HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Kwa muda mrefu sana, wapendwa wetu akina dada wamekuwa wakibanwa na utamaduni wa asili kwa kusubiri kuimbishwa na wakaka. Najaribu kufikiria kuwa, hata kama wao wamempenda mkaka ni ngumu kutamka wazi wazi, na wakijitahidi sana, huishia kuonyesha mapenzi kwa vitendo au kwa kumtega mtu.
Mara nyingi wao wakifunguka huwa inaleta tafsiri isiyo nzuri sana ndani ya jamii wakati kiukweli ilipaswa na wao pia wapate nafasi nzuri ya kumtamkia yule wanayempenda maana ni haki yao kimsingi.
Kwa tamaduni za wenzetu wahindi (sina uhakika kama ni wote), wanawake ndiyo huenda kumpropose mwanaume na hii imekubalika kabisa.
Naomba tuchangie jamani, kuna tatizo gani watanzania wakikubaliana na huu utaratibu wa kugawa fursa sawa kwa wote ikiwemo kuwakubalia na kutokuwatafsiri vibaya wadada wanaofunguka mbele ya wakaka?
Nawasilisha.
HP