Full Text: Hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi Agosti 2012


HOTUBAYA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 AGOSTI, 2012

Utangulizi
NduguWananchi;
Kilamwisho wa mwezi nimekuwa nazungumza na taifa kuhusu masuala mbalimbali muhimukwa taifa letu na watu wake. Leo ninamambo mawili ya kuzungumza nanyi. Lakini, kama ilivyo mazoea yetu hatuna budi kwanza tumshukuru MwenyeziMungu, muumba wetu, kwa kutujaalia baraka zake, za uhai na uzima na kutuwezeshakuwasiliana leo tarehe 31 Agosti, 2012.

NduguWananchi;
Jambola kwanza ninalotaka kuzungumzia leo ni zoezi la Sensa ya Watu na Makazilililoanza tarehe 26 Agosti, 2012 ambalo linatarajiwa kumalizika tarehe 01Septemba, 2012. Mtakumbuka kuwa tarehe25 Agosti, 2012 nilizungumza nanyi na kuwaomba mjitokeze kwa wingi na muwapeushirikiano unaostahili Makarani wa Sensa watakapopita majumbani mwenukutekekeza wajibu wao. Tumebakisha sikumoja kufikia kilele cha sehemu ya kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka2012.

Napendakuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu wote kwa kujitokeza kwa wingikuhesabiwa. Mpaka sasa mwelekeo ni mzurina ugumu ulioonekana kuwepo pale mwanzoni uliendelea kupungua siku hadi sikukadri utekelezaji wa zoezi ulivyokuwa unaendelea. Kwa mwenendo huu nina matumaini makubwa kuwaSensa ya mwaka huu itakuwa na mafanikio mazuri.

Ndugu Wananchi;
Napendakutumia nafasi hii kutoa wito kwa wale wote ambao hawajahesabiwa wafanye hivyo.Naomba waitumie siku moja iliyosalia yaani tarehe 1 Septemba, 2012 kufanyahivyo. Aidha, namuomba Mkurugenzi Mkuuwa Ofisi Kuu ya Takwimu ya Serikali ya Muungano na Mtakwimu Mkuu wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha kuwa kasoro zo zote zilizopo mahali po potezinatafutiwa ufumbuzi ili mambo yakamilike bila upungufu wowote.

NduguWananchi;
Baadaya kazi ya Makarani wa Sensa kuhesabu watu kufikia kilele chake, tarehe 2Septemba, 2012, linaanza zoezi la kuwashughulikia wale ndugu zetu ambaowatakuwa bado hawajahesabiwa. Itakuwepofursa ya siku saba kwa watu hao kuhesabiwa. Watatakiwa wao wenyewe kupeleka taarifa zao kwa Wenyeviti wao waSerikali za Mitaa au Vijiji. Taarifahizo zitafikishwa kwa Kamishna wa Sensa kwa ajili ya kujumuishwa. Baada ya muda huo kwisha, zoezi la kuhesabuwatu litakuwa limefika mwisho. Yuleambaye atakuwa hakutumia fursa hizo mbili atakuwa amekosa kuingizwa katikahesabu ya Watanzania ya mwaka 2012. Napenda kuwasihi ndugu zangu, Watanzania wenzangu kutumia siku ya tarehe1 Septemba, 2012 kuhesabiwa na kamahapana budi basi tumia fursa ya kupeleka taarifa zako kwa Mwenyekiti wako waMtaa au Kijiji katika siku saba zinazofuatia siku hiyo ili nawe ujumuishwe.

NduguWananchi;
Baadaya kazi ya kuhesabu watu kwa namna zote mbili kufikia mwisho, itaanza kazi yauchambuzi na kuunganisha takwimu na taarifa zilizokusanywa. Kazi hiyo ni muhimu na ni kubwa hivyo inahitajiumakini na uangalifu wa hali ya juu sana, kwani ikikosewa zoezi zima la Sensalitaingia dosari. Nafarijikakuhakikishiwa na Viongozi wa Sensa na Wakuu wa Idara za Takwimu za Serikalizetu mbili, kwamba wanatambua ukweli huo na wajibu wao. Wameniarifu kwamba kama mambo yatakwenda kamailivyopangwa, matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kuhusu idadi ya watuna jinsia zao yatatolewa mwishoni mwa mwaka huu. Taarifa nyingine zitafuatabaadaye. Narejea kuwasihi Watanzaniawenzangu kuwapa nafasi wataalamu wetu wafanye kazi yao kwa ufanisi ili tupatematokeo yaliyo sahihi.
Mpakana Malawi
NduguWananchi;
Jambola pili ninalotaka kuzungumza nanyi leo ni kuhusu mpaka baina ya Tanzania naMalawi katika Ziwa Nyasa. Kama mjuavyo, kwamiaka mingi nchi zetu mbili zinatofautiana kuhusu wapi hasa mpaka uwe. Sisi, Tanzania, tunasema mpaka upo katikatiya ziwa wakati wenzetu wa Malawi wanasema upo kwenye ufukwe wa ziwa upande waTanzania. Kwa maneno mengine wanasema ziwalote ni mali ya nchi yao.

Utata kuhusu mpaka wetu katika ZiwaNyasa haujaanza leo. Ulikuwepo tanguwakati nchi zetu mbili zikiwa bado zinatawaliwa na wakoloni na kuendelea baadaya Uhuru wa nchi zetu mpaka sasa. Jambokubwa lililo tofauti na jipya ni kwamba hivi sasa, nchi zetu mbili zimeamuakukaa mezani na tunalizungumza suala hilo.
Chimbukola Mzozo
NduguWananchi;
Chimbuko la mzozo wa mpaka ulioposasa, baina ya nchi zetu mbili jirani, rafiki na ambazo watu wake ni ndugu, nimakubaliano baina ya Waingereza na Wajerumani kuhusu mpaka baina ya nchi zetuyaliyofanywa tarehe 1 Julai, 1890. Makubalianohayo yajulikanayo kama Mkataba wa Heligoland, (The Anglo-Germany HeligolandTreaty) yalitiwa saini kule Berlin, nchini Ujerumani baina ya Waingereza naWajerumani. Wakoloni hao walikubalianakuhusu mipaka baina ya makoloni yao na baina yao na wakoloni wenginewaliopakana nao. Kwetu sisi hayo ndiyomakubaliano yaliyoweka mipaka ya Tanganyika na ile ya Zanzibar na majirani zake. Kwa upande wa Ziwa Nyasa, Waingereza naWajerumani walikubaliana kuwa mpaka uwe kwenye ufukwe wa nchi yetu. Kwa maana hiyo ziwa lote likapewa nchi yaMalawi. Kwa upande wa Mto Songwe mpakaulikuwa ufukweni upande wa Malawi kwa maana hiyo mto wote ukawa upande waTanzania.

Ndugu Wananchi;
Katika kipengele cha Sita(Article VI) cha Mkataba huo, wakoloni hao walikubaliana kufanya marekebisho yampaka mahali po pote kama itakuwa ni lazima kufanya hivyo, kulingana namazingira na hali halisi ya mahali hapo. Kwa mujibu wa kutekeleza matakwa ya kipengele hicho mwaka 1898 Tume yaMipaka iliundwa. Ilianzia kazi katika MtoSongwe kuhakiki mpaka baina ya nchi yetu na Malawi. Tume ilikubaliana kuhamishampaka kutoka ufukweni mwa Mto Songwe upande wa Malawi na kuwa katikati yamto. Baada ya uhakiki katika eneo hilokukamilika, mwaka 1901 mkataba mpya ulisainiwa kuhusu mpaka huo.
Tume iliendelea na kazi yake katika ZiwaTanganyika na kuhamisha mpaka kutoka ufukweni hadi katikati ya ziwa na mkatabampya kusainiwa mwaka 1910. Tume iliendeleakatika ziwa Jipe ambapo mpaka ulihamishwa pia hadi katikati ya ziwa.

Ndugu Wananchi;Bahati mbaya Tume hiyohaikufanikiwa kufanya uhakiki wa mpaka katika Ziwa Nyasa kutokana na kutokeakwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kati ya mwaka 1914 - 1918. Kama tunavyokumbuka, Waingereza na Wajerumaniwaligeuka kuwa maadui na kupigana hata hapa nchini. Baada ya vita hivyo na Ujerumani kushindwa, Barazala Umoja wa Mataifa (The League of Nations) liliikabidhi Uingereza udhamini wa Tanganyika.Hivyo, Uingereza ikawa inatawala Malawi na Tanganyika.

Ndugu Wananchi;
Wakati Tume ya Uingereza naUjerumani ilipokuwa imekufa, Tume ya Mipaka kati ya Uingereza na Urenoiliendelea na kazi. Matokeo yake, mwaka1954, Uingereza na Ureno zilitengua mkataba wao wa mwaka 1891 ulioweka mpaka waZiwa Nyasa katika ufukwe wa mashariki ya Ziwa, yaani kwenye ufukwe wa Msumbiji,na kuuhamishia katikati ya ziwa.

Ndugu Wananchi;
Jambo la kustaajabisha ni kuwa,Waingereza walioona umuhimu na busara ya kurekebisha mpaka kati ya Malawi naMsumbiji, hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo kati ya nchi yetu na Malawi. Inashangaza, kwa sababu wakati huo Uingerezailikuwa mtawala wa nchi zetu mbili hivyo kazi ya marekebisho ingekuwa rahisi,lakini hawakufanya hivyo. Na, baya zaidini kuwa hata pale watu wa nchi yetu walipotakakupatiwa ufafanuzi na kutaka ukweli uwekwe wazi kuhusu mpaka hawakusikilizwa. Watu walitaka ufafanuzi kwa sababuinasemekana kati ya mwaka 1925 na 1938, taarifa ya Uingereza kwa Umoja wa Mataifaziliweka mpaka katikati ya ziwa. Lakini,kuanzia mwaka 1948 mpaka ukawekwa tena ufukweni.

Ndugu Wananchi;
Mwaka 1959, 1960 na 1962, suala lampaka wa Malawi lilijitokeza tena na kujadiliwa na Bunge la Tanganyika, wakatiule lilijulikana kuwa Baraza la Kutunga Sheria, (Legislative Council – LEGCO). Hoja ya Wabunge wa Tanganyika ilikuwa kwamba mpakakuwekwa kwenye ufukwe wetu kunawanyima wananchi wa Tanganyika wanaoishi kandokando ya ziwa haki yao ya msingi ya kutumia maji kwa kunywa, kuoga, kuvua samakina kupata manufaa mengine yatokanayo na ziwa bila ya kuomba ridhaa ya Serikaliya Koloni la Nyasaland kama Malawi ilivyokuwa inajulikana wakati ule. Hoja iliyotolewa ilikuwa kwamba Serikali yaTanganyika ijadiliane na Serikali ya Nyasaland kupitia Serikali ya Malkia waUingereza ili ufumbuzi upatikane. Wakolonihawakujali na wala hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka Tanganyika ikapata uhuruwake tarehe 9 Desemba, 1961 na Malawi kupata uhuru wake mwaka 1964.
Juhudiza Kubadili Mpaka wa Ziwa Nyasa Baada ya Uhuru
NduguWananchi;
Wakatitulipopata Uhuru mwaka 1961, mjadala kuhusu mpaka wa Tanganyika na Malawiuliendelea Bungeni, ambapo ilitolewa hoja kwamba zifanyike juhudi za makusudiza kuanzisha na kuendeleza mazungumzo ya kurekebisha mpaka huo kwa manufaa yawananchi wote wanaoishi pembezoni mwa ziwa. Iliamuliwa kwamba tusubiri mpaka wenzetu wa Malawi wapate uhuru ili yafanyikemazungumzo baina ya nchi mbili huru. Kulijengeka matumaini kuwa mambo yangekuwa rahisi. Bahati mbaya haikuwa hivyo na kwamba mamboyakageuka na kuwa magumu na ya uhasama. Miakamitatu baada ya Malawi kupata Uhuru wake (1964), kunako tarehe 3 Januari 1967,Serikali ya Tanzania iliandika barua kwa Serikali ya Malawi kuelezea tatizo la mpakawa ziwani na kupendekeza nchi zetu mbili zizungumze na kulitafutiaufumbuzi.

Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri tarehe 24 Januari,1967, Serikali ya Malawi ikajibu kukiri kupokea barua hiyo na kuahidi kuwa itatoamajibu baada ya muda si mrefu. Hatahivyo, tarehe 27 Juni, 1967, Rais Kamuzu Banda akilihutubia Bunge la Malawi, alikataamaombi ya Tanzania. Alisema hayanamsingi na alidai kuwa kihistoria Songea, Mbeya na Njombe ni sehemu yaMalawi. Hivyo basi, mazungumzo yakafa.

Tanzania haikukata tamaa. Alipochaguliwa Rais wa Pili wa Malawi, MheshimiwaBakili Muluzi, juhudi zilifanyika lakini nazo hazikufika mbali. Bahati nzuritarehe 9 Juni, 2005, Rais wa Tatu wa Malawi, Mheshimiwa Bingu Wa Mutharika,ambaye sasa ni marehemu, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa nchi yetu wakatiule, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kushauri nchi zetu zifanye mazungumzokuhusu mpaka wa ziwani. Alipendekeza iundweTume ya Pamoja itakayojumuisha Mawaziri na Wataalamu kutoka nchi zetumbili. Tume hiyo itatoa mapendekezo kwaMarais wa nchi zetu mbili ambayo yatakuwa msingi wa majadiliano baina yao. Alisisitiza umuhimu wa kulipatia ufumbuzisuala hilo.

Ndugu Wananchi;
Kwa kuwa ilikuwa kipindi champito kuelekea kuchaguliwa Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Benjamin Mkapahakuwahi kuishughulikia barua hiyo. Nilipoletewa barua hiyo nikaijibu kukubaliushauri na mapendekezo yake. Aidha, nilipendekezaWizara na Idara zipi za Serikali zetu zishirikishwe katika Tume hiyo. Bahati nzuri Rais wa Malawi alikubalimapendekezo yangu pamoja na lile la kwamba Malawi waitishe mkutano wa kwanza waTume hiyo.

Ndugu Wananchi;
Mpaka sasa mikutano mitatu ya Tumeya Pamoja imeshafanyika, wa kwanza ulifanyika tarehe 8 – 10 Septemba,2010. Mkutano wa pili ukafanyika tarehe27 – 28 Julai, 2012 hapa Dar es Salaam na wa tatu ukafanyika Mzuzu na Lilongwetarehe 20 – 27 Agosti, 2012. Hatua kadhaa zimepigwa lakini bado muafakahaujapatikana kwa maana ya madai yetu ya kutaka mpaka uwe katikati ya ziwa namadai yao kuwa mpaka ubaki ufukweni kwetu kama ilivyo kwenye Mkataba wa Heligoland wa Julai1, 1890. Hoja ya wenzetu ni kuwa huondiyo mpaka tuliorithi wakati wa uhuru. Wanataka tuthibitishe hivyo na kwamba tuzingatie kauli ya OAU yakuheshimu mipaka tuliyorithi kwa wakoloni. Wananukuu kauli ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere akisisitiza hoja hiyo katika mkutano wa OAU mwaka1963.
Hojaza Msingi za Kutaka Mpaka Uwe Katikati ya Ziwa
NduguWananchi;
Kwa upande wetu tumekuwa na hojakadhaa za kutaka mpaka uwe katikati ya ziwa. Ya msingi kabisa ni ukweli kwamba Mkataba wa Heligoland umekosewa kwakuamua kuwanyima wananchi wa Tanzania wanaoishi ufukweni mwa ziwa haki yao yamsingi ya kutumia maji na rasilimali zilizomo katika Ziwa Nyasa. Zipo sababu kadhaa kwa upande wetu kudaihivyo. Mojawapo ni sheria ya kimataifa inayoelekezakwamba po pote kwenye maji ya asili kama vile ziwa na mito iliyopo kati ya nchimbili mpaka huwa katikati. Ndiyoutaratibu unaotumika duniani kote, na mifano iko tele. Kwa nini iwe tofauti katika ziwa Nyasa na kwaupande wa Tanzania tu wakati kwa upande wa Msumbiji mpaka upo katikati ya ziwa?

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Mto Songwe, mpakabaina ya nchi zetu mbili upo katikati. Iwejehapa kanuni hiyo itambulike na kuheshimiwa lakini isiwe hivyo ziwani? Kama nilivyoeleza awali, mwanzoni Mto Songwe woteulikuwa umewekwa upande wetu, lakini Tume ya Mipaka iliyoundwa mwaka 1898ilifanya marekebisho na kuweka mpaka katikati ya mto. Kama nilivyokwishagusia kwenye ziwa hilo hilola Nyasa kwa upande wa Msumbiji mwaka 1954 mkataba wa mwaka 1891 ulioipa Malawiziwa lote ulirekebishwa na mpaka kuwekwa katikati. Kwa nini isifanyike hivyo hivyo kwa upande waTanzania? Hivi hasa ni kipi ambachowenzetu wa Msumbiji walichotuzidi na kustahili kupata haki yao ya msingi ya kumilikina kutumia maji ya Ziwa Nyasa ambacho sisi Tanzania tumepungukiwa?

Ndugu Wananchi;
Maji ni zawadi ya Mwenyezi Mungukwa wanadamu wake, waitumie kwa uhai na maendeleo yao. Iweje leo, kwa watu wanaoishi pembeni mwaziwa hilo hilo wengine wapewe na wengine wanyimwe haki ya kulimiliki na kulitumia?Kwa nini wanyimwe haki ya kunufaika na zawadi hiyo? Hivi kauli ya wakoloniwaliokaa Berlin ya kusema fulani apate na fulani asipate inatosha? Hivi kweli ni rahisi kiasi hicho?

Mpaka wa kwenye maji ni tofautina ule wa nchi kavu. Huu una rasilimaliambayo huwezi kuamua kumnyima mwanadamu mwingine anayeishi pembeni yake kwavile haina badala yake. Unapowaambiawatu wa Mbamba Bay, Liuli, Lituhi, Manda, Ngonga, Matema, Mwaya, Itungi nawengineo waishio kando ya ziwa kuwa maji hayo si yao bali ni mali ya Malawihawakuelewi na watakushangaa sana. Watadhani umechanganyikiwa kwani tangu waumbwe wamekuwepo hapowanamiliki na kutumia maji ya Ziwa. Unatakawafanyeje? Waende Malawi kuomba kibalicha kuyatumia? Wao watakuuliza swalimoja tu “hivi hao wenzao wanaoishi ng’ambo ya pili wamewazidi nini katikaubinadamu wao hata wapewe maji yote na wao wanyimwe?”

Ndugu Wananchi;
Kwa maana halisi ya Mkataba waHeligoland tangu tarehe 1 Julai, 1890, wananchi wa upande wa Tanzania wamekuwawanakunywa, kuoga, kuvua samaki na kusafiri katika maji ya Ziwa yasiyokuwa yaobali ya nchi nyingine. Na kwa kuwa wamekuwawanafanya hivyo bila ya kupata kibali cha Malawi wamekuwa wanaiba maji nasamaki wa Malawi na kusafiri isivyo halali katika nchi ya watu. Jambo hili haliingii akilini hata kidogo. Ndiyo maana tunadai haki yetu stahili.

Ndugu Wananchi;
Na hiyo pia, ndiyo maana, busara na hekima ya Sheria ya Kimataifa kuhusumpaka wa kwenye maji kuwakatikati. Sheria hii inazingatia halihalisi ya maisha ya jamii inayozunguka ziwa ambayo imekuwa inalitegemea maishayao yote kwa shughuli zao za kuwapatia uhai na maendeleo yao. Haiwezekani kuwatenganisha watu waishio kandoya Ziwa Nyasa kumiliki na kutumia maji hayo na rasilimali zake. Hawataelewa wala kukubali kuambiwa kuwa wanatumiamaji na rasilimali za ziwani kwa hisaniya nchi ya Malawi.

Kwa watu waliokuwepo tangu Mungu anawaumbawao na wenzao wa ng’ambo ya pili, siyo sawa na siyo haki hata kidogo kuwafanyiahivyo. Kwe kweli ni unyanyasaji wa haliya juu. Ndiyo maana wazee wetu walidaisuala hili liwekwe sawa wakati wa ukoloni, kabla na baada ya Uhuru. Na ndiyo maana na sisi tunafuata nyayo zaokatika madai haya ya haki.

Ndugu Wananchi;
Kuna mambo mengine mawili ambayo yanatufanyatudai haki ya kumiliki na kutumia Ziwa Nyasa. La kwanza ni ule ukweli kwamba mito mingi ya Tanzania nayo inachangiakujaza maji katika ziwa. Iweje leo maji yanayojazaziwa ni jambo jema, lakini yakishaingia ziwani, ziwa hilo si mali yao wenyemito hiyo tena na wakiyatumia wanaiba mali ya watu wengine. Hivi kwelindivyo wanavyostahili kufanyiwa watu wanaotunza vyanzo vya mito hiyo na kuruhusumaji yake kutiririka na kuingia ziwani?

Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ni kwamba mpaka waTanzania na Malawi kuwa ufukweni kunafanya ukubwa wa nchi zetu kuwa haujulikanikwa uhakika. Unategemea mabadiliko kutokanana kujaa na kupungua kwa majiziwani. Kunafanya mpaka wa nchi kuwahautabiriki na unaweza kuwa tatizo siku moja mbele ya safari. Isitoshe kuwa na nchi isiyojulikana ukubwawake nalo ni tatizo la aina yake. Ndiyomaana mpaka kuwa katikati ya ziwa ni bora zaidi.

Ndugu Wananchi;
Kama nilivyokwishasema, chimbukola mzozo huu ni mkataba wa Heligoland ambao umepanda mbegu ya fitina baina yanchi zetu. Bahati mbaya sana Tume yaMipaka haikumaliza kazi ya kuhakiki mipaka yote ya nchi yetu na majirani zake kufuatiakuzuka kwa Vita Kuu ya Kwanza mwaka 1914. Ujerumani ikashindwa vita na koloni lake kuwa sehemu ya himaya yaUingereza. Bahati mbaya kwetu Waingerezawaliotawala nchi zetu mbili tangu 1918 hawakuchukua hatua za kurekebisha mpakakabla ya uhuru wa nchi zetu. Ni maoni yetukuwa nchi zetu sasa zifanye kile ambacho hakikufanywa na Tume ya Mipaka ya wakoloni– Waingereza na Wajerumani. Tukifanyesisi wenyewe kama nchi mbili huru kwa njia ya mazungumzo.
Bahati mbaya majaribio ya mwaka1967 hayakufanikiwa. Bahati nzurikufuatia uamuzi wa kijasiri wa marehemu Rais Bingu wa Mutharika nchi zetu sasa zinazungumza. Bado hatujafikia muafaka kuhusu kurekebishampaka na huenda ikatuwia vigumu kufikia muafaka. Jambo linaloleta faraja, hata hivyo, ni kuwasote wawili tumekubaliana kuwa tutafute mtu wa kutusuluhisha.

Ndugu Wananchi;
Hayo ndiyo matokeo ya mazungumzoya Tume yetu ya pamoja tangu ngazi ya Wataalamu, Makatibu Wakuu mpaka kwaMawaziri, katika vikao vya Mzuzu na Lilongwe kati ya tarehe 20 – 27 Agosti,2012. Katika mkutano wao wa tarehe 27Agosti, 2012 Mawaziri husika wa nchi zetu chini ya uongozi wa pamoja wa Waziriwa Mambo ya Nje wa Malawi, Mheshimiwa Ephraim Chiume na mwenzake wa Tanzania,Mheshimiwa Bernard Membe, wameafiki mapendekezo hayo. Aidha, wamekubaliana kuwa pande zote mbiliwakutane tena Dar es Salaam kati ya tarehe 10 – 15 Septemba, 2012 kukubalianajuu ya usuluhishi wa aina gani unafaa.

Ndugu Wananchi;
Mtakubaliana nami kuwa tumepiga hatua muhimukuelekea kwenye kupata ufumbuzi wa kudumu wa suala hili. Hata hivyo, bado safari ni ndefu na huendaikawa na magumu mengi. Maombi yangu kwa viongozina wananchi wa Tanzania na Malawi ni kuendelea kuunga mkono jitihada hizi. Tuwaunge mkono wataalamu na Mawaziri wetu iliwafanikishe vizuri jukumu lao. Tuzingatie na kuheshimu walichokubaliana Lilongwe kuwa viongozi nawananchi wa nchi zetu wajiepushe na kutoa kauli au kufanya vitendo vinavyoweza kuchafuahali ya hewa, kuleta uchochezi na kuathiri majadiliano yanayoendelea.
Nawasihi Watanzania wenzangu kuzingatiaushauri na rai hiyo ya Mawaziri na wataalamu wetu, ili kuwe na mazingira mazuriya mazungumzo na kuwezesha mzozo huu kuisha kwa amani na kirafiki.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napendakusisitiza kuwa si makusudio yangu wala ya Serikali yetu kutafuta suluhisho lasuala hili kwa nguvu ya kijeshi. NawahakikishiaWatanzania wenzangu kuwa hatuko vitani na Malawi na wala hakuna maandalizi ya vitadhidi ya jirani zetu hawa kwa sababu ya mzozo wetu wa mpaka katika Ziwa. Ondoeni hofu na endeleeni na shughuli zenu zaujenzi wa taifa letu kama kawaida.

Nilimhakikishia hivyo Rais waMalawi, Mheshimiwa Joyce Banda nilipokutana naye Maputo, Msumbiji tarehe 18Agosti, 2012. Tanzania haina mpango wakuingia vitani na Malawi. Mimi nawenzangu Serikalini tunaona kuwa fursa tuliyoitafuta miaka mingi ya kukaa nandugu zetu Malawi kuzungumzia suala hili lenye maslahi kwetu sote sasatumeipata. Hatuna budi kuitumiaipasavyo. Naamini, tukifanya hivyo,inaweza kutufikisha pale tunapopataka. Ni muhimu, kwa ajili hiyo kwa pande zetumbili, kuipa fursa ya mazungumzo nafasi ya kuendelea bila ya vikwazovisivyokuwa vya lazima.

Ndugu Wananchi;
Kwasababu hiyo basi , napenda kutumia nafasi hii kuwasihi ndugu zetu wa vyombo vyahabari na wanasiasa wenzangu tuepuke kauli au matendo yatakayovuruga mazungumzona kuchochea uhasama kati ya nchi zetu mbili jirani na rafiki. Kuna manufaa makubwa ya kumaliza mzozo wetukwa njia ya mazungumzo kuliko kwa njia ya vita. Kufikiria sasa kutumia njia nyinginezo hasa za nguvu za kujeshi, siwakati wake muafaka. Aidha, tukitumianjia ya vita, badala ya kuwa tumepata suluhisho inaweza kuwa ndiyo mwanzo wamgogoro mpana zaidi. Tuendelee kuwaungamkono wawakilishi wetu katika Tume yetu ya pamoja. Naahidi, Serikali itakuwa inawapa taarifakadri mazungumzo yetu na wenzetu wa Malawi yatakavyokuwa yanaendelea. Nina hakika tutamaliza salama.
MunguIbariki Tanzania!

MunguIbariki Afrika!

Asantenikwa Kunisikiliza


Asante kwa kukusikiliza wakati tumesoma
 
Wandugu. lkn watu wengi waliosoma historia ya mgogoro huu walieleza vizuri mambo haya. hapa jamvini wakaaitwa wasaliti au wamalawi walio mafichoni. na sasa tumesikia ukweli huo. tuwe tunazungumza kisomi.

Mimi nimeandika sana kuhusu hili. Waliojionyesha kwamba wana akili ngumu kuelewa wala sijahangaika kuwabembeleza eti wasiniite mmalawi. Sanasana jinsi siku zinavyoenda ndivyo wanaumbuka kwamba uzalendo ni kuhakikisha unalipa taifa picha kwamba ni taifa lenye vichwa vilivyoenda shule.

Kama ni uzalendo wa kurukaruka basi wamasai ni warukajirukaji sana na sime zao hadi wanagalagala eti wamepandwa na mori.

Huo ndiyo uzalendo wa kipumbavu uliowatawala mambumbumbu wasiojua chochote kuhusu mgogogoro zaidi ya kujua kubonyeza keyboard na kutuma post JF!
 
Kumbe tumekuwa tukifanya uhuni kudai mpaka uko katikati ya ziwa! Hoja tunazo lakini hatukustahili kupotosha umma kwamba mpaka ni kati ya ziwa.
Sasa hivi ndo tunaomba tuweke mpaka upya, hiyo inaeleweka lakini siyo hizo hadithi za tangu enzi ya JK Mwalimu.

Tatizo la watu kama wewe ni kutaka kuaminishwa na kauli bila kufauatilia research. Kwenye thread zangu humu, nimezungumza mengi zaidi ya aliyosema Kikwete. Sikuwahi hata siku moja kubabaika kwa kutamka kwamba hatuna hata tone moja la ziwa Malawi. Nimesema na ninarudia hatutaki wizi kuwaibia wenzetu ziwa lao.

Binafsi JK hajaniongezea kitu katika uelewa na sanasana hotuba yake imejaa uongo ambao hautaisaidia vyovyote Tanzania.
 
tusiwe tunalaumu kwa kila jambo ile hotuba kikwete kaandaliwa na amezungumza kwa hekima sana na busara na ni kweli hakuna sababu ya kuingia kwenye vita saizi na kwa kawaida mwanaume awezi pambana na mwanamke hata kidogo siku zote mwanamke ni dhaifu akizidi kuleta uchokozi atapelekewa mama anna kilango akajibishane naye au mama migiro.

Maajabu ya dunia hii ni kwamba dunia imejaa wapumbavu wengi kama wewe, mambumbumbu wengi kama wewe kiasi kwamba hawajui Queen Elizabeth aliipiga Spain mwaka 1588 akiwa mwanamke, Queen Victoria aliikolonize dunia akiwa mwanamke, Magreth Thatcher aliipiga Argentina pale Falkland na akaipiga Libya mwaka 1986.

Wapuuzi kama wewe ndiyo tumekuwa tukiwatoa tongotongo machoni kwa kuwaambia kwamba hatuna hata tone moja la ziwa Malawi na kwamba hata sikuhitaji kusubiri hotuba ya JK kutamkiwa hilo, na hata JK angetamka kinyume mimi nisingetumbukia kuamini ujinga kama wapumbavu wengi walivyoamini humu na kuwaita wenzao wasalati na sasa wanapata kigugumizi kumuita Kikwete msaliti.

Jifunzeni adabu ya kusoma vitabu na si kunywa kahawa au kubonyeza keyboard kuleta mpiasho JF.
 
HUJAMUELEWA Raiswetu. Hakika katika hotuba bora kabisa za Mzee Kikwete ni hii ya leo. Ilikuwa crystally clear na aliposema Tz hatuna ubavu wenye akili tumemuelewa!


Sasa ulitaka asemeje, huo ndo ukweli mkuu

Anajua kabisa ziwa si letu na hata Malawi isingekuwa na mwanajeshi hata mmoja au hata risasi moja basi angefuata tambo za wapumbavu wanaojisema wazalendo angekiona cha mtema kuni.

Lesotho iko katikati ya South Africa na inazidiwa kijeshi na South Africa. Lakini South Africa ikileta ujinga eti iitwaange Lesotho basi dunia haiwezi kukubali ujinga huo na kichapo itapewa South Africa kama Hitler wa Ujerumani alivyopewa kichapo ilipodhani kuivamia Austria ni vita kati ya wawili hao kumbe dunia nzima ika-ally.
 
FAKE PRESIDENT...sijui hanaga washauri au wanajaza matumbo tu...

Wmamedanganya kwamba Heligoland-1890 ilipitisha mpaka kwenye Songwe River kwenye pwani ya Malawi wakati ni uongo mkavu. Heligoland inasema hivi:

{Turning north, it continues along the eastern, northern, and western shores of the lake until it reaches the northern bank of the mouth of the Songwe River. It then continues up that river to its intersection point with the 33rd degree of east longitude. The line continues along the river until its closest point with the border of the geographical Congo Basin as described in Article I of the Berlin Conference and marked on the map appended to its ninth protocol}
 
Duh basi tena naona hatuna haki na ziwa malawi sisi haki yetu ni mito tu. Nimenyong'onyea! Nilikuwa nakunywa safari yenye kizibo chekundu naiacha naenda kulala nikitafakari.

Kimbunga,

JK kakuongezea uelewa gani hadi sasa umeanza kuamini? Maana thread zangu zina details zaidi kuliko kisehemu kidogo cha hotuba ya Kikwete.

Nikiwachambua watu kama wewe mnaoamini sasa kwamba hatuna ziwa baada ya kuaminishwa na Kikwete ni kwamba watanzania ni wavivu wa kusoma na ni watu wa kuaminishwa tu. Kumbe mlikuwa mnasubiri Kikwete anaamini nini kuliko post tulizofuruliza kuelimisha hapa kwamba Tanzania haijawahi kuw ana hata tone moja la ziwa Malawi.

Kama ni utalii basi hakuna sababu ya Tanzania kuacha kuvuna mapato ya utalii ili watalii waje kujionea taifa lilivyojaa wakuda wasiojua kupekua documents hata kama ungewashuahia.

Ni document gani ambayo haikushuka hapa JF ikionyesha kwamba ziwa sil letu.

Sasa, subirini kugombana na Rais JK na tume zake siku itakapoamriwa rasmi kwamba Tanzania ilikuwa inapoteza muda bure na mpaka umethibitishwa kwamba uko na utabaki vilevile kama ulivyowekwa kwenye Heligolang Treaty.
 
Kama ni hivyo inabidi watu waishie kando ya ziwa na wala wasivue huko hadi mazungumzo yakamilike manake vinginevyo tutaonekana wavamizi wa ziwa la watu.

Ni kweli kabisa Tanzania ni wavamizi na ukitaka soma thread yangu kwamba vile visiwa viwili vilivyo kilomita 11 toka Mbamba Bay lakini viko kilomita 45 toka Malawi ni vya Malawi.
 
Ahsante sana rais kwa kuongea. Kwa mara ya kwanza leo nimekuita rais kwa kuwa umelisemea hili.
 
Wmamedanganya kwamba Heligoland-1890 ilipitisha mpaka kwenye Songwe River kwenye pwani ya Malawi wakati ni uongo mkavu. Heligoland inasema hivi:

{Turning north, it continues along the eastern, northern, and western shores of the lake until it reaches the northern bank of the mouth of the Songwe River. It then continues up that river to its intersection point with the 33rd degree of east longitude. The line continues along the river until its closest point with the border of the geographical Congo Basin as described in Article I of the Berlin Conference and marked on the map appended to its ninth protocol}[/QUOTE]

Napenda sana watu wenye data kama wewe
 
kwa suala hili la mpaka sisi ndo tunabembembeleza turekebishe.....mpaka wa mto songwe huo ilubadilishwa na wakoloni sasa nasi tuendeelee kubembeleza wa ziwa.....we are on weak side
 
Kimbunga,

JK kakuongezea uelewa gani hadi sasa umeanza kuamini? Maana thread zangu zina details zaidi kuliko kisehemu kidogo cha hotuba ya Kikwete.

Nikiwachambua watu kama wewe mnaoamini sasa kwamba hatuna ziwa baada ya kuaminishwa na Kikwete ni kwamba watanzania ni wavivu wa kusoma na ni watu wa kuaminishwa tu. Kumbe mlikuwa mnasubiri Kikwete anaamini nini kuliko post tulizofuruliza kuelimisha hapa kwamba Tanzania haijawahi kuw ana hata tone moja la ziwa Malawi.

Kama ni utalii basi hakuna sababu ya Tanzania kuacha kuvuna mapato ya utalii ili watalii waje kujionea taifa lilivyojaa wakuda wasiojua kupekua documents hata kama ungewashuahia.

Ni document gani ambayo haikushuka hapa JF ikionyesha kwamba ziwa sil letu.

Sasa, subirini kugombana na Rais JK na tume zake siku itakapoamriwa rasmi kwamba Tanzania ilikuwa inapoteza muda bure na mpaka umethibitishwa kwamba uko na utabaki vilevile kama ulivyowekwa kwenye Heligolang Treaty.

Mkuu nilisoma post zako na nadhani comment zangu uliziona. Unajua katika kila jamii lazima kuwe na mtu wa mwisho anayetoa kauli. Imekuwa ni kizungumkuti ambacho kimetuvua mavazi. Niliposikia Membe akiongea Bungeni kwa kukemea na kutoa vitisho kwamba waache kufanya utafiti mara moja tena akirudia basi nikajua ngoma inogile manake sisi wengine wazee wa mapambano. Nikajua huo ni uamuzi wa Serikali kwamba mpaka upo katikati ya ziwa nami nikawa najiandaa kisaikolojia nikisubiri amri ya Amiri Jeshi Mkuu, hamadi nakuja ambiwa Ziwa lote la Malawi, nguvu zimeisha. Mkuu samahani sana kwa yaliyotokea.
 
Tatizo la watu kama wewe ni kutaka kuaminishwa na kauli bila kufauatilia research. Kwenye thread zangu humu, nimezungumza mengi zaidi ya aliyosema Kikwete. Sikuwahi hata siku moja kubabaika kwa kutamka kwamba hatuna hata tone moja la ziwa Malawi. Nimesema na ninarudia hatutaki wizi kuwaibia wenzetu ziwa lao.

Binafsi JK hajaniongezea kitu katika uelewa na sanasana hotuba yake imejaa uongo ambao hautaisaidia vyovyote Tanzania.

Kwani hata hili unahitaji research? Mbona research zingine unazilazimisha? Unaweza kufanya Research ya kutafuta mwaka uliozaliwa wakati umeandikwa kwenye cheti cha msajili wa vizazi na vifo?

Unaweza ukawa na ukweli tofauti na huo uliotolewa na mkuu wa nchi lakini huo ukweli wako utafikaje kwenye majadiliano ya mpaka wetu?

Nilichokisikia toka kwa mkuu wa nchi ni traverse of history na mwishoni akakubali kwamba mpaka wetu ulipowekwa kando ya ziwa haukurekebishwa kama ilivyofanywa kwa mto Songwe, Ziwa Tanganyika, Natron, n.k. Nikasema kama ni hitimisho la aina hiyo basi kumbe sisi kudai mpaka uko kati ni uhuni wa siku nyingi.. Thread hii ni ya hotuba iliyotolewa na Rais ndo maana tunasema kwa maelezo ya aina hiyo basi tuseme kwamba sasa hivi TZ tunaweza kuheshimu mpaka wa kado ya ziwa mpaka hapo marekebisho yatakapofanyika kama tunavyoomba. Au tubaki kibabe hapo tulipo kwa ukorofi wakati hata Rais ana amini kwamba mpaka huo haukurekebishwa!

Haki uliyonayo hapa wewe sema Rais ni mwongo, basi!
 
Mkuu nilisoma post zako na nadhani comment zangu uliziona. Unajua katika kila jamii lazima kuwe na mtu wa mwisho anayetoa kauli. Imekuwa ni kizungumkuti ambacho kimetuvua mavazi. Niliposikia Membe akiongea Bungeni kwa kukemea na kutoa vitisho kwamba waache kufanya utafiti mara moja tena akirudia basi nikajua ngoma inogile manake sisi wengine wazee wa mapambano. Nikajua huo ni uamuzi wa Serikali kwamba mpaka upo katikati ya ziwa nami nikawa najiandaa kisaikolojia nikisubiri amri ya Amiri Jeshi Mkuu, hamadi nakuja ambiwa Ziwa lote la Malawi, nguvu zimeisha. Mkuu samahani sana kwa yaliyotokea.

Mkuu,

Hapo kwenye RED sina maneno ya kukusifia. Ni wachache wanaokubali na kukiri kama wewe na ni mfano ambao sikuutarajia.

Mimi nashauri watanzania wenzagu kitu kimoja. Binafsi nina tabia ya kupenda sana kusoma vitabu. Libary zipo, archives zipo, bookshops ziko tele.

Ukienda kwenye library yetu pale Tanganyika Library Service utakuta vitabu tele, vizuri sana vya history. Siku moja niliazima kitabu kimoja cha history ya Uingereza. Kitabu kina detalis nzuri lakini ajabu ni kwamba nimekiazima mwaka jana mwezi November wakati tarehe zinaonyesha kuwa mimi ni mtu wa pili kukiazima. Wa kwanza alikiazima mwaka 1971!

Maana yake kitabu hicho kina miaka 40 hakijawahi kuazimwa! Palepale nilimuuliza librarian hivi kama hali iko hivi mtanzania atawezaje kuchangia mawazo kwenye masuala kama ya katiba wakati katiba kama usomaji wenyewe ndiyo huu.

Narudia ushauri wangu ni kwamba watanzania tujfungie kwenye vitabu tuutafute ukweli wa mambo bila kujali wakuu wa nchi ama wanasema nini.

Mgogoro huu wa Malawi umenifanya nisiwe na imani na watendaji wengi wa serikalini na kwamba yanapokuja masuala ya mikataba basi tutarajie kulimwa tu.

Ona hoja zote zilizokuwa zinaibuka humu. Mara hili mara lile na kila linalokuja linapingika kirahisi kama umesoma mzozo huu kihistoria.

Hivyo, tujikite kwenye kusoma, na hiyo ndiyo njia pekee ya kujua mambo na kuweza kuya-defend.
 
Kwani hata hili unahitaji research? Mbona research zingine unazilazimisha? Unaweza kufanya Research ya kutafuta mwaka uliozaliwa wakati umeandikwa kwenye cheti cha msajili wa vizazi na vifo?

Unaweza ukawa na ukweli tofauti na huo uliotolewa na mkuu wa nchi lakini huo ukweli wako utafikaje kwenye majadiliano ya mpaka wetu?

Nilichokisikia toka kwa mkuu wa nchi ni traverse of history na mwishoni akakubali kwamba mpaka wetu ulipowekwa kando ya ziwa haukurekebishwa kama ilivyofanywa kwa mto Songwe, Ziwa Tanganyika, Natron, n.k. Nikasema kama ni hitimisho la aina hiyo basi kumbe sisi kudai mpaka uko kati ni uhuni wa siku nyingi.. Thread hii ni ya hotuba iliyotolewa na Rais ndo maana tunasema kwa maelezo ya aina hiyo basi tuseme kwamba sasa hivi TZ tunaweza kuheshimu mpaka wa kado ya ziwa mpaka hapo marekebisho yatakapofanyika kama tunavyoomba. Au tubaki kibabe hapo tulipo kwa ukorofi wakati hata Rais ana amini kwamba mpaka huo haukurekebishwa!

Haki uliyonayo hapa wewe sema Rais ni mwongo, basi!

Mkuu,

Kwanza nafurahi kwamba hatimaye tunaanza kuwa wengi tutakaoliangalia hili sasa kwa jicho moja wote kwamba ziwa Malawi si letu. Wote sasa tuanze safari tutumie hoja gani au mbinu gani ya kihalali ili tupate sehemu ya ziwa hili.

Ila comment yako hapo kwenye RED ni kwamba hata kama nina ukweli basi ni vigumu mimi kusikika hadi kwa Rais ambaye yuko Ikulu na ndiye anayesubiriwa kusikilizwa na watanzania wote hata kama ni muongo au hajui kama mimi.

Lakini unaposema hivyo, maana yake tuwapongeze wote walioleta networks kama hii ya Jamii Forum. Bila Jamii Forum basi haya mambo ningekuwa nayaongea labda na girfriend wangu tu au ndugu zangu na marafiki wa karibu sana, tena wakati mwingine nikiogopa labda kuna usalama wa taifa pembeni wananifuatilia ninachozungumza.

Lakini nimepitia idadi ya waliosoma thread hizi za Malawi na Tanzania. Jumla ni zaid ya watu 3,000 waliosoma thread hizi! Hao 3,000 ni zaidi kuliko hata ungeandika article gazetini. Gazeti unaweza kununua na usisome lote na wengi hawasomi article. Humu mtu akisoma thread ameidhamiria na anaisoma. Achana na zile post za kuwaponda wengie kuwa ni wamalawi.

Lakini nikukumbushe kitu kimoja. Unakumbuka thread yangu niliposema kwamba Membe kakosea kutaja coordinates za linapoanzia na kuishis ziwa Malawi (hii hapa). Nilisema katajza latitude 9 hadi 11.

kwa taarifa yako, siku moja niko kazini pembeni yangu akaja jamaa mmoja staff mwenzetu akaanza kusimulia jinsi serikali inavyotakiwa kuwa makini kutaja mambo ya kitaalamu bungeni. huyo jamaa akasema ameona mtaalamu mmoja katuma post kwenye Jamii Forum akieleza jinsi Membe alivyokosea zile latitude na kusema ni 9 hadi 11.

Binafsi nikashtuka ili nidadisi na kwa taarifa yenu hakuna hata mmoja anayejua kwamba mimi ni member wa JF tena wengi wanajua kuwa hata mitandao huwa sifungui. Akaeleza kwa ufasaha kama ile thread yangu na kundi kubwa limemzunguka.

Mimi nikawa msikilzaji zaidi ili nijue matunda ya JF. Eeh Bwana, JF ina nguvu. Walifungua thread yote na kuisoma na hivi wanajua mambo ya geography na ramani ziko karibu walihakikisha na kila mmoja akatoka pale ameridhika kwamba Tanzania tuna shida ya kuutambua mgogoro huu. Huu ni mfano mmoja niliouona live.

Mfano wa pili ni kwamba kama ulifuatilia leakage ya mazungumzo kule Malawi, hili la latitude 9 na 11 liliulizwa na jamaa wakatoa speecha ya Membe mle bungeni. hayakupatikana majibu sahihi na ikatoa picha kwamba ni ubabaishaji unaoendelea.

Sasa, kama wenzetu wa Malawi wanasoma JF na kuitumia katika hoja zao, iweje wanasiasa wetu washindwe kuja humu na kuangalia tunavyojadili na kuchota mawazo yetu humu hata kama ni kidogo, hatutaki sifa kwa sababu hata majina yetu ni ya bandia kama Nikupateje.

Hivyo, hilo ni tatizo la serikali kutosaka information ambazo sisi kazi yetu inamalizika tunapozi-broadcast kwenye mitandano kama hivi.

Asante.
 
Back
Top Bottom