From zero to hero

Catherine

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
1,261
758
Hellow wadau wote wa business forum!

Naamini watu wengi wapenda mafanikio huwa wanajifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. Ukitaka kufanikiwa ni vizuri kujichanganya na waliofanikiwa na sio wale waliokata tamaa hata za kujaribu. Katika kutafuta mafanikio kila mtu ana mbinu zake, wapo wapenda shortcut na wapo wanaofight kwa nguvu zao.

Watu wengi ni waoga wa kuthubutu, wapo vijana tunajiuliza how/where do we start?, simple answer ni kwamba we have to start where we are. Swali linabaki how?. Naamini Wapo wadau wameanza from zero (hapo namaanisha walikuwa na akili zao tu, nothing else). Nawaomba hao wadau watupe inspiration, naamini wengi tutajifunza from them na roho ya kutojaribu au kukata tamaa haitokuwepo tena. Nakaribisha mawazo yenu, (waweza hata niPM then nitawakilisha mchango wako hapa bila kutaja ID yako).

LET YOUR SUCCESS BE OUR INSPIRATION.
 
Naamini mtu asiye kuwa na kazi au ajira ni mwepesi kuingia kwenye biashara kwa sababu hana option. Challenge inakuwa zaidi kwa mtu mwenye kazi yake nzuri ku resign na kuingia kwenye business. Huyo na muheshimu sana.
 
Unaweza usiwapate walengwa kwa sababu tafsiri ya kufanikiwa ni ngumu kuipata na inakuwa wakati mwingine wengi hatuelewi kama tumefanikiwa au bado.

Mawazo yangu ni haya, omba michango toka kwa watu walioanzia zero mpaka hapo walipofikia kwa njia za haki ili mradi bado shughuli zao zinaendelea kusonga mbele, hapa utapata michango mingi sana na kupitia hiyo michango utapata unachohitaji.
 
Malila, palipo na mafanikio panaonekana isipokuwa kiwango cha kuridhika na hayo mafanikio ndio hutofautiana na ndio maana tafsiri ya mafanikio kati ya mtu na mtu hutofautiana. Wapo watu wakishajenga nyumba na kununua gari tayari huona wamefanikiwa (hapo ni sababu wamekamilisha malengo yao na wamekuwa satisfied ). Apart from that wengine hutaka kumiliki companies kwahiyo akiwa na nyumba na gari huona hajafanikiwa (hapo sababu hajawasatisfied na alipofikia).
Watu wa kundi la pili inawezekana hawajaridhika kwasababu hawajaachive goals zao tofauti na watu wa kundi la kwanza.
Ningependa kupata maoni ya wadau ambao wameanza from zero na wanaona they are succesful (sababu wameachive goals zao na wapo satisfied with their success).
 
Last edited by a moderator:
Naamini mtu asiye kuwa na kazi au ajira ni mwepesi kuingia kwenye biashara kwa sababu hana option. Challenge inakuwa zaidi kwa mtu mwenye kazi yake nzuri ku resign na kuingia kwenye business. Huyo na muheshimu sana.

kuingia kwenye biashara chash si sababu ya kukosa kuajiriwa. Wapo watu hawajawahi kuajiriwa kwasababu hawapo willing kumfanyia mtu kazi. Suala la challenges hata yule ambaye hana kazi anazo tena nyingi tu.
 
Last edited by a moderator:
ahsante mpenzi, mi mzima. upo chit chat maeneo gani nikufate?

Leo sijapita kabisa jukwaa pendwa CC.....nipo kisiasa na kimapenzi zaidi lol

Samahani mleta mada Catherine kwa kuchakachua mada .....kwaheri nisijerushiwa mawe !
 
Last edited by a moderator:
Leo sijapita kabisa jukwaa pendwa CC.....nipo kisiasa na kimapenzi zaidi lol

Samahani mleta mada Catherine kwa kuchakachua mada .....kwaheri nisijerushiwa mawe !

orait, nakuja ulipo. Zipuwawa tukutane baadae stress free zone. Wadau wote plz endeleeni kutoa mawazo, hawa wachakachuaji wa threads nawamuvuzisha.
 
Last edited by a moderator:
No.-- Jina-- kiasi-- umri-- biz-- Uraia

#1. Carlos Slim Helu-- $69B --72-- telecom-- Mexico
#2. William Gates III-- $61B -- 56-- Microsoft-- United States
#3. Warren Buffett-- $44B-- 81-- Berkshire Hathaway-- United States
#4. Bernard Arnault-- $41B-- 63-- LVMH-- France
#5. Amancio Ortega-- $37.5B-- 75-- Zara-- Spain
#6. Larry Ellison $36B-- 67-- Oracle-- United States
#7. Eike Batista $30B-- 55-- mining oil-- Brazil
#8. Stefan Persson-- $26B-- 64-- H&M-- Sweden
#9. Li Ka-shing-- $25.5B-- 83-- diversified-- Hong Kong
#10. Karl Albrecht-- $25.4B-- 92-- Aldi-- Germany

Hao jamaa hapo juu ndio matajiri duniani sasa hivi. Kati yao namba 1,2,3,5,6,7,9,10 wametafuta hela wenyewe yaani ‘self made'.

