Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,408
- 8,902
Ningependa kumuuliza Mzee Bw. Edwin Mtei natumaini huwa labda anasoma humu au kama kuna mtu anayeweza kumjibia pia sio mbaya!
Ni hivi majuzi nilinununua Kitabu chake kiitwacho From Goatherd to Governor au (kutoka uchungaji kondoo mpaka kufikia Cheo cha Ugavana wa Benki Kuu)!
Na lengo hasa la kununua hicho Kitabu lilikuwa ni kupata undani wa Mwana Chadema Nr.1 TZ ili kuweza kupata angalau picha ya ni nini nitegemee endapo CHADEMA ikiweza kupata nafasi ya kuongoza!
Moja ya jambo lililonigusa ni pale hasa alipoelezea yeye kutofautiana na Raisi wa 1 wa Tz
Bw. JK Nyerere hasa kuhusiana na sera, ambapo yeye alitaka kwamba sisi tukubali ushauri wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ili kunusuru hali mbaya ya uchumi wetu, jambo ambalo bosi wake wakati huo alilikataa, na hivyo kupelekea yeye kujiuzulu!
Baadaye Tanzania ikaja kukubali kufwata mfumo na ushauri wa Benki ya Dunia, na yeye
Bw.Mtei kulingana na maelezo yake mwenyewe ndani ya Kitabu, alishiriki ktk kuishauri Serikali ya awamu ya 2 jinsi ya kufanya mageuzi ya kiuchumi wakati huo akiwa yuko Shirika la Fedha, na moja ya Ushauri ulikuwa ni sisi kukubali kushusha thamani ya fedha yetu (jambo ambalo Bw.Nyerere alilipinga siku zote ingawaje mwisho wa siku ilibidi asalimu amri) na pia kufungua Uchumi wetu Duniani, mambo ambayo Serikali ilitekeleza!
Sasa swali langu ni hivi, Je bado unaamini kwamba ushauri ulioupa Serikali ya Awamu ya 2 ulikuwa sahihi? ukichukulia kwamba matatizo au changamoto zinazotukabili sasa zimetokana na sisi kufwata ushauri wako wakati wewe ukiwa mshauri wa Shirika la Fedha Duniani?
Je bado unafikiri kwamba swala la sisi kukubali kushusha Thamani ya Shilingi yetu lilikuwa sawa ukichukulia sasa pesa yetu imepoteza thamani kabisa? Sasa hivi Tz haina maana hata kuweka akiba kwani kila siku Fedha yetu inashuka thamani ukiwa na milioni 2 leo miaka 2 baadaye haina maana yoyote!
Je CHADEMA bado watafuata hizo Sera ulizoshiriki kuishauri Serikali ya awamu ya 2 izifwate?