Fungua hapaaaa!

Nafikiri bado hatuna mfumo baada ya ule wa Mwl. Nyerere wa Elimu ya kujitegemea iliyohusisha ufundi mashuleni. system iliyopo ndiyo tegemeo la wazungu na mapendekezo yao katika mtaala wa elimu 'kutengeneza mtanzania asiyeweza kujitegemea bali kuwa tegemezi' kwahiyo usitegemee mfumo wa elimu ya tanzania kuwezesha mwanafunzi kufikia malengo yoyote zaidi ya kujifunza ku-repair na ku-cope and paste
 
Hivi mfumo wetu wa elimu unawawezesha wanafunzi kufikia malengo yao?

Karibu sana hapa JF. Naona unajifunza namna ya kuanzisha mada. Siku nyingine tulia, fikiria na andika jambo la maana. Sasa unapolazimisha wasomaji unakuwa kama hujaenda shule.
 
ukweli ni kuwa mada hii ni nzuri sana. ila kichwa cha habari kama inawezekana kifanyiwe marekebisho. Elimu yetu hata kule VETA naona ni mh!!! kuajiriwa na si kujiajiri. Na ukiajiriwa tu imepotea elimu yako.
 
Karibu sana hapa JF. Naona unajifunza namna ya kuanzisha mada. Siku nyingine tulia, fikiria na andika jambo la maana. Sasa unapolazimisha wasomaji unakuwa kama hujaenda shule.

mijitu mingine bwana,inajifanya inajuuuuuua....aah! hukulazimishwa kuisoma bwana.
 
Inavyoonekana unapenda sana habari za kimbea so hatuwezi kukushangaa kwan watu kama wewe tushawazoea
 
tatizo ni siasa ama viongozi wetu hawana utashi na nchi,ni kila wizara ikawa waziri mwenye taalamu husika nb vigezo
 
Malengo yatafikiwa tu ikiwa kutakuwepo na SERA YA ELIMU elimu ya msingi,sekondari ya juu ya ufundi n.k kusipokuwepo na hiyo sera atakuja waziri mwingine aanzishe somo la Kiswaenglish kama waziri fulani alivyoanzisha somo la Physchemistry,huku akijua anaharibu jamii ya wasomi Tanzania,hata hivyo mfumo wa elimu hivi sasa ni wa kucopy na kupest masomo yaleyale mtindo wa kusahihisha kutunga maswali uleule toka msingi hadi chuo,hata Thesis mada ni zilezile hii inatoa nafasi ya copy and paste.hakuna jipya.waalimu hawataki kuharibu ubongo wao kwa kufikiri mambo mapya.
 
Wakati wa Nyerere, kwenye shule zetu za UPE tuliimba shairi lifuatalo lihusulo elimu ya kujitegemea

Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, elimu ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ta sasa, yawafaa wananchi

Kulikuwa na consistency katika kufundisha

sasa hivi kila waziri wa elimu anakuja na mitaala yake.

Yaani mambo ni hovyo hovyo tu!!
 
Back
Top Bottom