Fumanizi la Mwaka.... Duh!

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
jamani nimepata shuhudia fumanizi nyingi, pia nimepata simuliwa mengi bt sijawahiona KALI KAMA LILE ambalo Mke na hawala yake walipogongwa na kufungwa pamoja na Nyoka aina ya Chatu kwa masaa kazaa guest hausi fulani mpaka mume na mganga wake walipo watokea kuwafumania na kuwafungua. Tukio hili si'lamuda, nadhani wiki 4 zimepita sasa.
Swali; je kwa mwendo huo ndio kutatua tatizo? Mme anataka tuelewe yeye haibiwi au ndio uchawi? Unadhani hata km kutakuwepo na msamaha ndoa itakuwa na amani? Itakuwepo or ndio kwishinei? Tujadili..
 
Uaminifu ni jambo jema sana, ukikosa kuaminika huna tofauti na mzoga au mfu kwa lugha nyepesi. Siku za mwizi, alidhan ataendela kudanganya siku zote, Mungu hachunguzwi wala kudhihakiwa.

Poleni sana wale msio waaminfiu anzeni leo hamajachelewa.
 
Dawa ya uchawi ni kikombe cha babu. Kunywa in advance kamwe hutodhurika na uchawi
 
1.KAMA UNAMPENDA MWENZIO HUWEZI KUMUWEKEA MAMITEGO YA AJABU AJABU,NA YA NINI ULIMUOA KAMA HUMUAMINI?
2.NA AKIGUNDUA UMEMTEGA HALAFU AKATEGUA.....BASI ATAKUIBIA MILELE NA MILELE.
3.KUMUWEKEA TEGO HAIMALIZI TATIZO,MTU KAZOEA LABDA ROUND TISA KWA SIKU ATAZIPATA ZOTE KWAKO???
4.JIULIZE KWANZA TATIZO LIKO WAPI.
Kwa ujumla mambo ya madawa madawa kwenye mapenzi hayafai kabisa.
 
UAMINIFU. Mpaka kuwekewa tego ni kwamba amezidisha. Hivi kwa nini kama hupati kile ulichotegemea kwa mwenza wako usiachike instead unaabishwa? Kama ulizoea tisa na mumeo hawezi,ni chanzo tosha cha wewe kuachwa salama bila kinyongo na ukaendeleza ukahaba wako.

Nachukia sana watu wasiowaaminifu kwenye ndoa zao ukiuliza analeteta za sababu za kishenzi.
 
sasa ndio umuendee mwenzi wako kwa mganga? Si uchawi huo jaman?
 
1.KAMA UNAMPENDA MWENZIO HUWEZI KUMUWEKEA MAMITEGO YA AJABU AJABU,NA YA NINI ULIMUOA KAMA HUMUAMINI?
2.NA AKIGUNDUA UMEMTEGA HALAFU AKATEGUA.....BASI ATAKUIBIA MILELE NA MILELE.
3.KUMUWEKEA TEGO HAIMALIZI TATIZO,MTU KAZOEA LABDA ROUND TISA KWA SIKU ATAZIPATA ZOTE KWAKO???
4.JIULIZE KWANZA TATIZO LIKO WAPI.
Kwa ujumla mambo ya madawa madawa kwenye mapenzi hayafai kabisa.
Tall kwahiyo ni bora kupata msaada sio?
 
ukishaona unamwekea mpenzi wako mitego ujue huna mapenzi, uaminifu wala maana
 
Natumai hudanganyi hapo,acha nisubiri foleni ipungue nami nikapate kikombe kwa Babu.lol!

Ni kweli cup ya babu ni kinga tosha kwa wachawi, kuna jamaa walienda na hirizi zao sasa dawa ya babu inawatesa wako nyaka nyaka hawajiwezi. Ukienda kwa babu haikisha uko msafi kiroho na huna mahirizi au majini kwani yanapigwa hapo hapo na kukatika.

babu hoyeeee
 
Kwa inavyosemekana ni kwamba uchawi hauvuki bahari sa huyo jamaa haoni kama kuna wezekano wa bibie kwenda kufanyia uo upuuz zenj. So kama vip labda amfungie meter.
 
Back
Top Bottom