Fumbo gumu kuliko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Kumnenepesha mbuzi alingane na ng'ombe!
Kusahau kwamba walipakodi wakuwa Tanzania ni wachuuzi wadogowadogo ambao hawategemei umeme,
laiti kama wafanyibiashara wakubwa na viwanda vingelikuwa vinahtaji umeme na wangelikuwa wao ndo walipa kodi wakubwa basi hii leo msingelikuwa katika balaa la mgao wa umeme!!

Lakini kwa vile wao umeme hauathiri kodi za TRA basi na tutarajie wachuuzi na wajasiriamali wakiendelea kuathirika na kodi zinaokaribia kuwatoa roho...
Huku wenye viwanda wakineemeka kwa misamaha ya kodi na kuleta sokoni bidhaa duni na zisizokidhi viwango...

Hakuna anaegomea kulipa kodi kwa sababu hapati huduma stahiki...
Hakuna anaegoma kuilipa Tanesco kwa kutopata umeme anaouhitaji...
Hakuna anaegoma tumia maji machafu na yasiopatkana kwa muda wote toka mamlaka za maji 'taka' na safi!!
Hakuna anaesema kwanini bili imepanda na umeme hana!! (majibu rahisi "umeme unatumika sana kwa muda mfupi ili kufidia...!!!")

Ufumbuzi (kwa maoni yangu)
Kama hoja ni umeme tutumie umeme upepo (VETA WAPO WATUSAIDIE) ili tuepuke kuwalipa mafisadi pesa wasizostahili kwani sasa watatubalidilishia majina kila uchao.. sijui ikitoka hiyo Symbion power litakuja jina gani!!!
Tuchimbe visima vyetu... kwani hayo maji ya mamlaka na maji ya visima tunavyochimba bora hata haya yetu kwani tunaujua uchafu wetu!
Tuvune maji ya mvua.. alau ya kutosha miezi sita.

Kwa hayo machache tutajinasua na kuepukana na mafisadi...

Ahsanteni

Hakuna wa kulalamika...
Hakuna wa kudai...
Tunasubiri mpaka wakati wa uchaguzi ndipo tuanze kelele za kutafuta umaarufu...
 
Loh,mkuu una machungu kweli.
mkuu si utani..
wanakera, wanaudhi na wanatuchefua!
Hebu fikiria:
Mtu anaambiwa KILIMO KWANZA....
Hakuna miundombinu!
kama hakuna mvua je kuna mabwawa yatakayotumika kama njia mbadala?
mkulima amepewa tila je litakuwa na faida gani?
Alitembelee kwenye vilabu vya ulabu?
Asombee mbolea?
Hata sijui nisemeje? Ndio utamaduni wa Tanzania na sisi wenyewe labda!?
Hii si haki wanatutendea visivyo! wanatupa majembe na kutuonesha tukalime kwenye miamba!!
Wanatupa ndoano na kutuonesha tukavue samaki jangwani!!
 
Kweli hili ni fumbo gumu sana kulitatua hasa kwa watz wanaopigiwa kelele ya amani na utulivu kila siku, kwa hiyo wajanja wanaendelea kula nchi
 
Ndiyo maana wakati mwingine nasema bora tuuane tu kuliko huu ushenzi unaofanywa na serikali ya CCM, ila nikisema basi kesho napigwa ban eti natishia amani,potelea mbali nimeshasema
 
Laiti kama Tanzania kungelikuwa na WANASIASA... basi hizi ngonjera na blah blah sizingelikuwepo lakini kwa sababu wengi wa wale tunaoamini ni wanasiana kuwa ndio WAKOMBOZI wako si vile wanavyofikiriwa! kwani nao wanahitajika kujivua jumba la UANASIHASA!
Tunahitaji WANASIASA na si WANASIHASA,
Tunahitaji WAPAMBANAJI na si WABISHANAJI,
Tunahitaji watu wanaojali MASLAHI ya Taifa na si MASLAHI BINAFSI,
Tunahitaji kuwa WAMOJA na si KUTENGANA!
Tunahitaji ufumbuzi wa matatizo yetu na si kuambiwa matatizo tuliyonayo....
Waliozeeka wapishe damu changa ambazo hazijui upele na makovu ya zamani....
wajing'atue kila mahala wawaachie vijana wenye uwezo na uchungu waendeshe mambo...
laa si hivyo basi tutegemee mawazo mgando kuendelea kutawala nchi hii!!
 
Back
Top Bottom