Shairi: Funika Funua

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
FUNIKA FUNUA.

1)kimesikika kishindo,cha pupu cha mfa maji.
Mbeba jembe na nyundo,nae du mjuaji.
Sera imetupwa kando,anena su msusaji.
Haya funika funua,umeshakufa ukuta.

2)Jambo limeshindwa mambo,wanaogopa majaji.
Hukumu apewe kombo,moshi mjanja wa jiji.
Sangara kumbe ni fumbo,lililokosa mlaji.
Haya funika funua,ulishakufa ukuta.

3)lazidi noga igizo,kwa hila za mtungaji.
Zile zake ndio hizo,wamefeli walengaji.
Tuwapeni angalizo,kwamba huu urembaji.
Haya funika funua,ulishakufa ukuta

4) wanaanza tapa tapa,waganda kama saruji.
Hata wao ni mapapa,vipi wagombea uji ?.
Wataka mengi kwa pupa,mwili wazama kwa maji.
Haya funika funua,ulisha kufa ukuta.

Shairi:FUNIKA FUNUA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arushq.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page:Idd ninga mashairi.
 
Duh!!!
mtani legeza kamba,vichwa maji tumeganda!
fito yenye uzito,aijuae mbebaji!.
 
Back
Top Bottom