G55 bado mpo?

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
JF,

Wakati huo sikuwa nafuatilia sana mambo ya siasa, lakini kuna kipindi nikapata kujua kwa juu JUU kuwa kuna Group moja ndani ya bunge lilikuwa linadai tanganyika yetu - hili lilikuwa likijiita G55- kundi machachari ndani ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sasa niwekeni sawa kwa mambo yafuatayo
a) Hili kundi bado lipo na msimamo wake au liliteketezwa kabisa
b) Je members wa hili Group bado wapo hai na wako katika siasa, nakumbuka mmoja tu Njeru Kasaka kama sikosei
c) Je lilikuwa na hoja za msingi kudai tanganyika ila likazimwa tu kunusuru
muungano
d) Kama mtu ana list nzima ya wabunge waliounda G55 hapo aniwekee hapa.

wana JF waliobobea naomba ufafanuzi.
 
Sasa lipo kundi jipya la CCJ ,nafikiri tuongelee current issues na sio past History , itatufaa zaidi
 
Sasa lipo kundi jipya la CCJ ,nafikiri tuongelee current issues na sio past History , itatufaa zaidi

nilikuwa naenda huko huko umeniwahi - nina wasiwasi hawa G55 ndiyo wakawa hawahawa CCJ kama siyo wote ila masalia yake. bado natoa hoja

Pia kumbuka huwezi kuwa na current issues zilizo sahihi kama uta-ignore past history mkuu, yote yanaendana.
 
Utakumbuka G55 ilisababisha hadi Malecela akaitwa muhuni tu na Nyerere ukiitaka list nzima muulize Philipo Marmo nakumbuka ndiye alikuwa katibu.
 
Back
Top Bottom