Fuvu la albino lililokutwa baa: RPC Kinondoni hajui kama ni la binadamu

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Mara nyingine nashangazwa sana na kauli za Polisi, kama hii iliyotolewa na RPC wa Kinondoni kwamba lile fuvu lililopatikana katika baa ya mfanyabiashara pale Kawe, haijulikani kama ni la binadamu. Taarifa zinasema ni fuvu (au kichwa) la albino, RPC anasema hajui kama ni binadamu. Hivi kauli za polisi kama hizi ni kutoa mwanya fulani kwa ajili ya kusafisha watuhumiwa au nini hasa?

Je, RPC anachotaka ni kwamba tusishangae polisi watakapotangaza kwamba lile fuvu si la binadamu bali la sokwe na hivyo mtuhumiwa atashitakiwa kwa kosa la kuwa na nyara za serikali na sio mauaji ya binadamu?

Kweli Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
Back
Top Bottom