Fursa: Mkopo wa boat ya uvuvi kutoka TIB

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Wana Jamii, jana nilitembelea banda la Tanzania Investment Bank katika maonyesho ya Nane Nane hapa Dodoma na nikakutana na watengenezaji wa boat za kisasa za uvuvi (SONGORO MARINE BOAT YARD) ambao wanapatikana Mjini Mwanza.

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=60973&stc=1
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=60974&stc=1

Hawa jamaa wamefanya makubaliano na benki ya TIB kwamba mvuvi (mfanyabiashara) anaweza kupata boat ya uvuvi kutoka kwao kwa mkopo ambapo mvuvi atatakiwa kulipia asilimia 20% ya gharama na benki watamlipia asilimia 80% iliyobaki kwa mkopo. Boat inaweza kugharimu kiasi cha Tsh. 68,000,000/= inategemea na ukubwa, hivyo basi mvuvi au mfanyabiashara anatakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 12,000,000/= na kiasi kinachobaki kulipwa na benki; dhamana itakuwa ni hiyo boat (hakuna dhamana nyingine).

Huyu jamaa wa kutengeneza hizi boat aliyekuwa ananipa maelezo alisema kwamba kwa biashara ya uvuvi ndani ya mwaka mmoja utakuwa umerudisha pesa yako, kama kuna mwanajamii ambaye anafanya biashara ya uvuvi anaweza kutusaidia huu upembuzi yakinifu juu ya hiyo return.
 
Attachments

  • DSCN0331.JPG
    DSCN0331.JPG
    791.8 KB · Views: 604
  • DSCN0332.JPG
    DSCN0332.JPG
    1.1 MB · Views: 624
kaka hiyo boti naona si mahsusi kwa ajilli ya uvuvi,na hiyo si price yake halali,kama unataka kujua botii mahsusi ya uvuvi,tembelea chuo cha uvuvi mbegani bagamoyo,wale ni wataalamu na wana boti za uvuvi
Wana Jamii, jana nilitembelea banda la Tanzania Investment Bank katika maonyesho ya Nane Nane hapa Dodoma na nikakutana na watengenezaji wa boat za kisasa za uvuvi (SONGORO MARINE BOAT YARD) ambao wanapatikana Mjini Mwanza.

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=60973&stc=1
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=60974&stc=1

Hawa jamaa wamefanya makubaliano na benki ya TIB kwamba mvuvi (mfanyabiashara) anaweza kupata boat ya uvuvi kutoka kwao kwa mkopo ambapo mvuvi atatakiwa kulipia asilimia 20% ya gharama na benki watamlipia asilimia 80% iliyobaki kwa mkopo. Boat inaweza kugharimu kiasi cha Tsh. 68,000,000/= inategemea na ukubwa, hivyo basi mvuvi au mfanyabiashara anatakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 12,000,000/= na kiasi kinachobaki kulipwa na benki; dhamana itakuwa ni hiyo boat (hakuna dhamana nyingine).

Huyu jamaa wa kutengeneza hizi boat aliyekuwa ananipa maelezo alisema kwamba kwa biashara ya uvuvi ndani ya mwaka mmoja utakuwa umerudisha pesa yako, kama kuna mwanajamii ambaye anafanya biashara ya uvuvi anaweza kutusaidia huu upembuzi yakinifu juu ya hiyo return.
 
Thanx 4 information ,nipo rock city,songoro marine najua kiwanda chao kilipo,kuna matajiri wawili nawafahamu ambao mmoja ana meli ya kubeba watu mwingine ni meli ya mizigo ntajaribu kuwaulizia,,but hadi kupata bank loan c mpaka statement ya bank ya mwaka iwe imepitisha kiasi cha kutosha ama?
 
Nimerudi sasa mwaweza niuliza maswali,kwanza ni lazima ujue ni meli ya aina gani unayoitaka,,1:ya mizigo 2:ya abiria..kwa hiyo inategemea na route na soko unalotarget
 
duh! mil 68?

Bei za kujenga meli kwa kweli si mchezo, lakini milioni sitini na nane kwa mtumbwi huu...dah! labda waje wataalam!
Lakini kwa vile ni mkopo (wa muda mrefu) ni fursa jamani mnaofanya uvuvi changamkieni deal hilo, dhamana si mtumbwi wenyewe, isipokulipa wanachukua chao hauna hasara!
View attachment 173941
kununua nje na kulisafirisha nako tabu tu..dah!
 
sidhni kama kuna wavuvi walio wengi wanaoweza kuweza bei ya hiki kifaa!

kama kweli serikali iko serious bwana iachane na kufukuzana na mwenge itoe sponsorship kwa vitu vya msingi kama hivi watu wapate ajira!

cc Zitto kabwe W. J. Malecela, Halima Mdee, angalieni hili kwa maslahi ya taifa.
 
Last edited by a moderator:
sidhni kama kuna wavuvi walio wengi wanaoweza kuweza bei ya hiki kifaa!

kama kweli serikali iko serious bwana iachane na kufukazana na mwenge itoe sponsorship kwa vitu vya msingi kama hivi watu wapate ajira!
hahaha mkuu umesema la maana sana
 
mi nina boti kiasi meter 9 na ice box ndani upana ni 2meter ndani 98 cm ENGINES 40 HP mbili Bei yaKe ni Tsh 24000000
Mwedo kasi 28KPH
 
Hiyo nayo ni fishing boat? Huu ni wizi. Wanajua wanafanya dhuruma ndiomaana dhamana ni boat yenyewe. Huu ni mpango wa kuwauzia wavuvi kwa bei ya kukata na shoka.
 
mbona ni kiasi kidogo sana kwani wewe hukuwepo kwenye ule mgawo wa pesa za exscrow?

hizo ni kama unampa mama aende sokoni kununulia samaki na mboga tu hapo bado viungo sijui itakuwaje hk zimbabwe
duh! mil 68?
 
sidhni kama kuna wavuvi walio wengi wanaoweza kuweza bei ya hiki kifaa!

kama kweli serikali iko serious bwana iachane na kufukuzana na mwenge itoe sponsorship kwa vitu vya msingi kama hivi watu wapate ajira!

cc Zitto kabwe W. J. Malecela, Halima Mdee, angalieni hili kwa maslahi ya taifa.
umechangia vizuri ila umeharibu kwa hao ulio wa cc zitto,malecele na mdee wao ni nani katika nchi hii hawana mamlaka wala madaraka wala maamuzi yoyote ni vidampa tu
 
boti zangu nirahisi na kusaidia wa vuvi ziko aina tanu ndogo za meter 6-7 na engine yake 15hp Tsh 9000000

nember ya simu +269 3218059

kobali556gmail.com
 
Attachments

  • SAM_0752.JPG
    SAM_0752.JPG
    2 MB · Views: 366
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom