Hivi speech/hotuba yake atakayoitoa haijavuja tu tuanze mjadala?!! Ina maana leo JF imeshindwa kuiweka 'in advance'?? Je, Baraza kuvunjwa?
Cheki tbc live mkuu anaongea hoja ya kwanza ni madaktariPasco kuna dalili ya TV yoyote kuwa live? TBC wapo?? Nina hamu ya kujua TBC watachagua wapi? Arumeru kwenye pesa ama Diamond kwa mwenye mali!
There are currently 121 users browsing this thread. (49 members and 72 guests)
vibalaghashia vimejaa ukumbini.Mkuu wa mkoa anadai rais kila akitaka kuzungumza mambo ya msingi huwa anawaita hao wazee.Kama rais anazungumza mambo ya msingi na vihiyo sijui nchi inaenda wapi
mzee atauliza swali gani?
Anazungumzia mgomo wa madaktari. Wamegoma mara tatu.
Binafsi nadhani JK ana tuma ujumbe kwa "mahasimu" wake wanaodhani
wana mzidi nguvu,....kwamba ana hutubia siku ambayo wana "mtangaza mteule wao"
huko arumeru!
Anaonesha kwamba anaweza tumia kila anachotaka,kwa kuanza tu,vyombo vyote vya
habari viko kwake na arumeru ni kimya.
Kesho sasa,magazeti yata muongelea JK katika front page,Arumeru itakua page moja kabla
ya page ya michezo.
...hivi hapo Dar es salaam hakuna wazee wengine zaidi ya hao wa CCM?...kunahaja sasa ya wazee ambao sio wanachama wa CCM kujitokeza kudai haki yao ya kusikilizwa,la sivyo sisi vijana wa leo tutawajumlisha ktk lawama hao wazee wengine walioamua kukaa kimya na kuwangalia wenzao wa CCM wakilipotosha na kulipeleka kombo taifa...Sitting arrangment iko poa, waheshimiwa wabunge upande wao, viongozi wa serikali upande wao ila sijaona upande wa mhimili wa mahakama!.
Ukiangalia mawazi ya wengi wa hawa wazee wa Darisalama, wamevalia sare ya chama chao wanachokifahamu tangu zamani, nadhani organization ya mahudhurio ni kupitia wale mabalozi wetu wa nyumba kumi kumi!.
Serikali nzima iko hapa wakiongozwa na mawaziri, miongoni mwao ni wale mawaziri na naibu wake ambao ndio muhimu kuliko mawaziri wengine wote. Hawa ni wale wanaoshikilia ile wizara nyeti kwa afya na uhai wa Watanzania!. Kama kuna watu mnadhania kuwa JK atawatemesha mzigo mtakuwa mmepotea sana!.