Ukiangalia umri wao na ulinganishe na average ya wana JF unabaini ya kwamba kuna miaka nyingi kabla kufikia huu umri wa hawa matajiri.Hivi nataka kuwaambieni ya kwamba kuna mda wa kutosha wa kila mmoja hapa JF kuwa tajiri duniani. Usiwe na haraka yakuwa tajiri, usiogope kuchukuwa carefully calculated risks, ukifeli usiogope kunyanyuka, kujifuta mavumbi na kuanza upya, usiwe na regret ya uliyo yafanya huko nyuma, ukifika kiwango fulani cha hela wekeza kwenye asset ambazo hazitaweza kupotea kwa bahati mbaya, yaani uweke cushion ya kuto rudi sifuri,kuwa na malengo makubwa na ujipe moyo mwenyewe hata kama hakuna mwingine anaye kuunga mkono. Usichezee hela nyingi kwenye starehe , do not just work hard,work smart, utafurahia kuanza kupanda hiyo ngazi ya matajiri wa duniani. Mhimu saaaana ukipata idea ambayo haipo au haijajaribishwa popote,usiogope kuifanyia kazi. Matajiri wa kupindukia wana tabia za kufanya mambo hayajafanywa na mwingine.

"I've failed over and over and over again in my life. And that is why I succeed."Michael Jordan
 
Ahsante sana chash. Umetupa ujumbe mzuri hapo. Nitajitahidi nitafute information zao zaidi, wapo wapi 'self made' wa nyumbani!.
 
Last edited by a moderator:
Ningependa kupata maoni ya wadau ambao wameanza from zero na wanaona they are succesful (sababu wameachive goals zao na wapo satisfied with their success).

mimi nilianza from zero kwa njia zinazo mpendeza mungu huku mtaji wangu ukiwa ni ubunifu wa kuyasoma na kuyatumia mazingira yanayonizunguka, kutopenda sifa (kufanya kazi ili kuwafurahisha watu).. how?.. ukifungua threads za nyuma za ujasiriamali utanielewa vizuri.

"wanaona they are succesful" hii kitu huwa haipo kwa mjasiriamali wa ukweli kutokana na sifa yake kuu ya kuwa innovative na kutaka vya juu zaidi, karibu kila wiki huwa napata mawazo mapya kuendeleza kilimo na ufugaji
 
wanyumbani wapo kama Dr. Reginald Mengi ambao ni mfano wa kuigwa ila mimi nime taja wanao ongoza duniani kwa sababu ni vyema mtu ajipime na walio namba moja na sio walio namba 200 na kuendelea.
 
Unaweza usiwapate walengwa kwa sababu tafsiri ya kufanikiwa ni ngumu kuipata na inakuwa wakati mwingine wengi hatuelewi kama tumefanikiwa au bado.

Mawazo yangu ni haya, omba michango toka kwa watu walioanzia zero mpaka hapo walipofikia kwa njia za haki ili mradi bado shughuli zao zinaendelea kusonga mbele, hapa utapata michango mingi sana na kupitia hiyo michango utapata unachohitaji.

mkuu umenena vyema. kwa sababu businesswise others we belive hata kama umefanya kitu na kisifike uliptaka au kufeli by any means pia hayo ni mafanikio maana utakua unauzoefu zaidi ya anaeogopa kuthubutu.
 
Kufanikiwa kupo. Huwezi kufeli na useme umefanikisha, utakuwa unajifajiri tu wakati umefeli.mafanikio ni kufikia malengo. Kwenye biashara kuna mtu tutasema amefeli, mwingine tutasema anajitahidi mwingine ameweza, tunapima kwa kukisia kuwa malengo yalikuwa yapi. Pia kusema mtu amefanikisha sio mwisho sababu kesho unaweza kupata kafeli. Kipimo kinaendelea hadi kufa. Unaweza kupata bilionare kafilisika.isitoshe jamii inajua kupima mafanikio na huwa tunakubaliana kuwa fulani yupo vizuri nk.sasa ambaye hakufaulu hatuwezi kujua amefaulu kiasi gani huko nyuma ya pazia.kinacho onekana ndio kinacho hesabika. Hata forbes wanatumia njia hiyo kupima mafanikio. Kama umeshindwa kufikia malengo yakuonekana na kutambuliwa naomba mjitahidi msijipe moyo wakujidanganya nyanyukeni mpige kazi. Mie bado sijakaribia kufikia malengo yangu.
 
tatizo mtoa mada umesema unataka wale wa from zero to hero! mm bado sijafika kwenye hero ila siko kwenye zero!
 
Naamini mtu asiye kuwa na kazi au ajira ni mwepesi kuingia kwenye biashara kwa sababu hana option. Challenge inakuwa zaidi kwa mtu mwenye kazi yake nzuri ku resign na kuingia kwenye business. Huyo na muheshimu sana.

Hakuna hata tajiri mmoja ambaye ni muajiriwa, matajiri wote ni wafanyabiashara. ajira ni utumwa wa kumtumikia mwenye mali ili akulipe mshahara, ajira inatokana na woga wa kuthubutu. ni wajasiri walioweza kuthubutu tu ndo wamefanikiwa. Mshahara hata uwe mkubwa kiasi gani, once a slave always a slave.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom