona ma white wanachukuwa utajiri wetu mchana kweupe na bado tumewakumbatia na tunapokea misaada yao ya kinafiki?

Hatuwezi kuichukia uganda au waganda wote kwa sababu ya vita vya kagera, tunajua wazi aliyesababisha vita ni idd amin kwa kutaka kuuteka mkoa wa kagera pia kumbuka kuwa wananchi wengi wa uganda walikuwa begabega na majeshi ya TZ na walifurahia kunyukwa kwa idd amin na vilevile hata leo hii hatujasikia uganda wakidai kuwa kagera ni ardhi yao ikimaanisha kwamba idd amin alifanya uchokozi kwa sababu zake binafsi na si kwa niaba ya waganda.
 
Ila bora wamemuondoa huyo dictator, Libya ni ya walibya wote, Me nilikuwa naangalia al jaz kweli watu wanalalamika tena wanamwiita devil wanalalamika kaua watu wengi, kama kweli alikuwa mtenda haki na kujenga miskiti allah angemuokoa maana watu dodoma wamemswalia lakini bado akanyimwa akili mpaka umauti ukamfika
Hukohuko alipo bila yakutambua, ukweli ni kwamba akupenda afe na uwezo wakuepuka kifo ulikuwepo na yeye amefanya mchango mkubwa sana kwa kujenga mskiti lkn hakupata chance yakutumia ufahamu au kwa lugha nyingine hakuwa ukupewa mbinu na allah ili amuokoa, sasa hivi ana hukumiwa maana imeandikwa baada ya kifo ni hukumu. Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga. . .
 
Ni unafiki tu kujifanya hatuoni ilhali macho tunayo. Hivi kama alikuwa anapendwa kweli mamia kwa maelfu ya watu wake wangefurahia? Sipendi mtu kuuawa kwa namna yoyote ile, lakini kama walibya wenyewe wamemuua na wao wanashangilia, sie wengine tucheke ama tulie tuna sehemu gani kule? Gaddaf anayo mazuri aliyoyafanya, but hiyo haifichi mabaya aliyoyafanya pia. Walibya wameamua na wametenda, mbona sie ya kwetu yanatushinda! Unafiki mkubwa, mnadandia gari kwa mbele mtakufa.
 
mimi sifurahii kabisa kifo cha gaddafi kuna mengine mazuri amewafanyia watu wake pia. mbona tz kuna viongozi wako hoi mbona hauwasemi.
 
by mwanakijiji
.........we can not blame nato, the west or accuse the libyan people of being "used" by the western powers
. We will be denying what is very clear before own eyes. His time was up and the people of libya ensured that he understands that.so the end of gaddafi is simply and absolutely an end to a despotic tyrant. ....

tumika baba, tumika, tumikia kafiri upate mradi wako!.......too cheap and shame on you!
 
Katika vita kati Tanzania na Uganda Libya ikiwa chini ya utawala Gaddafi ilitoa msaada wa kijeshi kwa nchi ya Uganda. Kutokana na msaada huo mamia ya watanzania waliokuwepo kwenye maeneo yalivamiwa na Uganda ( wakati huo ikiwa chini ya utawala wa Idi Amin Dada) walipoteza uhai wao. Hivyo leo hii mtanzania ambae anasikitishwa na kifo cha Gaddafi hana moyo wa kizalendo. Au mnasemaje wanaJF kuhusu mtazamo wangu?

Mie naona uko sawa kabisa, Gaddafi hakua malaika, na hata kama alisaidia kujenga misikiti kadhaa hapa nchini bado haikumsaidia kujisafisha na mauaji kwa wananchi wake, kujilimbikizia mali na kujinunulia bastola ya dhahabu ambayo inasikitisha haikutumika hata kwake mwenyewe.
Huyu bwana kuondolewa kunazidi kudhihirisha jinsi wananchi walivyo na nguvu, just imagine wale viongozi wenye tamaa nchini kwetu, ambao wangepewa uraisi, na uhakika wangeishia hivi hivi!
Kiongozi huwezi kuwa tajiri namna hii, kuua wananchi wako kisha wanakuponda na kuifanya nchi ni mali binafsi!
Hii iwe fundisho kwa akina Mugabe, na wenzake, na hasa wale waroho wanaotaka cheo kama EL!
 
tumika baba, tumika, tumikia kafiri upate mradi wako!.......too cheap and shame on you!

Hakuna cha ukafiri wala kutumika hapo, kama wananchi wa LIbya wanasherekea kuuwawa kwa Gaddaffi, sie ni nani kijifanya tuna masikitiko kuliko wao?!
Kama kweli angekua kiongozi bora, basi tungeona wananchi wake wakiwa na majonzi, kujenga misikiti kadhaa kusiwe sababu ya kuleta uislamu humu JF, nenda na reality tunayoiona huko Libya
 
wewe hujui unachokizungumza!, kuna raisi anayependwa na raia asilimia mia moja?- je wale wanaomchukia kiongozi wao wakichukua silaha kisha wakapewa msaada na jeshi lenye Nguvu kama NATO Kuasi utasema ni nguvu ya UMMA?.

Nadhani labda hujui Ghadafi kaifanyia nini Libya! na si Libya tu bali Afrika! kamuulize Mandela aliyefunga safari kwa gari Libya kwenda kushukuru mchango wa Ghadafi dhidi ya Apartheid!.

Usilishwe Propaganda za west Ukahadaika!, Kilichofanyika Libya ni Kusurpot upande mmoja wa Civil war dhidi ya Upande mwingine!, kuna raia wengi sana Libya wanamuunga mkono Ghadafi na pia kuna kundi lingine halikuwa likimuunga mkono, sasa iweje uside na upande mmoja?.
 
Ni unafiki tu kujifanya hatuoni ilhali macho tunayo. Hivi kama alikuwa anapendwa kweli mamia kwa maelfu ya watu wake wangefurahia? Sipendi mtu kuuawa kwa namna yoyote ile, lakini kama walibya wenyewe wamemuua na wao wanashangilia, sie wengine tucheke ama tulie tuna sehemu gani kule? Gaddaf anayo mazuri aliyoyafanya, but hiyo haifichi mabaya aliyoyafanya pia. Walibya wameamua na wametenda, mbona sie ya kwetu yanatushinda! Unafiki mkubwa, mnadandia gari kwa mbele mtakufa.

Nadhani umemaliza mzizi wa fitina...... wenyewe wanashangalia Membe na wenzake wanalia!!
 
Back
Top Bottom