Elections 2010 Friends of Dr.Slaa FOD kuhakikisha Slaa anaingia ikulu hatari tupu........

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
WANAHARAKATI wa kada mbalimbali nchini, wameanzisha umoja unaojulikana kwa jina la Friends Of Dk. Slaa (FOD) kwa ajili ya kumsaidia kwa hali na mali kuhakikisha mgombea huyo wa kiti cha urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anashinda.

FOD ambao wameanza harakazi za kuhamasishana nchini nzima, leo wanatarajia kuwa na kikao kizito kwa ajili ya kuangalia namna bora ya kuhakikisha Dk. Slaa anaibuka kidedea.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Mratibu wa FOD, Seleman Rehani, alisema kuwa kundi hilo linajumuisha wafanyabiashara wakubwa nchini, wanafunzi wa vyuo, wanawake na kada zingine katika jamii ambao pia wana itikadi tofauti za vyama.

"Marafiki wa Dk. Slaa (FOD) ni jumuiya kubwa ambayo inaundwa na watu mbalimbali wenye itikadi tofauti za vyama. Kundi hilo linaunganishwa na masuala ya msingi yanayolihusu taifa na linakerwa na ufisadi na umaskini wa Watanzania.

Limeamua kuuanzisha umoja huo kuhakikisha mpiganaji wao anaingia Ikulu, kuleta maendeleo," alisema Rehani.

Kwa mujibu wa mratibu huyo, FOD imefungua akaunti maalum na mtandao wa mawasiliano unaoelekeza namna ya kujiunga na kumsaidia Dk. Slaa katika mkakati wake wa kutaka kuingia Ikulu.

"Tumeanza hivi karibuni, tulipoanza tulikuwa kama marafiki 200, lakini sasa mtandao wetu ni mkubwa. Tumejipanga kuhakikisha Dk. Slaa atakapoanza kampeni, anawafikia wananchi wote na kundi letu kwa sasa lipo nchi nzima," alitamba mratibu huyo.

Alisema hivi sasa wanaangalia namna bora ya kuwafikia vijana wa kati ambao bila shaka wanampenda Dk. Slaa, lakini hawakujua namna ya kumfikia na kumchangia.

"Kundi letu sio la matajiri tu. Tunataka hata Mtanzania wa chini mwenye mchango wa mawazo na kila hali amsaidie Dk. Slaa na ndio moja ya malengo ya FOD kuwa na mkutano huo kesho (leo)," alisisitiza.

.........Yaani kampeni za Slaa kama ya Obama vile..........mwaka huu yetu macho.
 
Nilikuwa nafikiri Dr. Slaa atakapokuwa kwenye Kampeini aruhusu kuulizwa maswali. Maana naona CCM hawana hiyo nafasi ya maswali, Nadhani kama wataruhusu maswali 3 hadi matano kila mkutano itapendeza sana kuonyesha ukaribu wake na wanchi na pia kuonyesha ufahamu, dhamira yake ya ukweli itakuwa wazi
 
Luteni hiyo kitu nzuri sana na inatia moyo na sisi hapa tunonga mkono tuchangie japo senti chache ila tunachangia maneno hapa ,walio karibu ni vema kushawishi mtu wako wa karibu naye ajue jinsi ya kupiga kura kwa hekima yaani kwa slaa.
 
Luteni hiyo kitu nzuri sana na inatia moyo na sisi hapa tunonga mkono tuchangie japo senti chache ila tunachangia maneno hapa ,walio karibu ni vema kushawishi mtu wako wa karibu naye ajue jinsi ya kupiga kura kwa hekima yaani kwa slaa.
FOD ni kundi zito lina wafanyabiashara wakubwa waliojitolea nasikia Sabodo ni mmojawapo, watafanya kampeni sambamba na presidential campaign team lakini kwenye makundi tofauti yanayojitegemea na maeneo tofauti, kweli inatia moyo. Mimi huwa naona mwaka huu ni kama mwaka wa kupata uhuru Mungu isaidie Tanzania sikiliza kilio chetu.
 
Ila Luteni!, Sabodo si mwanachama wa CCM? ok alichangia Chadema mil100 ili kuimalisha upinzani na alisema anaona Chadema ni chama makini.

Je bado yuko nyuma ya chadema ? wampe kadi basi ahaaaaaaaa
 
Ila Luteni!, Sabodo si mwanachama wa CCM? ok alichangia Chadema mil100 ili kuimalisha upinzani na alisema anaona Chadema ni chama makini.

Je bado yuko nyuma ya chadema ? wampe kadi basi ahaaaaaaaa
FOD haina itikadi ni mtu yeyote mwenye mapenzi na ushindi wa Slaa na hasa anayekerwa na ufisadi na umasikini.

"Marafiki wa Dk. Slaa (FOD) ni jumuiya kubwa ambayo inaundwa na watu mbalimbali wenye itikadi tofauti za vyama. Kundi hilo linaunganishwa na masuala ya msingi yanayolihusu taifa na linakerwa na ufisadi na umaskini wa Watanzania".
 
FOD haina itikadi ni mtu yeyote mwenye mapenzi na ushindi wa Slaa na hasa anayekerwa na ufisadi na umasikini.

"Marafiki wa Dk. Slaa (FOD) ni jumuiya kubwa ambayo inaundwa na watu mbalimbali wenye itikadi tofauti za vyama. Kundi hilo linaunganishwa na masuala ya msingi yanayolihusu taifa na linakerwa na ufisadi na umaskini wa Watanzania".

Nimekusoma vyema ,ila still nina swali sorry kama I'm slow.
Kwa hiyo Sabodo ham support JK kwenye huu uchaguzi? Anyway inatima moyo kwepo kwa FOD
 
Tunawaungeni mkono kwa dhati. Tuko tayari kuchangia sio mawazo tu bali fedha vile vile. Kama hairuhusiwi kutuma michango toka nje (this needs verification), basi tutawaambia ndugu zetu walio Dar watoe michango kwa niaba yetu.

Tupeni details za namna ya kushiriki.

Na kweli huu ni mwaka wa UHURU. Uhuru wa koundokana na ukiritimba wa madaraka wa CCM. Iweje wahodhi madaraka miaka 49 na badala ya kuendeleza nchi walee tu mafisadi?

Na hawana aibu hata kwenye hotuba zao. Badala ya kuomba msamaha kwa kuzorotesha Elimu, wenyewe wanasema oh, nilikuwa graduation Kenya juzi wakapata PhD watu 100, graduation hapa kwetu PhD moja tu. Huoni ni kosa la utawala wako wa CCM? Unatulaumu sisi?
 
Ndugu zetu FOD,

Kwa ishu ya talking points, you have your work cut out for you. Yaani huyu JK ameanza kwa kuhaha sana. Hajajua kwamba anatakiwa aseme amefanya nini miaka 5 iliyopita. Yaani anasema:
  1. Sijawahi kunyonga​
  2. Sijawahi kukataa kura za wafanyakazi.​
Yaani hivi amewahi kufanya nini? Aseme hicho, sio sijawahi hiki sijawahi kile. Au nimuulize: umewahi kulea mafisadi? Yaani watu waliohujumu uchumi, na ushahidi ukapatikana, Tanzania, Uingereza, Italia nk, kisha ukawalinda? Unataka tukuchague ili uendelee kuwalinda?​
 
Tahadhari: Concentration isiwe kwa Dr. Slaa peke yake, iwe na kwa wabunge wake ili kurahisisha uongozi wake.
 
Tatizo letu watanzania ni kuangalia wengine wanafanyi nini, na sio sisi tunauwezo gani. Ndio maana baadhi yenu mnatuletea lugh aza KiCCM kuwa FOD kuna wafanyabiashara wakubwa. Acheni hiyo habari. Kama kuna kitunkama hicho waliokianzisha wanastahili pongezi disseminate true and correct information of how everybody can participate voluntarily and in partcular financially ili kuwezsesha CHADEMA na wagombea wake wote particulary Dr Slaa waweze kufanya kampeni
 
Tunaomba mawasiliano, namba za simu, email n.k. Tuko wengi tunataka kumsapoti Dr. Slaa. Tumechoka mno na CCM hasa huyu mbabaishaji JK
 
Naomba mnipigie simu 0659 28 19 64 mje kuchukua shilingi laki moja. Niko maeneo ya Mwenge na Mlimani City kwa sasa.
 
Back
Top Bottom