From Mhimbili: 100,000 kila daktari wa kijeshi anaposaini, usafiri wa kurudi nyumbani nakuja ofisini

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,338
Nimetoka mhimbili mda si mrefu na nikaonana na daktari bingwa mmoja samahani sitamtaja jina hapa.........na akasema wao ndio wanaolea hicho kilichopo sasa wameamua kugoma ili serikali itimize wanachodai!!!! Akaongeza kua kila daktari wa kijeshi anaposaini asubuhi kufanya kazi ana laki moja nje ya mshahara wa kazi na hapo bado hajaitwa "Call",na kuna chakula special wanaletewa kutoka catering flani hivi hii nadhani ni ya fisadi mmoja......na hawaruhusiwi madaktari wa mhimbili kula pale .....alisogea mmoja akaambiwa samahani Dr. hiki ni kwa ajili ya madaktari wageni tu.......mmmmmh....akiongea kwa uchungu akasema wao hutumia usafiri wao kila wanapoitwa call na kulipwa pesa kiduchuuuuuu sana na si hivo tu usafiri wa kurudi nyumbani na kuja kazini wanajitegemea.....!!!!! Mi nilishindwa kuzungumza nilikua nawalaumu sasa naelewa madai yao ni ya msingi!!!!!!!
Naomba serikali iwasikilize na itekeleze wanachotaka.....nawasilisha:canada:
 
kwa hiyo chanza cha madaktari bingwa kugoma ni hao madaktari wa jeshi???

bongo bana tumekaa kizuzuzuzu, yaan nao wanataka kulipwa 100000 kila wakisaini na waletewe chakula??? kutoka cafteria

duuu haya bana bongo hii.
 
Duu hii kali hat mie ningegoma.SH 10,000 KWA LAKI MOJA hakuna wiano sawa hapo.
Mi najua wao wanjeshi wajitolea kumbe wanalipwa,
 
100000 zidisha kwa siku 15......................zidisha kwa 'madaktari' wa jeshi 15...................



nchi ina hela hii hebu walipeni madaktari tuendelee na mengine.
 
wale wa jeshini wanalipwa na JWTZ mwajiri wao, kwa hiyo wana haki kupata marupurupu yao kama vile mikataba yao inavyosema na hawa wa kwetu wanalipwa na serikali ambayo tumeshaambiwa madai yao yanashughulikiwa.

Msiniulize kwamba serikali ina bajeti ngapi, hilo swali muulizeni waziri wa fweza.
 
Sasa napata picha kuwa kumbe hela ipo ila serikali inafanya kiburi maana kama wanaweza kutoa 330,000 plus 100,000 in a maana wanaweza kuwalipa madai yao hao madaktari
 
Bogo zaidi ya uijuavyo. SISi wa TZ tumelala ilibidi tuungane na ma Doc tuingie barabarani wafanyakazi wooote, kupigania haki zetu, after all huyu jamaa wa mbayuwayu alisema hazihitaji kura zetu sasa wa nini kumlea lea tuu, aondoke bana anserikali yake dhalimu
 
Sasa ni wakati wa wale wajiitao manabii na mitume kutenda miujiza kwa kufika mahospitalini kuwaponya wagonjwa kama wafanyavyo ktk makanisa yao!
 
watanzania inabidi tuunge mkono wataalam wa afya ili serikari iweze kutoa malipo na posho kwa wataalamu wetu
 
Sikubaliani na hoja kwamba madrk wa kijeshe wana posho ya laki na wa kiraia hawana.kwanza hata jeshi linalipwa na serikali na hili jeshi limekuwa likitumika kwa manufaa ya watu binafsi mfano biashara ya meremeta na mgodi wa buhemba nk.hivyo kuwa na matabaka hapa sii sahihi watu wapewe stahiki zao ili kuondoa chuki na sii kuonyesha kwamba serikali inaweza kulipa posho wanajeshi na ni bora kuliko na wakati huo huo hawawezi kulipa madaktari madai yao.mapambo hayo kwa vyo vyote vile yanaumiza wananchi wanyonge.
 
kwa hiyo chanza cha madaktari bingwa kugoma ni hao madaktari wa jeshi??? bongo bana tumekaa kizuzuzuzu, yaan nao wanataka kulipwa 100000 kila wakisaini na waletewe chakula??? kutoka cafteriaduuu haya bana bongo hii.
Ua haki ya kujibu lolote sababu nawe ni mwana jf , lakini zama ndani uchambue mada kulikokulipuka.Jiulize je hawa madaktari wa kijeshi wanatosha kumudu kutoa huduma katika hospitali zote teule?je kama watakuwa wakutosha hayo mafao wanayopewa yatakuwa mengi kiasi gani?je hili watanzania ndo nanalihitaji?na je hao madaktari wa kijeshi ndo suluhu kubwa ya matatizo ya sekta ya afya? je kama si hivyo je hayo matatizo ya madaktari wengine yatamalizwa kwa kutoa posho kubwa kwa madaktari wa kijeshi?ndugu yangu jitahidi kuchambua matatizo ya nchi kwa masilahi ya nchi yetu kuliko kulipuka.Hao madaktari bigwa wamegoma sababu serikali inafanya mzaha kwa kuona matatizo ya sekta ya afya yanaweza kumalizwa na madaktari wa kijeshi kwa kuwapa posho kubwa huku serikali ililalamika haina fedha.
 
wale wa jeshini wanalipwa na JWTZ mwajiri wao, kwa hiyo wana haki kupata marupurupu yao kama vile mikataba yao inavyosema na hawa wa kwetu wanalipwa na serikali ambayo tumeshaambiwa madai yao yanashughulikiwa.

Msiniulize kwamba serikali ina bajeti ngapi, hilo swali muulizeni waziri wa fweza.
unajihami!!!!! crap
 
kwa hiyo chanza cha madaktari bingwa kugoma ni hao madaktari wa jeshi???

bongo bana tumekaa kizuzuzuzu, yaan nao wanataka kulipwa 100000 kila wakisaini na waletewe chakula??? kutoka cafteria

duuu haya bana bongo hii.

Hustahili kuitwa great Thinker: Period.
 
nawe elewa somo!! anamaanisha fedha zinatumika vibaya sana na si katika mambo ya msingi. kwanini serilkali isifanye maamuzi mazuri ya kuwalipa vzr na kwa heshima watu wanaoshughulikia maisha yetu, na hasa kuwafanya wakae katika mazingira mazuri ili wafanye kazi yao kwa moyo wenye furaha!! lakini unampandishia posho mbunge mwimbaji au wa darasa la 7 akifika bungeni analala hatetei wala hakosoi matakataka ya serikali huku nyuma unamsahau mtu anaejitoa usiku mzima kuwahudumia watanzania wawe na afya bora!
serikali yetu ina madudu sana sana! kupoteza hela kwenye sherehe za ccm ndilo waliloona la maana tena hata bila kuongelea kinachosibu nchi matokeo yake wanaongelea eti wasio na maadili wajitoe kabla hawajatolewa! matope matupu! inaudhi sana hawana uwezo wa kuamua chochote ni kukenua tu meno.
Madkari wamefanya uamuzi mgumu sana na hawafurahii lakn bila hivyo hawatasikilizwa na hii nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom