Future ya Vijana Ipo Chadema, Ndio Ukweli

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Tatizo la chama kukaa madarakani muda mrefu ni kutokea recircling. Walewale vijana wa makamba, Nauye, Mwinyi na wengine ndio utawaona kwenye system. Ukienda balozi za nje utawakuta vijana wengi wa vigogo ambao hata hawajasomea kazi hiyo ila wale waliosomea na ni competent wapo mtaani wanazurura. Ni halali akina Makamba kutetea system ya CCM maana ikiendelea kuwepo wataendelea kuweka mirija yao hapo. Wewe kijana uliyetoka familia duni ukiiunga mkono CCM ina maana unataka wewe uendelee kuwekwa pembeni au ule makombo. Wakiingia watu wapya, nafasi zitafunguliwa na uwezekano mkubwa ni wewe kunufaika kuliko kupata tabu. Wakiingia wapya hawatakuwa na backlog ya kulipa fadhila na vijana tutakuwa na say ila hawa CCM ni ngumu wewe kuingia. Vijana 2015 tulete mabadiliko, tuanze upya na Chadema ndio chama muafaka. nao wakikaa miaka kumi tukiona wanaanza U ccm tutawabwaga, nchi itakuwa na uadilifu maana aliye madarakani atakuwa kwenye kiti moto muda wote. Sisemi tuingie nasi tule ila tuingie nasi tujenge nchi, tulete mambo mapya, wale wenye uwezo kiakili wapewe nafasi, tusiangalie wewe mtoto wa nani bali una nini kichwani kwa ajili ya ku deliver:hug:
 
Lengo letu si CHADEMA kuukwaa uongozi, tunataka MAISHA BORA kwa kila mtanzania. Miaka mitano kuanzia sasa mpaka 2015 ni mingi sana. Hawa jamaa waliovua magamba ya zamani wakavaa magamba mapya, hata kama yanang'ara wanatakiwa kubanwa wabadili nia zao (their minds). Tunusuru nchi yetu na umaskini unaoendelea.
Tunatakiwa tuwe na vyama vingine vyenye nguvu kama CDM, ili isijisahau na yenyewe.
 
Jaman ccm tumewachoka mda wote mlio itafuna nchi nakufanya maovu umefika kikomo. Mmzoea dhambi atamkifanya wizi undugunisation mnaona kawaida kumbukeni mnatutesa masikini ambao wazaz wamejkamua kutusomesha lakn kazi bdo mmejipachika nyie kwakujuana......
 
Na ninyi mfanye kazi kwa bidii, msomeshe watoto wenu kama akina Mbowe na Ndesamburo wanavyofanya la mkiendelea kulalama wajukuu zenu watabaki kuwa watazamaji kama ninyi. Maana mnawalaumu akina Nnauye wakati babu zenu waliona kuoa ndio sifa akina mzee Nnauye walitumia pesa zao kusomesha watoto wao.
 
Tatizo la chama kukaa madarakani muda mrefu ni kutokea recircling. Walewale vijana wa makamba, Nauye, Mwinyi na wengine ndio utawaona kwenye system. Ukienda balozi za nje utawakuta vijana wengi wa vigogo ambao hata hawajasomea kazi hiyo ila wale waliosomea na ni competent wapo mtaani wanazurura. Ni halali akina Makamba kutetea system ya CCM maana ikiendelea kuwepo wataendelea kuweka mirija yao hapo. Wewe kijana uliyetoka familia duni ukiiunga mkono CCM ina maana unataka wewe uendelee kuwekwa pembeni au ule makombo. Wakiingia watu wapya, nafasi zitafunguliwa na uwezekano mkubwa ni wewe kunufaika kuliko kupata tabu. Wakiingia wapya hawatakuwa na backlog ya kulipa fadhila na vijana tutakuwa na say ila hawa CCM ni ngumu wewe kuingia. Vijana 2015 tulete mabadiliko, tuanze upya na Chadema ndio chama muafaka. nao wakikaa miaka kumi tukiona wanaanza U ccm tutawabwaga, nchi itakuwa na uadilifu maana aliye madarakani atakuwa kwenye kiti moto muda wote. Sisemi tuingie nasi tule ila tuingie nasi tujenge nchi, tulete mambo mapya, wale wenye uwezo kiakili wapewe nafasi, tusiangalie wewe mtoto wa nani bali una nini kichwani kwa ajili ya ku deliver:hug:

ibange you are 100pc right. the future for tz youths is in chadema.
 
ibange you are 100pc right. the future for tz youths is in chadema.

Future ya vijana ni juu yao, kama unadhani kuna chama kinakuja kujenga maisha utakufa masikini, jitume fanya kazi kwa bidii kama mwanafunzi soma kwa bidii hivyo vyama vitakutafuta wewe ulipo.
 
Hujui effect ya chama tawala. Mimi nimesoma na watu wengi sana. Kuna watu brains balaa, kuna watu wanafanya kazi hadi unawaone huruma. Wanaopewa nafasi si hawa wenye uwezo, ni akina Makamba. Watch out men! Kuna watu nawajua shuleni walikuwa hawajui kitu, anapewa kazi hadi unamwonea huruma. Hujasikia kuna watu wamepewa ujaji hawajui kuandika hata hukumu hadi waombe watu wawaandikie? Kuna wanasheria wangapi competent? hujasikia au kuona wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri na manaibu wanapewa tu nafasi kwa vile ni mtot wa fulani wakati hana uwezo? Mfano mdogo, Malima asingekuwa mtoto wa malima angepewa uwaziri? Je, ukiwaangalia wabunge wa CCM, ni wangapi bora kuliko malima ila hawapewi kazi?
 
Back
Top Bottom