Full Text: Hotuba ya P. Msigwa, Kambi ya Upinzani Wizara ya Maliasili na Utalii 2015/2016

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
HOTUBAYA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHESHIMIWA MCH. PETER SIMON MSIGWA, (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAWIZARA YA MALIASILI NA UTALII, KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

(Inatolewachini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)

UTANGULIZI

MheshimiwaSpika,Kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la2013, naomba kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungenikuhusu mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya 2014/2015 na makadirio yamapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wafedha 2015/2016.

MheshimiwaSpika,kwanza, napenda kuchukua nafasi hii kwa kipekee kabisa nimshukuruMwenyezi Mungu kwa kunipa uzima na afya njema. Kwa kipekee niishukurufamilia yangu hasa mke wangu na watoto wangu pamoja na wananchi wanguwa Iringa mjini kwa kunipa ushirikiano mkubwa katika majukumu yake.

Zaidi, namshukuru kiongozi wa Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman A.Mbowe kwa kunikabidhi jukumu la kusimamia wizara hii toka aundeBaraza Kivuli la Mawaziri kama Msemaji Mkuu wa Wiizara ya Maliasilina Utalii. Pia, kwa wabunge wa kambi nzima ya upinzani kwa kuwa kitukimoja. Na pia kipekee, niwapongeze viongozi wangu ambao niwenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na viongozi wa CHADEMA wa jimbola Iringa mjini kwa kuja kuniunga mkono.


MheshimiwaSpika, katikamaandiko Matakatifu ya Biblia tunaelezwa jinsi ambavyo Mwenyezi Mungualimtuma Musa kwenda kuwaokoa wana Misri kwa kumwambia kuwa‘nenda ukawaambie kuwanimeyaonamateso yao, nimekisikia kilio chao na maumivu yao ninayajua, naminimeshuka ili niwaokoe na Farao'

MheshimiwaSpika,UKAWA inapenda kuwaambia watanzania KUWA Mwenyezi Mungu amesikiakiliochenu, ameyaona mateso yenu na anayajua maumivu yenu'hivyo UKAWA imekuja kuwaokoa kutoka kwa utawala wa kidhalimu waSerikali ya CCM ili mnufaike na rasilimali na maliasili za nchiyenu(maliasili na utalii)!

MheshimiwaSpika, kwatakribani miaka mitano nimekua mstari wa mbele kuishauri Serikalikupitia Wizara hii ya Maliasili na Utalii kwenye masuala ya ujangili,misitu, vitalu vya uwindaji, utunzaji wa mazingira na maliasilipamoja na njia mbadala za kuweza kuinua ya utalii ikiwemo ukuzaji waajira. Lakini, Serikali ya CCM imeendelea kuwa kiziwi , kipofu nakufikia hatua ya kubeza, kupuuza na hata kukebehi juhudi zetu katikakuiinua Sekta hii muhimu kwa uchumi nchini. Ikumbukwe kuwa, Sekta yautalii inachangia takribani dola bilioni 2 ambazo ni sawa natakribani trilioni 4 za pato la taifa. Lakini, Serikali ya CCMimekua na kigugumizi cha kuweza kuitumia Sekta hii ipasavyo zaidi yailivyo sasa kama ambavyo imeshauriwa na Benki ya Dunia (WB)

MheshimiwaSpika,pamoja na Serikali kufanya mabadiliko ya mara kwa mara ya mawaziri waWizara hii, wizara bado imeendelea kukumbwa na changamoto kubwaikiwemo kuongezea kwa vitendo vya kijangili, uwindaji haramu nautoroshaji wa wanyama na nyara za taifa.

MheshimiwaSpika,katika hotuba zetu za miaka mitano mfululizo tumezungumzia umuhimu wakuanzisha sera ya diplomasia ya uchumi ambayo mabalozi wetu watapimwautendaji wao kutokana na utendaji wao na ubunifu wao wa kiuchumi.Tulipendekeza mabalozi hawa wapatikane kwa kuhakikisha kuwa wanaombanafasi za kuendesha balozi hizo kwa kuonesha mipango mikakatiitakayochochea masuala ya kiuchumi ikiwemo uwekezaji, utalii,biashara na kadhalika. Lakini Serikali hii imeziba masikio. Sasa mudaumefika wa Serikali hii kukaa kando na kuacha akili kubwa iwezekufanya kazi.

MheshimiwaSpika, miakamichache iliyopita nilielezea ndani ya Bunge lako kuwa watanzaniatumeruhusu akili ndogo itawale akili kubwa. Na maneno yangu hayayanajidhihirisha pale ambapo wizara nyeti katika Taifa, inapokumbwana kashfa kubwa ikiwemo kashfa ya kulinda mtandao wa majangili,kashfa ya operesheni tokomeza ambayo bado haijafutika machoni pawatanzania; lakini matokeo ya kukabiliana na changamoto hiyoyamegeuzwa kuwa ni kuwabadili watu na wala si kubadilisha mfumo.Labda tuseme kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii haina tatizo lakupata kiongozi bora wa kuweza kukabiliana na changamoto za utaliinchini lakini inakabiliwa na changamoto ya kufanya mabadiliko yamfumo wa kiutendaji na kiuwajibikaji ili kuiwezesha wizara kufanyakazi kwa ufanisi.

MheshimiwaSpika, seraza Chama cha Mapinduzi (CCM) zimeshindwa na zimeshindwa si kwa kukosawatekelezaji wazuri bali zimeshindwa kwa sababu ni sera mbaya ambazozimegeuka kuwa janga la kudumu la Taifa. Sera hizi katika ujumla wakendizo chanzo, kiini, na sababu ya kudumaa kwa maendeleo nchini nandizo chanzo kikuu cha umasikini Tanzania. Sera hizi ambazozimejaribiwa kwa miaka 50 na zaidi sasa zimethibitisha kitu kimoja tu– kushindwa kwake.

Sera ya CCM kuhusu maji imeshindwa; sera ya CCMkuhusu elimu imeshindwa ; sera ya CCM kuhusu nishati imeshindwa; seraya CCM kuhusu madini imeshindwa; sera ya CCM kuhusu gesi imeshindwa;sera ya CCM kuhusu ulinzi wa rasilimali za asili imeshindwa; sera yaCCM kuhusu kupambana na ujangili imeshindwa, sera ya CCM kuhusuulinzi na usalama imeshindwa; Sera ya CCM kuhusu Usalama wa Taifaimeshindwa. Kwa kila kipimo sera zote za CCM zimeshindwa na hakunailiyofanikiwa.


MheshimiwaSpika,mojawapo ya mambo mabaya kabisa ambayo ni matokeo ya sera hizi mbovuza CCM ni kutegemea fedha za wafadhili katika mradi mingi yamaendeleo huku Taifa likiwa limebarikiwa kuwa na rasilimali nyingiambazo zinaweza kuendesha miradi ya maendeleo pamoja na uchumi bilakutegemea miradi ya wafadhili. Kosa hili lilifanywa mara baada yauhuru lakini Nyerere – Baba wa Taifa – alilitambua hilo mara mojana katika kutangaza Azimio la Arusha alitangaza ukweli ambao ulikuwayakini wakati ule kama ulivyo leo hii.

MheshimiwaSpika,azimio la Arusha lilisema hivi kuhusu kutegemea fedha kama msingi wamaendeleo:
"Lakinini dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua silaha; kwanisilaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa unyonge wetu kwakutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na vitendo vyetu ni kamatumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi yetu hayawezekani. Nikama tumesema, "Fedha ndiyo msingi wa maendeleo. Bila fedha hakunamaendeleo"

MheshimiwaSpika,niazimio la Arusha ambalo lilieleza kuwa ;

"Viongoziwa TANU mawazo yao ni kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasana watumishi, mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongoziwa wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA (ilikuwa chama chawafanyakazi), Bunge, UWT., Vyama vya Ushirika, TAPA (kilikuwa chamacha wazazi) na makundi mengine ya wananchi, mawazo yao na maombi yaona matumaini yao ni FEDHA. Ni kama wote tumekubaliana na tunasemakwa sauti moja, "Tukipata fedha tutaendelea, bila fedhahatutaendea."

MheshimiwaSpika,ndio maana kila Mbunge wa CCM akisimama hapa anawaza kuhusu fedha,fedha na wala hachangii ni jinsi gani Taifa linaweza kutumiarasilimali tulizo nazo kujitosheleza kiuchumi bila kutegemea fedha zawafadhili. Ni maono ya baba wa Tafa ambayo yanatanguliwa kushindwakwa Serikali ya CCM kutatua matatizo ya ujangili na kuamini kuwajumuiya ya kimataifa ndio ina wajibu wa kuisaidia Tanzania kupambanana ujangili.

MheshimiwaSpika, ndaniya asasi za uongozi na utawala, na katika mfumo mzima wa siasa ,Serikali ya CCM imeendelea kulea uozo huo,maovu hayo yanayofanywa nawatu wale wale kwa mfumo ule ule na kwa uwajibikaji ule ule. Kwamfano ni wizara ile ile inayokabiliwa na matatizo yale yale nauwajibikaji wake ni ule ule wa kubadilisha mawaziri na kuwateua wachama kile kile na utegemee utapata matokeo tofauti kwa kupitia watuhao hao. Hii taratibu, inageuka kuwa saratani inayolitafuna taifaletu. Tunajua sasa kwamba pasipo na uongozi thabiti na wenye nia yakutenda mema na makubwa, tutabakia kuwaona wenzetu hasa nchi zilizopokatika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) wanapiga hatua nasisi tukibakia nyuma, huku tukiwa na rasilimali ambazo wenzetu hawanalakini tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania wenyewe.

IDARAYA MISITU

MheshimiwaSpika, idaraya misitu au Tanzania Forest Services (TFS) imeoza nchinzima,watendaji kila mmoja anafanya lake katika ofisi yake nahawafanyi kazi kwa mujibu wa Sheria ya misitu ya mwaka 2002 no14.Kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha kutoka kanda moja kwendakanda nyingine .Kama tujuavyo, mazao mengi ya misitu hutoka mikoambali mbali na kusafirishwa kwenda kwenye miji mikubwa hasa Dar EsSalaam kwa matumizi ya ndani ya jiji hivyo Es Salaam imekuwa kitovukikubwa cha soko la biashara ya mkaa na kulifanya jiji hilo kuwakituo kubwa cha ukusanyaji wa ushuru wa Serikali kwa wale wanaokuwawamekwepa kulipia ushuru kutoka huko kwenye chanzo cha mazao hayo yamkaa.

MheshimiwaSpika,kwa muda mrefu meneja wa kanda ya mashariki Ndugu Salim Bakarimaarufu kama Mwarabu badala ya kuwa mdhibiti yeye amekuwaakiwatetea wafanyabiashara wanaokiuka kulipa kodi na ametuhumiwa kwamuda mrefu kuwa mfadhili wa wafanyabiashara haramu kutoka Tabora,Katavi, Kibondo, Bukombe, Tunduma, Dodoma, Kilindi na Bagamoyo. Vilevile, ili kufanikisha malengo yake ameweka watu wasio na taalumakatika vituo vya ukaguzi (checkpoints) na hali akijua hawana sifa zakukagua nyaraka wala mizigo.

Kwa Mfano; Katika vituo vya Ukaguzi vyaKibaha, Vikindu pamoja na Mbagala kumekuwepo na malalamiko ya mudamrefu ya uwepo wa vijana waliopo chini ya mtandao wa Mwarabu ambaowanafanya kazi kama maafisa misitu wakati hawana sifa lakini piawamewekwa kimkakati ili watu waweze kupitisha biashara zao bilaukaguzi yakinifu. Majina ya vijana hawa tunayo pamoja na vituo vyaovya ukaguzi.


MheshimiwaSpika,imekuwa kawaida ktk sekta ya misitu watu kukiuka sheria na kufanyabiashara kiholela kwani mwongozo wa uvunaji endelevu wa 2007 umesemabayana kuwa ili ufanye biashara ya mazao ya misitu utatakiwa kutimizayafuatayo:



  1. [*=center] Kuwa na Usajili wa unapovuna na unapopeleka kuvuna
    [*=center] Uwe na leseni ya biashara pamoja na nambari ya utambulisho wa mlipakodi (TIN)
    [*=center] Awe na leseni ya uvunaji,
    [*=center] Ulipe ushuru wa Serikali kwa kuingia na Halmashauri husika
    [*=center] Awe na kibali cha kusafirisha mazao ya misitu (Transportation Pass)

MheshimiwaSpika,Kambi ya Upinzani Bungeni imeelezwa kuwa mtandao huu wa usafirishajiwa mazao ya Misitu chini ya Bwana Mwarabu unafahamika hata kwaMkurugenzi wa Misitu na bado mtandao huu umeendelea kuota mizizi nahivyo kulikosesha taifa mapato lakini pia kuhatarisha ustawi wa mazaoya misitu nchini kwa kuwa ukaguziwa mazao ya misitu na usafirishajiwake haufanywi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa.

KUZOROTAKWA UWINDAJI WA KITALII

MheshimiwaSpika,uwindaji wa kitalii ni tasnia muhimu sana kwa mapato ya taifa letu naukuzaji wa uchumi, ambayo imekua ikiingiza kiasi cha shilingi billion34 kwa mwaka. Jambo la kushangaza ni jinsi ambavyo Serikali ya CCMimekuwa ikipuuza mambo ya msingi ambayo yanaweza kuangamiza kabisatasnia hii. Sheria ya wanyamapori ina mapungufu makubwa ambayoyamekua kikwazo kikubwa kwa wawekezaji na hivyo Kambi ya Upinzaniinaamini kuwa ikichukua nchi, itafanya mabadiliko kwa kurekebishaSheria hii ili iwe na tija hivyo kufanya uwindaji wa kitalii kuwaendelevu na kuongeza pato la taifa.

MheshimiwaSpika,hivi karibuni karibu vitalu 28 vya uwindaji vilirudishwa na Wizaratayari imeshatangaza ili kutafuta wawekezaji. Kadhia kubwa ambayoimesababisha kurudishwa kwa vitalu hivi ni pamoja na kuwa wawekezajihawana imani kuwa wataendelea kufanya uwindaji katika vitalu ambavyomuda wa uwekezaji kwenye vitalu hicyo ni miaka mitano tu. Ikumbukwekuwa mwekezaji hupewa miaka mitano tu ya kuweza kuendeleza kitalu.

MheshimiwaSpika, kwa mfano ili Simba avunwe sheria inataka awe na umri wa miakakuanzia miaka mitano, kama mwekezaji atapewa kitalu wakati Simba anachini ya mwaka mmoja maana yake hataweza kumvuna ifikapo ukomo wamiaka mitano ya umiliki wa kitalu na hivyo kupoteza gharama ambazoametumia. Msumbiji , ambao ni jirani zetu; wameweka ukomo wa umilikiwa kitalu kuwa miako kumi. Pamoja na miaka hii kuonekana kuwa nimingi , inasaidia mwekezaji kuwa na uhakika wa kuvuna wanyamaanaowagharamia.

MheshimiwaSpika,Kambi ya Upinzani Bungeni inaamini kuwa, uwepo wa Sheria na Kanunibora za wanyamapori ndio utakaostawisha uwindaji wa kitalii nakuliongeza taifa mapato. Hii pia itavutia wawekezaji kuwekeza kwakufuata na kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa kama vile ,kulipa ada , tozo ,uhifadhi na uwindaji endelevu.

KUPOTEAKWA MAPATO KUTOKANA NA WAGENI KUTOLIPIA TOZO WANAPOINGIA HIFADHINIMARA YA PILI.

MheshimiwaSpika,toka kuanza kazi kwa Waziri Nyalandu, Waziri atakumbukwa kwa kufanyamaamuzi yasiyo na tija nay a kukurupuka ikiwemo; swala la ulipaji wasingle entry na kuchelewesha utekelezaji wa amri ya mahakama ya tozokwa mahoteli ya kitalii; kutaka kutoa sehemu ya hifadhi ya taifa yasaadani; mgogoro wa hifadhi ya taifa ya Ruaha (Ihefu); pamoja nakutangaza muda wa kurefusha uwindaji kutoka miezi sita mpaka tisa.

MheshimiwaSpika,uingiaji wa wageni hifadhini zaidi ya mara moja bila kulipa tozostahiki wanapoingia mara ya pili (yaani Double Entry) umeendeleakuikosesha TANAPA na taifa mapato. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo,katika kipindi cha Juni, 2013 hadi Machi, 2015 kupitia Hifadhi zaSerengeti na Ziwa Manyara, TANAPA ilipoteza mapato zaidi ya ShilingiBilioni 1.3, hii yote ikiwa ni maamuzi ya Waziri Nyalandu.

Aidha,baada ya kuanza kwa utekelezaji wa mgeni kulipa tozo kila anapoingiahifadhini kwa kipindi cha siku 16 kwa lango moja tu la Ikoma katikaHifadhi ya Serengeti, TANAPA iliweza kukusanya zaidi ya ShilingiMilioni 17 ambazo zingepotea endapo wageni wangeruhusiwa kuingiazaidi ya mara moja bila kulipa tena.

MheshimiwaSpika, ni dhahiri kuwa wizara ya maliasili na utalii imeendeleakutengeneza mianya ya kupoteza mapato na hivyo kulisababishia Taifahasara. UKAWA imejiandaa kuhakikisha kuwa wageni wanaoingia katikamaeneo ya Hifadhi za Taifa zaidi ya mara mbili bila kulipa tozostahiki wanadhibitiwa na hivyo kuchangia ukusanyaji wa mapato.

KUPOTEAKWA MAPATO KUTOKANA NA KUCHELEWA KUTEKELEZA AMRI YA MAHAKAMA KUU YATOZO YA PANGO (CONCESSION FEE)

MheshimiwaSpika,kuchelewa kwa makusudi kwa Wizara hii kutekeleza amri ya Mahakama Kuuiliyotolewa Septemba, 2014 kumelifanya Shirika la Hifadhi za Taifakupoteza kiasi cha Shilingi Bilioni 3 katika kipindi cha kuanziaOktoba, 2014 hadi Machi, 2015. Fedha hizi zilizopotezwa kwa uzembe waWaziri Nyalandu zingeweza kununulia madawati ya watoto wanaokaamashuleni, ama kununua vitanda vya wajawazito wanaozalia chini amapia kupunguza deni la MSD .

Leo hii, Waziri Nyalandu anaposimamakusoma mafanikio ya Wizara yake aeleze ni kwa nini amelisababishiahasara taifa! Halafu leo hii anakuwa mmoja ya watu wanaojitokezakuwania uraisi, anapata wapi nguvu hiyo?


MheshimiwaSpika,leo hii waziri anapolikosesha Taifa mapato, anajua kuwa hawezikuwajibishwa na ndio maana UKAWA inaamini kuwa itakapopewa ridhaa yakuliongoza Taifa hili, haitovumilia uzembe wowote utakaolisababishiaTaifa ukosefu wa mapato kama huu uliofanywa na Waziri Nyalandu.

KUMEGWAKWA MAENEO YA HIFADHI ZA RUAHA NA SAADANI

MheshimiwaSpika,hivi karibuni Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Waziri Nyalanduilitoa tamko la kubadili Tangazo la Serikali lilioanzisha Hifadhi zaTaifa za Ruaha na Saadani kwa kumega baadhi ya maeneo ya hifadhihizo kinyume cha Taratibu na Matangazo ya Serikali. Sababu za kumegwakwa maeneo hayo ni kutokana na migorogoro ya ardhi na wananchi na/auwadau wengine katika maeneo husika. Maeneo yanayopendekzwa kumegwakwa mujibu wa Tangazo hilo ni pamoja na maeneo muhimu ya kiiokolojiana kwa maendeleo ya uchumi na maisha ya wananchi wake.

Kwa mfano eneola vijiji 21 ambayo Mhe. Waziri amesema limegwe kutoka eneo laIhefu/Usangu kwenye hifadhi ya Ruaha ni maeneo muhimu ya Ardhi oevukwa Bonde, ambalo ndio chanzo kikuu na pekee cha maji ya mto Ruaha. Ikumbukwe kuwa mto Ruaha ni tegemeo pekee kwa ajili uzalishaji waumeme kwa ajili bwawa la Mtera, maji kwa ajili ya viumbe hai ndani yahifadhi ya Ruaha na kwa ajili matumizi ya wananchi wanaoishi mwishowa mto (Downstream) nje ya Hifadhi ya Ruaha.


MheshimiwaSpika,Kambi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuacha eneo hililiendelee kuwa sehemu ya ardhi oevu na hivyo kufanya mto Ruahakutiririka kwa kipindi kirefu cha mwaka. Aidha, lazima eneolilotengwa kama sehemu ya hifadhi katika eneo la Usangu-ihefu libakiehivyo na kwamba Serikali ya CCM ijue kuwa kutoa sehemu ya hifadhi kwawananchi sio suluhisho endelevu kwa mustakabali wa maendeleo mapanaya nchi yetu na uhifadhi.

MheshimiwaSpika,kwa hifadhi ya saadani; Waziri alitangaza kumega eneo kubwa lahifadhi kwa ajili ya kilimo kikubwa cha miwa, na kulitoa kwa kampuniiitwayo eco-energy. Eneo hilo ni muhimu sana kwa maisha ya viumbembali mbali wakiwemo wanyama na miti aina ya mikoko, kwenye mto wamiambalo ni muhimu kwa mazalio ya samaki. Eneo hilo ni muhimu sana kamamapito ya wanyama na kwa uwepo wa hifadhi ya saadani. Umegaji wanamna hii wa hifadhi zetu tena ndani ya muda mfupi unaweka rehaniuwepo wa hifadhi zetu. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kama inawezakuwa rahisi hivi kwa hifadhi za Saadani na Ruaha kwanini lisiwezekanekatika hifadhi nyingine za hapa nchini?

MheshimiwaSpika,kama tunavyofahamu hifadhi za Taifa ni maeneo yanayotengwa kwamahitaji muhimu ya kiikolojia na maendeleo ya kiuchumi kwa nchi yetu.Aidha nchi yetu imepata umaarufu na heshima kubwa ya kuwa na vivutiovingi vya aina mbali mbali kutokana na maeneo yaliyohifadhiwa.Umegaji wa hifadhi za Taifa na maeneo mengine yaliyohifadhiwa siosuluhisho la utatuzi wa migogoro ya ardhi. Kutokana na kuongezeka kwamigogoro baina ya wananchi na TANAPA , UKAWA inawaahidi watanzaniakuwa tutatengeneza mpango wa muda mrefu wa matumizi bora na endelevuwa ardhi (land use plans) utakaowekewa sheria na kanunizitakosimamiwa vizuri.

MheshimiwaSpika,ni dhahiri kuwa kufanya maamuzi ya kukurupuka na yasiyozingatiaushauri wa Kamati wa Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa WaziriNyalandu ndipo kulipokulisababishia hasara ambazo zingeweza kuepukikaina ikumbukwe kuwa maamuzi haya ndiyo yaliyosababisha hata kamati nawadau kuigomea bajeti yake kwenye vikao vya Kamati Dar Es Salaam nahivyo kusababisha hasara nyingine ya kuleta wataalamu wa wizara hapaDodoma kwa siku mbili , gharama ambazo zingeweza kuepukwa , kamaangesikiliza ushauri wa kamati. Je, Waziri anaweza kuliambia bungehili ni kwa nini alifanya maamuzi makubwa kama haya kwa kukurupuka nakutokuzingatia ushauri wa kamati kwa maslahi ya nani,? Kwa niniwaziri alikuwa na kigugumizi kutekeleza maamuzi ya mahakama?

VITADHIDI YA UJANGILI NCHINI
MheshimiwaSpika,mwaka 2010 Novemba ziliibuka tuhuma za kutoroshwa kwa wanyama kwakutumia ndege ya jeshi la Qatar, baada ya bunge kupokea taarifahusika na ikiwa imepita miaka tatu toka kuwasilishwa kwa taarifahiyo kuna haja ya kujiuliza mambo yafuatayo kuhusu kutoroshwa kwawanyama wetu;



  1. [*=center] wakati taarifa ya kamati inawasilishwa bungeni kulikuwa na kesi mahakamani kuhusu utoroshaji wa wanyamapori hai na hivyo Bunge kutopata nafasi ya kujadili jambo hilo, kwa sasa kesi hiyo imekwisha, je Waziri Nyalandu anatoa majibu gani?
    [*=center] Mhusika mkuu katika utoroshwaji wa wanyama hao hai Bwana Kamran alitoroka kwenda nje ya nchi na kwa kuwa Serikali ya CCM inajidai kuwa na mtandao mkubwa wa intelijensia, je Bwana Kamran yupo nchi gani na ni hatua gani zinachukuliwa na Serikali kumrudisha nchini kukabiliana na mashtaka dhidi yake?
    [*=center] Inawezekanaje ndege ya jeshi kutoka nchi nyingine kutua na kupakia wanyama katika viwanja vyetu bila vyombo vya usalama kufahamu?

MheshimiwaSpika,Kambi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kuwa Qatar inadai kuwahawakuiba wanyama bali waliwachukua wanyama hao kihalali na ndiomaana Serikali yao ilikataa kutoa visa kwa wale maafisa wa Serikaliwaliokuwa waende huko kuchunguza sakata hilo kwa kuwa Serikali ya CCMiliwauza kihalali wanyama ambao leo inadai kuwa waliibwa. Maelezo yaserikali, ushahidi, wa mazingira ya utoroshaji wa wanyama pori haiuna viashiria vyote kuhusu uhusika wa badhi ya watumishi, usalama wataifa, jeshi la polisi na viongozi wa Serikali na CCM kuhusukuhusika moja kwa moja kwao katika masuala ya ujangili kwa kuwa hataRais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM anawajua majangili hao, je ni kwanini hawafikishwi mbele ya Sheria?

MheshimiwaSpika,Mwezi Machi mwaka 2014 Jumuiya ya kimataifa iliadhimisha kwa mara yakwanza Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo iliasisiwa na Umoja waMataifa (UN) kwa lengo la kuyahamasisha mataifa yote duniani kutambuana kuthamini umuhimu wa wanyamapori kwa maisha ya binadamu ili kuwekamikakati na mbinu za kulinda wanyamapori Kwa namna moja ama nyingine,hatua hiyo ya UN imeonekana katika macho ya wengi duniani kamainalenga kuishawishi dunia kupambana na vitendo vya ujangili katikasehemu mbalimbali duniani, hasa Tanzania na nchi nyingine kadhaaambazo zimeshindwa kabisa kudhibiti vitendo vya ujangili nakusababisha mauaji makubwa ya wanyamapori ambao wako hatarinikutoweka, wakiwamo tembo na faru.

MheshimiwaSpika,ni jambo la kusikitisha kuona kwamba jina la Tanzania kwa muda mrefusasa limetawala vichwa vya habari katika vyombo vingi vya habariduniani kutokana na Serikali kushindwa kukomesha vitendo vya ujangilidhidi ya wanyamapori hao walio katika hatari ya kutoweka, ingawaimekiri wazi kwamba inayajua vizuri majangili hayo. Siyo siri tenakwamba linapozungumziwa tatizo la ujangili, dunia inajielekeza mojakwa moja kwa Tanzania kama marejeo. Kama tulivyoeleza kwa miaka mingikuwa Tanzania inaonekana mbele ya jumuiya ya kimataifa kama taifaambalo halitambui kwamba kushamiri kwa vitendo vya kuangamizawanyamapori kutalifanya kuwa maskini milele na pia Serikali ya CCMimeshindwa kabisa kukabiliana na ujangili na hivyo kuzua maswali juuya tuhuma za muda mrefu kuwa Chama hiki kinafadhiliwa na majangilikwa kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ujangili ni makada nambari moja waCCM.

MheshimiwaSpika,pamoja na kushutumiwa na kusutwa kila kona ya dunia kutokana nakutopambana na ujangili unaosababisha mauaji ya tembo 11,000 kilamwaka, Serikali bado imeshikwa na kigugumizi kutekeleza ahadi yake yakuteketeza tani zipatazo 90 za shehena ya meno ya temboyaliyohifadhiwa katika maghala yake baada ya kuzikamata kutoka kwawahalifu sehemu tofauti. Badala yake imekuwa ikifanya juhudi kwa mudamrefu ikitaka ipewe kibali cha kuuza shehena hiyo, lakini juhudi hizozimegonga mwamba.

MheshimiwaSpika,pengine ni vyema tukakumbuka kwamba hadi miaka ya hivi karibuni,Serikali imekuwa na mkakati wa kuzishawishi nchi zilizosaini Mkatabawa Kimataifa Dhidi ya Biashara ya Wanyamapori na Mimea Iliyo KatikaHatari ya Kuangamia (CITES), ili iuze shehena hiyo katika soko lakimataifa. Pamoja na msimamo wake kwamba fedha hizo zingesaidiakatika vita yake dhidi ya ujangili, nchi hizo ikiwamo Kenya zilipingavikali ombi hilo. Hali ya nchi kushutumiwa na kuaibishwa kimataifailijitokeza pia jijini London wakati wa kongamano lililoitishwa naSerikali ya Uingereza kujadili mbinu za kulinda wanyamapori dhidi yaujangili. Kongamano hilo lilihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 46,wakiwamo marais wanne kutoka Afrika na wakuu wa mashirika 11 yakimataifa. Tanzania ndiyo iliyoonekana kuwa katikati ya masikitiko nashauku za wajumbe wa kongamano hilo kutokana na ukubwa wa tatizo laujangili hapa nchini.

Ni wakati wa kongamano hilo, ndipo ujumbe waTanzania ulioongozwa na Rais Jakaya Kikwete ulipotangaza kwambaumefuta mpango wake wa kuuza shehena ya meno ya tembo, pengine ikiwani hatua ya kuonyesha kwamba Tanzania sasa inayo dhamira ya kupambanana ujangili na biashara ya meno ya tembo. Na hatua hii ilisabbabishwana vikwazo ambavyo nchi wahisani walionesha iwapo ingeendeleakupigania kuuza shehena ya pembe za ndovu ilhali ikijua biashara hiyoni haramu duniani kote.


MheshimiwaSpika,ni muda mrefu umepita sasa tangu ahadi ya kuteketeza shehena ya menoya tembo ilipotolewa. Sisi tunauliza: Kama kweli Serikali imedhamiriakupambana na ujangili na kuionyesha dunia kuwa ina dhamira ya kweli,ni sababu zipi zinazokwamisha utekelezaji wa ahadi hiyo? Kigugumizicha Serikali ya CCM ambayo yenyewe ndiyo yenye dhamana ya kulindashehena hiyo, inatupa wasiwasi kuwa; haitoweza kutetekeza shehena hiiharamu kama inavyofanya kuteketeza madawa ya kulevvya kwa kuwa badoina nia ya kuuza shehena hiyo kwenye black market yaani soko haramukwa njia za siri na kutumia fedha hizo kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba2015.

MheshimiwaSpika,huku taifa likiwa limegubigwa na taswira ya kuhalalisha ujangilimbele ya jumuia ya kimataifa, Rais Kikwete na Waziri Lazaro Nyalanduwakitumia fedha za walipakodi waliamua kujisafisha duniani kupitiaCNN na BBC dhidi ya madai kwamba haijachukua hatua za kutoshakupambana na tatizo la ujangili nchini. Vyovyote vile, yeyotealiyeishauri Serikali itafute kampuni ya Uingereza ya masuala ya PRkumuunganisha Rais Kikwete na Christian Amanpour, na baadayekumuunganisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu naStephen Sackur wa kipindi cha Hard Talk cha BBC, kujisafisha hukuwakijua kabisa Serikali ya CCM haina nia ya dhati ya kupambana naujangili kwa kuwa Serikali hii hii imekua ikiwalea majangilialisababaisha taifa lipate aibu kubwa. Hatua ya Serikali ya CCMkukimbilia London kujisafisha kimataifa; ilhali nyumbani bado kuchafuni hatua ya kuonesha kuwa Serikali hii inawaogopa majangili.

MheshimiwaSpika,swali kubwa ambalo tunajiuliza ni iwapo Rais Kikwete ‘alifanikiwa'kuisafisha Tanzania dhidi ya tuhuma hizo kwa kuiambia BBC kwambaanawafahamu vigogo 40 wa biashara ya ujangili nchini, lakinihajawakamata? Kwa kauli yake hiyo, ameichafua zaidi nchi kulikokuisafisha. Rais hawezi kuwafahamu vigogo 40 wa biashara haramu yaujangili pamoja na kiongozi wao na asiwakamate, na badala yakeanakwenda London kutangaza kuwa anawajua japo hajawakamata, na kishatuamini kuwa ‘ameisafisha' nchi dhidi ya tuhuma hizo! Hii nidhihaka kwa watanzania wote. Vilevile ni dhahiri kuwa BBCinatazamwa na kusikilizwa na wengi duniani , swali kubwa ambalomamilioni ya watazamaji duniani watakua wanajiuliza ni Rais wa namnagani anayewafahamu kwa majina vinara 40 wa uhalifu nchini mwakelakini hawakamati? Iwapo taasisi kubwa inawafahamu vinara wa ujangiliiweje ishindwe kupambana nao? Kauli hii ni kithibitisho kuwa ikulu nausalama wa taifa kwa kiasi kikubwa wanahusika na mtandao wa ujangili.

MheshimiwaSpika,kauli za Rais Kikwete zimeendeelea kuushangaza umma hasa wananchianaowaongoza kwa kuwa alishawahi pia kutamka hadharani kuwa anayoorodha ya vigogo wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, na hata yamagogo; lakini kauli zake hizo hazikufuatiwa na kamata kamata yoyotempaka leo. Hata hiyo orodha ya vigogo 40 wa ujangili amebaki nayomwenyewe mpaka sasa anapokaribia kukabidhi madaraka kwa Serikali yaUKAWA. Tunamtaka Rais Kikwete kuhakikisha kuwa siku ya kutukabidhiIkulu hasahau majina 40 ya majangili nchini.

MheshimiwaSpika,Mafanikio ya operesheni dhidi ya ujangili hayapimwi kwa idadi yapembe za ndovu zilizokamatwa (seizures), na wala hayapimwi kwa idadiya waliokamatwa (arrests); bali hupimwa kwa idadi ya waliohukumiwa(convictions). Serikali ituambie , katika kipindi cha miaka mitanoiliyopita, ni watu wangapi mpaka sasa wanatumikia vifungo jela baadaya kutiwa hatiani kwa ujangili? Na kati ya hao, Wachina ni wangapi navigogo wangapi? Na ni watuhumiwa wangapi waliotajwa na Raiswameshatiwa hatiani mpaka sasa?

UDHIBITIWA BIASHARA YA MENO YA TEMBO

MheshimiwaSpika, ikiwa ni moja ya nchi wanachama waliozindua Mpango waKulinda Tembo Duniani uliosainiwa huko London mwezi Februari, 2014na kuhudhuria makongamano na mikutano mbalimbali iliyofuata, Tanzania imejiwekea maazimio kadhaa ambayo yanahitaji kutekelezwa:




  • [*=center] Kufanya ukaguzi wa wazi kujua ni kiasi gani cha meno ya tembo kilichopo;
    [*=center] Ni kiasi gani cha meno ya tembo yaliyopatikana kihalali (legally acquired);
    [*=center] Ni kiasi gani cha meno ya tembo yamepatikana kinyume cha sheria;
    [*=center] Kuteketeza meno yote ya tembo yaliyopatikana kinyume cha sheria katika hali ya uwazi kama nchi nyingine za China, Hong Kong, Ufilipino na Marekani zilivyofanya;
    [*=center] Kufanya jitihada za kuwaelimisha wale wale wawindaji haramu ili kupunguza biashara ya meno ya tembo.

MheshimiwaSpika,kwa kiwango kikubwa mapendekezo hayo hayajetekelezwa ikiwemokuteketeza shehena ya meno ya tembo pamoja na nyara nyenginezilizopatikana kinyume na Sheria yaani kwa njia haramu.

MheshimiwaSpika,kwa muda mrefu Kambi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikpendekeza kuwa nilazima kufanya jitihada zaidi ili kuongeza kiwango cha utambuzi nauelewa wa kujua watanzania wanashiriki vipi katika biashara haramu yameno ya tembo ambayo bado inaendelea kufanyika. Mwaka 2013 kulikuwana matukio mawili makubwa ya kukamatwa kwa meno ya tembo Dar esSalaam na Zanzibar.

Mojawapoya mambo ambayo tumekua tukishauri kwa muda mrefu ni pamoja nakuitaka Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kuhakikishakwamba shehena kubwa za pembe za ndovu zinazokamatwa (zaidi yakilogramu 500) zinachunguzwa kwa kupima DNA. Jambo hili badohalijafanyika. Aidha, tulielezea umuhimu wa kufanya uchunguzi kamahuu ili kuongeza weledi katika kubainisha maeneo ambayo uwindajiharamu unafanyika kwa viwango vya juu kwa kuwa Tanzania imepotezasehemu kubwa ya urithi wake wa asili na mapato endelevu. Kama tembowakiondoka, basi na watalii wataondoka vilevile na hivyo kuhatarishaustawi na ukuaji wa sekta utalii.

Kambiya Upinzani Bungeni natambua kuwa kuna hitaji kubwa la kutekeleza kwaukamilifu na kwa wakati sheria ya wanyamapori ili hatua madhubuti zakisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahalifu wote waliopo katika mtandaowa biashara hii haramu. Hii ina maana kwamba watakaoshtakiwa si waletu wanaojihusisha na uwindaji haramu, bali pia washiriki wakubwakatika kuchakata, kuuza nje ya nchi, kununua kutoka nje ya nchi,kusambaza, kupokea, na kumiliki meno ya tembo kinyume cha sheriapamoja na wale wanaofadhili kifedha biashara ya meno ya tembo nakughushi nyaraka, matumizi ya fedha chafu (money loundering),ukwepaji wa kodi na ufisadi wowote kuhusiana na biashara haramu yameno ya tembo.

MheshimiwaSpika,wakati nchini Kenya, watetezi wa hifadhi waliishinikiza serikalikuanzisha sheria kali dhidi ya ujangili ili kuwepo na adhabu stahiki,pili idara ya wanyamapori ya kenya (KWS) na wahifadhi maliasilikutangaza teknolojia mpya ambayo itasaidia kupambana na ujangili kamailivyotangazwa na Daily Nations ya tarehe 26 Machi 2013, na tatuserikali ya Kenya kuongeza askari zaidi ya 1,000 ili kukabiliana naujangili, haya yote yakifanyika Kenya kukabiliana na ujangili,Serikali ya Tanzania inaendelea kujikita kupiga vijembe kwa UKAWA nakuendelea kulinda majangili ambao taarifa zao zimekuwa zikizifikiamamlaka zilizo chini ya serikali.

MheshimiwaSpika,kambi rasmi ya upinzani bungeni inaitahadharisha CCM kuwa pamoja nakejeli na udhalilishaji kwa kambi yetu ya kuashiria kuwa na chuki yawazi na UKAWA, UKAWA imejipanga kimkakati kuhakikisha kuwainakabiliana na aina zote za ujangili ulioozesha taifa letu hasambele ya jumuia ya kimataifa.

UHARIBIFUWA MAZINGIRA KATIKA MLIMA KILIMANJARO

MheshimiwaSpika,Mlima Kilimanjaro ni urithi wa dunia unaoteketea kutokana nauharibifu wa mazingira unaochangiwa na shughuli za kibinadamu ndaniya hifadhi hiyo muhimu katika sekta ya utalii. Hadi sasa wataalamu wamazingira wamethibitisha kwamba barafu katika Mlima kilimanjaroimepungua kwa asilimia 82 ya theluji yote iliyopo tangu mwaka 1912 nakwa asilimia 52 ya theluji iliyopo sasa tangu mwaka 1962. Hali hiyoimechangiwa na vitendo vya kupungua kwa uoto wa asili hasa ukanda wamisitu ya asili ya mlima huo, ambao umekuwa ukiliingizia taifa mapatomakubwa kutokana na utalii unaofanywa kila mwaka hapa nchini.Halihii inatishia theluji hiyo kupotea kabisa na kufanya kizazi kijachokuiona theluji hiyo kupitia picha za kitalii au vitabu vya hadithitu.

MheshimiwaSpika,kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjarona Bwana Lonnie Thomson, mtaalamu wa Sayansi ya Theluji(Glaciologist) unaonyesha kwamba kuyeyuka kwa theluji ya MlimaKilimanjaro unaendelea kwa kasi kubwa. Utafiti huo umebaini kuwazaidi ya robo ya kiwango cha theluji kilichoufunika Mlima Kilimanjaromwaka 2000 kilipotea ilipofika mwisho wa mwaka 2007. Bwana Thompsonna washirika wake walitoa ripoti hiyo tarehe 2 Novemba 2009, katikamhadhara uliondaliwa na Chuo cha Kitaifa cha Sayansi cha Marekani(National Academy of Science).

Takwimu hizo zinaonyesha kwambauyeyukaji wa theluji katika Mlima Kilimanjaro uliongezeka kwa kiasikikubwa miongo ya hivi karibuni, anasema Bwana Thompson. Inasemekanakuwa kuanzia mwaka 1912 hadi 1953 theluji inayofunika MlimaKilimanjaro ilipungua kwa kiwango cha 1.1% kwa mwaka. Vivyo hivyo,kati ya mwaka 1953 na 1989 wastani wa kiwango cha kupungua kwatheluji kwa mwaka kiliongezeka na kufikia 1.4%.


MheshimiwaSpika,inakadiriwa kuwa zaidi ya mito 20 na vyanzo vya maji vipatavyo 70vilivyokuwa vikitiririsha maji yake kutoka ndani ya Hifadhi ya Taifaya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) katika wilaya za Rombo, Hai na MoshiVijijini, vimekauka na kusababisha upatikanaji mdogo wa maji. Lakinihoja ni je, nani atamfunga paka kengele, kama wanaopaswa kutekelezamaagizo mbalimbali ya utunzaji wa Mlima Kilimanjaro ndi wanaotuhumiwakujihusisha na vitendo hivyo vinavyouweka mkoa wa Kilimanjaro katikamikoa inayokabiliwa na uharibifu wa mazingira kwa kiwango cha juukabisa?

Kasi ya ongezeko wa uharibifu wa mazingira ni dalili kuwautekelezaji wa sera, sheria na kanuni za mazingira una mapungufu nani lazima Serikali ya CCM ikae kando ili Serikali itakayoundwa naUKAWA ichukue hatua madhubuti na za haraka katika kuulinda MlimaKilimanjaro.


UWEKEZAJIKATIKA SEKTA YA UTALII NCHINI

MheshimiwaSpika, kwaeneo kubwa la ardhi lililofunikwa na wingi wa misitu pamoja na ainambalimbali za maua na viumbe, Tanzania ni mojawapo ya vivutiovikubwa vya utalii barani Afrika. Nchi yetu ina raslimali nyingiasilia ikiwemo pamoja na maeneo mengi ya nyika za mapori yenye ainanyingi za banoai.

MheshimiwaSpika, Miongonimwa vivutio vya utalii ni pamoja na Mbuga za wanyama , hifadhi zataifa, hifadhi zilizozuiliwa na maeneo ya kihistoria. Hata hivyo kwasababu ya ongezeko la joto, baadhi ya hivi vivutio ikiwemo thelujikatika kilele cha mlima Kilimanjaro iko katika hatari ya kupotea. Nabaadhi ya wanyama katika mbunga zenye ukame mkubwa wameanza kupunguana kuathirika.

MheshimiwaSpika, KambiRasmi ya Upinzani, kwa muda mrefu , imeshauri Serikali ya CCMkuwekeza katika njia mbadala ya nishati ya umeme ili kuinua sekta yautalii hasa wa mbugani. Mojawapo ya vipaumbele vya Serikaliitakayoundwa na UKAWA ni pamoja na kuhakikisha kuwa nishati ya jua(solar energy) inatumika kama chanzo kikubwa cha umeme ili kuwezakukabiliana na tatizo la umeme katika maeneo yanaongoza kwakutembelewa na watalii hasa mbuga za wanyama, maeneo ya kihistoria namajengo ya kale.

MheshimiwaSpika, uwekezajikatika Sekta ya Utalii ni suala lenye tija kubwa katika uchumi wetukwa kuwa sekta hiyo imekuwa ikichangia katika uchumi wa Taifa lichaya uwekezaji mdogo uliofanyika katika sekta hiyo.

MheshimiwaSpika, takwimuzilizopo zinaonyesha kuwa katika maeneo yote ya hifadhi zetu kwasasa kuna kuna hoteli zenye uwezo wa kutoa huduma za malazi(carrying capacity) kwa watu 6,681 ambapo kwa miaka mitano ijayoidadi hii itafikia uwezo wa kulaza watu 8,421. Hiki ni kwango kidogosana cha huduma za malazi kiasi kwamba tunapoteza fursa ya kunufaikakatika sekta ya utalii.

MheshimiwaSpika, miundombinuya usafiri na usafirishaji ya ndani ya nchi, uwekezaji katika ujenziwa hoteli kwenye maeneo muhimu ya utalii kama vile kwenye hifadhi,mikoa inayozunguka mlima Kilimanjaro kutasaidia sana kuvutia watalii.Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kuwa uboreshaji wa miundombinuya usafiri hasa wa anga ilini kipaumbele kikubwa cha kuinua sekta yautalii nchini na kujenga hoteli za viwango vya Kimataifa katikamaeneo yenye vivutio vya watalii ili kuvutia mashirika ya mengi yandege toka nje kuja hapa.

MheshimiwaSpika, kwamuda mrefu tumekua tukileta mapendekezo kwa Serikali kuhusu umuhimuwa kufufua shirika letu la Ndege la Taifa ili tuweze kumudu ushindanikatika usafiri wa anga na hapohapo kuongeza idadi ya watalii katikanchi yetu. Aidha, tumeshauri umuhimu wa kuboresha Uwanja wa Ndege waKilimanjaro na ule wa Julius Nyerere Dar es Salaam ili kuwa kitovucha usafiri wa anga na kuyafanya mashirika mengi ya kimataifa kutumiaviwanja hivyo vya ndege na kuongeza idadi ya watalii wa njewanaotembelea nchini.

