FROM CD to DVD to ........ CHANGAMOTO KWA WASANII WETU

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Nimesoma articles mbali mbali mbali zinzotabiri kuwa bidhaa inayoitwa CD& DVD storage and Drive zitakosa umuimu kwenye soko. kama ilivyokuwa Diskette. Leo hii Diskket drive na diskette zimebaki kama maonyesho tu na story. Haina umuhimu

Makadirio yanaonyesha mauzo ya CD yalishuka 17% mwaka 2007 na kwa % 20 mwaka 2008 ( Refer to Is the CD Becoming Obsolete? — Reviews and News from Audioholics)

Kwa sasa makadirio haya yanaweza yasiwe sahihi kwa nchi zetu za afrika kama Tanzania sababu mara nyingi tuko nyuma ya teknolojia lakini yanaonesha muelekeo wa tuendako

Ukisoma hiyo article imetaja sababu zinazopelekea kupunguza umuhimu wa CD/DVD. kwenda mbali zaidi ni kwamba hata CD au DVD drive zitakuwa hazina maana sana hapo mbeleni kuwa kifaa cha muhimu kwennye laptop / computer.

Baadhi ya sababu zinakazofanya CD/DVD kuzidi kukosa umuhimu.

  • Technolgy ya flash sorage kama USB imechangia kwa kiasi kikubwa

  • Teknology ya manufacture kuweza BIOS za kompyuta kuweza ku boot na kuinstall software kutoka kwenye flash drive kama USB

  • Uwezo wa USB kuwa na storage space kubwa kuhifadhi mambo mengi kuliko CD/DVD

  • Binafsi naona Data zinakuwa salama(Security& Safety) zaidi kwenye USB kuliko zikiwa kwenye CD

  • Wakat gharama ya CD ni nafuu kuliko USB gharama ya CD/DVD Drive inaongeza gharama za kompyuta hivyo bei za kompyuta zitashuka sana bila kuwa na CD/DVD drive
  • Teknolojia ya MP3 na MP3 player za kisasa
UKisoma article niliyotaja hapo juu inaonyesha sababu nyingine Kushuka matumizi ya DVD hasa kwa wenzetu

  • Kuazima movie sio lazima mtu aende physicaly library anaweza kudownlod au kuangalia movie kwenye website aliyolipia umember
  • Kuna website mfano Amazon zinauza legal soft copy za movie/miziki/Vitabu
  • Sababu nyingine ni internet imewezesha piracy kuwa rahisi
Changamoto kwa wasanii wana wadau wengine

Wakati wasanii na wawezeshaji wao bado wanakazania kuuza na kutengeneza hard copy CD ya kazi zao nawapa changamoto washirikiane na wadau wajaribu kuuza kazi zao online katika softcopy pia.

Mfano wanaweza kuuza soft copy ya kazi zao kwa watanzania walio nje . Sababu watanzania wa nje wengi hawana urahisi urahisi wa kuapata CDau DVD za wasanii wa kitanzania kihalali. So ni kikwazo kama mtanzania anataka kuchanagia kwa kununua kazi halali ya msanii.. . Afanyeje.??!!!!! Hakuna jibu zaidi ya piracy sababu ndio njia iliyo accesible.

Something is better than nothing.

Any Idea U have to add ,suggest, advice ,critize about my my observation ?

Karibu​
 
Kufa kwa matumizi ya CD/DVD, itachukuwa miaka mingi kidogo... Kwa sababu matumizi yake ni makubwa na nchi nyingi bado wanatumia sana hizo bidhaa.

Hayo hayo makampuni makubwa ya kutengeneza CD/DVD ndio makampuni yenye hisa kwenye tasnia ya muziki na sinema, na wao ndio watakao hamua lini wazimalize CD/DVD, lakini kama bado wanapata faida kutoka kwenye hizo CD/DVD, sidhani kama wataziondoa kwenye soko...!

Japokuwa sasa hivi kuna Lunginga (HDTV) zenye kuweza kucheza video/mziki toka moja kwa moja kwenye external Hard, kwa kupitia USB, lakini bado itachukuwa miaka mingi mpaka kuacha kutumia CD/DVD... Na ndio kwanza muendelezo wa CD/DVD umeanza upya, na sasa kuna blu-ray ambazo zina uwezo wa kuifadhi data nyingi sana, kiasa ambacho imekuwa rahisi kucheza filam zenye high-definition.
 
Bado huo muda huo ndugu yangu. Research nyingi zinaonyesha kwamba cd/dvd zinaweza kutunzwa kwa muda mrefu zaidi kuliko media zingine zote za storage. Kwa mfano kuna librabry moja huko america ina cds za early sixties lakini unaambiwa hizi usb devices are mal-function prone. Cds zikiwa na scratches zinaweza zikasafishwa kuondoa scratches lakini hizo usb devices.........!!!
 
Xpaster said:

X paster uko right lakini ebu fikiria jinsi laptop itakvyouwa portable zaidi iwapo DVD drive ikiondolewa . Sasa hivi laptop zinaweza kuboot kwenye USB. Sitashangaa kuona ukiangiza OS kama ya windows kwa sasa unatumiwa kwenye USB. I mean hivi sasana kazi hasa ya CD or DRD drive ni nini sasa amabyo haiwezi kufanywa na USB drive?

Vile vile nilichotaka kusisita ni wasanii wetu waangalie fusra ya kuuza miziki yao online. Watazania waliopo nje hawawezi kupata mizii kihalali sababu haipo.

Wanamuziki hata wa ulaya walianza kupinga biashara za amazon kuuza miziki online lakini baadae wakawa wapole. Atleast kuna watu badala ya kudownload illagal copy wanadowload legal ones. kuliko kugoma kabisa. Hiyo ndo changamoto kwetu na kwa wasanii wetu

Bado huo muda huo ndugu yangu. Research nyingi zinaonyesha kwamba cd/dvd zinaweza kutunzwa kwa muda mrefu zaidi kuliko media zingine zote za storage. Kwa mfano kuna librabry moja huko america ina cds za early sixties lakini unaambiwa hizi usb devices are mal-function prone. Cds zikiwa na scratches zinaweza zikasafishwa kuondoa scratches lakini hizo usb devices.........!!!

Anyway ili kuendelea mjadala Hivi CD & DVD na USB kipi kinatunzika kirahisi na kiusalama zaidi? nadhani hiyo reseach ilifanywa kabla ya USB kuingia sokoni . Kwa kigezo chao cha usalama je CD au DVD ikivunjika? To me USB ni more secure na ni easy kurecover hata ikiharibika than CD or DVD.
 
X paster uko right lakini ebu fikiria jinsi laptop itakvyouwa portable zaidi iwapo DVD drive ikiondolewa . Sasa hivi laptop zinaweza kuboot kwenye USB. Sitashangaa kuona ukiangiza OS kama ya windows kwa sasa unatumiwa kwenye USB. I mean hivi sasana kazi hasa ya CD or DRD drive ni nini sasa amabyo haiwezi kufanywa na USB drive?
Bado kuna faida nyingi ya kuwa na CD/DVD, pia kwa taarifa yako kuna laptop ambazo hazina cd rom, zinaitwa NetBook. Pia kuna hizi ambazo zinapata sifa hivi sasa kwa jina la Touch Pad. Zote hizo hazina CD/DVD rom.

Lakini matumizi ya CD/DVD hazihishii tu kwenye Computer, CD/DVD zina matumizi mengine mengi yakiwemo kucheza muziki kwenye radio CD, au kucheza filamu kwenye DVD player.

Na wataalam bado wanaona kuifadhi data kwenye CD/DVD ni more secure kuliko kwenye USB. Uko mbeleni hao wenye kuhodhi hizi teknolojia watakapo amua kuziondoa sokoni, na wakithibitisha kuwa kutawaletea faida zaidi basi wataziondoa, lakini kwa sasa bado sana kufikia kuziondoa kwenye soko kwani zingali zinaleta faida kubwa kubwa kulinganisha na USB.
 
Samahani kama nitakuwa off-topic, ila sidhani kama teknolojia ya namna ya kuhifadhi (storage) ndio tatizo kubwa.
Tatizo ninaloliona mimi ni migration from making 'video' to making 'films'. Hapa ndipo waandaaji walipo na changamoto, with the rise in cloud computing na kuimarika kwa internet bado naona namna ya kufikisha kazi zao sokoni si tatizo kubwa
 
Gurta Kufikisha kazi sokoni kwa wasanii wa wetu tanzania bado ni tatizo . nimetolea mfano watanzania walio nje wakitaka nyimbo au movie halali za wasanii wetu wazipataje.??

Au soko wanalolenga wasanii na wasambazaji wao ni lipi? kuna fursa ya ICT ikitumika vizuri wanaweza kuwafikia wateja wa nje ya mipaka kirahisi
 
Kwa huo mfano wa upatikanaji wa hizi 'video' au nyimbo nje ya TZA, unajaribu kueleza ufinyu katika usambazaji (distribution).
Sioni ni kwa namna gani hoja ya 'CD to DVD to...' inavyoingia hapo.
Bado sidhani kama kuna future ya prod company au distributor kuuza thumb drives fully loaded with a movie. Mfano, Netflix pamoja na kuuza filamu online bado wana-rent DVDs na Bluray, sidhani kama wanashindwa kuuza kwa kutumia flash disks.
Pia kuna tatizo la legislation na copyright (and copyleft too), ili ku-decode DVD unahitaji programu maalum wakati kwa flash unahitaji PC pekee.
Then, tofauti na unavyotaja kuwa flash inauwezo wa kubeba content zaidi; tatizo ni kuwa ili iweze kutumia with full functionality unahitaji kuisanikisha kunako kompyuta yako.
 
Gurta nilivyosema from CD to DVD to ........... nilitaka kuonyesha jinsi teknolojia inavyobadiliaka na wadau wanatakiwa kujua njia za ziada za kuuza kazi zao.

Nachosema sio wasaniii na wasambazaji walale na CD na DVD wanatakiwaa kutimia na fursa nyinginzo e zilizopo. Amazon wanauza nyimbo nyingi za wasanii wanachukua commision yao na wasanii wanachukua chao. I mean tanzania kuna fusra ya kuuza kazi zao online. Wanaweza kuunda umoja wao na kutengezewa Tovuti amabayo itakuwa na collection ya kazi zao.

Hapa bongo wadau wa IT kushirikiana na wasanii wanaweza kuweka kitu kama hicho cha amazon na wengineo.

Hii ya USB haihusiani na wasanii but niliandika kuonyesha wapi tunaelekea. May be in future Majumbani tutakuwa na "USB player" na sio DVD player. Kwenye magari tayari kuna music system haziitaji CD au DVD ukichomeka USB unakula mziki. Kwenye Ipad tayari tunaona So may be miaka mitatu au mitano ijayo Laptop zitakuwa hazina DVD drive. USb will be eveything

USB ndo future DVD player na DVD drive zitapotea. ni muda tu

Nadhani tatizo nimeongelea vitu tofauti katika mada moja. ila mambo mawili makuu niliyoandika

  • DVD drve na DVD player zitapotea mbeleni may be USB ndo itachukua nafasi
  • Wasanii wa Tanzania na wawezeshaji waangalie uwezekano wa kuuza kazi zao online may be kwa watu wa nje. Something is better than nothing.
 
kwa kuongezea tu imeshatengenezwa BD yenye 400GB na kuna iliyoko kwnye development ambayo itakua realesed 2013 yenye uwezo wa 1TB so itachkua mda!
 
  • DVD drve na DVD player zitapotea mbeleni may be USB ndo itachukua nafasi
  • Wasanii wa Tanzania na wawezeshaji waangalie uwezekano wa kuuza kazi zao online may be kwa watu wa nje. Something is better than nothing.
Mbona radio player na TV zenye kutumia USB zipo nyingi tu.

Yaani kama una USB na kama ina movies ndani unaichomeka kwenye TV yako na una play kama kawaida.
 
Goooood!--Kuhusu suala la kuweka movie online--nilifikiria mimi, kwani distributor wetu hapa TZ wananamiwa na mavideo na kushindwa kununua kwa msimu mmoja-coz ni gharama kubwa kuaanda CD/DVD/VHS ya halali-So ni good idea kuweka movie zetu Online, lakini tujiulize.
1.Mfano mimi nilioko TZ tena hukoooooo mwisho wa mto-ninayo internet yanye speed ya uploading ya movie yangu mbayo ni HD-High Quality?
2.Kama ipo!-si itakuwa akisha kudownload mmoja na wengine watarushiwa kama acht hapa JF or kwengineko.!!!-Wizi utakuwa simple then DVD.
3.Rabda awepo distributor maalumu wa online-ambaye, atahakikisha usalama wa kazi akisha kununua.
4.USB Drive sio bootable hadi ufanyie uchakachuzi--na huwa secondary drive permanent.
5.Na kadha wa kadha
 
Asikwambie mtu DVD/CD na sasa hivi BD ndio mpango mzima, hauwezi ukaweka document kwenye flash zikakaa muda mrefu bila ya kushambuliwa na virus lakini kwenye cd zinaweza zikakaa mudamrefu sana labda cd uikwaruze,wataalam wanasema unaweza ukaifukia cd chini ya ardhi kwa miaka 50 na ukatoa ukaitumia naikafanya kazi kama kawaida.
 
Back
Top Bottom