fumanizi,usiombe kufumaniwa,valangati mtindo mmoja

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
4.jpg

Richard Bukos na Issa Mnally
USIOMBE yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Lulu John (mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe (siyo Mr. Nice), Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Lulu alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
SINEMA ILIKUWA HIVI
Kwa mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko ya kusaka bingo, alitonywa na mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif yupo kwenye nyumba hiyo ya wageni akiigagadua amri ya sita nje ya mkataba.
Lulu, baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje kapu’ ndipo akakodi bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye siyo mgeni wa uwanja huo wa mechi za kitandani.
Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio.
MPAKA CHUMBANI
Aliendelea kusema kuwa baada ya kutimba mahali hapo alikwenda moja kwa zote hadi kwenye chumba walichojichimbia wawili hao na kuanza kubamiza mlango huku akipiga mayowe ya kuomba msaada.
WENGINE WADHANI WAMEFUMANIWA
Huku akizidisha kupiga kelele akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu za watu wengine waliokuwa wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine ambao walitoka kwa kihoro wakidhani wamefumaniwa wao.
MUME ATIMKA NA NGUO YA NDANI
Aliendelea kusimulia mkasa kuwa watu walianza kujaa nje ya chumba hicho ndipo Abdulatif akafungua mlango kwa kasi na kutimka kama mkizi akiwa na nguo ya ndani pekee kisha akaruka fensi.
WATU WEWEEE!
Alisema kuwa wakati anachomoka nduki alimgonga kikumbo Lulu na kumwangusha chini huku akimwacha akigaragara ambapo watu walikuwa wakimkimbiza wakisema: “Weweee.”
VITA
Baada ya kunyanyuka na Abdulatif kumchomoka hivihivi ndipo vita kuu ikaanza dhidi ya mgoni wake.
ANG’ATWA PUA
Alisema kuwa ngumi za uhakika zilipigwa hadi yeye (Lulu) akang’atwa pua ambapo alitokwa na damu chapachapa usoni huku aliyefumaniwa akitafuta njia ya kujisitiri baada ya kuchaniwa nguo na kubaki mtupu.
Baada ya hali kuwa mbaya, Lulu alisema walitokea wasamaria wema na kuwatuliza ambapo yeye alikimbilia Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kumfungulia mgoni wake shitaka la shambulio la kudhuru mwili lenye jalada la kesi namba OB/RB/12675/2012.
Kwa mujibu wa Lulu, kitendo cha kumfumania mwanaume huyo kimemuumiza kwani amekuwa akimtunza kwa hali na mali na hakuweza kuamini kama angeweza kumsaliti.
Juhudi za kumpata Abdulatif hazikuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mitamboni hata hivyo zinaendelea.
KWA NINI USIOMBE YAKUKUTE?
Lilikuwa ni tukio la aina yake ambalo halikuishia pale gesti tu bali liliingia mtaani ambapo vitendo vya Abdulatif kukimbia akiwa mtupu na Lulu kung’atwa pua viligeuka gumzo na kila mtu akimuomba Mungu asikutwe na kasheshe kama hilo.
 
Attachments

  • 7.jpg
    7.jpg
    71 KB · Views: 365
  • 6.jpg
    6.jpg
    73.4 KB · Views: 436
"Huku akizidisha kupiga kelele akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu za watu wengine waliokuwa wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine ambao walitoka kwa kihoro wakidhani wamefumaniwa wao".Hiki kipande kimenifanya nicheke sana.Dah! Ugoni ni balaa.
 
mi pia iko kipande kimeniacha hoi,kumbe wanaoingia gesti wengi ni wenyeji siyo wageni tena wanaingia kwa muda mfupi tu si lazima walale
 
Masikini weee mi nawahurumia tu waliokatishwa starehe zao kwa fumanizi lisilo lao,hii inanikumbusha jamaa mmoja aliyeingia baa kashika panga na kupaza sauti leo aliye na mke wangu ni halali yangu,kilichofuata ni wanaume kama saba waliokuwa wamekaa na wanawake walitoka mbio..
 
du! hiyo kali,kumbe wengi wanachukua take away,chips funga
 
Masikini weee mi nawahurumia tu waliokatishwa starehe zao kwa fumanizi lisilo lao,hii inanikumbusha jamaa mmoja aliyeingia baa kashika panga na kupaza sauti leo aliye na mke wangu ni halali yangu,kilichofuata ni wanaume kama saba waliokuwa wamekaa na wanawake walitoka mbio..

Mkuu nimecheka sana,wezi ni wengi sana
 
Masikini weee mi nawahurumia tu waliokatishwa starehe zao kwa fumanizi lisilo lao,hii inanikumbusha jamaa mmoja aliyeingia baa kashika panga na kupaza sauti leo aliye na mke wangu ni halali yangu,kilichofuata ni wanaume kama saba waliokuwa wamekaa na wanawake walitoka mbio..
Du nimecheka kumbe bar nyingi muda wote waliokaa wa2wa2 sio mke na mume AFANAALEK
LULU namlaum sana kwani yeye hayo mambo ya kuwanyan'ganya wame za watu kayafanya sana
, sasa kwanini kamwadhiri mwenzake kwa kumvua nguo zote hata hicho kitauloo nimechukia sana maana kwa desturi yake hata huyo Abdulatif wataachana tu (Shame on you LULU)
 
Masikini weee mi nawahurumia tu waliokatishwa starehe zao kwa fumanizi lisilo lao,hii inanikumbusha jamaa mmoja aliyeingia baa kashika panga na kupaza sauti leo aliye na mke wangu ni halali yangu,kilichofuata ni wanaume kama saba waliokuwa wamekaa na wanawake walitoka mbio..
Hahahahahah!
 
Back
Top Bottom