MheshimiwaSpika, wataliitoka nje wanapenda sana kupanda ndege za nchi wanazotembelea zaidikuliko kupanda ndege za kuunganisha ili kupunguza gharama za usafiri.Mfano mzuri ni miaka ya themanini wakati Air-Tanzania ilipokuwainafanya safari zake nchi za Ulaya, watalii wengi walikuwa wanakujakwa ndege zetu. Hoja ni kwamba Serikali imeshindwa kabisa kufufuaShirika la Ndege la Taifa (ATC). Pamoja na kuwa Kambi Rasmi yaUpinzani ilipendekeza umuhimu Serikali kuingia ubia na makampunibinafsi kupitia mpango wa Private Public Pertnership – ( PPP) ilikuboresha na kuinua huduma za usafiri wa anga hapa nchini , Serikaliimeshindwa kutekeleza mapendekezo yetu.

MheshimiwaSpika , ikumbukwe kuwa sekta ya utalii nchini inaongoza kwa kuingiza fedhaza kigeni nchini ikifuatiwa na madini. Kwa mujibu wa Benki Kuu yaTanzania (BoT), mwaka 2014 sekta ya utalii iliingiza Dola 2 bilioniza Marekani na kuizidi sekta ya madini ambayo ilikusanya Dola 1.7bilioni.

MheshimiwaSpika,mgogoro ulioibuka baina ya Kenya na Tanzania unapaswa kuwa somo toshakatika kuhakikisha sekta ya utalii nchini inakuza uchumi na kuimarikaili kuliongezea taifa mapato. Mgogoro huo uliibuka baada ya nchi ztukuwekeana masharti ikiwemo Kenya kuzuia magari yenye usajili waTanzania kubeba au kushusha watalii katika maeneo ya vivutio vyawatalii na Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Kwaupande wa Tanzania sharti lililokuwapo ni kupunguza kupunguza safariza Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuingia nchini, kutoka 42 hadi 14kwa wiki.

MheshimiwaSpika,kwa kumbukumbu za Bunge lako , mgogoro huu ulianza Desemba 22, mwakajana, baada ya Kenya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kupakiaau kuteremsha watalii kwenye vivutio vya utalii na viwanja vya ndegenchini humo. Baadaye mwezi huohuo, Waziri wa Masuala ya AfrikaMashariki, Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie alikutana naWaziri wa Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu na walipeana wiki tatuza kulitafutia ufumbuzi suala hilo. Baada ya muda huo kwisha bilamuafaka, Februari 6, mwaka huu, Kandie alirejesha marufuku ya awalikwa madai kuwa Tanzania imeshindwa kuchukua hatua.

MheshimiwaSpika,katika hali iliyoonekana ni kulipiza kisasi, Machi 18, mwaka huu,Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA) ilipunguza safari zaShirika la Ndege la Kenya kutoka 42 hadi 14 kwa wiki, ambayo nikaribu na asilimia 60. Mpango huo ulitekelezwa kwa mujibu wamakubaliano yaliyosainiwa kati ya shirika na Serikali ya Tanzaniaambayo ni safari 14 kwa wiki. Kuongezeka hadi safari 42 ilikuwa nikinyume na makubaliano.

MheshimiwaSpika,mgogoro huu ulikuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Tanzania kwa kuwasekta ya utalii nchini, imeendelea kuwa chanzo cha mapato kwawananchi wa mikoa ya kaskazini hasa vijana ambao wanaotegemeashughuli za utalii kujipatia kipato ili kuendesha maisha yao yakilasiku.

MheshimiwaSpika,watalii wanapitia Kenya kwa sababu ya usafiri. Shirika la Ndege laKenya (KQ) linafika katika nchi nyingi ambako watalii wanatoka. Namnapekee ya kukabiliana na hali ni kuwa na Shirika la Ndege la Taifakama ilivyokuwa ATC zamani. Tayari Tanzania imetajwa kama mojawapo yanchi saba duniani zinazovutia watalii kwa wingi. Kwa sababu yaushindani, ni wazi kuwa majirani watafanya kila jitihada kuhakikishawanashindana nasi. Ni Shirika la Ndege la Taifa pekee ndilo litakuwasuluhisho la kudumu.

Kuna wanaolikataa kwa madai kuwa litaingizahasara. Ukweli ni kwamba, shirika la ndege mara nyingi huchocheaukuaji wa sekta nyingine. Shirika la Ndege la Taifa litachocheawatalii wengi kuja nchini moja kwa moja na hivyo kukuza utalii.Litasaidia wafanyabiashara wa kilimo cha maua na mbogambogakusafirisha bidhaa zao haraka kwenda ughaibuni.


MheshimiwaSpika,Kambi ya Upinzani inaamini kuwa ina uwezo wa kuiinua sekta ya utaliinchini kwa viwango vya kimataifa zaidi na kuifanya ichangie pato lataifa kwa asilimia kubwa zaidi ya sasa kutoana na mipango mikakatiambayo tuemjidhatiti kuisimamia.

MheshimiwaSpika,kwa bahati mbaya sana, miaka 35 mfululizo ya CCM kuliongoza hilitaifa sio tu kwamba imeshindwa kulisaidia hili Taifa kuwashinda nakuwatokomeza maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini baliwamezidi kuimarika kwa njia tofauti-tofauti. Ahadi nyingi za CCMnyakati za uchaguzi na katika hotuba mbalimbali zimekuwa zikioneshakwamba CCM inatambua changamoto zilizopo na inajua ni nini kinawezakufanyika ili kukabiliana na changamoto hizo.

Tatizo limekuwa katikauwezo mdogo wa CCM kuweka mifumo sahihi ya utekelezaji wa mipango namikakati inayowekwa na kuisimamia ili kuhakikisha kuwa mipango namikakati hiyo inazaa matunda yanayotakiwa. matokeo yake maadui haowameendelea kuimarika na kwa Upande wa CCM, Chama kimeendeleakujiimarisha katika kubadilisha ahadi, kauli mbiu na ngonjera zakuhalalisha kuendelea kuwepo kwa matatizo hayo!


HITIMISHO

MheshimiwaSpika,wakati wa utawala wa Rais wa Mareani Jimmy Carte , Ronald Reaganambaye alimshinda Jimmy Varter akiwa madarakani aliwahi kusemayafuatayo;

'inthis current crisis, the government is not the solution to ourproblem, the government is the problem'
Kwakifupi maneno ya Ronald Reagan, yalimaanisha kuwa;
'Katikakadhia hii, Serikali hii siyo suluhisho la tatizo letu, Serikaliyenyewe ndiyo tatizo'.

MheshimiwaSpika,sasa umefika wakati wa watanzania kutambua kuwa Serikali ya CCMhaiwezi kutatua matatizo yao kwa kuwa Serikali hii hii ya CCM ndioTatizo.

MheshimiwaSpika,naomba kuwasilisha.

..................................................

Mch.Peter S. Msigwa (MB)MSEMAJIMKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI,
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.
28.05.2015
 
Back
Top Bottom