Fursa za kibiashara nchini Congo

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,526
3,801
Habari zenu wakuu,

Nina mtaji wa sh milioni kumi, nahitaji kufanya biashara nchini Congo. Mimi nilikuwa na mawazo ya kufanya biashara ya vitenge kutoka Congo na kuleta Tanzania na biashara ya kuchukua vifaa vya ujenzi kutoka Tanzania kupeleka Congo.

Ninafahamu fika kuwa humu ndani kuna watu wenye uzoefu zaidi wa biashara ambao yawezekana tayari walishakwenda Congo hivyo wanafahamu fursa zilizopo huko.

Naombeni sana mnisaidie mawazo yenu ili nisipoteze mtaji wangu nilioupata kwa shida.

Asanteni sana
 
Leta vitenge toka Congo safi, vifaa vya ujenzi kwenda Congo sijui ila ukipeleka samaki au dagaa that is business jamaa wanauhaba sana wa mboga.. Ukienda nA hivyo vitu soko ni kubwa sana
 
DRC ni nchi ngumu sana kufanya biashara, wana kodi za kila aina, watu wengi (wageni) wanashindwa kufanya biashara huko, wenyeji wanafanya kwa sababu wanajuana kwa vilemba na wanajua jinsi gani ya kukwepa kodi

Naona kuna mdau anazungumzia vifaa vya electonics, hivyo vifaa pamoja na mambo ya nguo, viatu, perfum ni bidhaa za wenyeji kwa maana ndio biashara wanayoifanya kwa ufanisi sana huwa wanasafiri sana kwenda Dubai na Tanzania kuhemea hivyo vitu hasa nguo

Biashara ya vifaa vya ujenzi inalipa lakini pia inakufaa ujaribu kufanya visit huko ili upate soko,

Congo ni kubwa na haiko connected, kwa mfano watu wa Goma, Bukavu wanategemea sana cement, Nondo, na mabati kutoka Rwanda lakini hasa vitu vyao vinatoka Uganda, kwa bidhaa za chakula zinatoka hasa Kenya na Tanzania na Rwanda kidogo

Kwa upande wa Katanga province (Lubumbashi, Kolwezi, Likasi, Kalemie nk) nao wamegawanyika, baadhi ya Vifaa vinatoka Tanzania, lakini vingine ni Zambia na RSA kidogo

Kweli biashara hipo kubwa sema mazingira ya wageni kufanya biashara ni Magumu sana
 
Mkuu, bidhaa za vyakula kama sembe,dagaa na nyingine zinazofanana na hizo kama ndau alivosema unaionaje hapo...????
 
Mkuu, bidhaa za vyakula kama sembe,dagaa na nyingine zinazofanana na hizo kama ndau alivosema unaionaje hapo...????

Hizo ni biashara nzuri na hata Unga wa Muhogo unatumika sana,

Sasa sijui unapendelea kufanyia biashara sehemu gani ya Congo, kama ni East Congo, ambayo ina provinces za Kivu Kaskazini- Goma na Kivu ya Kusini ambayo ina miji mikubwa kama Bukavu, Uvira, Baraka na Fizi ambayo iko kwenye Ziwa Tanganyika

So watu wengi huwa wanakuwa na store Rwanda au Burundi, kwenye miji iliyo mipakani na DRC na wanavusha mizigo kuingia DRC kutokea miji hiyo na hiyo yote inafanyika kukimbia kodi za DRC

So Kwa Goma na Bukavu njia ni kupitia Rwanda na kwa Uvira, Baraka njia ni kupitia Burundi Gatumba- Kamvivira

Pia kuna soko la Kalemie, huu mji upo province ya Katanga na upo kwenye shore ya Lake Tanganyika, huu ndio mji ambao ulikiwa unaonekana ndio mlango wa bidhaa za Tanganyika kwenda DRC, Huu ndio mji unaoingiza bidhaa kwenye province ya Maniema (Manyema), nako ni kuzuri sana kwa biashara za vyakula, biashara kama Unga, Chumvi, Dagaa na hata mchele, niliona hata dawa za whitedent zinapendwa sana

Shida ya DRC ni rushwa na Kodi zisizokuwa na Kichwa wala miguu

Njia nzuri ya kufanya biashara DRC ni kitembelea huko na kuestablish masoko, Congo ni kubwa sana, japokuwa ina ardhi kubwa nzuri na maji mengi lakini watu wa DRC hawalimi wao ni kutafuta Madini na kufanya starehe, so biashara ya chakula hipo
 
Kongo ukipeleka unga wa maindi ulio fanyiwa processing "kuparaza, kusangwa, na kupakiwa vizuri utapata pesa hata mzee azam na mo wanaanzisha viwanda vya kufanya hivyo soko kubwa ni Uganda, Burudi, S.sudan, Zambia na nchi za kusini mwa Tanzania" KAMA UNAANZA ANZA LEO UKISUBIRI KESHO UTAKUA UMECHELEWA OPPORTUNITY NEVER COME 2 MKUU.
 
Back
Top Bottom