Gaddafi (Qaddafi) yuko sahihi?

huyo anasema Ghaddaf kaongea pumba yeye ndie pumba tena Ziliozoozaaa zinanukaa
 
..nilivyomuangalia nimeona kama mwehu/chizi fulani hivi.

..hata sura yake anaonekana kama mtu aliyechoka kwa kukosa usingizi, au anayetumia madawa makali-makali.

..halafu hakuwa mtulivu na makini wakati akitoa "hotuba" yake. vitendo vya kujikuna, kuvuta mtandio wake, kuchambua makaratasi, vina-distract wasikilizaji.


..kuchekesha zaidi akamaliza hotuba na kusahau lundo la makaratasi yake pale kwenye podium.

..next time wamtayarishie telepromter.
 
Dah jamaa kichwa hakuna rais wa Afrika anaye weza kumwaga ladhi kama huyu dah kafunika katika historia mtake msitake huyu sio kibaraka wa weupe nimependa sana kawabwatukia weupe.

Yaani huyu mjinga mjinga unamwona kichwa? Toka lini kuongea ujinga ujinga na pumba ikawa sio ukibaraka? Uliwahi kumwona Mchonga aki act kama hana akili nzuri? Uliwahi kumsikia Mchonga akiongea pumba zisizoeleweka?

Hili lijamaa lijinga na halina akili. Halina hata chembe ya ustaarabu. Utapandaje jukwaani na kuanza kurusha rusha makaratasi kama kichaa. Hoja hujibiwa kwa hoja na si antics kama alizoonesha jana. Angemgonga Mama Migiro je na kile kitabu alichorusha? Mthenge sana huyu Kadafi....
 
Nahisi Africa itaendelea kuwa chini ya Watawala Wapya (Ukoloni mamboleo) sababu bado tunavibaraka wengiiiiiiiiiii tena saaana hilo utalijuwa na kuliona pale shuja moja anapopambana na Wanyonyaji huitwa mpumbavu Leo Hii Mugabe Yuko wapi ili hali alikatazwa hata asisafiri nje ya Zimbabwe utafikiri George W Bush Kawaoa Viongozi wa africa Pia Sipendi Mjinga akacomment kitu ambacho hajakisikiliza wala kukiona
 
An mengi kichwani matokeo yake hajui aanzie wapi aishie wapi ikizingatiwa kuwa muda haumruhusu sana.
 
Safi sana Gaddafi, wewe ndiye mwaname wa Afrika ambaye umethubutu kuwaambia hao wazungu wanajidai ku-dominate uhuru wa dunia. Nilifurahi sana ulipokatupa kale ka UN Charter!!

Wengine wanabaki kusifia sifia tu ili kujikomba wakati Afrika imejaa matatizo lukuki na partly yamesababishwa na siasa na uchumi wa mataifa makubwa ambayo ndiyo yanajiita Super powers!!

Ni vita vingapi vinamaliza innocent citizens duniani?? Utashangaa wanatumia nguvu kubwa pale ambako kuna maslahi, wakikuta nchi ni maskini hakuna maslahi acha wauane. Tell them, you had the courage Muamar Gaddaf, Keep it up.
 
Yaani huyu mjinga mjinga unamwona kichwa? Toka lini kuongea ujinga ujinga na pumba ikawa sio ukibaraka? Uliwahi kumwona Mchonga aki act kama hana akili nzuri? Uliwahi kumsikia Mchonga akiongea pumba zisizoeleweka?

Hili lijamaa lijinga na halina akili. Halina hata chembe ya ustaarabu. Utapandaje jukwaani na kuanza kurusha rusha makaratasi kama kichaa. Hoja hujibiwa kwa hoja na si antics kama alizoonesha jana. Angemgonga Mama Migiro je na kile kitabu alichorusha? Mthenge sana huyu Kadafi....

Hongera mkuu NN kwa kuwa na ID pacha Julius. Kumbe naweza badili ID bila ku-affect details nyingine?? Poa ni PM jinsi ya kufanya??

Ila pacha Julius namsifu anaandika kirefu zaidi kuliko ile short and stimulating!!! Ha ha ha mkuu. Hapo kwenye bold du kweli unajua kukwepa zile ******.
 
Toka lini mwarabu toka Jamhuri ya Kiarabu(sio Kiafrika) ya Libya akawa "King of Africa"! Njaa kweli mbaya...haya bana...

Waarabu wa africa wakati wa kudai uhuru walijitambua kweli kuwa ni wafarica hii ya kuwaona ni warabu imekuja sasa. Ukisoma hostoria inaonyesha kuwa akina Nasser walikuwa wapigania uhuru na ndio waanzilishi wa OAU akisaidiana na akina Nkrumah. Nkrumah alioa mke wake huko Misri. Ghadhaffi ni mwagrika na anafikria kiafrika ila tu ni too extermist hata kwa wafrika wenzie
 
Ukiangalia vizuri utaona kana kwamba Gaddafi alikua amechoka
kusikia vicheko vya hawa mabwana katika picha ya kwanza. Nd'o
basi akaamua...."kama hawanisikizi hebu niwatupia kitabu chao"

...mwanamume kiboko kweli.

Hahaha huyo Ali Treki ni Mlibya mwenzake Gaddafi naona anaangangua kicheko kwa kwenda mbele.
Tuacheni ushabiki Gaddafi kama kiongozi wa muda mrefu alitakiwa kuwa na hekima na diplomasia huwezi kupanda jukwaani na kuanza kurusha makaratasi, kutokuheshimu muda na kumuita rais mwenzako mtoto wangu. Cha kusikitisha ni kuwa viongozi wetu wengi wa Afrika wanamfuata/msikiliza huyu kwa ushauri.
 
Waarabu wa africa wakati wa kudai uhuru walijitambua kweli kuwa ni wafarica hii ya kuwaona ni warabu imekuja sasa. Ukisoma hostoria inaonyesha kuwa akina Nasser walikuwa wapigania uhuru na ndio waanzilishi wa OAU akisaidiana na akina Nkrumah. Nkrumah alioa mke wake huko Misri. Ghadhaffi ni mwagrika na anafikria kiafrika ila tu ni too extermist hata kwa wafrika wenzie

Ukisoma historia hiyo hiyo inasema Misri na Syria waliunda kitu kinaitwa United Arab Republic (1958-1961), baada ya Syria kujitoa Egypt waliendelea kujulikana kama Jamhuri ya Kiarabu mpaka mwaka 1971 chini ya huyo huyo Gamal Abdel Nasser. Kati ya 1972-77 Libya, Egypt na Syria walijaribu kuunda Jamhuri ya Kiarabu.
 
...Ni ujinga kusifia MJINGA, kitu gani cha maana alichosema gaddafi zaidi ya lawama na unfertile criticisms zisizokuwa na maslahi kwa nchi yake wala africa...lkn ameprove that arabshv no any contribution to the global affairs!!

Uungwana ni kitu cha bure,hata hilo limemshinda!!dk 96 kwa kuongea pumba!!!

Tatizo ni pumba zake ama uarabu wake?

omarilyas
 
.Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton na balozi wa Marekani kwenye baraza la umoja wa Mataifa Susan Rice wakipinga ujio wa Gaddafi Marekani walitoka mapema kwenye ukumbi huo kabla ya Gaddafi kuanza hotuba yake.

Huu ni utamaduni wa siku nyingi wa wamarekani na baadhi ya washirika wao kama UK ambao wao wanajiona ni wajuvi, wasafi na wastaarabu kuzidi wengine ambao wana tofauti nao.

Ni tabia ya wamarekani ama kuondoka wote ama kuacha interns wakati viongozi ama wawakilishi wa mataifa ambayo wanatofautiana nao ama wanaona siyo ya kiungwana kama wanavyojiona wao.

Kihistoria wamekuwa wakifanya hivyo kwa Urusi (sasa wamaacha), Cuba, Iran, Libya, Mynamar, enzi zile Irak pia, na mataifa mengi ambayo hayafuati misingi wanayoiona wao kuwa ndio misingi bora ya kiutawala.

Mara nyingi huwa najiuliza endapo ikatokea siku wale wote wenye tofauti na marekani nao wakatoka ukumbini ama kuwacha junior officers mezani wakati kiongozi wa Marekani ama UK anahutubia itakuwaje.

Wanasahau kuwa mantiki mazima ya kuwa na GENERAL ASSEMBLY inayotoa haki sawa kwa wote ni kuwezesha kuwakutanisha mahasimu wakuu wote wenye misimamo, mitizamo, haiba, maslahi na hata tamaduni tofauti...

Ndio maana kwa mtazamo wangu ni bora UN ikahama na kila kitu na kuhamia GENEVA ambao wao neutrality ni sehemu ya utamaduni wao

omarilyas
 
Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi huku akimwita Obama mtoto wetu aliliponda baraza la usalama la Umoja wa mataifa na kuliita 'Baraza la Magaidi' huku akisisitiza kuwa mataifa ya ulaya lazima yazilipe fidia nchi za Afrika kwa kuzitawala kikoloni.Akilihutubia kwa mara ya kwanza baraza la umoja wa Mataifa baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kumaliza hotuba yake, kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi alitumia muda wa dakika 96 tofauti na muda wa dakika 15 aliotakiwa kuutumia kutoa hutuba yake.

Akimwongelea Obama kama 'Mtoto Wangu' Gaddafi alisema "Tunafuraha kwamba kijana wetu wa Kenya amepigiwa kura na kuwa rais wa Marekani, je Marekani inaweza ikatuhakikishia kuwa baada ya Obama kutakuwa na serikali? Tungefurahi kama Obama angekuwa rais wa milele wa Marekani".

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton na balozi wa Marekani kwenye baraza la umoja wa Mataifa Susan Rice wakipinga ujio wa Gaddafi Marekani walitoka mapema kwenye ukumbi huo kabla ya Gaddafi kuanza hotuba yake.

Gaddafi aliliponda baraza la usalama la umoja wa Mataifa na kuliita "baraza la Magaidi" akisema kuwa tangia kuanzishwa kwa umoja wa mataifa kumetokea jumla ya vita 65 duniani.

"Hakuna mtu anayelijali baraza la usalama wa umoja wa mataifa" alisema Gaddafi na kuongeza "Baraza hili liliundwa na magaidi".

Gaddafi alisema kuwa baraza hilo liliundwa na mataifa makubwa na limetumiwa kuziporomosha nchi ndogo akitoa mfano wa vita vya Iraq, Afghanistan na Korea na Vietnam.

Kuna wakati Gaddafi alitaka kukichana kitabu cha bluu cha mkataba wa Umoja wa Mataifa lakini alisita baada ya kuona viongozi wa dunia wameduwaa kwa mshangao.

Gaddafi ambaye alitambulishwa kama kiongozi wa mapinduzi, rais wa umoja wa Afrika na mfalme wa wafalme wa Afrika alitetea haki za waafrika kwenye baraza hilo akitaka nchi za ulaya zilipe fidia ya dola trilioni 7.7 kwa nchi za Afrika kwa kuzitawala kikoloni.

"Mataifa ya Afrika yana haki ya kwenda popote pale na kudai dola trilioni 7.7 zilizoibwa toka Afrika", alisema Gaddafi.

Gaddafi alimalizia hotuba yake kwa kulitaka baraza la umoja wa mataifa kuchunguza sababu zilizopelekea kunyongwa kwa Saddam Hussein, kutupwa jela nchini Marekani kwa rais wa zamani wa Panama,Manuel Noriega na kuuliwa kwa rais wa zamani wa Marekani John F Kennedy pamoja na aliyekuwa mpiganiaji wa haki za watu weusi Marekani, Martin Luther King.Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi huku akimwita Obama mtoto wetu aliliponda baraza la usalama la Umoja wa mataifa na kuliita 'Baraza la Magaidi' huku akisisitiza kuwa mataifa ya ulaya lazima yazilipe fidia nchi za Afrika kwa kuzitawala kikoloni.

Akilihutubia kwa mara ya kwanza baraza la umoja wa Mataifa baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kumaliza hotuba yake, kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi alitumia muda wa dakika 96 tofauti na muda wa dakika 15 aliotakiwa kuutumia kutoa hutuba yake.

Akimwongelea Obama kama 'Mtoto Wangu' Gaddafi alisema "Tunafuraha kwamba kijana wetu wa Kenya amepigiwa kura na kuwa rais wa Marekani, je Marekani inaweza ikatuhakikishia kuwa baada ya Obama kutakuwa na serikali? Tungefurahi kama Obama angekuwa rais wa milele wa Marekani".

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton na balozi wa Marekani kwenye baraza la umoja wa Mataifa Susan Rice wakipinga ujio wa Gaddafi Marekani walitoka mapema kwenye ukumbi huo kabla ya Gaddafi kuanza hotuba yake.

Gaddafi aliliponda baraza la usalama la umoja wa Mataifa na kuliita "baraza la Magaidi" akisema kuwa tangia kuanzishwa kwa umoja wa mataifa kumetokea jumla ya vita 65 duniani.

"Hakuna mtu anayelijali baraza la usalama wa umoja wa mataifa" alisema Gaddafi na kuongeza "Baraza hili liliundwa na magaidi".

Gaddafi alisema kuwa baraza hilo liliundwa na mataifa makubwa na limetumiwa kuziporomosha nchi ndogo akitoa mfano wa vita vya Iraq, Afghanistan na Korea na Vietnam.

Kuna wakati Gaddafi alitaka kukichana kitabu cha bluu cha mkataba wa Umoja wa Mataifa lakini alisita baada ya kuona viongozi wa dunia wameduwaa kwa mshangao.

Gaddafi ambaye alitambulishwa kama kiongozi wa mapinduzi, rais wa umoja wa Afrika na mfalme wa wafalme wa Afrika alitetea haki za waafrika kwenye baraza hilo akitaka nchi za ulaya zilipe fidia ya dola trilioni 7.7 kwa nchi za Afrika kwa kuzitawala kikoloni.

"Mataifa ya Afrika yana haki ya kwenda popote pale na kudai dola trilioni 7.7 zilizoibwa toka Afrika", alisema Gaddafi.

Gaddafi alimalizia hotuba yake kwa kulitaka baraza la umoja wa mataifa kuchunguza sababu zilizopelekea kunyongwa kwa Saddam Hussein, kutupwa jela nchini Marekani kwa rais wa zamani wa Panama,Manuel Noriega na kuuliwa kwa rais wa zamani wa Marekani John F Kennedy pamoja na aliyekuwa mpiganiaji wa haki za watu weusi Marekani, Martin Luther King.

Naona kama paragraph inejirudi vile, au ni mambo ya copy and paste watachambua wenyewe?
 
"How can we be happy about the world security if the world is controlled by four or five powers?" he complained. "We are just like a decor."
-Gaddafi
 
Gadaffi afyatuka, ataka Afrika ilipwe fidia


RAIS wa Libya Muammar Gadaffi, amesema, wakoloni walioitawaka Afrika waliiba rasilimali na malighafi hivyo bara hili linastahili fidia ya dola za Marekani trilioni 7.7.

“Umefika wakati kwa nchi za Afrika kulipwa fidia kutokana na wingi la rasilimali zake kuibiwa katika miongo mingi iliyopita wakati wa utumwa na utawala wa kikoloni,” amesema Gadaffi leo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Afrika (AU) amezikosoa nchi tajiri duniani zinazoendele kutawala kwa mbinu mbalimbali.

Amesema, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Urusi zina nguvu kubwa na mamlaka dhidi ya mataifa zaidi ya 190.

“Wanachama wote wa UN wanatakiwa kuwa sawa, lakini kuna baadhi ya nchi zimejitwalia kinachoitwa nguvu na kutawala nchi zingine,” amesema.

Gadaffi amesema, yanahitajika mabadiliko UN yakiwemo ya mfumo ili kubadilisha tabia ya baadhi ya nchi kuwa na haki ya kutawala na kuzionea nchi nyingine.

Kiongozi huyo ametaka kuwe na demokrasia katika Baraza la Usalama la U, N na kwamba, Afrika inastahili kuwa na angalau kiti ndani ya baraza hilo.

Ameshauri Makao Makuu ya UN yahamishwe kutoka New York, yawe katika eneo ambalo ni la katikati kama vile Geneva, Uswisi.

“Kwa nini baadhi ya wajumbe walazimike kusafiri kwa zaidi ya saa 20 kwenda Makao Makuu. Wakifika hapa wanakuwa wamechoka hata kufanyakazi na wanaishia kulala badala ya kuchangia majadiliano,” amesema Gadaffi.

Awali, Rais wa Brazil Louis Ignacio Da Silva, alitaka kuwapo kwa ushirikiano wa uchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya sawa katika maeneo yote duniani.

Amesema,UN inahitaji mfumo mpya iweze kukabiliana na changamoto za karne ya 21 katika maeneo ya uchumi, siasa, na kijamii.
 
HOTUBA YA KIONGOZI WA MAPINDUZI M/KITI WA AU MUAMMAR GADHAFI MBELE YA JUMUIYA KUU YA UMOJA WA MATAIFA.
23-09-2009


Kiongozi ameanza kwa jina la Allah,nakutoa salamu kwa wajumbe wa jumuia kuu ya umoja wa mataifa kwa niaba ya Umoja wa Afrika,nakuelezea matarajio yake ya kikao hicho kuwa cha kihistoria katika maisha ulimwenguni.Na kwa niaba ya jumuia kuu ambayo inaongozwa na Libya ,kwa niaba ya umoja wa Afrika ,kwa niaba ya Mamlaka elfu moja ya kifalme ya kijadi ya Afrika ,na kwa niaba yenu nyote ….natoa pongezi kwa mtoto wetu raisi "Obama"
Kwa mara ya kwanza kuhudhuria kikao cha jumuia kuu akiwa raisi wa Marekani ,na tunampongeza kwa nchi yake kuwa mwenyeji wa kikao.
Kikao kinafanyika tukiwa tunakabiliwa na changamoto kadhaa ,ambazo zinahitaji dunia kushikamana pamoja ili kuzishinda kwani zinatukabili sote:
"Changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ,tatizo la fedha au kuporomoka kwa uchumi wakibepari,tatizo la chakula duniani na maji,Jangwa ,Ugaidi,Uhamiaji,Kusambaa magonjwa yanayotengenezwa na binaadamu na yale yasiotengenezwa,kwani baadhi ya vimelea vimetengenezwa kama silaha zakivita kasha wakashindwa kuvidhibiti. Huenda mafua ya nguruwe ni miongoni mwa vimelea vilivyotengenezwa katika maabara kama silaha ya kivita kisha vikashindikana kudhibitiwa. Vilevile kusambaa kusikokawaida kwa silaha za nuclear,
Ugaidi,Unafiki,Woga,Kufuru,Kuporomoka kwa maadili na fedha kutawala.Mambo haya yote yanajenga adui mmoja kwetu sote.
Ndugu zangu :
Mnajua kama Umoja wa Mataifa uliundwa na nchi tatu au nne dhidi ya Ujerumani …huu ndio Umoja wa Mataifa, na sio Shirika la Umoja wa Mataifa.
Shirika la umoja wa mataifa ambalo sisi tumo sasa hivi ni kitu chengine ,ama umoja wa mataifa ni yale mataifa yalioungana dhidi ya Ujerumani wakati wa vita ya pili ya Dunia,nchi hizo ndio zilizounda baraza na kuliita Baraza la Amani,nakujipatia viti vya kudumu na kura ya turufu.
Sisi hatukuwepo,mataifa yakatengwa,wakatutaka tuvae nguo hii ambayo walijitengea nchi hizi tatu au nne zilizoungana dhidi ya Ujerumani.
Huu ndio ukweli,na huu ndio msingi wa shirika hili lakimataifa.
Hayo yametokea nje ya nchi "165" hii ni asilimia "1" kwa "8",alihudhuria mmoja wanane hawapo.Hao ndio waliotengeneza hati mnayoisoma-hati ya umoja wa mataifa-utangulizi mwengine na yaliomo ni mengine kabisa. Vipi mambo haya yanakua ?!
Mwaka 45 waliohudhuria Sanfransesco walishiriki kuweka utangulizi,wakawacha vipengele vyengine vikiwemo vile vidogo vya ndani vinavyoitwa baraza la amani,kwa wataalamu na mabingwa na wanasiasa wanchi zinazojihusisha na mambo haya,ni zile nchi zilizotengeneza baraza la amani,na nchi zilizoungana dhidi ya Ujerumani.
Utangulizi unavutia sana wala haupingiki,lakini yaliokuja baadae yote yanakwenda kinyume na utangulizi,na haya leo ndio tunayapinga nakuyakataa,na hayumkiniki kuendelea kwani wakati wake umepita katika vita ya pili ya dunia.
Utangulizi wasema Mataifa yote ni sawa makubwa na madogo. Je viti vya kudumu tuko sawa?abadan,hatukosawa.
Utangulizi wasema katika umoja wa mataifa mataifa yapo sawa katika haki. Nzuri…..je haki ya kura ya turufu tupo sawa ?! hivyo "veto" ni dhidi ya hati,na viti vya kudumu ni dhidi ya hati,haya hatuyatambui na hatuyakubali.
Utangulizi wasema " tunajidhatiti kutotumia nguvu za silaha bila ya maslahi ya pamoja "…tulifurahi kwa hili,na tukatia saini na tukajiunga katika umoja wa mataifa kwa msingi huu,lakini badala yake kumetokea vita 65 baada ya kuanzishwa umoja wa mataifa na baada ya kuanzishwa baraza la amani kwa mtindo huu ulio,na baada ya mkataba huo wahanga wake ni mamilioni na zaidi ya vita vya dunia. Je vita hivi na nguvu zilizotumika katika vita 65 ni kwa maslahi ya pamoja?!abadan…..ni kwa maslahi ya dola maalumu mbili au tatu-tutavitazama vita hivyo kama ni kwa maslahi ya pamoja au dola maalumu-Huu ni mkanganyiko wa utangulizi wa hati ambayo tumeikubaki nakujiunga na shirika hili. Ikiwa mambo hayaendi na utangulizi ambao tumeukubali basi hata kuwepo kwetu katika shirika hili hakutoendelea kuanzia sasa.sisi hatumfurahishi mtu,hatuzungumzi kwa diplomasia,hatuogopi,hatunatamaa,wala hatumfurahishi mtu dhidi ya hatma ya Ulimwengu.Tunazungumzia hatma ya Dunia na wanaadamu…na kwa hali hii hapa hakuna diplomasia wala unafiki kwani woga unafiki na mapuuza yamepelekea kutokea vita 65 baada ya kuundwa umoja wa mataifa.
Utangulizi wasema"endapo nguvu itatumika lazima iwe yakimataifa,nguvu ya pamoja "…sio nchi moja au mbili ama tatu…ni umoja wa mataifa ndio unaamua kutumia nguvu ili kulinda amani ya dunia. Endapo dola moja itaipiga nyengine baada ya mwaka 1945,baada ya kuanzishwa shirika hili ,basi umoja wa mataifa kwa pamoja itaurudi uadui huo.yaani kwa mfano Libya itaipiga Ufaransa –ni juu ya umoja wa mataifa kuurudi uadui wa Libya kwani Ufaransa ni dola huru na mwanachama wa jumuia kuu ya umoja wa mataifa na nchi yenye mamlaka.
Tunatakiwa kutetea mamlaka ya mataifa kwa pamoja,lakini vita 65 vimetokea bila ya umoja wa mataifa kuvirudi,-vita vinane vya nguvu vikatokea wahanga wake ni mamilioni –na nchi kuu zenye viti vya kudumu na veto hazikufanya kitu.Nchi tulizokua na matumaini nazo kuleta amani na utulivu wa mataifa ndizo zilizohatarisha utulivu wa mataifa na pia kutumia nguvu za ziada.Tulidhania zitaleta utulivu na kulinda mataifa na amani duniani,lakini zikatumia maguvu huku zikijitanua na kura ya turufu na viti vya kudumu.
Katika hati hii hakuna eneo linalouruhusu umoja wa mataifa kuingilia mambo ya ndani yaliochini ya mamlaka ya ndani ya dola,kwa maana mfumo wa utawala ni mambo ya ndani ya dola husika,hakuna haki ya kuingilia katiikiwa mfumo wako ni wakidikteta au democrasia au ujamaaa au ubepari au ukandamizaji au songambele,hilo ni jukumu la jamii husika…ni swala la ndani.
Kuna wakati Roma ilipiga kura yakumfanya "Yulious Qaisar"kuwa diktete na baraza la wakongwe likatoa baraka zake kwa kuona udiktete wakati huo utaleta manufaa kwa Roma…ni swala la ndani nani atasema kwanini waroma walifanya hivyo ?!.
Utangulizi ni kitu tulichokubaliana nacho ama baada yake kuja mambo ya veto ambayo hayakutajwa katika hati,na laiti wangalituambia kuwepo kwa veto,tusingelijiunga katika umoja wa mataifa,tumejiunga kwa kuwa tu sote tupo sawa katika haki.Lakini kutokea dola moja inahaki yakupinga maamuzi yetu yote na ina kiti cha kudumu ,na nani hasa aliempa kiti cha kudumu ?! Ni nchi moja tu tulioipigia kura katika jumuia kuu ili iwe na kiti cha kudumu katika baraza la amani nayo ni China. Ni nchi pekee iliopo hapo kidemocrasia lakini nchi nne zilizobakia hazipo kidemokrasia,bali zipo hapo kidikteta ,nasi hatuzitambui.
Marekebisho ya umoja wa mataifa-ndugu zanguni-sio kwa kuongeza viti. Kuongeza viti kunazidisha matatizo"dongo linajaa maji"-sijui mkalimani katafsiri vipi-ni vigumu kutafsiri kwa kiingereza,nitasaidia :"to add insult to injury",nikimaanisha kuzidisha zaidi matatizo,vipi ? kwani huko ni kuongeza dola kubwa katika kubwa nyingine zinazotusumbua nakutufanya zitusumbue zaidi.
Hivyo tunapinga ongezeko la viti kwa mtindo huu. Suluhisho si kwa kuongeza viti,na hatari zaidi ni kule kuongeza nchi kuu nyengine….huku ni kukandamiza mataifa ya ulimwengu wa tatu,na mataifa madogo yanayunganisha "g.100"…kuna nchi 100 ndogo zimejikusanya katika jumuia moja ya "forum of" "ffs 100.g"…"100.states…"small states". Nchi hizi zitapondwa pondwa na viti vipya,hili tunalipinga kwa nguvu zote na mlango huu ufungwe.
Kufungua mlango huu wa kuongeza idadi ya viti vya baraza la amani kutazidisha chuki na wasiwasi duniani ,na ushindani kwa viti hivyo,na kuwepo mashindano kati ya makundi muhimu sana ya nchi. Kutakua na mashindano kati ya Italia,Ujerumani,Indonesia,India,Pakistani,Phillipins,Japani,Brazili,Argentina,Nigeria,Algeria,Libya,Misri,Congo,Afrika kusini,Tanzania,Uturuki,Irani,Ugiriki,Ukrain.
Nchi zote hizi zitataka kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la amani,mashindano haya yataendelea hadi idadi ya wajumbe wa baraza la amani itakua sawa na idadi ya wajumbe wa jumuia kuu,si jambo lakiutendaji.hivyo suluhisho ni nini?
Suluhisho lipo kwa jumuia kuu chini ya uraisi wa " Ali Treki"ambalo litachukuliwa maamuzi kwa kupigiwa kura,na maamuzi ya lazima katika jumuia kuu ni ya wengibila kutazama upande wowote ule,nayo ni kufungwa mlango wa ujumbe kwa nchi,na kufungwa mlango wa ongezeko la viti vya baraza la amani-maoni haya yapo kwa jumuia kuu ,katibu mkuu ,na Treki- ,na pahala pake kuchukuliwa na uwakilishi wa miungano,na kuleta demokrasia ya usawa kati ya nchi wanachama,na kupeleka uwezo wa baraza la amani kwa jumuia kuu.
Uwakilishi uwe kwa miungano na sio nchi,ili kuondosha ushindani wakunyakua kiti kwani kwa mujibu wa utangulizi hiyo ni haki ya kila nchi kwani nchi zote ni sawa…vipi uizuie ? nani ana haki yakuzizuia nchi hizo ?!nani mwenye uwezo wakuiambia Italia isigombee kiti pale Ujerumani itakapopewa ?Italia itasema mimi ni bora zaidi kwani niliungana na washirika ,ama Ujerumani alikua ni adui na kushindwa mathalan-ni Ujerumani ya zamani ya wanazi sio ya sasa – India nayo ikipewa kiti Pakistani itapiga kelele…nchi hizi ni za nuclear ,zipo katika hali yakivita,ni hatari. Japani tukimpatia,kwa nini Indonesia dola kuu ya kiislamu duniani isipewe?! Kasha nini tutasema kwa Irani ,Ukrain ,Brazili ,Argentina na Libya ambayo imefunga mpango wake wa silaha za nuclear nayo inastahiki kiti cha kudumu katika baraza la amani kutoka na kusaidia amani ya dunia.?! Inafuatia Misri, Nigeria ,Algeria ,Congo ,Afrika kusini na Tanzania zote hizi ni nchi muhimu.
Huu mlango lazima ufungwe ,wazo la upanuzi wa baraza la amani ni hadaa tupu,vipi tutarekebisha umoja wa mataifa kwa kuingiza dola kubwa nyingine ndani ya kuu zilokuwepo zikitutatiza?! Hivyo suluhisho ni kuleta usawa katika ngazi ya seneti ya dunia ambayo ni jumuia kuu ,nakunyakua uwezo wa baraza la amani na kuupeleka katika jumuia kuu,hapo baraza la amani kuwa chombo cha kutekeleza maamuzi ya jumuia kuu basi.
Haya ndio mamlaka kisheria….hawa ndio watunga sheria wa jumuia kuu.
Kilichoandikwa ni "jumuia kuu inatekeleza kadhaa wa kadhaa kwa mujibu wa maelekezo na amri ya baraza la amani" hili ni kosa ,sahihi ni hivibaraza la amani litatekeleza kadha wa kadhaa kwa mujibu wa maelekezo na amri ya jumuia kuu.. huu hapo ummah 190….huu ndio umoja wa mataifa na sio baraza la amani lililopo katika chumba cha jirani ,watu kumi ..ni demokrasia gani hii ?vipi tutachunga anani ya dunia iwapo ipo chini ya rehema za watu kumi,na nchi nne au tano,au nchi moja,nasi mataifa 190 tukiwa kama pambo la botani ya "haiden park" ?!!
Wamekufanyeni kama picha tu…nyinyi ni "haiden park"…nyinyi hamna thamani …ni membari ya kutolea hotuba tu , mfano wa hotuba zinazotolewa katika bostani ya "haiden park"….hapo unatoa hotuba yako kesha waondoka,hawa ndio nyinyi.
Baraza la amani ni mtekelezaji tu wa maamuzi yanayotolewa na jumuia kuu ya umoja wa mataifa,wakati baraza la amani litapokua mtekelezaji wa maamuzi ya jumuia kuu …katika hali hii hakutokuwepo mashindano ya kuwania viti vya baraza hilo.Baraza la amani liwe muwakilishi wa mataifa yote na sio dola,wazo lililopo sasa mbele ya jumuia kuu ni kuwepo kiti kwa kila umoja…kila muungano…:
-Umoja wa ulaya nchi 27,uwe na kiti cha kudumu katika baraza la amani.
-Umoja wa Afrika nchi 53,uwe na kiti cha kudumu katika baraza la amani.
-Umoja wa nchi za marekani ya latinia ,uwe na kiti cha kudumu katika baraza la amani
-Asian nchi 10+2au+3 au+4,kiti cha kudumu katika baraza la amani.
-Umoja wa Urusi,upo hivi sasa ,kiti kimoja cha kudumu katika baraza la amani.
-Muungano wa Marekani nchi khamsini UNITED STATES OF AMERICA''''Tayari inakiti cha kudumu "already"
-Sarc,ipo njiani ikisimama,nayo kiti cha kudumu katika baraza la amani.
-Jumuia ya nchi za kiarabu nchi 22,kiti cha kudumu katika baraza la amani.
-Umoja wan chi za kiislamu nchi 45,kiti cha kudumu katika baraza la amani.
-Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote nchi 120,kiti cha kudumu katika baraza la amani .
-Tuna "G.100" tunaifikiria inawezekana kwa dola ndogondogo "Forum of small states"FSS kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la amani.
Kukiwepo dola nje ya miungano hii nilioitaja,kunawezekana kuwepo kiti cha kudumu kwao na kupokezana kila baada ya miezi sita au kila mwaka .Huenda Japan au Australia au Newslander zikawa nje ya umoja wowote ule,uwe wa Asiana,Urusi, Afrika, Ulaya,Marekani ya kusini au Marekani ya kaskazini ,inawezekana kupatiwa kiti .Hili ndilo suluhisho lililombele yenu…lipo mbele ya jumuia kuu linahitaji kupigiwa kura.Hili ni swala nyeti na la msingi kabisa,lipo mbele ya jumuia kuu ambayo ndio yenye mamlaka duniani…hiyo ni bunge la dunia…ni seneti ya dunia,hakuna anaeipinga wala hatumkubali yeyote yule nje ya Ukumbi huu,sisi ndio Umoja wa mataifa.
"Ali Treki" na "Kin Mon"wataweka michakato ya kiuendeshaji na kikanuni ,kuunda kamati zitakazosimamia upigaji kura huo,baraza la amani kuanzia sasa litawakilishwa na mimoja na miungano.
Huu ni uadilifu na demokrasia,nakukomesha baraza hilo kudhibitiwa na dola maalumu…dola moja inamiliki bomu la nuclear,moja ina nguvu za uchumi,moja ina Teknolojia na nyengine inamiliki mbinu zakiufundi…huu ni Ugaidi.Hatuwezi kuishi katika baraza linalomilikiwa na wenye maguvu…huu ni ugaidi,tukitaka kuishi katika dunia yenye amani na salama tutekeleze haya,ama mkitutaka tuishi katika ugaidi basi na iwe hivyo tuishi katika mivutano hadi kiama.Viti hivi ima vyote view na kura ya veto au vyote visiwe nayo kabisa.Baraza la amani kwa mtindo huu mpya ima kila umoja uwe na veto au veto ifutwe kabisa.
Hili ndio Baraza la Amani la uhakika.Muundo huu mpya wa baraza la amani unaotakiwa kupigiwa kura na jumuia kuu ndio utakaokua chombo cha utekelezaji cha jumuia kuu ya umoja wa mataifa. Mamlaka yapo kwa mataifa…mataifa 190 yaliopo hapa….hapo mataifa yote yatakua sawa ndani ya baraza la amani kama hali ilivyo ndani ya jumuia kuu.Katika jumuia kuu sauti zetu zipo sawa na vivyo hivyo tuwe sawa ndani ya chumba cha jirani yetu ambacho ni baraza la amani.Ama dola moja kuwa na veto na nyengine haina,nyengine kuwa na kiti cha kudumu na nyingine haina…hali hii imefutwa kuanzia sasa,hatuitambui hata ikiwepo.na maamuzi yoyote yatakayotolewa na baraza la amani kwa mtindo ulio sasa hatutoyakubali.Sisi tulikua tumetawaliwa ,tulikua chini ya himaya,tumepata uhuru na tumeungana tunataka kuchukua maamuzi ya dunia kwa njia yakidemokrasia itakayolinda amani na utulivu wa dunia kwa mataifa yote na wote kuwa sawasawa mkubwa na mdogo.
Ugaidi sio wa Alqaida pekeee hali ilivyo sasa ni ugaidi pia.Wingi ndio utakaokubalika katika jumuia kuu pekee na sio upande mwengine wowote,na jumuia kuu ikilikubali wazo hili litafanyiwa kazi na hakuna atakaepinga akidai kuwa yeye yupo juu ya jumuia kuu,na ataedai hivyo atoke katika umoja wa mataifa na abakie peke yake.Demokrasia sio kwa mwenye maguvu,au tajiri au gaidi anaetutisha…kuwa na neno la mwisho.neno la mwisho ni kwa mataifa tena wote kwa usawa.
Baraza la amani hivi sasa ni la makabaila….wanasiasa wenye viti vya kudumu,wanalitumia kwa kujilinda dhidi yetu,hivyo hili si baraza la amani bali ni baraza la kutisha.Ndugu zangu natumai mnawaona pale wanapokua na maslahi yao dhidi yetu wanalitumia ,wakiwa hawana maslahi yao dhidi yetu wanalipuuza,na wanapokua na maslahi yao dhidi yetu huitumia na kuitakasa hati ya umoja wa mataifa,nakukitafuta kifungu cha saba kuyakomoa mataifa masikini au ummah huu,ama wakitaka kufanya kitendo kinyume na hati hiii hujifanya kama haipo wala hawaitambui.
Nchi kuu zina maslahi kadhaa duniani ,wanatumia veto na baraza la amani na nguvu za umoja wa mataifa kulinda maslahi yao…mtindo huu umetishia nchi za ulimwengu wa tatu,ulimwengu wa tatu sasa upo katika vitisho.Baraza la amani tangu mwaka 1945 lilipoanzishwa hadi leo hii halijatupa amani,bali limetupatia adhabu na vitisho..linatumiliwa dhidi yetu basi..hivyo sisi hatulazimiki kulitii na maamuzi yake kuanzia hotuba hii ya arubaini.Vita 65 dhidi ya ulimwengu wa tatu vimezuka baada yakutiwa saini uanzilishi wa baraza hili ..dhidi ya dola ndogo..ima kupigana wenyewe kwa wenyewe,ama nchi kubwa kuipiga ndogo,wala baraza la amani halijasimama kuzuia uadui huo unaopingana na hati kuu..
Jumuia kuu itapigia kura suluhisho hili lakihistoria,baada ya hapo ima tuendelee pamoja katika umoja mmoja,au tugawike pande mbili: Mataifa yaliosawa yenye baraza lao wote wakiwa sawa,na wakubwa wenye viti vya kudumu na veto wakiwa katika baraza lao la watu wane au watano au watatu,kama watakavyo,nasi hatupamoja nao,wazitumie veto zao dhidi yao wenyewe,sisi hatujali,wabakie na viti vyao vya kudumu,hatujali,wakudumu ni Allah.Sisi hatujawapa cheo hicho natutakua wajinga mno kufanya hivyo kuyapa mataifa Fulani veto na viti vya kudumu na mataifa mengine kuyaita mapumbavu na yachini hayana sifa hiyo,kwa nini tuyadokeze mataifa?!.
Mataifa haya ndio mama wa dunia nayo ni 190.Mnajua kutokea kupuuzwa maamuzi ya baraza la amani baada ya kutambulika udhalimu dhidi yetu tu nasio dhidi ya mataifa makubwa.Hivyo ni baraza linalotumika dhidi yetu sisi,baadae maamuzi yanayotolewa huwa vichekesho na kupuuzwa ni dharau kwa umoja wa mataifa,na kazi zimekua zikifanywa nje ya umoja wa mataifa :uadui na vita,kukiuka mipaka ya nchi huru na mamlaka yake,kufanya uharamia wakivita na mauaji ya halaiki dhidi ya hati kuu,baraza la amani likiwepo…hawaliheshimu kabisa. Jambo muhimu zaidi ni kwamba kila makundi yakimataifa yamekua yakiunda baraza lao la amani ili wajadili maswala yao yanaowahusu,kidogokidogo baraza hili la sasa litakimbiwa nakususiwa :
-Umoja wa Afrika una "mas"baraza la amani na ulinzi Afrika.
-Umoja wa ulaya utaunda baraza la amani.
-Asian itaunda baraza la amani.
-Marekani ya kusini itaunda baraza la amani.
-Nchi zisizofungamana na upande wowote"dola mia na ishirini"zinawazo lakuunda baraza la amani.
Hii inamaanisha kuwa baraza la amani limetukosesha uaminifu,amani na hivyo tukageukia mabaraza ya kikanda.kwa mtindo uliopo sasa hatulazimiki kulitii baraza hili ambalo hatukushiriki kuliunda,muundo wake ni wakidikteta,wakiukandamizaji,nahakuna awezae kutulazimisha kubaki katika baraza hili au kutii amri zake.
Ndugu zangu Umoja wa mataifa hauzingatiwi…jumuia kuu ambayo ni msingi wa umoja wa mataifa haithaminiwi,na haina athari katika mwenendo wa dunia,amani ya dunia na haina maamuzi yoyote ya lazima.
Mahkama yakimataifa maamuzi yake ni kwa nchi ndogo na za ulimwengu wa tatu,na maamuzi hayo yaheshimiwi na nchi kubwa.mbele yangu kuna hukumu zilizotolewa na mahkama yakimataifa,na nchi nyengine zikakataa kuzitekeleza.
Shirika lakimataifa la nishati ya nuclear ni taasisi nyeti ya umoja wa mataifa ,nchi kubwa haziitii,punde tukang`amua kumbe ipo dhidi yetu sisi tu.Ikiwa ni taasisi yakimataifa hivyo itiiwe na dola zote,ama ikiwa sio yakimataifa nasi twaifungia milango yetu,nahatuitambui kuanzia sasa…kutoka hotuba hii ya arubaini.Na "Ali Treki"aliepo jumuia kuu atamuita mkurugenzi wa nishati ya nuclear "Al baradei"na wa kabla yake wamuulize iwapo anakagua malimbikizo ya nuclear ya dola zenye nishati hiyo na ongezeko au punguzo la malimbikizo hayo.?Akijibu ndio ,nasi tutaitii taasisi hiyo ama akisema la mimi sinauwezo wakuzikagua nchi hizo wala haziitii taasisi hii …basi nasi usitukaribie vivyo.
Nataka mjue wakati wa tatizo la bomu la nuclear la Libya ,mimi nilimuita mkurugenzi wa zamani "Al baradei" nikamuuliza mikataba ya kupunguza silaha za nuclear iliofikiwa na dola za nuclear ,hivi unaifuatilia?je wamepunguza?iwapo kuna nchi imeongeza au kupunguza unazifuatilia kwa karibu na unafahamu?akanijibu ,"abadan, nchi hizo kubwa sinauwezo wakuziuliza wala hatuzikaribii".
Hivyo umetujia sisi tu ,toka.hii si taasisi yakimataifa ni panga tulioelekezewa.
Taasisi ya nuclear ipo dhidi yetu.
Mahkama ya kimatifa ipo dhidi yetu kwa maslahi yao.
Baraza la amani lipo dhidi yetu.
Huu si uadilifu…hili si baraza letu…haya tunayapinga.
Kwa Afrika – Dk Ali Treki – iwe wamerekebisha umoja wa mataifa au hawajarekebisha,na hata kabla yakupigiwa kura wazo lakihistoria niliolitoa mbele ya jumuia kuu,Afrika inataka kiti cha kudumu na uwezo wote ndani ya baraza la amani ikiwa ni haki yake kwa yaliolikumba kale,hata iwapo swala la marekebisho ya umoja wa mataifa halijazungumzwa.
Afrika ni bara lilikuwa chini ya ukoloni,limetengwa,walilifanya kama mnyama,wakalitazama kama watumwa ,baadae wakaliweka chini ya himaya zao.Bara hili…Umoja wa Afrika…linastahiki kiti cha kudumu kama China ,wala swala hili halihusiani na marekebisho ya umoja wa mataifa.hii ipewe kipaombele…mbele ya jumuia kuuwala hakuna wakupinga kwamba umoja wa afrika kuwa haustahiki kuwa na kiti cha kudumu.Mwenye hoja aseme sasa hivi ,hakuna wakujibu.
Tumetoa wazo katika jumuia kuu la kulipwa fidia nchi zilizokuwa chini ya ukoloni,kwa nini? Ili ukoloni usirejee,na uporaji wa mali asili za watu usirudiwe,wala uhamiaji wa wale walioporwa mali zao kwenda katika nchi zilizowapora. Kwa nini waafrika wanakimbilia ulaya?na pia waasia ?na kwa nini wamarekani ya kusini wanakimbilia ulaya?!kwa sababu ulaya iliwaweka chini ya ukoloni wakachukua dhahabu,fedha,almasi ,shaba,chuma ,ureniamu na madini yenye thamani,vyote ,petroli ,matunda, binaadamu na wanyama.Leo kizazi kipya cha Afrika ,Asia na Marekani ya kusini wanazikimbilia mali zao zilizoporwa,wanahaki,nasi tumeshindwa kuwazuia.Mimi ninapowazuia wahamiaji wanaoelekea ulaya katika mipaka ya Libya,nikiwauliza mnaenda wapi?wanasema wanafuata mali zao zilizoporwa,turejeshee tutabaki hapa,nani awarejeshee?warejesheeni…wekeni maamuzi yakurejesha mali zao ,uhamiaji utasita.turejesheeni kuanzia Philipins hadi marekani ya kusini ,Moritious na India.
Afrika malipo yake ni trilioni 777,na itadai malipo haya kwa nchi iliozikoloni.Hakuna uhamiaji wa walibya kwenda Itali kutokana na Itali kukubali kuilipa fidia Libya kwa kipindi cha ukoloni na pia kuiomba radhi,nchi mbili hizi zikatia mkataba wakusahau yaliopita na kukubaliwa na wananchi wa Libya na Italia.Italia ikakiri kuwa ukoloni ulikua kosa na hautorejea tena.
Italia imekubali kutoruhusu shambulizi dhidi ya libya iwe la nchi kavu,baharini au angani na kupitishwa na bunge la Italia,Italia italipafidia ya miaka 20 ilioikalia Libya …kila mwaka italilipa Libya robo bilioni,na ujenzi wa hospitali ya uungaji viungo kwa raia walioathiriwa na mabomu ya ardhini yaliotegwa na Italia au kwa sababu ya vita ya kwanza nay a pili ya dunia.Ni Italia ilioandika historia wakati wa "Balaskoni"lazima awe kigezo na wenzake waliolifikisha swala hili panapohusika.
Ulipaji fidia utazifanya nchi za ulimwengu wa tatu pale zitakapokua na nguvu zikifikiria kuzitawala nchi nyengine dhaifu,zitawaza kwamba nasi tutakuja kudaiwa fidia hivyo zitarudi nyuma,hii ndio hatua itayokomesha ukoloni.
Kina kitu chengine nitakigusia ambacho ni nyeti nacho ni kuwa "bila shaka sisi na hasa waafrika tumefurahi sana kuwa mwana wa afrika anatawala Marekani ,ni tukio lakihistoria,kuna wakati mtu mweusi alikua haingii mgahawa ulio na mtu mweupe…wala gari yenye kupanda weupe,leo wamarekani kwa hamasa kubwa wamemchagua "Obama"kijana mweusi mkenya muafrika awe raisi wa Marekani.twatarajia huenda ukawa mwanzo wa mageuzi,nae amekuja na kaulimbiu ya mageuzi.
Kwangu mimi Obama ataendelea kwa miaka mine au minane baada ya hapo nani ataidhamini Marekani ?je "Ali" au "Kin Mon"mnaweza ?! hakuna awezae.
Tungelifurahi kama daima Obama angalikua raisi wa Marekani,hotuba yake alioitoa sipingani nae,anatofautiana kabisa na maraisi wa marekani waliopita,wao walikua wakisema:tutakumwagieni risasi,mabomu ambayo hata tafsiri hayana ambayo ni "massif ordenance benetraite"- tutakuleteeni kimbunga cha mvua za joto,radi,waridi lenye sumu kwa watoto wa Libya mwaka 86"hii ilikua mantiki yao,pale wasimamapo juu ya membari.walikua wakitisha dunia.wakisema tutakufanyeni kama vile Vietnum au Iraq au Misri mwaka 56-pamoja na marekani kuwa kinyume na operesheni ya alfaris wakati huo- au waridi la sumu "aldorado""kat noy"alilopeleka Regani kwa watoto wa Libya mwaka 86"
Tazameni raisi wa dola kuu ambayo twategemea kuurudi uadui dhidi yetu anasema" atapeleka waridi la sumu kwa watoto wa libya ,atakaelinusa atakufa". Ni lipi hilo waridi la sumu?ni bomu la leza likibebwa ndege za kivita f-111.
Walikua wakisema tutaiendesha dunia na atakatupinga tutamuadhibu,atake asitake"maneno aliozungumza motto wetu Obama ni tofauti na yanatoa wito wa kuondokana na silaha za nuclear kikweli,tunampongeza.anasema marekani haiwezi kutatua matatizo ya dunia pekee,dunia itatue matatizo yake.amesema "hali ya kuja hapa kuhutubia kasha kuondoka isiendelee",kitu hiki tunakiwafiki.amesema "umoja wa mataifa daima umekua membari ya tofauti,tunakutana ili kuhujumiana" ni sahihi lazima likomeshwe hili na sote tuwe katika taasisi za kimataifa kwa usawa ili nyoyo zitulie.
Amesema "demokrasia hailazimishwi kutoka nje"wakati raisi wa marekani karibu tu,alisema "lazima tusimike demokrasia huko Iraq,na kwengineko..na kwengineko.."yeye kasema "hilo ni swala la ndani..dola inafanya demokrasia …kila mmoja na utamaduni wake aliorithi "sahihi maneno haya yalikua yamesahaulika.dunia sasa itazame kidogo juu ya nukta hii "dunia ya pande tofauti" hivi ni muhimu dunia yetu kuwa na pande tofauti?..mataifa yote ysiwe sawa ?tujibuni ?kuna mwenye jawabu ataesema ni bora kuwepo pande tofauti.kwa nini tusiwe mataifa yaliosawa pasi na pande tofauti,hivi ni muhimu kuwa na Batririk,mapop au waungu?!sisi twaishi katika ukandamizaji wa pande tofauti,tunaupinga mfumo huu,twataka dunia ilio sawa sote,wakubwa na wadogo.
Nukta nyeti ni juu ya makao makuu ya umoja wa mataifa…nyote mnatokea nyuma ya mabara na bahari…mmekata bahari ya atlantiki ,pacific ,bara la Asia ,ulaya na Afrika hadi kufika hapa kwa nini ?!hivi hii nyumba tukufu?hivi hii ni Vatican? Hivi hii ni Makka?!Nyote mmechoka na mmejaa usingizi,na wakati umebadilika na hata kifizikia…kuna alietumia saa 20 angani,baadae mnataka azungumzie juu ya hatma ya dunia,nyote mmelala,naona nyote mmechoka. Kwa nini taabu yote hii?kuna waliokua nchi zao zimelala wakati huu hivyo walikua walale sasa hivi,kuna waliomacho sasa hivi,mimi nimeamka saa kumi za alfajiri kwa saa za New York,kwa sababu Libya ni sawa na saa tano za mchana …kwa wakati huo nitakua nimechelewa kuamka nikiwa Libya na museme kwa nini tabu yote hii? Na kama jengo hili limewekwa tangu mwaka 45 hivi ni kuna ulazima wa kuendelea kubaki hapa na kutofikiria sehemu munasaba ya katikati. Hili ni moja.
Jengine na muhimu ni kwamba Marekani taifa linalosimamia ugeni huu inabebea majukumu ya kuhakikisha usalama wa makao ya Umoja wa mataifa, wajumbe wa kudumu na makumi ya maraisi wa ulimwengu wanaokuja kila mwaka katika makao haya. Ni usalama wa juu na gharama kubwa. Na kwa mimi nataka kuwapunguzia mzigo huu, nanyi pia wapunguzieni wamarekani mzigo huu na muishukuru New York kwa kazi iliyofanya kwa kipindi chote hicho na sasa tunaitaka Marekani ipumzike na jukumu hili.
Tujaalie atokee gaidi airipue ndege ya raisi au gari la raisi. Na mujue tu kwamba jengo hili (makao ya Umoja wa mataifa) linaangaliwa na Al-qaeda.
Tujiulize kwa nini halikupigwa siku katika tukio la septemba 11, ni jambo lilikuwa nje ya matakwa yao, pengine ndege iliyotenguliwa ilikuwa imeelekezwa kwenye jengo hili. Na bila shakashambulio lijalo limeelekezwa jengo hili. Na msione kwamba ninachozungumza kuwa ni upuuzi. Tunawafungwa wafuasi wa Alqaeda wapo magerezani na fikira zao ni mambo ya kimaujiza, jambo ambalo linaifanya Marekani iwe na wasiwasi mkubwa kwamba pengine mara nyengine mashambulizi ya ndege yataelekezwa kwenye jengo la Umoja wa mataifa. Na huenda makuni ya maraisi wakapoteza maisha kwa pamoja.
Kwa hivyo tunahitaji kuiondolea Marekani mzigo huu, na tuyaondoe makao haya kuyapeleka sehemu nyengine.
Baada ya miaka 50 inapaswa makao haya yahamishwe yapelekwe sehemu nyengine ya Dunia, miaka 50 hii ilikuwa upande wa magharibi mwa Dunia inatosha. Miaka 50 mengine iwe ni zamu ya kati au Mashariki na kubadilishana namna kama hivyo kila baada ya miaka 50.
Sasa ni maika 64 ambapo 14 imezidi muda unaopaswa.
Huku ni kuisaidia Marekani kuondokana na mzigo huu na tunaishukuru sana.
Hii ni ajenda inayohitaji kupigiwa kura katika mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa kwa sababu mada 23 ya makubaliano 47/7/26 yanasema kwamba haipaswi kuhamisha makao ya Umoja wa mataifa ila kwa maamuzi ya asilimia kubwa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa... hivyo asilimia 51% ikikubali kuondoshwa kwa makao haya basi yaondolewe.
Haipaswi tupate tabu kiasi chote hiki, kutoka india, Philippines, Australia na Visiwa vya Comoro kuja hapa, nashangazwa sana ndugu yangu raisi Ahmad ametumia masaa 14 angani kutoka Comoro wakimwita aje azungumzo kwenye baraza la Umoja wa mataifa. Vipi atahutubia wakati akiwa na machofu na hata nyakati zinatofautiana? Na kwamba Marekani imeweka sheria nzito katika mchakato wa safari kuja maerkani lakini yote tumeyavumilia, ni jukumu lake kwa sababu ipo katika hali ya hatari.
Lakini kwa nini tuje masafa yote haya kutoka mbali hadi New York?
Kuna raisi mmoja aliniambia kwamba msadizi rubani wake hawezi kuingia Marekani kwa sababu ana vipingamizi na kutoruhusiwa kuingia Marekani, Marekani ikisema kwamba ndege ije bila ya rubani msaidizi kwa madai kwamba silazima aje.
Na mwengine akaniambia akanisumulia kisa kama hicho, mwengine daktari wake nae haruhusiwi kuingia Marekani. Hivyo ni mambo magumu yanatukabili sisi viongozi wakuu wa nchi. Na kama kuna nchi ina matatizo na Marekani huwa inamtishia mjumbe wa nchi ile na ujumbe wake..upande huu unaruhusiwa kutembea hatua 50 na upande huu mwengine unaambiwa mita 500, sasa tumekuwa tupo katika gereza la Guantanamo?
Tunakutaka M/Kiti Dkt. Ali Treiki kulifuatilia jambo hili la kuhamishwa ka Makao ya Umoja wa Mataifa. Ikiwa asilimia 51% itakubali kuyaondoa makao haya tutapiga kura nyengine kujua ni wapi tuyahamishie kati, au Mashariki. Na tujaalie kama tuamue kuyaweka kati, basi kuna Sirte na Vienna tutazipigia kura. Tembea kilomita 1000 nje ya Sirte hakuna atakaekuzuia, na uje na milioni ya watu wako na hata bila ya Visa, madamu uko na Raisi njoo nao tu. Ni nchi yenye amani kabisa.
Libya ni nchi isiyo na uadui na yeyote, kadhalika Vienna sidhanii kama kuna vipingamizi kama hivi. Mwisho mtatushukuru kwa mapendekezo yetu haya kwa kukuondoleeni mzigo huu nasi tutapumzika kukuaa angani kwa masaa 14, 20, na 5 ili kuja hapa. Na wala sidhani kwamba Marekani itaacha kutoa mchango wake na haifai kudhania vibaya Marekani kwani ni nchi ya majukumu kwenye kitengo hiki cha kimataifa, haitokasirika wala kusema lolote. Bali itatoa shukrani za dhati.
Jambo jengine muhimu ambalo mkutano mkuu unapaswa kulifanyia uchunguzi chini ya Uenyekiti wa Dkt. Ali Treiki. Tutauhukumu Umoja wa Mataifa, ima uvunjwe au tuuanzishe upya kuondoa majukumu kwenye baraza la usalama na kupewa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa sababu hiki ni kikao kisicho cha kawaida kama alivyosema mwanangu “Obama” kabla ya mimi kwamba kikao hiki ni cha aina yake na cha kihistoria.
Kwanza natuangalia vita vilivyotokea baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa mataifa, kwa nini vita hivi vilitokea na baraza la usalama lilikuwepo wapi na Baraka la kuu pia nalo lilikuwa wapi na kwa nini vita hivi vitokee na hati ya kimataifa iko wapi.
Hapana budi bali kufanywe uchunguzi juu ya vita hivyo na kutolewa hukumu, kutokana na mauaji ya halaiki yaliyotoekea katika vita hivyo.
Tutaanza na vita vya Korea vilivyotokea baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa mataifa, kwa nini vita hivi vilipotea na mamilioni ya watu kupoteza maisha yao, na ilikuwa karibu kidogo yatumike mabomu ya nyuklia. Vita hivi bado vingalipo havijamaliza kwa sababu kuna mabaki ya mabomu yanayoripuka baada ya muda fulani. Hivyo kuna uwezekano mkubwa kutokea vita kama hivi wakati mwengine wowote na kuna uwezekano mkubwa wakutumika silaha za nyuklia.
Ni jambo la hatari mno, ni wajibu wetu kuwahukumu wote waliosababisha vita hivyo na hasara zake.
Baadae tunakuja kwenye vita vya Suise mwaka 56. Lazima kufanyike uchunguzi na kufunguliwa jalada, na kwanini nchi yenye kiti katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa na yenye kura ya veto inafanya hujuma dhidi ya nchi ambayo ni mwanachama wa Umoja wa mataifa, nchi yenye Mamlaka ya Misri ikiharibu miji yake na raia zake na jeshi lake na kuuawa maelfu ya wamisri kwa sababu ya kuufanya upenyo wa Suise kuwa ni wa taifa? Kwa hivyo kuna bima gani ambayo inaweza kutuhakikishia kwamba hili haliwezi kutokea tena?
Kadhalika tunakuja kwenye suala zima la vita ya Vietnam vilivyopoteza watu milioni 3. Vita ambayo ndani ya siku 12 yalitumika mabomu ziadi ya yale yaliyotumika miaka minne wakati wa vita ya Pili ya Dunia. Sasa vipi tuyanyamazie haya? Wakati baada ya vita ya pili ya Dunia tumekubaliana kwamba hakuna tena vita, leo vimetokea ndio tuviache vipite tu hivihivi? Ni masuala yanayohusu wanadamu vipi tuyanyamazie? Hili ndio bunge la ulimwengu ndio mwelekeo wa ulimwengu.
Suala jengine ni Panama, nchi ambayo ni mwanachama wa Umoja wa mataifa lakini waliuawa kiasi ya watu 4000, akakamatwa Raisi wake Noriega akiwa ni teka wa kivita, akahukumiwa na kufungwa nchi nyengine mbali na nchini mwake. Kivipi nchi kubwa iivamie nchi ndogo na kumkata Raisi wake na kumchukua na kumfunga kwenye gereza lake nje ya nchi yake? Vipi tukubali mambo kama haya?
Ni mambo ambayo kuna uwezekano yakatokea tena, na hatuwezi kuyanyamazia kimya na lazima yafanyiwe uchunguzi na Umoja wa mataifa kutokana na kitendo cha nchi kubwa ikatoka na nguvu zake za kijeshi kuivamia nchi ndogo isiyo na uwezo wowote.
Baada ya kusimama Umoja wa mataifa na kuunda baraza la usalama kwa viti vya kudumu na kura ya veto baadae unatokea uadui kwa nchi ya Grenada nchi mwanachama na kuuliwa raisi wake “Mores Bishop” kivipi mambo kama haya yapite kimyakimya na tupuuze maafa kama haya?
Kwa hivyo ni wakati wakutathmini vipi baraza hili linatufaa au la!
Kadhalika kuna suala zima juu ya mashambulizi ya Somalia nchi ambayo ni mwanachama wa Umoja wa mataifa wakati wa raisi Farah Aidid na baadae tuchunguze matokeo ya mashambulizi hayo, kwa nini? Na nani ameruhusu yafanyike?
Vilevile vita vya Yugoslavia, iliyokuwa imetulia ilibomolewa na Hitler na tunakuja sisi tunaibomoa tena kwa mara ya pili kama Hitler wa pili! Nchi hii ilijengwa na Tito lakini wanakuja Ma-Imperalia wanaibomoa kwa maslahi yao binafsi. Kivipi wengine tutakuwa na amani na mambo kama haya yanatokea kwenye zama za Umoja wa mataifa? Je nchi hii ya Yugoslavia inahatarisha nchi yeyote iel? Inapaswa uchunguzi ufanywe na Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa.
Kasha kuna vita vya Iraki, vilivyochukuwa uongozi, Umoja wa mataofa ufanye uchunguzi wa vita hivi chini ya usimamizi wa Baraza kuu la Umoja na uenyekiti wa Dkt Ali Treiki. Vita hivi vinajumuisha mambo manne makubwa na muhimu sana:-
Kwanza, vita hivi vimekuja kwa ukiukaji wa Hati ya Umoja wa mataifa. Bila ya sababu zozote za msingi nchi kubwa mwanachama wa kudumu wa katika baraza la usalama inaifanyia uadui nchi ndogo Iraki mwanachama katika Umoja wa mataifa. Kwa nini na kivipi ifikie hali kama hiyo? Na kwa nini hati ya kuzuia uadui haifanyi kazi yake?
Awali nimekusomeeni maandiko ya Umoja wa matiafa unavyopinga uadui na nitakutoleeni mfano:
“wakati Iraki ilipoivamia Kuweit, moja kwa moja walikuja na hati ya Umoja wa mataifa wakisema kuwa lazima Umoja wa mataifa uzuie uadui na sote tukakubaliana na nchi za jirani na Iraki zilishirikiana bega kwa bega kuzuia uadui wa Iraki nchini Kuwait, tukapigana kwa ushurukiano wa nchi ya kigeni kuzuia uadui kwa jina la hati ya kimataifa. Suala ni kwa nini Iraki ilippofanyiwa uadui ile hati haikufuatwa? Awali hati hii ilikuwa takatifu, lakini mara ya pili hati hii ikawekwa kwenye debe la takataka, wakaidharau kwa sababu wanataka kuivamia na kuifanyia uadui Iraki”
Hivyo tunahitaju kujua kwa nini Uadui huu kaukuzuiwa na ulikuja kwa sababu gani? Umoja wa mataifa yapaswa ufanye uchunguziwa kina kwa hili, ni jambo lisiloeleweka na pia linaweza kututokea hata na sisi.
Pili, baada ya uvamizi huo nchini Iraki, kumefanyika mauaji ya halaiki ambapo kiasi wa watu milioni moja na nusu wameuawa baada ya tafiti kugundua hilo, na sasa tuione hiyo mahakama ya kimataifa iwatoe wale waliohusika na mauaji ya halaiki iwatie makuchani mwake?
Ni rahisi tu kusema “Bashiri” akabidhiwe kwenye mahakama ya kimataifa, au “Slobodan” au “Tailer” au “Hebri” au “Noeriga”!! sawa kabisa, Vipi huyu aliongoza mauaji ya halaiki kule Iraki yeye asifikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa?, ikiwa mahakama hii imewekwa kwa ajili yetu tu, basi tunaikataa kwa nguvu zote! Inapaswa kila mmoja awe mkubwa au mdogo awe chini ya mahakama hii, endapo utfanya uovu ufikishwe tu, kwani sisi si wanyama kwenye gulio watuchinje wanavyotaka hata kwenye siku ya Eidi.
Nasi pia ni umma wenye haki ya kuishi kwa utashi kwenye ardhi hii, tupo tayari kupigana, kupambana ili tusiishi katika halikama hii na tujaribuni muone.
Jambo la tatu ni kuwanyonga mateka wa kivita nchini Iraki.. Vipi yamefanyika haya? Raisi wa nchi anayongwa ilhali amekatwa kama teka wa kivita? Wakati nchi iliyovamia Iraki ilitangaza moja kwa moja mara tu baada ya kumkamata kuwa wamemkamata teka wa kivita. Teka wa kivita hanyongwi wala hahukumiwi bali huwekwa kizuizini hadi operesheni itakapomalizika.
Nani amemnyonga Raisi wa Iraki? Jibuni suala hilo?, tunamjua nani amemnyonga... Hakimu anatambulikana, sura yake inatambulikana, utaifa wake pia unajulikana. Lakini ni nani kamnyonga? Nani katekeleza kitendo cha kumnyonga siku ya Eid ya kuchinja? Watu waliojifunika vitambaa wametekeleza amri ya kunyonga, suali ni kivipi hii inafaa enyi walimwengu?
Ivi mnajua watu wanasema nini kuhusu hili?
Wanasema kwamba raisi wa Marekani na Uingereza ndio waliotekeleza hukumu ile ya kumnyonga raisi wa Iraki, na serikali yote ya nchi hii. Na tuhuma hizi zitabaki hadi pale utakapokuja uhakika wa jambo hili. Kwa nini wasionyeshwe nyuso zao siku ya kutekeleza tendo lile wakatambulikana kama ni maafisa wa cheo gani kama ni wanajeshi au polisi au ni wauguzi wa afya? Kwa nini anyongwe raisi wa nchi mwanachama wa Umoja wa mataifa katika nchi kama hizi zisizotambulikana?
Nchi zilizofanya uvamizi Iraki na kumkamata Raisi wa nchi ndio zenye kubeba jukumu la makosa haya ya mauaji na kunyongwa kwa viongozi wake na kubomolewa kwa serikali yao. Na wanapaswa kuja kujibu mbele ya Umoja wa mataifa.
Mwenye kuhukumiwa kisheria, wale wanaotekeleza tetndo la kumyonga hutambulikana kisheria kama maafisa wa mahakama, na wanabeba majukumu ya tendo lao hilo kisheria na kwa kuwepo daktari na kwa kutimia masharti yote ya sheria ya utekelezaji tendo lile kwa mwanadamu, hata akiwa ni mwanadamu wa kawaida, seuze raisi wa nchi ambae ni mwanachama wa Umoja wa mataifa?.
Jambo la nne katika vita ya Iraki ni suala zima kuhusu Gereza la Aboughureib, la kuwatesea watu.
Najuwa kwamba Marekani na serikali yake inaweza kufanya uchunguzi wa hili lakini Umoja wa mataifa kamwe hautoliwacha suala hili na italifanyia uchunguzi tu.
Gereza la Aboughureib lina mateka wa kivita waliofanyiwa unyama na kunyanyaswa kijinsia na hata kutumiliwa mbwa na kunajisiwa wakiwa wao ni mateka wa kivita.
Jambo ambalo hata sheitani hawezi kulifanya, nchi mwanachama wa Umoja wa mataifa inavamiwa na raia wake kukamatwa na kuwekwa gerezani na kufanyiwa unyama kama huu, liko wapi baraza la usalama la Umoja wa mataifa? Ni masuala ya kibinaadamu kamwe hatuwezi kuyanyamazia na Umoja wa mataifa ufanye uchunguzi na kutoa taarifa zake kwa walimwengu.
Hadi sasa kwenye gereza hili la Aboughureib kuna mateka wa kivita wapatao robo milioni wa kiiraki, wanawake kwa watoto. Uchunguzi ufanywe.
Jengine ni vita vya Afghanistani yapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Kwa nini tuwafanyie uadu Watalibani na kwa nini Afghanistani na ni akina nani hao watalibani?
Kama Talibani wanataka kufanya taifa la kidini wacheni wafanye, kuna Vatican ni taifa la kidini la linaishi kwa amani na halihatarishi yeyote kwa hivyo afghanistani nayo waachiwe wenyewe nini waamue wanataka kufanya.\
Kwani bin Laden ni Muafghani au ni Talibani? Hapana, si aktika watalibani wala si muafghani.
Je wale magaidi waliyoipiga New York mji ambao sisi tupo hivi saa ni Taliban au waafghanistani?, Abadan. Sasa suala linajitokeza kivipi Iraki au Afghanistan?
Laity kama ningependa kuwatia hatarini rafiki zangu wamarekani na waingereza, naweza kuwambia hivi lakini ninawapa moyo na nawambia wandelee kupeleka wanajeshi zaidi na zaidi nchini Afghanistani na Iraki hadi watakapowaona wanaogelea kwenye bahari ya damu kwa sababu hakuna watakachofanikiwa.
Mumuona nini kimewatokezea kule Iraki, licha ya kwamba Iraki ni jangwa na ardhi ya wazi kabisa, sasa vipi watafanikiwa Afghanistan ardhi ya majabali na mawe, kamwe hawawezi kushinda.
Lakini kuwambia hivi basi ni upendo toka kwangu kama hatuwapendi tungewahimiza waendelee na vita lakini huku ni kuwaokoa. Tunawambia waachane na vita ile ya Iraki na Afghanistan, watoke wawachie wananchi waamue mustakabali wao.
Kwa sababu hata huku Marekani kulikuwa na vita vya wenvyewe kwa wenyewe nani aliwaingilia? Hispania kadhalika kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, China pia na sehemu zote ulimwenguni. Waachieni hawa wairai na waafghanistani wapigane wao kwa wao wako huru mwishowe watapatana.
Waachieni talibani waunde dola watakayo, kwani wao wana maroketi yenye kuvuka mabara? Ivi ndege zilizotumika kufanya mashambulizi ya New York zilitokea afghanistani au Iraki? Zilitokea hapahapa kwenye uwaja wa ndege wa Kennedy, iweje leo mutoke mwende kuishambulia Afghanistan au Iraki? Hawakuwa wataliban wala waafghani wala wairaki! Sasa vipi tunyamaze kwa upuuzi huu wa shetani mbaya?
Hii ni haki yetu kwa sababu tunapigania amani ulimwenguni, na kumtetea mwanadamu mwenzetu.
Suala jengine tunaitaka Umoja wa mataifa ufunge mlango wa upelelezo wa mauaji yaliyofanyika kama vile kuuawa kwa “Patrice Lumumba” nin nani amehusika namauaji yake?
Tunataka tuandike historia ya afrika, leo vipi anauawa kiongozi wa ukombozi barani afrika? Tunahitaji itambulikane ili iweze kuwekwa katika historia ya afrika na watoto wetu waweze kusomeshwa na kujua viongozi wao.
Kadhalika tunataka kujua nani kamuua katibu mkuu wa Umoja wa mataifa “Homor Shold” mwaka 61 ambao ni mwaka huohuo aliouawa Lumumba. Ni nani aliyeitungua ndege yake? Kwa nini tunyamaze kimya wakati katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anauawa hivivi ni nani mwenye maslahi namauaji hayo.
Mauaji ya kennedy mwaka 63, Baraza Kuu la Umoja wa mataifa linapaswa kufungua jalada la mauaji ya Kennedy raisi wa zamani wa Marekani, kwa nini Muisrael “Jack Roby” aje kumuua aliyemuua “Kennedy” na ana uhusiano gani? Hivyo mambo yawekwe wazi katika mauaji haya. Tunalojua ni kwamba Kennedy alitaka ufuangua jalada la upekuzi wa Kinu cha nyuklia ya Israel cha Demona, je hii ndio sababu ya mauaje yake?
Kadhalika mauaji ya “Martin Luther King” Kasisi mlinganiaji mweusi na mtetezi wa haki za binaadamu, lazima ijulikane vipi ameuawa?
Nani amemuua “Waziri Khalil” mpalestina aliyefanyiwa uadui kwenye nchi yenye haiba Tunisia ambayo ni mjumbe wa Umoja wa mataifa, alihujumiwa kwa manuari mbili na ndege za bila ya kuheshimu uhuru wa nchi hii. Vipi tunyamaze na mambo haya?
Mauaji ya “Abou Eyad” nayo hayaeleweki, mauaji ya “ Kamal Nasser” na “Kamal Udwan” na “Abou Yussuf Najar” wapalestina hao wameuawa kwenye nchi mwanachama wa Umoja wa matiafa Lebanon. Lazima uchunguzi ufanyike ili mambo kama haya yasitokee tena.
Tunahaki ya kuishi katika ulimwengu huu ulioumbwa na Mola na sio Mataifa makubwa.
Mauaji ya halaiki ya Sabra na Shatela maeneo yaliyokuwa chini ya Israel na hatimae kiasi cha wapalestina 3000 wakauawa wengi wao wanawake na watoto vipi tuwe kimya na mauaji kama haya?
Kasha kuna mauaji ya Gaza 2008, wahanga wake ni wanawake 1000 kati ya waliouawa na kmajeruhi, na watoto 2200.... tasisi zaidi ya 50 za Umoja wa mataifa zimeharibiwa, taasisi 30 za kiraia zimeharibiwa, zahanati 60 nao pia zimeharibiwa katika mashambulizi hayo.. walifanya mauaji hayo wapo hai na wanapaswa wafikishwe mbele ya mahakama za kimataifa. Au tujue na tuwe wawazi kama mahakama hii ya kimataifa ipo kwa ajili ya nchi changa na zile zinazoitwa iulimwengu wa tatu? Haziwahusu nchi kubwa, Tasisi ya kimataifa ya nishati ya nyuklia ni kwa ajili ya nchi fulani tu, baraza la usalama la Umoja wa mataifa nalo pia ni kwa ajili ya nchi chache tu na hili baraza kuu la Umoja wa mataifa halina mpango wowte? Kwa hivyo uko wapi huo Umoja wa mataifa?
Jambo jengine ni kuhusu ujangili wa baharini, ni jambo limekuwa kubwa sasa na kama la kigaidi. Ujangili huu ninaoutaja hapa ni ule unaoneekana kule Somalia. Nakwambieni wazi kwamba wasomali si majangili lakini sisi ndio majangili tunaofanya uadui kupora neema za bahari na riziki za watoto na uchumi wa wasomalia kwenye bahari yao. Libya, China, Japan na Marekani n’k sisi ndio majangili tunaokwenda kupora neema za wasomali mara ya kuanguka uongozi nchini humo. Kisha mnatoka na kusema tupeleke meli za kivita kuwapiga majanili wa kisomali. Kwa nini tusipeleke meli za kivita kuzipiga meli za kigeni zinazovua bila ya ruhusa kwenye mwambao wa Somalia?
Nimewataka wasomalia niwe mpatanishi kati yao na ulimwengu, yaani ulimwengu uheshimu eneo la uchumi wa Somalia, kiasi cha eneo la meli mia mbili lisiingiliwe ni mali ya Somalia, hili ni moja.
Pili kila nchi ijizuie istupe mabaki ya viwanda yenye sumu kwenye mwambao huu wa Somalia ambao ndio chanzo cha uchumi wao... hili ndio suluhisho na sio kuengeza meli za kivita. Hivi sasa wamepeleka meli za kivita na kuwazuia wasomalia wasivue kuwatafutie riziki watoto wao.
Kwa kweli suluhisho lililotolewa kupambana na ujangili huu ni bovu, kadhalika suluhisho la kupambana na ugaidi pia halifai, vilevile sukuhisho la kupambana na maradhi ni bovu pia.
Ukiangalia upande wa maradhi, madawa kutoka mashirika ya utafiti wa afya yanauzwa ghali sana, sasa imekuwa ni biashara. Wanatengeneza virusi na kuvisambaza ili mashirika ya kibepari yaweze kutengeneza dawa na kuziuza. Hii ni aibu kubwa mno na haifai kabisa, kwa sababu dawa haifai kuziuza. Nakuombeni msome Kitabu cha Kijani haifai kabisa kuuza dawa.
Tangazeni kwamba dawa hutolewa bore, na kwamba hamtoeneza tena virusi kwa sababu ni sakata munaliandaa ili mashirika ya kibepari yaweze kupata faida kwa kutengeneza dawa.
Yote haya yanapaswa kufunguliwa jalada kwenye Umoja wa mataifa na kupatiwa ufumbuzi wake.
Jambo jengine ambalo ningependa kuligusia ni kuhusu makubaliano ya Ottawa kuhusiana na miripuko “Mines” makubaliano haya yanakataza kutengeneza, kusafirisha na pia kuuza miripuko ya namna hii. Hii si nyenzo au silaha ya mapambano bali ya kujihami tu kwa sababu ni silaha isiyotembea wala kuripuka wakati huohuo bali hukaa hadi atakapo kuja mtu na kuligusa ndio huripuka.
Unaweza kuyaweka kwenye mipaka ya nchi yako, anapokuja adui linamripukia na kumuangamiza. Makubaliano ya Ottawa myarejee upya. Zaidi juu ya hilo mnaweza kupata kwenye tovuti ya “Algadhafi is Speaking” Hivyo makubaliano haya yavunjwe au yarekebishwe.
Ondoeni na angamizeni silaha za nyuklia na makombora yanayovuka mabara.
Ama kuhusu suala la Palestina, kuunda mataifa mawili ni jambo lisilowezekana kamwe... na ninakuombeni msilizungumzie. Suluhisho ni kuunda taifa moja la kidemokrasia likiunganisha wayahudi, waislamu, wapalestina, wakristo na wengineo tukichukuwa mfano wa Lebanon. Hatuwezi kuunda mataifa maweili yakiwa jirani kwa sababu hivi sasa ni watu waliochanganyika. Na hata ukiangalia utaona kwamba sio nchi mbili zilizojirani bali zimeingiliana.
Ukenda kwenye Ukingo wa Magharibi kuna walowezi wa Israel nusu milioni na hiyo iitwayo Israel kuna zaidi ya wapalestina milioni moja, sasa vipi utaunda mataifa mawili hapo?
Ulimwengu unapaswa uelekee kuwajibisha taifa moja la demokrasia likiunganisha pande zote bila ya kujali dini au uasili ya kikabila na kitaifa au lugha... kauli za mataifa mawili ni za zamani ni mawazo ya walinzi wa vyuma, mawazo ya vita ya tatu ya ulimwengu mfano wa “Yaser Arafat” na “Sharon”, hawa wameshapita na kizazi cha sasa kinataka taifa moja la demokrasia lenye kusameheana. Vijana wote wa Israel na Palestina wanahitaji amani na utulivu na kuishi kwa raha bila ya khofu.
Kuna kitabu hiki “Cheupe” juu ya suala zima la Israel na Palestina la kuunda dola moja ya “Isratin”, Dkt “Ali Treik” chukua na wapatie baadae.
Waarabu hawana uadui na waisraeli, watoto binamu na wanaishi kwa amaniwanaishi katika taifa moja kwa amani lakini nyinyi ndio mliowawasha moto, mliowaua na kuwaandalia mahandaki ya gesi Ulaya.
Nyinyi ndio mnaowachukia wayahudi, na kamwe sio sisi.
Sisi tuliwapa makazi na kuwalinda enzi za utawala wa Kirumi, na wakati walipofukuzwa Indalus na wakati wa vita vya Hitler na mauaji mengine waliyofanyiwa.
Kuna siku wayahudi watajua umuhimu wa Waarabu na watarejea tena kwa Waarabu wakihitaji na hapo ndipo Waarabu watakapowakataa na kutowapa tena himaya yao kama walivyowafanyiwa hapo awali.
Angalieni jinsi alivyowafanya “Titos” na “Hadrine” na “Edward wa I” na “Hitler” pia?
Nyinyi ndio mnaowachukia, kama inavyochukiwa sumu.
Ama kuhusu suala la Kashmir, kiufupi suluhisho ni kuachiwa iwe ni dola huru ikipakana na India na Pakistani, na kumaliza kabisa mzozo huu.
Kuhusu “Darfour” ninakuomboni hiyo misaada ya kimataifa mnayoizungumza ibadilisheni iwe ni miradi ya maendeleo ya viwanda, kilimo na umwagiliaji huko Darfour hivi sasa hakuna mapambano darfour, ni yinyi mliolifanya suala hili kuwa ni kubwa ili mupate kuingilia kati kwa maslahi yenu ya kupata mafuta huku mkiwatoa muhanga wananchi wa darfour.
Ninasema hili kwa sababu lipate kufanyiwa uchunguzi nalo pia, kwa sababu kuna suala zima la kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanono “Hariri” Mungu amrehemu, suala hili lililetwa hapa kwenye Umoja wa mataifa ili kufanyiwa uchunguzi wa kimataifa. Mnaitumia kesi hii ili mpate kusawazisha mahesabu yenu na Syria.
Kwani Lebanon si ni nchi huru yenye mahakama na vyombo vyake kamili vya uchunguzu lakini mbona vimewekwa pembeni ili mkamilishe mahesabu yenu na Syria.
Haya ni masuala muhimu ambayo chini ya Uenyekiti wa Libya kwenye Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa tunataka yafanyiwe utafiti wa kina na kupatiwa ufumbuzi wake, tunatoa msaada wetu kwa ulimwengu ili tuweze kuishi kwa amani na utulivu.
Wassalam Alykum.
 
Hongera mkuu NN kwa kuwa na ID pacha Julius. Kumbe naweza badili ID bila ku-affect details nyingine?? Poa ni PM jinsi ya kufanya??

Ila pacha Julius namsifu anaandika kirefu zaidi kuliko ile short and stimulating!!! Ha ha ha mkuu. Hapo kwenye bold du kweli unajua kukwepa zile ******.
Alikuwa na Green Card mpya wakayi huo. Ha haaaa!
 
Back
Top Bottom