Funga kazi!!!!

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Hii ni siku maalumu kwako. Tumia siku hizi kumshukuru Mungu na kumwomba Mungu kuhusu 2012. Mweleze Yeye mikakati yako yote uliyoipanga na umwombe akufanikishe katika hiyo. Omba kama Mungu atakavyokuongoza. Katika mkesha wa mwaka mpya nia muhimu ukitumia wakati huo kumweleza Mungu mambo hayo yote,(pamoja na familia yako kama unayo), imba nyimbo za sifa,na DUA za kumwomba Mungu.
Mwisho napenda kusema;
Mwaka mpya ni neema kubwa kutoka kwa MUNGU na wakati huo huo neema hii inaweza ikabadilika na ikawa ni adhabu na mitihani mikubwa kwa mwanadamu. La msingi ni kufuata mambo yanayompendeza Mungu. Kufanya hivyo, ndio mwaka wako utakuwa ni mwaka wa neema nyingi. Kinyume na hayo, mwaka wako utakuwa ni adhabu na mitihani na misukosuko mbali mbali ya kilimwengu..
Tumuombe Mungu Atusamehe madhambi yetu yaliopita na Atuwezeshe kuwa na afya njema katika mwaka huu mpya, na Atuteremshie baraka na neema katika mwaka huu mpya.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom