Gaddafi (Qaddafi) yuko sahihi?

Makubwa haya. Hata kifo cha Kennedy na nani aliyemwua anataka Umoja wa mataifa upeleleze au uelezwe. Nani alimwandikia hiyo spichi?

Sidhani kama hiyo hotuba imeandikwa maana haina mpangilio kabisa. Mara anauliza adience maswali...mara anageuka nyuma...basi tu ili mradi.
 
Lakini uvamizi wa marekani kwa nchi zingine hapo kawagonga penyewe...pamoja na makucha ya UN kama yapo
 
For the 1st Time in 40yrs,

GREAT JOB, NIMEONA AMEmtupia Kitabu Dr. Asha Migiro!... duh!,

Naona ana-freestyling, Mpangilio hakuna lakini anasema kilicho moyoni Kwake, Inamuuma sana.

Kweli Hali ipo Tense,

B.
 
Huyu jamaa hajapitisha muda wake wa kutoa hotuba? Heheh naona amemaliza, zamu ya Museveni.
 
For the 1st Time in 40yrs,

GREAT JOB, NIMEONA AMEmtupia Kitabu Dr. Asha Migiro!... duh!,

Naona ana-freestyling, Mpangilio hakuna lakini anasema kilicho moyoni Kwake, Inamuuma sana.

Kweli Hali ipo Tense,

B.

Kama kawaida yake na madharau yake, nadhani ana hasira za kuzuiwa kupitch tent lake.
 
Wapambe wake kabla hajatinga New York walikuwa wanahaha kumtafutia sehemu yenye nafasi ya kutosha ili asimike Turubai lake la Kibedui kama kawaida yake. Sijui aliishia wapi na jambo hilo, maana jamaa huwa hataki kulala ndani ya mahoteli.

Turubai limepigwa mkwara wa kukosa kibali na inaonekana hawataki atie mguu huko.
 
capt.436ce3b2d958478c9e774e68ec51ed16.un_general_assembly_nyjd105.jpg


Wed Sep 23, 1:17 PM ET
 
Wakuu,

vipi Raisi wa Iran nae je speech yake ikoje??

wengine tumekumbwa athari ya Mgao wa Tanesco wajameni mtupe updates
 
Wamarekani kama hamtaki wageni, ondoeni makao makuu ya Umoja wa Mataifa nchini mwenu.

Hiyo habari ya town code ni ruse tu. Mbona kina Vaclav Klaus wanakuja Westchester every year na wanafanyiwa banquets kwenye vi outdoors tents kama hivyo na wala hatusikii kelele yoyote.

Angekuwa PM Gordon Brown hapo hata hizo paperwork zingefanywa na meya wa mji mwenyewe.

Semeni hamumpendi Gaddafi tu mueleweke.Gaddafi kawashtukia hoteli zao za Manhattan zote ziko bugged.
 
Last edited:
Back
Top Bottom