From Zanzibar: Kura za Maoni Shwari!

Leo hii nimeguswa sana na kura za maoni zilizofanyika Zanzibar pasipo kuelewa haswa malengo yake kitaifa zaidi ya kuchanganyikiwa. Ni rahisi sana kwa mtu yeyote kuchukulia uhalali wa kura hizi kama hataweza kuzingatia mfumo mzima wa kiutawala wa nchi yetu.

Majuzi nimemsikia rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh.Kikwete akihutubia kwa mara ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu ujao, na katika hotuba yake amezungumzia pia matumaini yake na wananchi kuhusiana na zoezi zima la kura za maoni yanayofanyika Visiwani na hata kudiriki kutoa mifano ya nchi kama Kenya, Zimbabwe S.A na Kongo, ili kuonyesha jinsi gani zoezi hili linaweza kuondoa uhasama uliopo baina ya vyama na wafuasi wa vyama viwili vya CUF na CCM hali nchi hizo zimetumia mfumo huo Kitaifa (federalism) na sio sehemu moja ya nchi zao.

Kwa hiyo pasipo kufikiria haya ni matumaini mazuri sana kuyasikia lakini sidhani kama yana ladha nzuri ukiyaweka kinywani kwa sababu nyingi na za msingi hasa ukizingatia mfumo wa kiutawala wa nchi yetu. Na kutokana na hilo yamekuja maswali mengi kichwani mwangu ambayo nimeshindwa kuyapatia jibu.

Kwanza tutazame muundo wa kiutawala kwa nchi yetu. Ni hivi karibuni tu bunge letu lilishikwa na mgogoro mkubwa unaohusu nafasi ya Zanzibar katika Muungano wetu. Mgogoro ambao unanikumbusha sana mgogoro wa kiutawala uliopo baina ya Canada na jimbo la Quebec ambao umedumu kwa miaka mingi sana pasipo ufumbuzi wa regulations zinazohusiana na maswala ya Kiuchimi, kodi za mapato na rasilimali..

Na nakumbuka vizuri Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akinukuu katiba yetu ya Muungano kwa maelezo kwamba Zanzibar sio Taifa (a nation) isipokuwa tuna Taifa moja tu nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Likaja swala la Zanzibar kama nchi nalo likapingwa pamoja na kwamba Zanzibar ni nchi inayoongozwa na rais wake, bunge lake na mahakama ktk muundo mzima wa serikali unaoiwezesha kuitwa nchi. Na hakika hadi leo hii nashindwa kuelewa nafasi ya Zanzibar ktk Muungano wetu hata baada ya kufikia muafaka baina ya chama cha CUF na CCM ulofanikisha upigani wa hizi kura za maoni.


Sielewi kama zoezi hili la kura za maoni zimelenga kuondoa tatizo la Muungano ama kuondoa chuki baina ya viongozi wa vyama na serikali ya Zanzibar ktk kuimarisha udugu baina yao. Na sielewi pia mafanikio yoyote ya hizi kura za maoni utawezesha vipi kujenga sheria zinazohusiana na kero za Muungano wa nchi zetu kisheria ikiwa nguvu kubwa imewekwa ktk kuridhisha matakwa ya vyama vya kisiasa.

Swali kubwa linalojitokeza ni mamlaka haya yataweza vipi kujenga na kuimarisha mfumo mzima wa uchaguzi nchini ikiwa vyama viwili vinaweza kukubaliana kuunda serikali ya mseto (share power) kabla ya uchaguzi mkuu kuvipa mamlaka ya kuunda serikali hiyo chini ya kifungu gani cha katiba ikiwa nchi yetu ni moja itawaliwe na mifumo miwili tofauti ya kiutawala.

Najiuliza ni vigezo gani vimetumika haswa kufikia maamuzi ya kuundwa kwa serikali ya mseto mbele ya matokeo ya uchaguzi mkuu pasipo kushirikisha bunge la Muungano, vyama vyote vya kisiasa, mwanasheria mkuu na taasisi zote za kiutawala zinazoweza kufikia maamuzi ya busara kuhusiana na kero za Kitaifa na sio kero za upinzani baina ya vyama viwili pasipo kutumia ushahidi wowote wa Uchaguzi mkuu.

Kisha sijawahi kusikia TAIFA MOJA (a nation) yenye kuunda serikali ya mseto sehemu moja kisha ikatawaliwa na chama kimoja Kitaifa.
Kama nilivyosema hapo juu rais wetu Mh. Kikwete ametoa mifano ya Kenya, sidhani kama hao Kenya wamefikia muafaka wa kuunda serikali ya mseto kwa jimbo moja iwe kanda ya ziwa kwa Raila au hata hao Zimbabwe au nchi za Marekani na Uingereza kuunda mfumo kama huu.

Kama Zanzibar sio Taifa wala nchi isipokuwa tuna nchi moja ya Jamhuri ya Tanzania. Au itumike lugha yoyote ile kutenganisha Visiwani na bara ktk muundo wa serikali hizi bado kikatiba sioni sheria inayoviwezesha vyama viwili kuunda serikali ya mseto ktk sehemu moja ya taifa kabla hata ya uchaguzi mkuu.

Je, kilichofanyika ni kuungana kwa vyama hivi (coalition) ili kuunda nguvu moja ya ushiriki ktk kutafuta ushindi wa uchaguzi mwezi October na sio kuunda serikali ya mseto (share power) kama tunavyotangaziwa.. Na kama kilichoundwa ni serikali ya mseto, Je sheria ya uchaguzi inaruhusu kuundwa kwa serikali ya mseto hata kabla ya matokeo ya uchaguzi mkuu na pia sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kawaida ya kura za maoni duniani kote ni lazima theluthi mbili, au asilimia 66.67 ipatikane kwa kinachopigiwa kura kipite. Kama katika kura ya maoni Visiwani ni asilimia 66.4 tu ndiyo wamesema "ndiyo" basi suala limeshindikana. I knew it -- it's all usanii.

Who told you, and where is that coming from?. Acha mambo ya kugeneralise kila kura huwa inawekeweka sheria yake na wanaopiga kura hiyo. Hakuna universal declaration of such thing.
 
Kawaida ya kura za maoni duniani kote ni lazima theluthi mbili, au asilimia 66.67 ipatikane kwa kinachopigiwa kura kipite. Kama katika kura ya maoni Visiwani ni asilimia 66.4 tu ndiyo wamesema "ndiyo" basi suala limeshindikana. I knew it -- it's all usanii.

Wale Quebec (Canada) walitaka kujitenga, kura ya maoni ilikuwa 51 kwa 49 kukataa. sasa wewe kawaida yako umeitoa wapi?
 
Kawaida ya kura za maoni duniani kote ni lazima theluthi mbili, au asilimia 66.67 ipatikane kwa kinachopigiwa kura kipite. Kama katika kura ya maoni Visiwani ni asilimia 66.4 tu ndiyo wamesema "ndiyo" basi suala limeshindikana. I knew it -- it's all usanii.
Dunia gani unayoishi wewe, wewe ni zezeta kweli, yaani sheria ya US, Japan na Tanzaina zanafanana mbona UK hawana hiyo anayemzidi mwenzake hata kwa kiti kimoja ndiye mshindi, endelea kujifariji nimeamini kweli wewe ni Kafibangi.
 
Wakuu zangu,
Mtanisamehe kuwarudisha nyuma kwa mara nyingine. Hapo awali niliuliza swali moja kuhusu NDIYO na HAPANA zinasimamia nini sidhani kama nimejibiwa. Kama tayari naomba kuonyeshwa ukurasa au mtu anaweza kuniwekea hapa tena. sababu ya kuuliza hivi nilitaka kujua swali lilokuwa katika kadi ya kupigia kura ili nipate kuelewa kulikoni, pia hizi Ndiyo na Hapana, zina mahusiano yapi na future system nzima ya vyama vingi nchini.
Mkuu Mkandara, ulijibiwa pale pale ilipouliza,
Hii ni utekelezaji wa Muafaka kati ya CCM na CUF. Mazungumzo yalianzia Bagamoyo, wakafikia makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto Zanzibar baada ya uchaguzi ujao.
Baraza Kuu la CUF lika endorse, NEC ya CCM kule Butiama wakagoma kwa kuweka sherti la kwanza Wanzazibari waulizwe. CUF wakasusa na hali ikawa stalmate mpaka November 4 mwaka jana Karume na Seif waliposhikana mikono na kukubali yaishe, ndipo CCM ikakumbushia hayeshi bila kufanya referendum, na ndicho kilichofanyika juzi na matokeo ndio hayo.

Swali ni Jee unakubali kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu ujao wa Octoba 31?.

Kma jibu ni ndiyo, weka alama ya vema kwenye kisanduku cha ndiyo kama ni siyo, weka alama ya vema kwenye kisanduku cha hapama.

Waliosema ndiyo wameshinda.

Matokeo ya Zanzibar ni indicator kuwa Tanzania lazima tufuate mtindo huu wa coalition goverment in future bila kuyasubiri ya Kenya na Zimbabwe. Kwa vile upinzani huku bara bado ni too weak, CCM inaendeleza kiburi cha supremacy yake kujifanyia kinavyotaka, lagic ni kuwa kama kule muundo wa serikali ni hivi, why not huku?.
 
Ushindi wa 66% ya wazanzibari kuwa wanataka serikali ya mseto,unazani izo ni kura za wanaCCM?Definately ni za wanaCUF.
Mwaka huu CCM kazi wanayo wameshindwa kuiba apo,anyway labda wanajipanga kuiba october
 
Wakuu zangu,

Haya mambo ni mchanganyiko sana! Watawala wetu wanasema hii ni nchi moja lakini baadaye mambo ukiyaona utagundua tuna nchi mbili zilizoungana kwa utaratibu usiojulikana duniani!!

Nawapa hongera wazanzibar kwa uamuzi wao, for sure watasonga mbele tu!!
 
Majimbo yaliyopiga kura za hapana kwa Zanzibar ni
Chaani kwa kura 3264(63.8%) za Hapana dhidi ya kura 1,864 (36.2%) za Ndiyo.
Donge kwa kura 3234(71.4%) za Hapana dhidi ya kura 1,296 (28.6.2%) za Ndiyo.
Kitope kwa kura 2,738 (59.8%) za Hapana dhidi ya kura 1,843 (40.2%) za Ndiyo.
Chwaka kwa kura 3,887 (59.5%) za Hapana dhidi ya kura 2,643 (40.5%) za Ndiyo.
Uzini kwa kura 4,235 (74.7%) za Hapana dhidi ya kura 1,437 (25.3%) za Ndiyo.
Makunduchi kwa kura 4,961 (64%) za Hapana dhidi ya kura 3,383 (21.8%) za Ndiyo.
Muyuni kwa kura 4,503 (74.5%) za Hapana dhidi ya kura 1,542 (25.5%) za Ndiyo.
Dole kwa kura 2,527 (51%) za Hapana dhidi ya kura 2,429 (49%) za Ndiyo.
Amani kwa kura 2,622(50.2%) za Hapana dhidi ya kura 2,601 (49.8%) za Ndiyo.
Kwahani kwa kura 2,709(60.1%) za Hapana dhidi ya kura 1,797 (39.9%) za Ndiyo.

Tuwasubiri Wabunge na Wawakilishi wa CCM toka majimbo haya kama kweli they will be votted in.


Duh! Ina maana kwamba Unguja yote wamekataa kata kata? Sikutarajia hii kitu kwa kweli. Sasa wasipo-vote kwa wawakilishi wao watakuwa wanajipiga miti wenyewe. Itakuwa ni sawa sawa na mtu anayegoma kula ati kupinga kitu.

Mheshmiwa nadhani hii lugha yako ina mushkeli. Unaonaje ukitumia lugha inayoweza kuzungunmzwa kwenye kadamnasi ya watu wa rika mbalimbali.
 
Back
Top Bottom