Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,702
WanaJF
1. Taaluma ya medicine ina karne nyingi sana. Utaratibu wa kumfundisha Daktari unaongozwa na kanuni na misingi ya pamoja inayokubalika duniania kote. Kiapo chao cha kazi ni kile kile cha kale dunia nzima. Kama yatakuwepo mabadiliko yanatakiwa yawe ya kimataifa. Kumfunza mtu kwa kutumia miili ya binadamu kuna maana yake kitaaluma na sio suala la kubadili na kutumia njia kama za plastic. Ni science inayoongoza hapa.
2. Taaluma ya medicine inaongozwa na principles na ethics, kwahiyo suala la miili ya binadamu lina taratibu zake zinazoratibiwa na watu wenye weledi wa hali ya juu sana kwa kuzingatia vigezo vyote vya kisayansi ikiwa ni pamoja na kuhifadhili miili hiyo, kuchagua ili kupunguza 'risk' kwa watumiaji, kuzingatia cultural and social behaviour vyote vikiongozwa na principles, Laws, regulations and ethics.
3. Taarifa nyingi za kitaalamu hapa nchini pasipokuwa na professional journalists huwa ima zinapotosha au hazina ukamilifu. Ikumbukwe kuwa afisa uhusiano sio lazima awe mtaalamu wa nyanja hiyo, na waandishi wahabari wengi (nawaheshimu sana na kazi zao) lakini wapo wanaokosa kutafuta vyanzo halisi vya habari. Kama taarifa ingetolewa na mtaalamu husika (mkuu wa chuo, taaluma au mkuu wa hospitali)tungeelewa mengi kuliko kusikia fuso limekamatwa tu na miili.
Yaweza kuwa miili hiyo ilihifadhiwa kwa muda baada ya kupokelewa kutoka sehemu nyingine nje ya nchi na uhamishaji kwenda Dodoma ndio umekuwa na matatizo. Alichosema msemaji ni taratibu za kuzika marehemu siku 14, na sidhani huo ndio utaratibu wa kuaandaa miili ya marehemu ya kufundishia
Kwa misingi hiyo, si haki au vema kuanza kutoa hukumu kwa ujumla wa suala zima, inaweza kuwa ni taarifa tu kwa walinzi ilikosekana kwa makosa lakini taratibu zingine zilizingatiwa.
Nawahakikishieni kuwa kama tulichokisoma ndicho, basi yapo makosa mengi na wahusika watachukuliwa hatua.
Ningeshauri kuwepo na ufafanuzi wa jambo hili kutoka kwa wahusika kwasababu limeitisha jamii kwa namna fulani, na jamii ya wataalamu wa afya wanadhani lipo ombwe la habari au makosa ya kiutendaji kwa kusoma tu habari hii kama ilivyo.
Wanahabari wafuatilie kubaini ukweli kutoka kwa vyanzo husika.
Umemaliza mzozo........nasi tusioelewa haya mambo tumeelewa......thanks..