Fumanizi la nguvu.....!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Leo nimeamua kumsindikiza mjukuu wangu kwa binti yangu wa mwisho, kwenda kwenye ofisi moja ambapo alikuwa na shida. Tulipofika kwenye hiyo ofisi (ambayo nimewazoea sana kwa kuwa nafanya nao kazi mara nyingi), tulipokelewa na mmoja wapo wa ma-secretary ambaye ametupa appointment ya kuonana na boss wake kesho. Basi ikabidi tuage ila wakati tunaondoka, niligeuka na macho yangu yakagongana na secretary mwingine ambaye alikuwa anatusikiliza muda wote huku macho yake kayakazia kwa dogo muda wote!! Yaani alikuwa kadondosha bonge la smile..kama lile linalomfanya mtu adondoke udenda (to salivate chini na juu aisee)!!

Nikamwangalia na huyo mjuu wangu (alikuwa ametoka bomba kishenzi...dizaini ya form 6 fulani), kavaa ki-Tshirt cha kubana na jeans bomba...Nikakumbuka kuwa bibi huwa anasema kwamba huyu dogo ni bonge la handsome (ingawa mie huwa sijui hawa akina bibi wanatumia vigezo gani)!!

Mzee mzima nami nikaishia kucheka na kuondoka...baadaye ndo akili ya kiume ikarudi. Nikasikitika kwamba, kwa nini mtoto wa watu sikupatia tip kuwa dogo bado yuko available??? Yaani, wale enzi zangu wangesema
"hajazuiliwa chini na juu"



Babu DC!!
 
Babu hufai wewe. Usije muingiza mkenge mjukuu atii, sio kila king'aacho ni dhahabu, japo it doesnt have to glitter to be precious.
 
Babu hufai wewe. Usije muingiza mkenge mjukuu atii, sio kila king'aacho ni dhahabu, japo it doesnt have to glitter to be precious.


Sijafanya kitu komando wangu King'asti,

Ni mawazo tu ya enzi zetu yamenijia nikahisi kuwa may be sijawatendea haki wajukuu...

Halafu...., kuna mdau mmoja nilikutana naye wakati bado ni nina vile vipele vya usoni na navaa don't touch ma shoes, akanambia kuwa wakati mwingine smile inasababisha mafuriko...sina hakika kama ni kumbukumbu za kweli au hallucinations!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Babu waonaje huyo mjukuu ukamuachia mikoba ya ukaguzi?


Kwani nani anayefanya ukaguzi?


Mkuu naona umeanza kuchanganya madesa....

Babu DC huwa hafanyi biashara hiyo, si kwa ujira wala hisani!!

Umeelewa wewe Judgement???

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Babu Dc si ukubali tu kwamba weye ndiye uliyedondokewa na bahati ya mtende, kumbuka una miaka dahari hujapata smile la tineja. Ng'ombe hazeeki maini ati
 
Babu Dc si ukubali tu kwamba weye ndiye uliyedondokewa na bahati ya mtende, kumbuka una miaka dahari hujapata smile la tineja. Ng'ombe hazeeki maini ati


Huu sasa ni uchokozi,

Na uzee wote huu hizo smiles nitaweza kuzitenda haki mie?

Niacheni jamani nipe PPF yangu!!

Babu DC!!
 
kaazi kweli kweli,ujana maji ya moto ujue.


Ndo maana kila siku zinavyokwenda mtu unazidi kuogopa kifo...

Ukifikiria kutangulia ukamuacha bibi na wajukuu unakaribia kufa kabla ya muda wenyewe!!

Hivi hakuna dawa za kurudisha umri na kila kitu nyuma (just to rewind)??

Babu DC!!
 
Mvua kubwa sana inanyesha hapa Jengo la Hali ya Hewa kama walivyotabir. Vipi huko kwenu jamani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom