Fwd: Sheria Namba 8 haiwezi kuwa Juu ya Katiba ya Zanzibar.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by Harith Ghassany // 15/02/2012 // Habari // 3 Comments

Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar.
Vipi sheria ya Mabadiliko ya Katiba iweze kufanya kazi Zanzibar wakati Zanzibar ni Nchi iliyo na mipaka yake Kikatiba? Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi wazi katika Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza kwamba: “Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar”. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba kupitia kifungu chake cha 19-(1) kinachohusiana na makosa na adhabu kwa watakaotoa maoni nje ya hadidu rejea za rasimu ya Katiba: kifungu hicho pamoja na sheria yenyewe ya marekebisho ya Katiba, mwisho wake CHUMBE !!
Pili, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi kuwa, Katiba ya Zanzibar ndiyo yenye nguvu za kisheria nchini kote, ambapo ikitokezea sheria yo yote kutofautiana na Katiba ya Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana. Hii ni kuonesha nguvu na uwezo iliyonayo Katiba ya Zanzibar mbele ya sheria namba 8 ya mabadiliko ya Katiba, na kwamba, Katiba ya Zanzibar ndio “(The Grundnorm, which is the highest form of validity, being of the highest authority, providing efficient and affordable legal representation).
Tatu, hata hiyo Mahakama ya Rufaa, nayo haina uwezo, wala mamlaka, wala haki Kikatiba ya kuitafsiri Katiba ya Zanzibar maana Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza katika kifungu cha 99 kinachohusiana na kazi na uwezo wa Mahakama ya Rufaa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kutafsiri Katiba ya Zanzibar. Kwa maneno mengine, Katiba ya Zanzibar inajitegemea, na kwa mantiki hiyo, Wazanzibari watahukumiwa kwayo tu, na si kwa sheria ya mabadiliko ya Katiba wala nyengine yo yote ile.
Nne, pamoja na vitisho vilivyomo kwenye kifungu cha makosa na adhabu ndani ya muswaada na sheria ya mabadiliko ya Katiba, bado sheria hiyo haiwezi kuwa JUU ya Katiba. Na sheria yo yote, itakayokwenda kinyume na Katiba, sheria hiyo pia inakuwa batili (unconstitutional). Tunakusudia kusema kwamba, hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, yenyewe, ambayo bado inatumika hadi sasa, inadhamini UHURU wa wananchi kutowa mawazo na maoni yao kwa uhuru kabisa. Kifungu cha 18, kinachohusiana na haki ya uhuru wa mawazo kinaeleza: “Kila mtu – (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake”. Aidha, kifungu kinachofuata cha 19-(1) nacho kinaeleza: “Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo”. Pia, Katiba hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano, Sehemu ya Tatu, inayohusiana na haki na wajibu muhimu, inaeleza kwenye kifungu cha 13-(2) kuwa: “Ni marufuku kwa sheria yo yote iliyotungwa na mamlaka yo yote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lo lote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake”. Neno ubaguzi, linatafsiriwa na Katiba hiyo hiyo ya Muungano kwenye kifungu cha 13-(5) kuwa ubaguzi ni pamoja na kunyima haki ya maoni ya kisiasa. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba inakwenda kinyume na Katiba kwa kuikana haki hiyo muhimu ya maoni ya kisiasa.
Tano, UHALALI wa sheria ya mabadiliko ya Katiba hauwezi kupatikana kwa kupitishwa na Bunge pekee. Ni LAZIMA sheria hiyo ya mabadiliko ya Katiba, pia ipitishwe na kuridhiwa na kukubaliwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Baada ya hoja na maelezo hayo, ni ukweli usio na shaka kuwa, sheria ya mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar, na kwa ajili hiyo, Wazanzibari Kikatiba, tunao uhuru na haki ya kutoa maoni yetu bila ya hofu wala woga; kama ambavyo Serikali yetu nayo kupitia Katiba ya Zanzibar, ina wajibu wa kudhamini uhuru huo. Ikiwa ni kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba, na si ule Muungano wa Katiba pia ni haki yetu ya Kikatiba. Zama za kutishana na kupigana zimekwisha. Hata Rais Kikwete katika hotuba yake alilisema hilo, na namnukuu: “Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya, nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Tutofautiane bila kupigana”. Mwisho wa kunukuu. Tunamtaka Rais Kikwete atembee juu ya kauli yake hiyo kama ambavyo nasi tutatofautiana kwa misingi ya HOJA bila ya kupigana.
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar KWANZA!




[h=4]Related Posts[/h][h=3]Fwd: Fitina za Kuifisidi Jamhuri ya Zanzibar na Watu Wake![/h]
[h=3]MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA UZINI – ZANZIBAR[/h]
[h=3]TUNATAKA SURA MPYA MZALENDO[/h]


[h=3]Balozi Seif afagilia Serikali ya Umoja wa Kitaifa[/h]
[h=3]Barua ya wazi kwa katibu mkuu wizara ya elimu[/h]





[h=3]3 Comments on "Fwd: Sheria Namba 8 haiwezi kuwa Juu ya Katiba ya Zanzibar."[/h]


  1. tash 15/02/2012 kwa 11:35 um · Jibu
    ndugu mwandishi maneno yako ni sawa utakapofika wakati wa kujadili mchakato wa katiba na kutiwa ndani au kupigwa hapo totakutafuta ili hivyo vipengele ututajie tena kwani tumesha ona mara nyingi wanasheria wa zanzibar yakitokea mambo wao huwa kama hawajuwi sheria inaseme nini hukaa kimya kama hawapo ulimwenguni kazi kupiga maneno kwenye mitandao na vikao vya karata kila siku tumeshachoka tunataka kweli
    zanzibar njeme
    zanzibar huru
    zanzibar mbele




  2. Ghalib 16/02/2012 kwa 10:07 mu · Jibu
    Wanifumbua macho na inaniosha brain hizi hoja..




  3. makame silima 16/02/2012 kwa 10:10 mu · Jibu
    Nawauliza ndugu zangu Wazanzibar kwani bado tumo katika Muungano na hawa Majambozi?, ikiwa tumo katika Muungano laumuhimu nikujiuliza huyo tulie Ungana nae ni yupi na yupo wapi hivi sasa?.a).
    b.) Ikiwa jibu litakuja kwa Hao majambazi ambalo hulitumia kwa kusema kuwa Serekali ya Tanganyika na Katiba ya Tanganyika imo ndani ya Serekali ya Tanzania au Muungano wa Tanzania?.
    Sasa tujiulize ni Mzanzibar gani alio changia au kukubali kuwa Tanganyika iwe Tanzania na mambo yote ya Tanganyika yasimamiwe na Serekali ya Tanzania, yuko mzanzibar yoyote alio kubali Tanganyika na Katiba yake yenye kusimamia mombo yake yasio ya Muungano.
    Ikiwa hakuna Mzanzibar yoyote mwenye kukubali Tanganyika na Katiba yake ya Tanganyika kujifunika katika Joho la Tanzania basi laumuhimu kwa Wazanzibar kabla hatuja anza step 1 nikupinga Muungano huu wa Tanganyika kujifanya Tanzania.
    Mimi nawaita Majambazi hawa sio kwamba ni wizi tu wa Kariakoo, kumwita mtoto mwana wa haramu sio kuwa hana baba laa, lakini kitendo kilicho tumika nichakiharamu hakiendani na makubaliano ya ndowa.
    Sasa na hawa wenzetu vitendo walivyo vifanya vya kuvunja makubaliano ya Muungano na kumtengua mshirikaa mkuu Tanganyika na katiba yake ni yakiaharu na kinyume na makubaliano ya Muungano.
    Sasa ikiwa Wazanzibar tutakubali kuburuzwa na kuburuzika basi na sisi tunaingia katika uharamu, maana Muungano umekufa tokea kufa kwa Tanganyika na katiba yake ambae ndie alikuwa mchirika na Zanzibar zikiwa nchimbili hizo ni huru na historia ya kila nchi na uhuru wake.
    Sasa ikiwa lie imekuja Tanzania na Zanzibar where is Tanganyika? ikiwa Zanzibar ipo kuna faida gani kuwepo Tanzania bada ya Tanganyika?. na jee ni kikao gani halali kilicho wakutanisha pandembili za Muungano na kusema tunaiondowa Tanganyika na katiba ya Tanganyika na tunaiweka mbele Tanzania ? nikikao kipi na mwaka gani twambieni ili tujuwe kuwa Serekali ya Tanzania ilipata Baraka kwa upande moja wa Muungano Zanzibar kuwa iwe hivyo ni lini?.
    Mimi hushangazwa sana na hawa Majambazi wanaposema kuwa Zanzibar ina kila kitu chake chakuwa nchi wakati Tanganyika haipo, sasa Nyiyi Watanganyika mujitao Watanzania na kuona aibu kujita Watanganyika si semeni tu kuwa nchi yetu tulioipigania uhuru tumeibadilicha jina Bada ya Kuita Kongo tumeita Zaire musitulahai Wazanzibar kutulazimisha tule matabishi yenu?.
    Kifo cha Tanganyika ni chakujitakia wenyewe Wazanzibar hakiwahusu wala hawamo, sisi siku zote tunapigania mufufue Tanganyika yenu na katiba yenu ya Tanganyika hatuna pingamizi na hilo, ili kulinda mambo yenu yasio ya Muungano lakini hamutaki na mumekuwa wakaidi na kubiruza na kupindisha mambo na kujitia utata wa kujizima mashkio na kila tukiwafahamicha kiungawana kuwa hakuna kero za Muungano ispokuwa kuna mambo munafanya ya kwenda kinyume na makubaliano ya Muungano na Mukiambiwa munasema Kero za Muungano.
    Sasa mujuwe tu wazanzibar wa kale sio hawa wa leo sisi tunatafuta kila njia kuvunja huu udanganyifu mulio fanya na sababu na vielelezo tunavyo, kwa hio hilo sio lakufiswa mujuwe wazi kuwa Wazanzibar hawataki Muungano huu na unaishi hivi sasa kwa nguvu za Dodoma na Kiswanduwi tu lakini hauna chauku mbele ya Wazanzibar.Muungano ulikwisha kufa tokea kufa kwa Tanganyika.
    KUSHEREWA KUFA KWA MUUNGANO NI MAUTI KWETU.
    Mungu ibariki Zanzibar na watu wake.
    Hii yote nikutimiza ujambazi wenu wa

 
nimechoka na hawa waznz nyie wenyewe mnajua tatizo ni CCM na ni CCM hiyo ndiyo inayong'ang'ania muungano leo hii uzini mmewarudisha hiv unafikiri huyo mbunge anaweza kuwapigania kuhusu muungano wakati inabidi a support sera za chama chake amkane kama hamtaweza ing'oa CCM kamwe muungano hauwezi vunjika na huu ndio ukweli wenyewe na mwenye masikio asikie na mwenye macho aone na ukweli ni uchungu lakini lazima muunywe uchungu huu kuweza kuiondoa ccm kwani Vyama vingine viko tayari kutazama muungano upya ila CCM haiwezi na nyie mmefunga ndoa na CCM kwene nyoyo zenu leo hii mnalalamika wakati hamjui kuwa hata hiyo katiba mnayosema inawagandamiza ilitungwa na CCM.

Acheni siasa za kishabiki ili mfunguke akili na kujua adui wa nchi yenu ni nani
 
Huyu Makame Silima kweli hamnazo. Jiulize ni lini Wazanzibari waliulizwa kuhusu Muungano in the first place, kabla ya kuuliza kuua Tanganyika!

Sera ya CCM ni Serikali 2 kuelekea Serikali 1. Ndiyo maana ikaamua kuua kwanza Tanganyika, halafu kitachofuata ni Zanzibar kufa na kubaki na Serikali moja ambapo Ugunja na Pemba itakuwa mikoa kama DSM na Pwani.

Kwakuwa Wazanzibari mnakubaliana na hilo ndiyo maana CCM na CUF wamefunga ndoa kutengeneza SUK. Ndiyo maana CCM na CUF walipitisha kwa nguvu moja mabadiliko hayo ya 8 ya katiba mpya.

Na kwakuwa Wazanzibari mnakubaliana na hali hiyo ndiyo maana Jumapili mmechangua Raza wa CCM kuwa mwakilishi wa Uzini kwa 91%.

Wazanzibari mmekuwa kama mwanamke asiyetosheka kila kuchwao kumlalamikia mme wenu Tanganyika, lakini ikifika usiku (mkienda Dodoma) penzi mnatoa tena kiulani.
 
Back
Top Bottom